Haki alizo pigania Marehemu Maalim Seif Hamad Sharif

GHIBUU

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
4,432
3,006
Vyombo vya habari vimekuwa vikimsifu Maalim Seif kama kiongozi alie pendwa sana na wazanzibari, kiongozi muadilifu na mwenye misimamo, kiongozi alie taka mabadiliko ya kisiasa Zanzibar na Uwongozi toka yupo CCM na hata nje ya CCM.

Lkn haki hizo baadhi ni muhimu zaidi pia hazikuwekwa wazi kwenye vyombo vya Habari.

Maalim alitaka kwanza wazanzibari wapate fursa ya uhuru wa kuchagua viongozi wao kama wawakilishi, wabunge , hata urais.

Maalim alitaka kila mzanzibar apate mwenye umri zaidi ya miaka 18 aandikishwe kwenye book la wapiga kura.

Maalim alitaka Zanzibar yenye mamlaka kamili katika Muungano, ndio kiu kubwa ya wazanzibari toka kuazishwa kwa chama cha CuF.

Ndoto ya wazanzibari ambayo hio ya mwisho kamwe hatutosita kupigania mpaka na Sisi tutangulie mbele ya haki.

Rais Mwinyi kama upo unasikia na umeeona mapenzi ya wazanzibari kwa kiongozi huyo ni vyama ukajifunza, Sisi kama wananchi tutaendelea kwa kile alicho tuachia Maalim umoja na kupigania haki na utawala bora.

Mungu amrehemu Amin
 
Dr. Shein alikuwa na ana rohobaya sana. Kwamaelezo ya Rais JPM jamaa sio kabisa
 
Back
Top Bottom