Haki iko wapi kama Serikali ndiyo inaongoza kwa kufanya unyama

blackcrow

Member
Sep 24, 2020
21
43
Askari wa bongo wakae wakijua kwamba ubinadam ni kitu cha kwanza kuzingatiwa kuliko kitu chochote kile hapa duniani na hao viongozi wanao wanyenyekea kiasi cha kuuwa au kuumiza watu wengine nao ni binadam kama jinsi walivyo wao.

Leo nimestajabu sana baada ya bodaboda mmoja kupigwa fimbo na askari maeneo ya mgongoni akiwa anaendesha piki piki tena akiwa kasi kidogo na kuangukia mtaloni hapo hapo alivunjika mikono yote miwili na kupata majeraha mengine mengi makubwa huku askari hao wakimuangalia tuu bila kufanya lolote wasamalia wema waliita amburace na jamaa akabebwa kupelekwa hospital.

Sababu ya jamaa kupigwa eti aliingia barabarani wakati ambao alikuwa hajui kwamba magali yote yalikuwa yamesimamishwa kisa makamu wa rais anapita. hivyo bac msafara wa kiongozi una thamani sana kuliko maisha ya mtu hii atua tuliyo fikia ni mbaya sana na ubinadam unapotea kabisa serikali ipo kwaajili ya kulinda watu na sio kuuwa watu tena watu hao hao ambao wana piga kula na kuwaingiza madarakani leo wanakuwa ni watu wa kufanyiwa unyama.

Haki iko wap jamana sawa hakuna haki kiiivyo bac angalau watu wasiwe wanafanyiwa unyama hivyo hadharani tutambue maisha ya mtu yana thamani kuliko kitu chochote kile na ndiyo manaa katika orodha za haki za binadam haki namba moja kabisa ni kuishi na mengineyo
 
Kwanini apite ikiwa wenzie wamesimama. Hapa mimi siwezi kumtetea au kulaumu askari polisi.Jambo la msingi namuombea apone mapema arudi katika ujenzi wa familia na taifa kwa ujumla.
 
Tatizo la waendesha pikipiki wengi na Mimi nikiwemo huwahatutaki kusubiria chochote barabarani.
Askari pengine wana kosa, Ila sijui wangemkamataje bodaboda huyo aliyekuwa speed kwa maana navyojua sisi waendesha pikipiki huwa hatusimamagi pale tunaposimamishwa.
 
Askari wa bongo wakae wakijua kwamba ubinadam ni kitu cha kwanza kuzingatiwa kuliko kitu chochote kile hapa duniani. na hao viongozi wanao wanyenyekea kiasi cha kuuwa au kuumiza watu wengine nao ni binadam kama jinsi walivyo wao.....
Sasa mkuu kiongozi wa nchi anapita alafu yeye anaingia barabarani hao waliyosima aliwachukuliaje?

Sometimes mnajitafutia matatizo wenyewe.
 
Bila shaka nguvu iliyotumika ni kubwa sana. Boda boda naye ana kosa la kutotii 'sheria bila shuruti' awapo barabarani.

Lakini nashauri kama kuna uwezekano, hawa viongozi wakubwa watumie usafiri wa anga kutoka eneo moja kwenda lingine! Mfano helcopter na ndege za kawaida. Maana wamekuwa wakituletea usumbufu mkubwa barabarani.

Mbona wasaidizi wao (Mawaziri) tunakula nao foleni! Na kama hawawezi kupaa juu kwa juu, basi wazitanue basi barabara ili wapitapo na sisi pia tuendelee na mishe zetu! Haya mambo ya kuwekana pembeni wakati mwingine mpakaa saa nzima, yanatukera pia sisi wananchi.
 
Askari wa bongo wakae wakijua kwamba ubinadam ni kitu cha kwanza kuzingatiwa kuliko kitu chochote kile hapa duniani. na hao viongozi wanao wanyenyekea kiasi cha kuuwa au kuumiza watu wengine nao ni binadam kama jinsi walivyo wao...
Hizi lawama siyo za serikali, ni za mtumia barabara huyo na askari husika(binafsi)! Maamuzi ya huyo askari hakutumwa na mtu, ni bunge lake mwenyewe kichwani mwake!

Tuwe makini ktk kupeleka lawama mahali husika!
 
Bodaboda janga la taifa kwa sasa, sheria hawajui, wajuaji sana, wanaharibu magari ya watu kwa kutoeshimu vyombo vyao.
Ukiwa na gari uwezi kuwakubali hata kidogo.
 
What if yule boda alikuwa ametumwa akasababishe ajali kwenye msafara wa mtu wa pili kwa umuhimu hapa nchini?
What if kitu gani? Tanzania nzima na duniani kote hakuna mwenye ugomvi na makamu wetu wa rais. Wasiopendwa na wwatu wapo lkn sio huyu mama.
 
Back
Top Bottom