Hakika nitakapooa, nitaoa mwalimu

Hakika nitakapooa, nitaoa mwalimu

1.wengi wao wana poor financial background hivyo ni rahisi kulaghaiwa hasa akikutana na mwanaume materialist.
4.jiandae kujenga ukweni ulimuona
5.jiandae kuwa na extended type of family
Acha kupotosha mkuu. Mimi nina ndugu 4 walimu (3 ni wadada na wameolewa).

1. Wazazi wetu sio maskini, Mungu kawapa uwezo wa kutulea na kutusomesha. Hapa umegeneralize vibaya!
4. Hakuna shemeji anayejenga kwa wazazi wangu. Wazazi wetu wanafanya kazi na sisi watoto wao ni wajibu wetu kuwatunza na SIO wa wengine.
5. Hakuna extended family. Kila mtu anaishi kwake na familia yake na tunakutana kwa wazazi kuwasalimia.

Watu huamua kusomea fani fulani kwa interest zao. Mungu akusaidie akili ya kufikiria vyema!
 
Kwanza, najituma sio tegemezi na ombaomba sababu naelewa umuhimu wakujitafutia na kuwajibika kama binadamu wanavyopaswa.

Pili, wanaheshma kwa wanaume kama walivyo na heshma kwenye taaluma zao, wanajua nini chakusema na wakati wakukisema bila kusahau namna yakukiwasilisha.

Tatu, wengi wao wana hekma na busara sana tena wapo soft and kind in nature na wengi ndoa zao hudumu (Logical)

Nne, hawazeeki mapema/upesi hapa ninauhuakika na mtaniunga mkono.

Tano, first-ladies hasa Tanzania, hapa ndo patamu sababu namie Magogoni napatamani.

__Leo ngoja tuwasifie wanawake zetu sababu tunawapondeaga sana.
"Walimu siku hizi ndo chaguo la kuoa"
 
Walimu wapo wengi sana kuliko kada yyte Tanazania, sasa ukianza kuainisha kufa, kuzaa, kutembea nje ya ndoa, kutokuwa wa kileo, pesa haitosh obvious watakuwa walimu 7bu wao ni wengi ndo maana hata hesabu yao kwenye u-first lady ni wao. Ila kumbukeni a brave man marries teacher. Walimu hata ukioa kila mtu anajua una mke!!
 
Inategemea ni mwalimu wa level gani. Lakini wengi wao siku hizi wako kimaslahi zaidi.

Wengine hawajatulia kabisa, kugawa penzi njenje.
 
teh....... kuanza kufikiri kuoa kwa kuangalia taaluma ya mkeo ni dalili ya kutojiamini....

kuna baadhi huwaza hivi kuogopa challenges...maana kuna proffesion nyengine kama law n.k lazima challenge ziwepo..watu hawatak kwa vile walimu ni watu wenye kuridhika.

atoto ni kweli .... Evelyn Salt ni kweli hii
images (1).jpg
 
teh....... kuanza kufikiri kuoa kwa kuangalia taaluma ya mkeo ni dalili ya kutojiamini....

kuna baadhi huwaza hivi kuogopa challenges...maana kuna proffesion nyengine kama law n.k lazima challenge ziwepo..watu hawatak kwa vile walimu ni watu wenye kuridhika.

atoto ni kweli .... Evelyn Salt ni kweli hii
Hahahaaaaaa!!! Ngoja kwanza niajiriwe nitakujibu bwana shemeji, Maghufuli kagoma kutoa ajira.
 
Erica mwaisumo haya ninayoongea sio kwamba naongea kwa mtu mmoja, ila waalimu asilimia kubwa ni rahisi sana, kufikia tar 15 mwlm hoi, haoo hata hela ya nauli ya kuendea kazin inasumbua hapo ndipo wanatafunwa vibaya sana, japo sio wote, kuna waalimu humu ni majembe mno. Ila wengi wapo hoi.
Teh teh teh teeeh!! Hivi wewe wanawake hawanaga jema kwako?? Itabidi tumtafute huyo alokuumiza aje akuombe msamaha.
 
Hawa watu wana kipaji cha ziada kutofautisha na wanawake wa kada zingine ,nadhani kitendo cha kuwa na watoto wa shule muda wote kuna mpa nafasi kubwa sana ya kupanua mawazo yake na pia kujifunza kwa hao watoto anao wafundisha ,hiyo inapelekea hata yeye kuikuza familia yake katika njia inayofaa , pia ni wavumilivu usifikirie ni mchezo kumfundisha mtoto akajua mathalani tu hesabu za kujumlisha,kutoa,kugawanya ,kutokana na huo uvumilivu ni raisi sana wao kukabiliana na changamoto za maisha au ndoa kwa ujumla wake ,
Mara nyingi watoto walio lelewa kwenye familia zenye walimu ni wenye heshima na maadili mema
Hongereni walimu wetu
Uko sawaa kk
 
Back
Top Bottom