Haiti yakumbwa na kimbunga kikali

Haiti yakumbwa na kimbunga kikali

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,623
Reaction score
8,427
Kimbunga Matthew kimeharibu miundombinu muhimu kama vile barabara ambapo maafisa wanasema kuanguka kwa daraja kumegawa sehemu ya kusini na sehemu nyengine ya nchi.

Mtu mmoja mpaka sasa amepoteza maisha nchini Haiti na wengine wanne kutoka nchi jirani ya Jamuhuri ya Dominica.

Bado mpaka sasa haijafahamika kiwango cha uharibifu wa kimbunga hicho nchini Haiti, lakini nyumba nyingi zimebomolewa, huku barabara zikiwa hazipitiki kutokana na miti iliyoanguka pamoja na mafuriko.

Wahanga wa kimbunga hicho wanaendelea kujaa katika makazi yaliyotengwa na serikali katika mji mkuu wa Port-au-Prince huku mamlaka ikiendelea kuomba msaada wa maji pamoja na chakula.
 
HAITI INATESEKA SANA. WAHAMIE AFRICA TU WAPUMZIKE.
 
Si kulikuwa na mpango wa kuwahamishiwa Afrika hawa? Sijui uliishiaga wapi maana kile kisiwa chao sio salama kabisha kwa kuishi; vimbumba/mafuriko yao; matetemeko ndio kabisa usiseme.
 
Back
Top Bottom