haki kwa walaji


C

cencer09

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2012
Messages
2,453
Points
2,000
C

cencer09

JF-Expert Member
Joined Oct 19, 2012
2,453 2,000
Wana jamvi kwanza kabisa naomba msaada wenu kuelekezwa zilipo ofisi za consumer association of Tanzania au chama cha walaji tanzania.
Pili ambalo ni muhimu kuna mtu anahitaji ushauri wa kisheria kuhusu haki za mlaji na mimi nimeona bora kulitupa hapa jamvini kwa wajuzi ambao wanaweza wakatuelimisha na sisi pia.
Kuna mtu alisubscribe kurespond kwenye tangazo la gazeti la mwanaspoti mwaka 2010 wakati wa kombe la dunia kuletewa habari kupitia short code5574,hakuona tangazo la kujitoa ingawa sasa hivi watumaji wanadai walitoa ,sasa ushauri tangazo la kuunsubscibe halitakiwi kuwepo kwenye option ya kila tangazo ili kama huridhiki na huduma uweze kujitoa?
Soon after kombe la dunia habari zikabadilika wanaendelea kukata na kuleta sasa hivi wakidai ni Mwananchi mobile kitu ambacho wala hakuomba kabisa na hakielewi,akaenda kwenye ofisi zao ili wamtoe september 2010 wakamwambia code ambayo hata hivyo ikashindikana,baada ya miaka miwili na miezi kadhaa akaenda tena safari hii kwa ukali ndipo wakasitisha.
Afisa aliyemsaidia kujitoa kwanza akasema kuwa wao walikuwa wanaendesha promotion hii hadi baada ya kombe la dunia baada ya hapo hawahusiki,baada ya kwenda TCRA mamlaka ya mawasiliano sasa wamekuja na habari ingine kuwa alijiunga mwenyewe kwenye habari hizi za kitapeli.
anataka ushauri wa kisheria jinsi ya kuwashitaki kwa sababu anaona hawana haki ya kumkata kwa muda wote huo bila ridhaa yake,pia walistahili walau kumuomba radhi badala yake baadhi ya maofisa wanaoshughulikia wanadai yeye aliingia mwenyewe.
Je sheria za haki za walaji zinasemaje kuhusu suala hili?maana anataka kuwadai usumbufu na mental torcher kwa muda wpte huo.
Hii inaweza kuwa fundisho kwani sasa hivi makampuni ya simu yatakukata na kukuingiza kwenye huduma usiyoiomba kama ya ring tone na kadhalika
Tunaomba ushauri wenu wana jamvi
 

Forum statistics

Threads 1,283,904
Members 493,869
Posts 30,805,639
Top