Haki Za Binadamu Walaani Kufungiwa MwanaHalisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Haki Za Binadamu Walaani Kufungiwa MwanaHalisi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by lukanda, Aug 3, 2012.

 1. l

  lukanda New Member

  #1
  Aug 3, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watetezi wa haki za Binadamu chini ya Mwamvuli wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDs),1 kwa ushirikiano na wadau wengine tunapinga vikali kufungiwa kwa gazeti la MwanaHalisi na Serikali mnamo tarehe 30th Julai 2012 kwa kutumia Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 Sura ya 229. Tunatambua kwamba Mwanahalisi ni gazeti la kujitegemea na la kichunguzi hapa

  Tanzania.


  Kwa pamoja, tumeona kuwa kufungiwa kwa Gazeti hili kunaonesha dhahiri nia ya serikali kuleta hofu na kuwanyamazisha wapigania haki za binadamu, vyombo vya habari, na watetezi wa haki za binadamu. Gazeti hili la MwanaHalisi limekuwa likitoa taarifa kwa umma kuhusu nani wahusika kwenye sakata la kutoweka na kuteswa kwa Dr Ulimboka, baada ya kuona serikali imelifumbia macho swala hili Mwahalisi limekuwa likifanya taarifa za kichunguzi ambazo zimekuwa zikitolewa kwenye mfululizo wa matoleo ya magazeti ya Mwanahalisi.  Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDs) tumeguswa na swala hili na tumeona kuwa hii ni nia dhahiri ya Serikali kuvizuia vyombo vingine kutokuzungumzia masuala nyeti yenye maslahi ya umma Tunahofia kuiona Serikali inatumia sheria ya Magazeti ya Mwaka 1976 Sura ya 229, ambayo ni moja ya sheria mbovu na isiyo na misingi ya haki za binadamu. Sheria hii kwa miaka mingi imekuwa ikipigiwa kelele na ni sheria kandamizi, pia na ni sheria ambayo inapingana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  <<<HABARI KAMILI>>>

   
 2. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #2
  Aug 3, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Ingawa Kubenea anastahili haki sawa na binadamu wengine, alijichanganya mwenyewe kwa kukubali kutibiwa na serikali halafu serikali hiyo hiyo akawa anaipiga madongo. Alipaswa achague moja kuwa moto au baridi. Serikali inayofungia magazeti haina tofauti na mbwa aina ya chihuahua ambaye hubweka sana lakini ukimkaribia hutimua mbio. Aliyemshauri Kikwete kufunga Mwanahalisi hampendi. Maana kama ni kutokana na hasira ya kufichuliwa waliomteka na kumtesa dr Ulimboka kila mtu sasa anajua kuwa kumbe walitoka nyumbani mwa Kikwete yaani Ikulu ambayo Nyerere alisema imegeuka kuwa pango la wezi.
   
Loading...