Haikuwa sahihi kwa Lissu na Ndugai kupambanishwa ktk mdahalo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Haikuwa sahihi kwa Lissu na Ndugai kupambanishwa ktk mdahalo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Jul 31, 2011.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Jul 31, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Kwa maoni yangu naona haikuwa sahihi kumpambanisha Mnadhimu Mkuu wa Chadema Bungeni Tundu Lissu na Naibu Spika, Job Ndugai kwani nafasi zao hazilingani.

  Ilitakiwa Lissu angepambanishwa na mwenzake katika nafasi kama yake Bungeni, yaani Mnadhimu wa CCM.

  Kwa kuwapambanisha Lissu na Ndugai, wananchi tayari wameshaona kwa nini huyo Naibu Spika ana upendeleo kwa wana-CCM wenzake (wabunge wa CCM) ndani ya Bunge, kwani tayari kishaonyesha chuki za waziwazi dhidi ya chama hicho – kama vile kuvaa kwao magwanda yanayoashiria shari na mapambano (kwa muono wake).

  Kuanzia sasa Watanzania watakuwa na kila sababu ya kumuona naibu Spika huyo kuwa si mtu wa kutenda haki Bungeni, nah ii ni plus kubwa kwa wapinzani, hasa Chadema.

  Tayari Ndugai kisha onyesha rangi zake halisi – hata akiwa ndani ya yale majoho, kwani mavazi huwa hayabadilishi tabia ya mtu.

  Nashangaa kwa nini CCM walimruhusu Ndugai kukubali kufanya ule mdahalo.
   
 2. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #2
  Jul 31, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ndo udhaifu mkubwa wa CCM
  Sidhani kama wataruhusu tena mwana-CCM ashiriki katika midahalo ya namna hiyo
  Ni ukweli usiopingika kuwa Ndugai kajiweka wazi namna alnavyoelemea upande mmoja anapoongoza vikao vya bunge
   
 3. m

  mzee wa njaa JF-Expert Member

  #3
  Jul 31, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 1,368
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huyo Ndugai asiwaumize kichwa. Yana mwisho hayo.
   
 4. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #4
  Jul 31, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Mie naona hata kinyaa kuona zile rangi za CCM!! wamevimbiwa madaraka kutokana na kuivuna nchi hii kwa miaka 50 bila kuleta maendeleo ya maana. Kufa kwa CCM ndio nafuu yetu sisi wananchi tunaoitwa wa kawaida!
   
 5. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #5
  Jul 31, 2011
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  CCM kuna watu wa ajabu sana na pia sasa ndio tumeona jinsi gani alivyokuwa mnanzi maana ana kila sababu ya kusema kuwa Spika asitoke kwenye chama chcochote kile maana alikuwa hana jabza kubwa sana
   
 6. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #6
  Jul 31, 2011
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,152
  Likes Received: 1,248
  Trophy Points: 280
  Ndugai keshaonesha alivyopwaya kwa hiyo hana jipya huyu, na aliyeandaa huu mdahalo tunamshukuru sana katusaidia kujua zaidi unazi wa huyu kabaraka wa ccm anapoongoza bunge
   
 7. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #7
  Jul 31, 2011
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,919
  Likes Received: 608
  Trophy Points: 280
  Mkuu ZK. Jana usiku nimelala nikiwaza sana Juu ya hili.

  Ndugai was 100% acting CCMly!!! Hivi huvi ndivyo anahitaji kufanya kulingana na nafasi yake?

  Jamani hii sio haki. Kuna lecturer Mmoja wa UDSM aliuliza swali Lenye muelekeo huu kwa Ndugai, lakini kama kawaida ya wanaCCM, majibu mepese kwenye maswali magumu.

  Hivi ndugai alikua nasimama kama Mwakilishi wa CCM au Mwenyekiti wa Bunge?
   
 8. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #8
  Jul 31, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,175
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  ccm hawana watu wenye upeo wa kuona mbali.
   
 9. Butho Mtenzi

  Butho Mtenzi JF-Expert Member

  #9
  Jul 31, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 328
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Unalosema Mkuu lipo sahihi lkn kiukweli the way alivyo Lisu asingeweza pambana na Mnadhimu Mkuu wa CCM kwani Lisu ni another Level ndo mana wakamruhusu Ndugai kwan kidogo ana upeo japo upeo wake sio wa kulinganishwa na Lisu na ndio mana Job alipwaya na kuanza kuleta kejeli ni hayo tu wanaJF
   
 10. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #10
  Jul 31, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,948
  Likes Received: 1,274
  Trophy Points: 280
  Ndugai is a looser, yeye alitaka kuua sifa ya CHADEMA (character assasination). Uwezo wake wa kufikiri una walakini sana, alipaswa kujenga hoja.
   
 11. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #11
  Jul 31, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Ndugai kadhihilisha ukilaza wake jana! Na tatizo la yeye na ccm ni kuona kuwa cdm ndio maadui wao, huku wakishindwa kuona kuwa hoja za cdm ndio adui wao maana wanashindwa kuzijibu kwa hoja na matokeo ya wanafanya madudu wanayofanya kama kuwatoa wabunge wa cdm na kuonyesha chuki kama alivyofanya.
   
 12. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #12
  Jul 31, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  nimesikia kulikuwa na mdahalo kama kawa jana Tanesco walichukua chao lakini nasikia kipindi kinarudiwa sijajua muda mwenye kufahamu atujuze
   
 13. Obe

  Obe JF-Expert Member

  #13
  Jul 31, 2011
  Joined: Dec 31, 2007
  Messages: 5,960
  Likes Received: 20,299
  Trophy Points: 280
  Kale kasafiri ka kwenda UK kalimpandisha chati ndani ya ccm na wakaona anafaa kusimama na TL, JN jana alisimama kama mbunge wa ccm na si spika wa BLJMT, kauli zake dhidi ya cdm zilikuwa zimejaa chuki na ni kama alikuwa akipanic na hivyo kushindwa kujibu hoja ama kusema yanayostahili.
  Kwa upande wa TL mwanzoni alitaka kujifagilia sana lkn baadae alirudi na kuwa objective sana na hii ilikuwa ni bonge la credit kwa cdm bungeni na kwake kama mnadhimu.
  Namna walivyohitimisha mjadala wao utagundua kuwa ushindi wote aliondokanao TL na aibu ya wazi ilikuwa kwa JN, siku nyingine anapaswa (JN) kuwa makini na kukontroo emotions zake hasa anaposimama kama n/spika lakini akisimama kama mbunge wa ccm hakuna shida kwani akili zao tunazijua.
  ONYO: Usifikirie, kutenda na kuamua kama mbunge wa CCM
   
 14. N

  NDOFU JF-Expert Member

  #14
  Jul 31, 2011
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 656
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hapana'alisimama kama naibu spika ambaye ameamua kutoyajua majukumu yake kwa makusudi! Amejianika wazi kuwa yupo pale kwa kutetea masi-lahi ya ccm na si ya taifa.Amesaidia kutupatia chekecheo sisi wananchi ili tupate pumba vizuri.
   
 15. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #15
  Jul 31, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  hawakuwa na mtu mbadala wa kumpambanisha na Tundu Lissu, wao wanamwona Ndugai ndiyo bora kuliko mwingine yeyote, yaani ni bora hata kwa JK.
   
 16. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #16
  Jul 31, 2011
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Ule mdahalo uliishusha CCM na kuipandisha CDM kwani ilijulukana kuwa CCM ipo kwa kuwa inapata upendeleo toka kwa kiti cha spika. Job kadhihirisha jana.
   
 17. Rugas

  Rugas JF-Expert Member

  #17
  Jul 31, 2011
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,053
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  kwa sisi ambao hatukuweza kuuona mdahalo!tungeomba pia kuwasikia wachangia wa upande wa pili!yaani ccm,ili tuweze kuupima mdahalo!Ccm mpo?
   
 18. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #18
  Jul 31, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,031
  Likes Received: 7,430
  Trophy Points: 280
  Kadharirisha vilaza
   
 19. Izack Mwanahapa

  Izack Mwanahapa JF-Expert Member

  #19
  Jul 31, 2011
  Joined: Apr 21, 2011
  Messages: 497
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Ndugai alikubali kwenda kwenye mdahalo kwasababu yupo psychological affected na makofi anayopigiwa na wabunge wa ccm Bungeni kwa kila anachokisema, so alidhani popote atakapokwenda na chochote atakachokisema kitapigiwa makofi kama ianavyotokea Bungeni, Matokeo yake akajikuta kati kati ya watu makini ambao hawababaishi na ushabiki bali nguvu ya hoja.
   
 20. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #20
  Jul 31, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Si kama kaizalilisha ccm bali uwezo wa magamba ndio huo,jamaa baada ya kukaa na kufikiria wakaona Ndugai anaweza ndipo wakamruhusu but amepwaya sana na anafanya watu wajiulize kuhusu uwezo wake wa kuliongoza bunge wakati hata kujenga hoja tu hawezi
   
Loading...