Haikuwa sahihi kwa Lissu na Ndugai kupambanishwa ktk mdahalo

Job alivaa kiatu kisiwokuwa chake, anyway CCM mpaka sasa hawana mtu wa kumweka apambane na Tundu kwa huja yoyote ile.
kama huyo simbachawene ndi kabisa, makinda mdio...., lukuvi ndio angejichanganya onyo ofcoz TUNDU kazeni buti hii ndio tanzania tunaoitaka
 
Obe ndug uko thawa anakosea thana huyo kilaz wamfunze adabu asiwe anakurupuka,kaz yake pale ilikuw ka naibu 2 ujng mwngne angeuacha
 
Kwakweli Ndugai alizidiwa kwelikweli, kwani ilifika wakati akawa amepoteza Muelekeo kabisa, Anaulizwa Waziri mkuu aliambiwa amedanganya, ukahitajika ushahidi ukaletwa, anaulizwa ni nini yalikuwa maamuzi ya bunge?.

Anajibu " Waziri mkuu ni mtu mzoefu sana na ni mtu mzima, na si vyema kimaadili kijana mdogo kumwita mtu ambaye ni sawa na baba yako Muongo". Ooooooh, wana JF wenzangu nilifedheheka sana kusikia jibu kama hili likitoka kwa kiongozi aliyepewa jukumu la kuliongoza bunge, nikatamani nizime TV kabisa.

HIVI SISI TUNAVIONGOZI WA AINA GANI JAMANI, AU NI LAANA HII????
 
Ndo udhaifu mkubwa wa CCM<br />
Sidhani kama wataruhusu tena mwana-CCM ashiriki katika midahalo ya namna hiyo<br />
Ni ukweli usiopingika kuwa Ndugai kajiweka wazi namna alnavyoelemea upande mmoja anapoongoza vikao vya bunge
<br />
<br />
Turejee kipindi cha kampeni 'mchakato majimboni' Makamba aliwambiaje wagombea wa ubunge kupitia Ccm?kwa hiyo Ccm wanajijua ni wadhaifu kihoja!
 
Mpaka sasa nimeshindwa kuamini kama kweli kuna kilaza kama yule ktk nafasi ya uspika.Lakini nawashukuru wahenga kwa kutuwekea taadhari mapema kwamba:"Kwenye nchi ya vipofu,chongo ndiye mfalme".

Basi ktk kundi lote la CCM huyo ndiye aliyewafaa na wakamchagua wote hadi wale ambao majia yao yamepambwa na elimu za hii duni mf:Dk, Prof, Eng, Mwl n.k.......Sasa watanzania wenzangu nchi inataka kuchukuliwa na wanaharakati (CHADEMA), Msisite kuwakabidhi nchi hii.

Freedom is coming tomorrow.
By:Mwanaharakati.
 
Tundu Lisu nimemkubali yuko juu, hata kama wangekusanywa akina Ndugai 3 bado wangetoka kapa. Chadema wako juu sana kuanzia Bungeni hadi Mitaani. Big up.
 
Mtoa mada kama ungesema kabla ya mdahalo kuwa nafasi ya Ndugai sio sawa kushiriki mdahalo na lissu ningekubaliana na wewe.Lakini naamini hii analysis yako imekuwa hivyo baada ya perfomance ya ndugai kwenye mdahalo wa jana.

Kimsingi kwa nafasi zao na ukizingatia mfumo wa bunge letu na matukio ya hivi karibuni bungeni utakubaliana na waliondaa mdahalo kuwa walikuwa sahihi.Lakini ndugai hakucheza kwenye role yake kama kiongozi wa bunge bali mbunge wa CCM na hata wakati mwingine alikuwa serikali.

Bado kuna tatizo ndani ya CCM na dhana ya midahalo.Wanategemea sana suport ya mashabiki wao ukumbini badala ya kujenga hoja zenye mashiko.

Hii hupelekea mtu wa CCM kuanza kuongea propaganda ili tu apate shangwe kutoka kwa watu ambao wako hapo kwa ajili hiyo bila kujali hoja.Watu nowdays hawajali kelele za wingi bali hoja.
 
Hata mm nilishangaa sannna y ndugai kakubal kupanda na Lissu (Another Class), ila thnx almighty God tumefaham upande wa pili wa Ndugai. Hana chuki zilizopitiliza na za waziwazi na chadema.

Ila moto ulioshawashwa na Makamanda Hautozimika mpaka kieleweke
 
Kimsingi kiongozi wa CCM bungeni ni Makinda na msaidizi wake ni Ndugai, hivyo mi naona ilikuwa sawa kwao kushindanishwa.
 
ningekuwa mimi CC ya CCM ningepiga marufuku mwanachama yeyote wa magamba kushiriki mdahalo na upinzani kwani ccm imeishiwa hoja za kuzungumza. Ccm inanuka kila kona kiasi kwamba lolote utakaloongea unakuwa kama unajivua nguo hadharani.

Ni aibu iliyoje kwa spika wa bunge la jamhuri ya muungano awe mwepesi vile...kama ****** kwa wepesi. By the way JN wa s the best choice kwa magamba.

Sidhani kama watakuja kukubali mdahalo wowote wa public baada ya jana
 
Naomba muangalie jinsi Al franken alivyomkatalia Joe lieberman wakati wa Healthcare debate,kwa wale wafuatiliaji, Lieberman ndiye aliyewakosesha wamarekani public option kwenye healthcare na democrats wanamind sana ingawa ni mwenzao.

Ndungai hakutakiwa kubembelezana na CDM, he dont have to.
 
..It is one thing Ndugai ku-behave in the way that he did, but it another thing for Tundu Lissu not calling him out during the debate.

..ni makosa makubwa sana kufikria kwamba wananchi "wataelewa", au kubweteka kwamba wananchi ndiyo "wataamua."

..watu wahuni-huni kama Ndugai wanapaswa kuumbuliwa hapohapo. hiyo itawatia moyo na ujasiri wananchi kutowaogopa.


..viongozi wa CCM wanatumia kila nafasi wanayoipata kuonyesha kwamba CDM ni watu wa hovyo-hovyo.

..CDM wanapaswa kujizatiti kujibu hoja hizo na siyo kubaki kushangaa-shangaa.
 

Kwa maoni yangu naona haikuwa sahihi kumpambanisha Mnadhimu Mkuu wa Chadema Bungeni Tundu Lissu na Naibu Spika, Job Ndugai kwani nafasi zao hazilingani.

Ilitakiwa Lissu angepambanishwa na mwenzake katika nafasi kama yake Bungeni, yaani Mnadhimu wa CCM.

Kwa kuwapambanisha Lissu na Ndugai, wananchi tayari wameshaona kwa nini huyo Naibu Spika ana upendeleo kwa wana-CCM wenzake (wabunge wa CCM) ndani ya Bunge, kwani tayari kishaonyesha chuki za waziwazi dhidi ya chama hicho &#8211; kama vile kuvaa kwao magwanda yanayoashiria shari na mapambano (kwa muono wake).

Kuanzia sasa Watanzania watakuwa na kila sababu ya kumuona naibu Spika huyo kuwa si mtu wa kutenda haki Bungeni, nah ii ni plus kubwa kwa wapinzani, hasa Chadema.

Tayari Ndugai kisha onyesha rangi zake halisi &#8211; hata akiwa ndani ya yale majoho, kwani mavazi huwa hayabadilishi tabia ya mtu.

Nashangaa kwa nini CCM walimruhusu Ndugai kukubali kufanya ule mdahalo.

ZaK

Kushangaa kwako kuna maanisha na kudhihirisha upeo wako wa juu wa kutizama na kuona unachokitizama na kukichukulia hatua sahihi!

CCM wangekuwa na sifa kama zako, Wasingefanya hicho walichokifanya, kwani wasingekuwa vipofu kama walivyo sasa....Na ushahidi ni hicho unachohoji na kuongelea!!!

Udhaifu wa CCM ni mkubwa na unahatarisha mwelekeo wa taifa!

Udhaufu uliodhahiri waliouonyesha kwa Kumchagua Job kuja kwenye mdahalo ule ...NI UDHAIFU MKUBWA! Ambao sio wa kufumbia machao!!

Udhaifu huo utajitokeza kwenye nyanja zote za kijamii kuanzia giza kutanda nchi nzima hadi vijemichezo vya magamba wanavyofanya!!

Jambo la msingi lazima lifanyike mara moja!! Kunusuru Roho na miili ya Watanzania!
 
Back
Top Bottom