Haka ndiko kabinti kangu......!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Haka ndiko kabinti kangu......!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Ligogoma, May 5, 2011.

 1. Ligogoma

  Ligogoma JF-Expert Member

  #1
  May 5, 2011
  Joined: Aug 27, 2010
  Messages: 2,132
  Likes Received: 847
  Trophy Points: 280
  Habari wana JF!!

  Kama title inavyosema ni kabinti kangu yaani katoto kangu ka kike kenye umri wa miaka 9.5 sasa.

  Majuzi nimekaa nako kwenye gari nikisubiri bidhaa nilizoagiza huku nataniana nae, kiukweli nampenda sana mwanangu ndiyo maana akawa rafiki yangu mkubwa!!!

  Katika kucheza cheza pale akanitupia swali, namnukuu `Hivi baba kwanini yule baba dukani kwa kina Robu hupenda kuniita ita kule uani kwao halafu anapenda kunishika shika matakoni na kifuani?` Kwani ndo nini hivyo?

  Kidogo nianguke kwa presure.....huyo baba mwenyewe ni mtu mzima sawa tu na mzazi wangu mimi!!! Na sikumjibu kitu ila nikamwambia nitakuelezea nyumbani tukifika, mama mtu akataka kumpiga but nikamwambia no!! Mwache

  Nilijaribu kumdadisi kama kuna anachopewa na huyo mzee akajibu hajawahi kupewa kitu chochote zaidi ya pipi na gumz basi.

  Natafuta namna ya kumjibu na kumwelekeza madhara yake na kuweka mtego wa kumnasa fataki!!

  Mama hataki mtoto aelekezwe kwa sasa juu ya swala zima la mapenzi kisa bado mdogo sana!!! Wana JF mnadhani ni sahihi?

  Nimeweka hapa pia kama tahadhari kwetu wana JF coz najua wengi wetu hapa ni wazazi na sikujua jambo kama hili lingeweza linitokee kwangu ila ndiyo hivyo limenifika!! So take care na watoto wetu jamani
   
 2. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #2
  May 5, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Usimwache huyo mtu mzima h***o alyekosa adabu. Tena ashindwe kabisa. Binti miaka 9?? Kama sio laana ni nini? Jamani wakati mwingine inabidi kumwogopa Mungu!
   
 3. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #3
  May 5, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Mh hii hatari sana hawa mababa wanamatatizo ni waharibifu wakubwa sasa haka kakinda mh.
  Hebu mtaarifu mjumbe huyo fataki achukuliwe hatua.
   
 4. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #4
  May 5, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  Niwie radhi... BUT I AM SO VERY MAD....

  Baba Mtoto.... NARUDI TENA!!!!
   
 5. Ipi dot com

  Ipi dot com JF-Expert Member

  #5
  May 5, 2011
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 267
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  yaani binafsi presha imepanda.njia nzuri ya kupambana na mabaya ni kutenda mema,nenda kampe warning ana kwa ana bila kuonyesha panic yoyote
   
 6. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #6
  May 5, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mkuu, kama hauna panga sema nikuazime, huyu bazazi si wa kumkawisha. hakuna haja ya kumvia umkamate kwa sababu una ushahidi wa kutosha (binti yako hawezi kukuongopea). Mwendee moja kwa moja na mpe onyo kali na binti yako apewe maelekezo kuwa fataki akijaribu kurudia kitendio hicho aripori haraka
   
 7. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #7
  May 5, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  mkuuu wewe mvumilivu mimi ningemfuata hukohuko pumbavu zake sana!
  imenisikitisha sana mkuu!
   
 8. mama D

  mama D JF-Expert Member

  #8
  May 5, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 1,755
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  khaa!

  nimepata hasira ghafla!!!!!!!!!!

  asiachwe huyo muuaji barazuli mkubwa!

  nitarudi na jibu muafaka baada ya muda
   
 9. mama D

  mama D JF-Expert Member

  #9
  May 5, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 1,755
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  hiyo ni child abuse na kisaikolojia ameshamuathiri sana huyo mtoto!!
   
 10. s

  shosti JF-Expert Member

  #10
  May 5, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 4,949
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  mara nyingi wazazi tunakosea sana,dunia si salama tena tuongee na watoto wetu bila kujali ana umri gani kinyume chake kuna majuha yatazungumza nae kwa lugha nyingine:A S cry:
   
 11. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #11
  May 5, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,268
  Likes Received: 19,412
  Trophy Points: 280
  nna bunduki hapa tuwasiliane
   
 12. mama D

  mama D JF-Expert Member

  #12
  May 5, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 1,755
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145

  nilvyopata hasira nahisi ningejeruhi hata kuua bila kukusudia
   
 13. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #13
  May 5, 2011
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Umechukua hatua gani kuhusu huyo baba? you need to do something ili kum expose maana utakuta kashawafanyia hivyo watoto wengi tu . jamii lazima imjue na ndio ataona aibu bila hivyo mtalea ugonjwa hapo mtaani kwenu na mtaja yavuna mabua.
  Kuhusu mtoto tafuteni muda mkae nae taratibu muulizeni aweze kuwambia extent ambayo huyo baba kafikia usijekuta kashaharibu, pia ni vizuri kama unavyosema mtoto yuko wazi kwako hivyo, mwambie tabia hatarishi zote ili ajiepushe nazo kama vile kukataa pipi au zawadi yoyote kutoka kwa strangers au wauza maduka, aripoti kwako kila anapoitwa na wababa au vijana, kila siku mnaweza kuwa mnapata wasaa wa kukaa naye anawambia details za siku yake ilivyokwenda, kama vile alikutana na nani, alicheza na nani, walicheza mchezo gani etc.. ni muhimu sana kulinda watoto wetu hasa katika kipindi hiki cha mafataki wasio na akili.
   
 14. Zanta

  Zanta JF-Expert Member

  #14
  May 5, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 2,017
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Hapa hauitaji kuweka mtego wala nini? maana unaeza kuta wakati wewe unapanga kuweka mtego huyo Fataki akawa keshambaka kabla ya mtego wako. Na nadhani utajilaumu milele kwa kosa kama hili. Cha kufanya we muibukie huyo mzee mpe kubwa zake bila hivyo utajakuta mtoto keshaharibiwa huyo. Anza kwanza na Bazazi then kwa mtoto uende nae taratibu.!
  Akianani naomba lisinikute hili maana wengine hua hatufikiri mara mbili tunaweza kuishia jele hivi hivi kudadadeki.
   
 15. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #15
  May 5, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180  Kwanza nakupongeza kwa mahusiano mazuri uloweka dhidi ya wewe na mwanao mpaka ana confidence in you ya confide each and everything kwako.... Kwa hilo am so proud of you mana wanaume wachache wana muda mfinyu kumuwezesha amzoe/wazoe na kuwajua watoto wao. Really, I am proud of you.

  Pili hiyo issue ni kubwa mno... Na ukisosea wewe na mkeo jinsi ya kuitatua mtaharibu kila kitu. Naomba kukujulisha kua ni muhimu saana bintiyo ajue what she said has not affected anything, kua kila kitu kiko normal - akigundua tu kua kimeleta tension humo ndani, next time hata kama bado wewe ni bff wake hatarudia kukwambia which is more dangerous. Kwa binti ambae yuko almost ten years she has a right to know kuhusiana na mambo yahusio sex na hata kua a expect menustration periods (watoto wakike wanavunja ungo siku hizi kati ya 8 - 12, ni wachache zaidi ya hapo); bahati mbaya mama si muelewa hii ilikua ni kazi yake kumwambia. Wewe pia waweza mwelekeza but haipendezi....

  Nashindwa kuelewa kwa nini mke wako alitaka kumchapa, haina logic; and please muelekeze, mueleweshe kaharibu kabisa trust ya mwanenu - na mtoto ili aelewe everything is alright kwa mtazamo wangu mkeo anatakiwa amuombe msamaha mtoto wenu; kamkosea (Katika issue kama hizi muite mtoto mulekeze kama vile unaongea na mtu mzima - ataelewa zaidi na next time atasema).

  Wewe Kijana Juzi ni mwanaume, hivyo you understand zaidi hata kuliko mimi kua from the explanations ya mtoto huyu baba ana tabia chafu. Usichukue maamuzi makubwa ya hasira, ila kwa mtazamo wangu inatakiwa mfuate na mwambie mzee binti yangu kanisumulia unapenda sana kumchezea naomba huo mchezo ufe! Ukiface hata kama ana nia hiyo chafu kwa mwanao, possibility ya kurudia haitakuwepo. Ana bahati huyo baba simfamhumu, tungefika mbali, achezee wanawake woote atakavyo lakini si mtoto mdogo..... Sometimes wanajamii tunaona na hatufanyi kitu,,,,INASIKITISHA....
   
 16. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #16
  May 5, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Hawa wazee wenye maduka wana tabia hizo sana kwa kutumia mwanya wa kuhonga bidhaa \za madukani, lakini hili la kabinti limekuwa too much!...Anataka kitu gani kwa mtoto huyo mbabu?...
  Bila ushahidi hapo hutompata huyu kibabu, cha kufanya mwelekeze mtoto akifanyiwa hivyo siku ingine apige kelele ili watu wa jirani wastuke na ikiwezekana wamkamate!
  Bila hivyo atasonga mbele zaidi kwa hatua ingine ya madhara kwa mtoto!
  Halafu muwe na utamaduni wa kukagua maabinti zenu!...Wengine hawasemi kabisa!

  Kuna mwanafunzi mmoja wa darasa la tano alishitukiwa akiwa ananuka mno darasani hadi wenzake kumkimbia kwenye dawati, baadaye aligundulika ana ligonjwa la kuambukizwa na mwanaume la kufa mtu!...walimu wakambembeleza hadi akaweka mambo hazarani...Wazazi hawajui kitu, wananajua kila kitu ni mswano, kumbe wana msiba ndani!
   
 17. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #17
  May 5, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Nani alikwambia kuua mtu kama huyo (fataki) ni dhambi?

  Anyone who will "abuse" my child I will KILL HIM "cold blood" - Everything I do is for my children! Kwahiyo siwezi kuvumilia mtu atakayemuambukiza mtoto wangu ukimwi au magonjwa ya zinaa! After all, Is it braver, to live for a cause or die for a cause!
   
 18. KasomaJr

  KasomaJr JF-Expert Member

  #18
  May 5, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 338
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Aise Bro. Nimepandwa na hasira, hofu imeniingia na mpaka kutokwa jasho. Hakika inasitikisha sana, Mtoto yupo honest wala hana kosa, mama ni kutokutafkari sana ndo maana alitaka kumpiga (hilo ni kosa kubwa sana). Cha msingi kufanya hapa nikum-face huyu Ibilisi mtu, mweleze ukweli na mpe onyo kali sana, lakini isiishie hapo tu, weka mazingira ya kufuatilia kama ataendelea kumwita mtoto kwa malengo yale yale ili upatikane ushahidi na achukuliwe hatua za kisheria.
  Wasiwasi wangu tu bado sijui ni mazingira gani unayoishi, kwani naamini una majirani ambao pia wana mabinti wa kike, sasa ili kutoa onyo lenye kusaidia jamii inayozunguka eneo hilo, ni vyema kutafuta majirani wa kuambatana nao hii itasaidia sana na utakuwa umeweka record ya ushahidi incase akifanya kitendo hicho hata kwa Binti mwingine.
   
 19. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #19
  May 5, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 253
  Trophy Points: 160
  Aya ya ya ya ya NAUA huyo FATAKI on the sport bila kuchelewa aiseee dah mori umepanda hapa dah
   
 20. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #20
  May 5, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,276
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  God forbid. Yaani I can imagine huyo baba si hajabu ni muhathirika! Hili limekuwa tatizo sugu pamoja na hukumu ya miaka 30 mafataki yaelekea ni wagonjwa wa akili. Mimi nina watoto wa kiume tu but I still feel that they are not safe maana watu siku hizi wanageuza watoto wa wenzao. Mungu tunusuru na hili ghalika!
   
Loading...