HAKI YA MWANAMKE YA KUJITOA KATIKA NDOA NDANI YA UISLAM

HAKI YA MWANAMKE YA KUJITOA KATIKA NDOA NDANI YA UISLAM

Relief Mirzska

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2017
Posts
13,976
Reaction score
22,418
Leo katika pitapita zangu jamvini nilikutana na uzi wa Sky Eclat unaosema "Ikitokea anakwambia hisia zake kwako zimebadilika utafanya nini?" ambapo miongoni mwa wachangiaji mfano Mother Confessor alisema "Kuna namna mbili juu ya jambo hili, kwanza kwenye ulimwengu wa kiroho na kwenye ulimwengu huu wa mwili na nyama" . Kutokana na kauli hiyo ndipo nlipoamua kufungua makabrasha yangu ili nije na huu uzi ambao naamini wapo baadhi ya watu watajifunza jambo/ mambo.

Katika kumjibu Sky Eclat lakini kwa kuangalia ulimwengu wa kiroho na kwa mtizamo/ msimamo wa dini ya kiislamu tena kwa upande wa mwanamke juu ya hali hiyo ni kwamba:-

Inapofikia hali mwenza wako akakuambia au mke wako akajihisi kwamba hana tena hisia za kimapenzi au hana tena upendo na wewe basi amepewa ruhusa ya kupata talaka yake i.e yeye mwanamke ndio afanye initiation na amlazimishe mwanamme ampe talaka yake, LAWFULLY.

Hii hali inaitwa KHULUU. Khuluu ni utenganishi kwa kutoa kikombozi cha kujivua uanandoa.

Hivyo basi, Khuluu ni aina ya "talaka" aliopewa (haki hiyo), kimsingi, mwanamke- kupitia utaratibu maalum- kumuwezesha kudai kujivua uanandoa endapo amefikia kikomo cha kutoweza kuvumilia vitendo viovu vya mume wake, vyenye kuweza kuhatarisha maisha yake, au kwenda kinyume kabisa na MAAMRISHO na maadili ya dini.

Miongoni mwa vitendo viovu hivyo ni KUMPIGA MARA KWA MARA, KUMUADHIBU, KUMTESA, UZINZI ULIOKITHIRI, ULEVI WA KUPINDUKIA UNAOPELEKEA KUMFANYIA UNYAMA NYUMBANI, UNYANYASAJI ULIOKUBUHU n.k

Hali nyengine ambayo mwanamke ameruhusiwa kufanya KHULUU ni pale ambapo kwa dhati ya moyo wake, amejiona hana mapenzi tena na mumewe/ hana hisia tena na mwanamme huyo au, mwanamme (kwa sababu yoyote ile hata kama ni maradhi au kifungo) ameshindwa kumkidhia haja yake ya kimwili, basi mwanamkee huyo amepewa ruhusa ya kufanya khuluu kwa sharti la kuwa huyu mwanamke atalazimika kurudisha kile alichopewa kama mahari wakati anaolewa na katika kesi hii hicho kitu kitaitwa (ajikomboleacho). Marejeo ni Qur an 2:229

TAHADHARI: Mwanamke anatakiwa awe bila kushawishiwa na mtu, na kwa uadilifu na ukweli wa hali ya juu hawezi tena kuvumilia juu ya ndoa hii.

Hakika Uislam umempa haki na nyadhifa kubwa mwanamke kuliko mfumo mwengine wowote, ila tu haki na nyadhifa hizo mwanamke amepewa ACCORDINGLY. Uislam upo mbali kabisa na kumkandamiza mwanamke kama wengi wetu tunavyodhani au tunavyoaminishwa! Hakika kila katazo ambalo mwanamke amepewa ni kwa faida yake mwenyewe 100%

Relief Mirzska
 
Swali:
hiyo mahari atairudisha mwanamke hata kama wameishi muda mrefu na kufanikiwa kupata mtoto/watoto?
 
Sawa ila mwanamke hapo atakua amekandamizwa.
Ukiangalia kwa makini masharti ya kutoa talaka...
Hayataki moja kwa moja muachane, bali yanataka mtu ujifikirie upya juu ya ile sababu inayomfanya mwenzako aombe talaka, au kutoa talaka...
Ili kama ni mtu mwenye akili na uelewa uweze kurekebisha makosa na muendelee na ndoa yenu...
Nimejaribu kueleza kwa uelewa wangu na fikra zangu juu ya Talaka...

Ndoa ni Ibada hivyo Mungu hatopenda kuona mnaivunja ibada...
 
Ukiangalia kwa makini masharti ya kutoa talaka...
Hayataki moja kwa moja muachane, bali yanataka mtu ujifikirie upya juu ya ile sababu inayomfanya mwenzako aombe talaka, au kutoa talaka...
Ili kama ni mtu mwenye akili na uelewa uweze kurekebisha makosa na muendelee na ndoa yenu...
Nimejaribu kueleza kwa uelewa wangu na fikra zangu juu ya Talaka...

Ndoa ni Ibada hivyo Mungu hatopenda kuona mnaivunja ibada...
Sawa
 
Back
Top Bottom