Haitatokea tena kupata Chama cha upinzani chenye nguvu kama NCCR Mageuzi chini ya Lyatonga Mrema

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
8,708
5,711
Nasema kweli hata kama watu wachukie na wanune. Kile kilikuwa ni chama kilichojua kila mikakati ya kisiasa. Iwe ni propaganda au ishu ya ukweli.

Chama kile hakikuwa na ukabila wala ukanda, kilijaa kila kabila na wasomi kedekede.Alikuwemo Mabere Marando, Marehemu Dk Sengondo Mvungi(Rip),Masumbuko Lamwai na wengine wengi.

Uchaguzi wa 1995 walitetemesha na kutingisha nchi mpaka Mwl JKN akaingilia kati kuinusuru CCM. Ikabidi asimame majukwaani ili kuiokoa CCM.

Nilikuwa Mwanza watu walisukuma gari iliyombeba L. Mrema toka uwanja wa Nyamagana mpaka iko hotel Capripoint iliyokuwa inamilikiwa na Cosmas Chenyenge.

Leo hii Chadema imejaa matapeli na wahuni tu. CCM haitikiswi wala kutishwa. Chadema wamejaa watu hata propaganda tu hawawezi.

Bora sisi wakulima tusio na vyama tukae kimya,tusubiri matokeo.
 
..umesahau tuliambiwa nccr ni ya wachaga?

..pia nccr kilikuwa chama kichanga mno kisichokuwa na mizizi huwezi kukilinganisha na cdm.

..tasnia ya habari ilikuwa changa mno na ilikuwa vigumu sana kusambaza habari.

..tofauti na leo hii ambapo mtu anaweza kuwa Ulaya au Marekani na akabadilishana habari na watu walioko kijijini Tz.

..wananchi wengi na wapiga kura walikuwa hawana mazoea na imani na vyama vya siasa.

..mwisho, nccr ilikuwa na wasomi ambao hawakuwa na uvumilivu wa kisiasa. Mambo yalipokuwa magumu kidogo tu waliacha siasa na kurudi kwenye kazi zao za taaluma.
 
Za kuambiwa changanya na zako, akili bora kabisa za mbayuwayu,, ahsante mzee wetu JK kwa hekima yako!!
 
chagu wa malunde, Bababuko, ole mhola ahene ??. Vinauawa na nani hivi vyama ?! Je vinakufa vyenyewe?

Wananchi wameonyesha mara nyingi kuwa wako tayari kuongozwa na vyama vingine. Lakini CCM kwa kutumia vyombo vya dola na vya maamuzi, hufanya hila kuvihujumu vyama hivyo. 1995 NCCR, 2000 & 2005 Cuf na 2010 & 2015 CHADEMA. Kwa nyakati zote hizi CCM imefanya hila na siasa chafu dhidi ya wapinzani wake (ref kauli ya GS wa chama). Sioni kwa nini CCM watambe wakati wanachifanya ni hila na si siasa.

Ni kama kipindi hiki. Jamaa yako anavipiga vyama vingine Pini . Huku yeye na watu wake wakifanya siasa tena chafu. Unatambaje kwa hali hii.

Odhis *
 
you are so stupid
Noooooo he is not stupid, INFACT HE IS VERY TRUTHFUL TO THE POINT, NCCR ya wakati ule, kilikuwa chama cha ajabu sana, kila unganisha watanzania , lakini baada ya kushindwa kwa nguvu ya vyombo vya serekali, NYERERE/Polisi/JESHI NA TISS, kukawa na mkakati mkubwa mwingine, kuhakikisha NCCR wanafurungwa na misingi ya fitina inajengwa, na kisitokea chama kingine chenye uwezo kama hicho.

Ni kweli hakikuwa na udini, ukabila, ukanda .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu, kuna siku yoyote umeiandika vizuri CHADEMA? Thread zako zote humu, ni kupambana na hao jamaa! Inawezekana bila hivyo, hiyo B7 hupati!
 
Odhiambo cairo,
Jamaa yangu? Alafu unsingizia vinauliwa na CCM? Mlifanyia nini Dk Slaa? Au umesahau hujui hapo ndipo mliharibu?

Ila kwa upande mwingine jamaa nae amepiga kazi, nasikia zimebaki siku chache Mv bukoba ianze kufanya kazi baada ya ukarabati mkubwa na mengine mengine unayafahamu.
 
We umepoteza mb zangu tu,Unataka kuifsananisha CHADEMA na chama cha gesi,kiko wapi sasa,ona alimopita chadema kwenye matanuru ya moto kwa miaka,na ndiyo kinazidi kuwa CHAMA BABALAO,IMARA kuliko jana.
 
Kuvuta bangi bila kula ndiyo mwanzo wa kutoka chumbani umevaa "suti ya kulalia" huku unachekacheka kama zuzu.Pole chagu wa mawingu aka malunde🤣🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom