Haki ya kuzaliwa ni tunda la uzalendo

Haki ya kuzaliwa ni tunda la uzalendo

Fue Fue

Senior Member
Joined
Jan 6, 2013
Posts
107
Reaction score
128
Haki ya kuzaliwa ni haki ya msingi, Taifa linalojali watu wake litawakubali popote duniani walipozallia kwa kulinda utaifa wao. Haki ya kuzaliwa ndio msingi mkubwa wa uzawa duniani na Tanzania. Tukilinde kizazi chetu kwa kukitambua na kulinda uraia wake popote pale kinapozaliana.

Leo dunia nzima Mtanzania anaona fahari kusafiri kwani atakutana na watanzania wenzeka na kurahisha maisha yake kwenye nchi ngeni.

Leo viongozi wa serikali, dini, siasa, makampuni na watu binafsi wanapata unafuu wa maisha wakiwa nje ya nchi zao kwasababu kuna watanzania wengi wakarimu huko nje.

Leo wasanii wetu wanapata world recognision kwasababu kuna diaspora wengi wapo nje na kukutumia kazi zao, kufanya shoo, kuwapelekea technologia na kupanua masoko yao.

Leo katika historia ya Taifa kunamakundi makubwa ya diaspora, makampuni kama bank crdb, akiba, nbc, nccf, ppf, shirika la nyumab, nk wanakwenda nje kwa watanzania kuuza bidhaa wakijua hili ni soko muhimu sana kwao.

Leo serikali inatoka kwenda nje kuwaomba watanzania wasomi, wenye ujuzi mbalimbali kuisaidia nchi.
Leo Serikali inaokoa fedha nyingi kwa kuwatumia watanzania walioko nje kuchunguza kama kampuni zinazoomba tender habari walizozipeleka Tanzania ni zakweli.

Tanzania sasa inawatumia watanzania kubaini wale wanaohujumu uchumi na kuficha fedha nchi zanje na kuokoa mabilioni ya shillingi.

Leo baadhi ya wafanyabiashra wa Tanzania wanapata fursa kuwekeza nje ya nchi kwa kutumia Watanzania wanaoishi nje kwa kuamini kabisa sio rahisi mtanzania mwenzeka kupote na mali.

Kwanini ikiombwa haki ya kutambua haki zao za kuzaliwa inakuwa ngumu wakati wote tunahitajiana? Ni rahisi kwa sasa kwani ni kizazi cha kwanza, je watoto na wajukuu wa hii diaspora tutawaachaje? Tuwape haki ya kuzaliwa ili huu mwingiliano usiishie kwenye kizazi chetu tu uendelee kizazi hata kizazi.

Haki ya kuzaliwa ni tunda la uzalendo, uaminifu na nchi yako, ulinzi wa nchi, we can do it now and today.

FUE FUE
 
Back
Top Bottom