TANZIA Hakimu Godfrey Mwambapa afariki dunia

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,627
218,056
Aliyekuwa Hakimu Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na baadaye kuhamishiwa Mtwara, Geofrey Mwambapa amefariki Dunia.

Hakujatolewa taarifa zaidi za ugonjwa wake wala hospitali aliyofia

Pumzika kwa amani

===========

Mahakama ya Tanzania inasikitika kutangaza kifo cha Mtumishi wake aliyekuwa Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mahakama ya Wilaya ya Nanyumbu-Mtwara, Marehemu Godfrey Mwambapa (pichani) kilichotokea leo Februari 11, 2021.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Mahakama ya Wilaya ya Nanyumbu zinasema kuwa marehemu alifikwa na umauti leo saa moja (1) asubuhi alipokuwa akipelekwa hospitali ya Wilaya ya Nanyumbu.

Kwa sasa msiba upo nyumbani kwa marehemu Nanyumbu-Mtwara huku taratibu za kusafirisha mwili kuelekea Mbeya zikifanyika.

Mahakama inatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki kwa kuondokewa na mpendwa wao.

BWANA AMETOA, BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.
===

Hakimu Mwambapa katika uhai wake alisikiliza na kutoa hukumu katika kesi mojawapo zilizokuwa zinaikabili JamiiForums na Viongozi wake mahakama ya Kisutu. Hakimu Mwambapa aliwaachilia huru Maxence Melo na Micke William kwa kuona hawana Hatia. Baadae hakimu Mwambapa alihamishiwa mahakama ya Mtwara

Zaidi, soma:
Kesi namba 457: Mahakama yasema Maxence Melo na Micke William hawana Kesi ya kujibu! Yawaachia huru

FB_IMG_1613029612238.jpg
 
Kuna watu wanaona sifa kupost habari za vifo. Huu upuuzi usiendekezwe jamani
Inakuuma nini mkuu? Mbona radio one kila siku kunamatangazo ya vifoo.

Kuna watu inatusaidia kujua marafiki/jamaa waliofariki na tulipotezana nao mda mrefu.

Kama jana nilipata habari ya Peter mamiro aliekufa na mkewe.

Achana na kuendekeza siasa kila mahali. Wengine wamekufa kwa ajali sio kila mtu ni corona.
 
Back
Top Bottom