GE2025 Haji Manara Aongoza Kwa kura za Maoni udiwani kata ya Kariakoo

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mkurugenzi Mtendaji wa Manara TV, Haji Manara , ameibuka kidedea katika kura za maoni za kuwania nafasi ya Udiwani katika Kata ya Kariakoo, jijini Dar es Salaam.

Kura hizo za maoni zilifanyika leo Jumatatu tarehe 4 Agosti 2025, chini ya usimamizi wa chama, ambapo wagombea wanne walishiriki katika mchakato huo wa ndani ya chama.

Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na wasimamizi wa uchaguzi wa CCM, matokeo ni Haji Sunday Manara Kura 136, Daudi Simba Kura 85, Abdul Masamaki (Diwani anayemaliza muda wake) Kura 31 na Siza Mazongela Kura .

Kwa ushindi huo, Manara ameongoza kwa tofauti ya kura 51 dhidi ya mpinzani wake wa karibu, Daudi Simba. Diwani aliyepo madarakani, Abdul Masamaki, ameangushwa vibaya kwa kupata kura 31 pekee, huku mgombea Siza Mazongela akikosa kura kabisa.

Kura za maoni ni sehemu ya mchakato wa ndani wa Chama Cha Mapinduzi katika kuwapata wagombea wake kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.

Kwa sasa, macho na masikio ya wanachama na wakazi wa Kariakoo yameelekezwa kwenye uteuzi rasmi wa chama ili kubaini nani atapeperusha bendera ya CCM kwenye uchaguzi wa udiwani katika kata hiyo maarufu jijini Dar es Salaam.
 
View attachment 3431144
Pongezi kwake.
 
Rekebisha hapo ni uchaguzi mkuu siyo uchaguzi wa serikali za mitaa
 
Back
Top Bottom