Naomba na Mimi mnijulishe kuhusu jambo hili.
Nilifanya kazi huko nyumbani Tz kwa kipindi cha miaka kadhaa, kwa waajiri wawili tofauti.
Baadaye nilipata mkataba wa kazi ktk nchi zingine, niliamua kuomba likizo isiyokuwa NA malipo ya miaka kadhaa kutoka KWA mwajiri wangu wa pili, naye amenikubalia.Mpaka sasa nipo nafanya kazi nje nchi na nimekuwa nikihama kutoka nchi moja mpaka nyingine, NA KWA kweli sina Mipango tena ya kurudi kuja kufanya kazi tena huko nyumbani Tz. Lakini kwenye mafao yangu niliacha fedha nyingi tu wakati nilipokuwa naondoka huko.
1.Naomba kujulishwa, kupitia mabadiliko haya ya Sheria niinaweza kuja kuomba pesa zangu za mafao nilizokatwa wakati nilipoajiriwa huko Tz?
2.Kama jibu ni ndiyo, process zake za kuomba ni zipi?
3.Kama haiwezekani, je ninaweza kuja kuchukua mkopo kupitia KWA mwajiri wangu NA kisha baadaye mkopo ukalipwa kupitia mafao yangu hayo? Bado sijamtaarifu rasmi mwajiri wangu kuwa Mimi sina Mipango tena ya kurudi huko nyumbani Tz na kuendelea na kazi, nataka niandike barua ya kuacha kazi baada ya kupata mkopo KWA sababu sitaki hela zangu za mafao zije kuliwa NA mfuko wa pensheni.
Naombeni ushauri wenu wadau, ingawaje nimevamia Uzi wa MTU hapa.