Bila shaka nguvu iliyotumika ni kubwa sana. Boda boda naye ana kosa la kutotii 'sheria bila shuruti' awapo barabarani.
Lakini nashauri kama kuna uwezekano, hawa viongozi wakubwa watumie usafiri wa anga kutoka eneo moja kwenda lingine! Mfano helcopter na ndege za kawaida. Maana wamekuwa wakituletea usumbufu mkubwa barabarani.
Mbona wasaidizi wao (Mawaziri) tunakula nao foleni! Na kama hawawezi kupaa juu kwa juu, basi wazitanue basi barabara ili wapitapo na sisi pia tuendelee na mishe zetu! Haya mambo ya kuwekana pembeni wakati mwingine mpakaa saa nzima, yanatukera pia sisi wananchi.