Haiwezekani hata kidogo mtu akawa ni mtu wa kumpuuza Mungu muumba wake kwa kinywa na matendo yake halafu wakati huo huo awe na moyo kukujali wewe(sanasana atajivika mavazi ya kondoo).Epuka kujifariji "faraja hewa",kama mtu hampendi Mungu muumba wake, Upendo wa kukupenda wewe ameutoa wapi?,Nani roll model wake? Nani anayemfahamisha/kumfundisha undani kuhusu thamani ya nafsi yako na kusudi la uwepo wako chini ya jua? Kujifariji anakupenda,ni kama kusubiri Meli Airport.Mi naskiaskia tu mara oooh! "Mapenzi ya kweli siku hizi hakuna",mara, "Hapendwi mtu inapendwa pochi" mara "Mwanaume pesa sura hata mbuzi anayo" na bla bla nyingine kama hizo,by the way hakuna jipya chini ya jua ilishakwisha tabiriwa tangu enzi "WATAKUWA WENYE KUPENDA FEDHA KULIKO KUMPENDA MUNGU",hakuna cha ajabu hapo! TATIZO NI KWAMBA TUKO SPIDI KUTAABIKIA MAMBO AMBAYO ALIYEYAUMBA YUPO HUKU TUKIMPUUZA NA KUJITANGULIZA WENYEWE,HATA HIVYO MAAMUZI JUU YA MAISHA YAKO YAPO MIKONONI MWAKO MWENYEWE,NA NI WEWE NDIYE UTAKAYEWAJIBIKA KWAYO!