Zawadini
JF-Expert Member
- Feb 2, 2012
- 2,937
- 2,149
Wanajamvi; nimeamka nikaona niseme kidogo. Kumekuwa na matukio mawili ambayo yamekuwa yakielezwa kama kigezo cha taswira njema kwa yaliyotokea nchini mwetu wakati na baada ya uchaguzi. Matukio hayo mawili ni fainali za AFCON25 na uchaguzi wa Uganda.
1. Katika fainali za AFCON, watu humu wamempongeza kocha wa Senegal kwa kuitoa uwanjani timu yake kwa kutoridhishwa na uamuzi wa mwamuzi kuipa penalti Morocco. Ila kwa kutumia uzoefu na hekima za mchezo alizonazo kimataifa, Sadio Mane akairejesha timu uwanjani, penalti ikapigwa na mchezo ukaendelea. Hivi leo yule kocha kamiminiwa lawama na huenda akaadhibiwa. Kama si busara na weledi wa Sadio Mane timu ya Senegal huenda ingekuwa inakabiliwa na adhabu. Sasa yale madai kuwa Senegal imefuata nyayo za chama fulani, huenda si nyayo sahihi.
2. Kuhusu uchaguzi nchini Uganda, tumeoma humu watu wakisema kwenye uchaguzi hule, Museveni hakuua ie hakukuwa na mauaji. Hili ni sahihi, ila pia kwenye uchaguzi hule chama kikuu cha upinzani hakikususia uchaguzi na zaidi kilisimamisha mgombea - Bobby Wine. Aidha hakuna mtu alimzuia mtu kuenda kupiga kura seuze kumpiga kwa kuamua kutumia haki yake ya kupiga kura. Sikuona wala kusikia kulikuwa na maandamano seuze uharibifu au wizi. Hivyo basi, ulinganishaji wa matukio haya mawili na yale ya kwetu, nayaona hayafanani.
Karibuni kwa michango. Sijatukana na kwa hivyo sitarajii matusi. Ada ya mja kunena muungwana ni vitendo.