STUNTER
JF-Expert Member
- Dec 15, 2015
- 13,077
- 17,262
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, LHRC kimelaani kitendo kilichofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda dhidi ya mtumishi wa serikali. Kupitia taarifa yake, Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho, Dkt. Helen Kijo-Bisimba, amesema Makonda alipaswa kumsikiliza mtumishi huyo na si kumkejeli kama alivyofanya.
Makonda alidaiwa kutoa kauli hiyo wakati wa ziara yake ya siku 10 kusikiliza
malalamiko ya wananchi wa mkoa wake. Sehemu ya taarifa hiyo inasema: Sote tumeshuhudia kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa katika ziara ya kuzungumza na wananchi huko Kinondoni.
Ndugu Makonda amemshambulia kwa maneno mtumishi wa Manispaa ya
Kinondoni, Bi. Rehema Mwinuka baada ya kumtolea matamshi ya kejeli na kumnyima haki yake ya asili ya kusikilizwa na hata kujieleza. Makonda alinukuliwa akimfokea Bi.Mwinuka “hawa ndio vichaa tunaohangaika
nao, toka hapa”.
Tanzania ni nchi inayoheshimu utawala wa sheria kwa mujibu wa Katiba ya waka 1977. Hivyo serikali yetu kwa mujibu wa katiba hiyo ina mihimili mitatu ambayo ni Serikali yenyewe, Bunge na mahakama . Katika utendaji chombo
kilichopewa mamlaka kusimamia haki na tafsiri ya sheria ni mahakama pekee.
Licha ya misingi hii ya kikatiba kuwepo viongozi wa serikali wamekuwa wakichukua nafasi ya Mahakama na kuhukumu na kuwahesabu watuhumiwa kuwa na hatia moja kwa moja pasipo kujua wanakiuka misingi ya
katiba waliyoapa kuilinda. Ibara ya 13 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania pamoja na mambo mengine inasema “ Mtu hata hesabiwa kuwa na hatia mpaka Itakapo thibitishwa na Mahakama yenye mamlaka”
Kitendo cha kuwahukumu watu mbele ya hadhara na kuwataja majina kama wezi , wajinga, wasiokuwa na akili timamu na lugha zingine zisizo na staha ni kudhalilisha utu wa mtu na kuvunja misingi ya Katiba. Tunasikitika kuwa mbali na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kukemea kwa nguvu
uvunjwaji huu wa sheria na ukiukwaji wa Haki za Binadamu unaofanywa na viongozi bado viongozi wetu wameendelea kuwa wakaidi na kusahau kuwa dhamana waliyo nayo iko kwa mujibu wa sheria na badala yake wanajiona
miungu watu kama alivyojifafanua Mhe. Makonda kwa kusema “huna wa kukutetea mimi nikisimama mahala Mungu amesimama”.
Aina hii ya kauli haitarajiwi kutumika kwa viongozi wa serikali ya Kidemokrasia .Kauli hizi ni aina ya kauli mbazo zimekuwa zikitumika katika serikali zilizofuata mifumo ya kifashisti. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ya mwaka 1977 Ibara ya 13(1) “Watu wote ni sawa mbele ya sheria, na wanayo haki, bila ya ubaguzi wowote, kulindwa na kupata haki sawa mbele ya sheria.”
Ibara hii ya katiba inatushangaza kuona ni wapi viongozi wetu wanatoa
mamlaka ya kujitangaza wao ni Mungu na waliopo chini yao hawana haki ya utetezi. Tunapenda kuwakumbusha kwamba kwa mujibu wa katiba Ibara ya 8
(1) inatanabaisha kuwa; “Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Nchi
inayofuata misingi ya demokrasia na haki ya kijamii, na kwa hiyo –
(a) wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi kwa mujibu wa Katiba hii;”
Hivyo tunapenda kumkumbusha mkuu wa mkoa Makonda kuwa yeye amepewa dhaman tu na wananchi na hivyo yeye si Mungu kama anavyodhani. Kanuni za utumishi wa Umma za mwaka 2014, Kanuni 107(1) na (2) zinaeleza bayana kama ifuatavyo:
“107 (1) Mtumishi wa umma anapofanya kosa kuhusiana na kazi yake,
Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi au Mkuu wa Idara husika atapaswa kuzingatia kama kosa hilo ni la jinai au ni la uvunjaji wa nidhamu za
kazi au aina zote mbili.
(2) Iwapo mtumishi atafanya kosa la kinidhamu, Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi au Mkuu wa Idara atampa taarifa ya dai hilo mtumishi husika na kupewa nafasi ya kujieleza na baadae kuchukuliwa hatua muafaka.
Taarifa ya mtumishi huyo itawasilishwa kwa maandishi kwa Katibu wa chama cha wafanyakazi au mwakilishi wa wafanyakazi aliyomo katika Kamati ya Uongozi.” Kifungu hiki kinatanabaisha wazi kwamba Mh. Makonda amekuwa akikiuka taratibu za kisheria za uwajibishaji wa watumishi wa serikali walio chini yake.
Hata hivyo kauli hiyo ya matusi pia ni udhalilishaji mkubwa wa kijinsia ukizingatia Dunia inaadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto. Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu
kinaendelea kuwasihi viongozi wa serikali kutopuuza misingi ya utawala wa sheria kwani kwa kufanya hivyo wanavunja haki za wengine na kukiuka misingi ya utawala wa sharia na utawala bora.
Tunaamini kwamba kuna watanzania wengi wanateseka huko mitaani na wanahitaji msaada. Nia ya serikali kufanya ziara katika maeneo mbalimbali inaweza kuwa ni njema sana katika kukuza uwajibikaji isipo kuwa tu
kama taratibu za kisheria na misingi ya utawala bora itazingatiwa katika zoezi hilo.
Ziara hizi zingetumika zaidi kugundua maeneo dhaifu na kupanga mikakati ya kuboresha kuliko kugeuka kuwa mahaka za wazi ambazo zinaweza kuwa chombo kikuu cha uvunjaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya katiba yetu. Hata hivyo tunamtaka Ndugu Paul Makonda kumwomba radhi Bi. Rehema Mwinuka kwa kumdhalilisha kwa matusi tena mbele ya
hadhara.
Tunaamini kwamba serikali inaweza kutimiza azma zake bila kukiuka utawala wa sheria kwani kuongoza bila kufuata katiba si ruhusa katika mfumo wa kidemokrasia.
Chanzo: Bongo5