Haki ukweli

Haki ukweli

Kibunago

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2008
Posts
300
Reaction score
122
Niliposikiliza speech ya Rais ya mwisho wa mwezi ambayo hakika Aaliongea mengi ya maana sana na kisha wimbo wa Taifa ukasikika; maneno ‘hekima, umoja na amani hizi ni ngao zetu’ nilisikia kuugua sana moyoni. Nikajiuliza hivi kwa nini nisianzishe kitu chenye mfano kama wa HAKI ELIMU; HAKI ARDHI tuwe sasa na kitu HAKI UKWELI ambapo tutakuwa na uanaharakati unaotambaa juu ya itikadi za vyama vya siasa kusimamia UKWELI. Kwamba UKWELI tu ndio uheshimiwe na kuwafikia wananchi kwa nguvu zote. Aidha tutakuwa na kazi pia ya ya kuwafichua WAZUSHI WANAOTAKA KUENDELEZA UONGO WAO KWA KUTAFUTA UMAARUFU HASA WA KISIASA.

Hivi Kwa nini kuna watu hawatumii HEKIMA hasa katika kauli na matendo yao; hawataki Tanzania tuwe na UMOJA na huumia sana wanapoona tuna AMANI hapa nchini??
 
Niliposikiliza speech ya Rais ya mwisho wa mwezi ambayo hakika Aaliongea mengi ya maana sana na kisha wimbo wa Taifa ukasikika; maneno ‘hekima, umoja na amani hizi ni ngao zetu' nilisikia kuugua sana moyoni. Nikajiuliza hivi kwa nini nisianzishe kitu chenye mfano kama wa HAKI ELIMU; HAKI ARDHI tuwe sasa na kitu HAKI UKWELI ambapo tutakuwa na uanaharakati unaotambaa juu ya itikadi za vyama vya siasa kusimamia UKWELI. Kwamba UKWELI tu ndio uheshimiwe na kuwafikia wananchi kwa nguvu zote. Aidha tutakuwa na kazi pia ya ya kuwafichua WAZUSHI WANAOTAKA KUENDELEZA UONGO WAO KWA KUTAFUTA UMAARUFU HASA WA KISIASA.

Hivi Kwa nini kuna watu hawatumii HEKIMA hasa katika kauli na matendo yao; hawataki Tanzania tuwe na UMOJA na huumia sana wanapoona tuna AMANI hapa nchini??

Mkuu wangu hapo kwenye rangi,adui namba moja wa amani ya nchi hii ni CCM.Lazima ieleweke hivyo na lazima kila mwenye nia njema aimbe hivyo bila kupepesa macho.

CCM ndio adui namba moja wa nchi hii na bila kuvunja mifumo na mitizamo ya ki CCM tunakokwenda ndio kubaya zaidi.Fastjet anapigana nchi isipasukie mikononi mwake huku ni kama anatoa mazingira ya kupasuka kwa kujua au kutokujua.
 
Back
Top Bottom