Haji Manara: Ahmed Ally ni shabiki kindakindaki wa Yanga

Manara yeye alichozoea ni kufitinisha watu anapenda kuongelea maisha ya watu ila yeye akizungumziwa ana bweka na kuona anaonewa wivu wakati yeye ndo bingwa wa wivu na hasad
 
Huo ni ukweli kabisa kuwa Ahmed ally ni mwananchi mwenzetu kwasababu ni yanga lialia ila hata huyu manara ni simba lialia pia ,asitudanganye sisi wananchi
 
Katika muendelezo wa tambo mbali mbali za Simba na Yanga pindi ukiotewa pale ambapo pana mshono hakika nawe lazima ukajipange kuja kurudisha mashambilizi.

Picha ya zamani ya Ahmed Ally akiwa ameshika kombe la Yanga sasa imetumiwa vizuri na Manara kwenye kuwaaminisha wananchi kuwa Ahmed naye pia ni mpenzi wa Yanga japo yupo Simba kwenye kujitafuta

Manara ameandika “Nakiri kwamba hata mimi wakati najitafuta, niliibukia kuwa Mfuasi feki wa Madunduka, na ilifika mahali nikawa nawacharura mno Yanga hadi mimi mwenyewe ilikuwa inanikera, lakini ndio kujitafuta huko, ningefanyaje ndugu zangu? Na bila kufanya hivyo GSM wangenionaje? Ile Siku waliyoniambia rudi home sasa, ooohh ilikuwa siku kubwa sana kwangu, SITASAHAU

Basi bhana Wakulungwa, ndio story ya huyu kijana mkazi wa Tambuka Reli, kelele na kebehi zote anazosema dhidi yetu, ichukuliwe ni kwenye kujitafuta na kujipapatua tu, huyu anaumwa na Yanga yake, hali hata Chakula siku Wananchi wakiwa wanacheza, Kigosi na Jimmy Mafufu waliwahi kuniambia walikuwa wanampa hadi hirizi kuvaa, siku ya mechi ya Yanga.

Miaka ya nyuma ilikuwa kila asubuhi anaenda Jangwani kubusu na kupiga picha na Makombe yetu, na akifika tu anaamkia, Shikamoo Makombe na Wazee wetu pale klabuni walikuwa wanampenda kwa ule usafi wake wa kusafisha kila siku Makombe yetu, hadi Jiki alikuwa anayaoshea.

Kwa hiyo msameheni Wanayanga, anajitafuta tu, ni kijana wetu mzuri na ana msaada mkubwa kwetu, Mtu wa maana sana na ni familia kabisa, Soon Mtanielewa Wananchi”

View attachment 2942262
Hii ni photo shop ya wazi kabisa. Manara leta uwongo mwingine. Hii tumeikataa
 
Leo ndio nimejua kuwa kebehi za semaji la Simba huwakera .

Nimejua pia Manara bado ana uchungu wa kuondolewa katika nafasi ya usemaji hapo Simba.

Madam Barbara popote ulipo ubarikiwe sana kwa kuchukua uamuzi wa kumfyekelea mbali huyo amphibian Manara
 
Picha imekaa kama kweli kabisa aisee hasa ratio ya semaji na kombe viko sawa sawia!

Ila tukumbuke teknolojia imekua upo uwezekano kuwa hii picha ni photoshop tu wameweka picha na Kombe kumchafua semaji la mbumbumbu fc, ila pia nimeona kama dizaini lile ni kombe la Mamelodi (Green and Yellow) au pia laweza kuwa labda Kombe ni la CCM (Green and Yellow) wakishinda ligi ya Silent Ocean Ramadan cup miaka ya tisini!!

Ila japo picha ni ya kutengeza pale inamuonesha Ahmed kakaa na kombe la Yanga, ila kuna nguvu zaidi ya ukweli kuliko uongo na my conspiracy theories!!

Huu ni mkuki mchungu mno kwa Ahmed Ally Bin Mwananchi!!

Noma sana kuharibiana ugali mjini
 
markup_1000050505.png
 
Anaruhusiwa kuwa msemaji wa simba maana Mpira ni ajira lakini deep down alicheka kimoyo moyo baada ya zile 5 na ndiyo maana hakuchulia serious baadae ya kufungwa Bali mizaha yake iliendelea .
 
Picha imekaa kama kweli kabisa aisee hasa ratio ya semaji na kombe viko sawa sawia!

Ila tukumbuke teknolojia imekua upo pamoja kuwa hii picha katika photoshop tu wameweka picha na Kombe kumchafua maji ya mbumbumbu fc, ila pia nimeona kama dizaini lile ni kombe la Mamelodi (Green and Yellow) au pia laweza kuwa labda Kombe la CCM (Green and Yellow). ) wakishinda ligi ya Silent Ocean Ramadan cup miaka ya tisini!!

Ila japo picha ni ya kutengeza pale inamuonesha Ahmed kakaa na kombe la Yanga, ila kuna nguvu zaidi ya ukweli kuliko uongo na my conspiracy theories!!

Huu ni mkuki mchungu mno kwa Ahmed Ally Bin Mwananchi!!

Noma sana kuharibiana ugali mjini
Kama manara, leo hii ameamini na kila anachoongea na Club aliyokua anaidhalilisha kadili inavyomtuma, kuwatukana anavyoweza nini Ahemed Ally ambae hajawahi kuvunjia heshima, bali kuipigania.
.
.Huyo anaedai yeye hata kabla, kwenda UTO, AKA MAMBWA ama MANYANI FC nafsi yake ilikua Uto pia aliisaidia zaidi Simba, na kuidhalilisha zaidi manyani wenzie.
MAneno yake sasa hayaumizi maana yanabaki yanabaki kuwa maneno ya nongwa, baada ya kupigwa.
.Na laana ikamuandama Ally Kamwe kachukua nafasi.
 
Wakulaumiwa ni viongozi wa Simba , wanawezaje kuwaajili kina Manara bila kujua chimbuko lao.
Mkuu haya mambo yapo tu mimi ni shabiki wa yanga ila mbona sisi tupo na canavaro wakati kiasili ni shabiki wa simba? Mbona yanga tunae haji manara wakati kila mtu anamjua ni simba damu? Na vipi mkude mbona kaitumikia simba kwa moyo wote hata kama ni yanga damu?namjua vizuri sana ahmed ally huyo ni yanga ila siamini kama anauwezo wa kuhujumu anapopatia ugali wake...manara ni mpuuzi mno mbona hamshangai bosi wetu GSM kuvaa jezi ya yanga wakati ni simba kindakindaki?
 
Sa Huyu si alisema alifanya kazi Simba Kwa kujitolea hakuna akipata chochote,

Sa alikua anajitaftaje mnafiki huyu.

Sijawahi kua shabiki wa maneno maneno hata alipokua timu yangu Simba alikua ananikera vile vile.
 
Mkuu haya mambo yapo tu mimi ni shabiki wa yanga ila mbona sisi tupo na canavaro wakati kiasili ni shabiki wa simba? Mbona yanga tunae haji manara wakati kila mtu anamjua ni simba damu? Na vipi mkude mbona kaitumikia simba kwa moyo wote hata kama ni yanga damu?namjua vizuri sana ahmed ally huyo ni yanga ila siamini kama anauwezo wa kuhujumu anapopatia ugali wake...manara ni mpuuzi mno mbona hamshangai bosi wetu GSM kuvaa jezi ya yanga wakati ni simba kindakindaki?
Manara ni yanga Ila alikuja Simba kwa ajili ya kutafuta maisha, Mimi simlaumu Ahmed Ally Kama ni yanga Ila nawalaumu viongozi wa Simba Kama itakuwa kweli kwanini hawakufanya uchunguzi wa kutosha kabla ya kumsajili?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom