Haitokuja kutokea Kampuni safi ya usafirishaji abiria Tanzania kama Scandinavian Express

fdizzle

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
1,891
2,367
Huu ni ukweli ulio wazi kwa Tanzania hakuna kampuni ya usafirishaji abiria itakayoweza kuzidi ubora wa huduma zilizokuwa zikitolewa na Scandinavian Express.

Kuanzia safety,reliability,comfort na coverage hawa jamaa walijipanga vizuri sana

1.Huwezi kukuta basi zao zimetaga njiani (kuharibika) na ikitokea hivyo kuna backup buses za haraka

2.Sikumbuki kama zilikuwa zinapata ajali hovyo

3.Mwendo safi sio wa kunyata wala sio mkali

4.Wanazingatia sana muda ukiambiwa saa nane basi la mwisho kwenda Iringa kama bado upo mbali na Kamata (zilipokuwa ofisi zao) jipange kukodi taxi ya kuanza kufukuzia

5.Hata kama basi lina abiria wawili linaenda Mwanza litaondoka na abiria hao wawili

6.Hazisimami hovyo njiani mfano basi la kwenda Iringa likiiinuka Kamata litapita Ubungo Terminal likitoka hapo ni mpaka Maili moja. Likitoka Maili moja ni mpaka Chalinze kisha Morogoro .

7.Madereva na kondakta wapo smart kimavazi.Nguo zimenyooshwa vizuri kabisa

8.Walikuwa wanafika Tanzania nzima kwa kuanzia Dar na nchi zote za Afrika Mashariki
Kwa sasa hakuna kampuni ya usafirishaji abiria iliyo na uwezo kuzidi huduma za kampuni hiyo
 
Kuna kampuni inaitwa dar lux kusema kweli wanajitahid wana gari nzuri
Hawajafikia ubora wa Scandinavian Express
Hujasikia watu wanalalamika mfano karma upo Mwanza unakuja Dar ni mpaka usubiri gari inayotoka Dar kuja Mwanza.
Na ikitokea ikalala Shinyanga basi mtaondoka Mwanza saa nne asubuhi
Pia wananyata sana barabarani
 
Alijifanya kufanya Kazi Kizungu AFRICA

Gari ikiwa hata na Abiria 14 anawash Gari hapa Nairobi kisa yupo on time

Niliwahi kupata tempo 1985-1988 kuwa Inspector wa ukaguzi
Hiki na yale madeni ndio yalimfilisi
 
Hawajafikia ubora wa Scandinavian Express
Hujasikia watu wanalalamika mfano karma upo Mwanza unakuja Dar ni mpaka usubiri gari inayotoka Dar kuja Mwanza.
Na ikitokea ikalala Shinyanga basi mtaondoka Mwanza saa nne asubuhi
Pia wananyata sana barabarani

Sijawah sikia hili kwa kweli mi nimepanda kwenda Bukoba na niliona wako vizuri sana
 
fdizzle, Ni kweli. Mimi hayo mabasi nimeyapanda sana. Sikumbuki vizuri lakini zamani yalikuwa yanaondokea kati ya Mnazi Mmoja au Kisutu au wapi? (Nimesahau mwenye kukumbuka tafadhali). Kipindi cha mabasi ya Kwacha yaliyokuwa yanaondokea Mnazi Mmoja.
 
Back
Top Bottom