Haikuwa sahihi kwa Lissu na Ndugai kupambanishwa ktk mdahalo

nimelisema sana hili jana hapa, watu walikuwa focused kwenye mechi kamam alivyoiita naibu spika bila aibu. ofisi ya spika imejivunjia heshima.
 
Kwa maoni yangu naona haikuwa sahihi kumpambanisha Mnadhimu Mkuu wa Chadema Bungeni Tundu Lissu na Naibu Spika, Job Ndugai kwani nafasi zao hazilingani.

Ilitakiwa Lissu angepambanishwa na mwenzake katika nafasi kama yake Bungeni, yaani Mnadhimu wa CCM.

Kwa kuwapambanisha Lissu na Ndugai, wananchi tayari wameshaona kwa nini huyo Naibu Spika ana upendeleo kwa wana-CCM wenzake (wabunge wa CCM) ndani ya Bunge, kwani tayari kishaonyesha chuki za waziwazi dhidi ya chama hicho kama vile kuvaa kwao magwanda yanayoashiria shari na mapambano (kwa muono wake).

Kuanzia sasa Watanzania watakuwa na kila sababu ya kumuona naibu Spika huyo kuwa si mtu wa kutenda haki Bungeni, nah ii ni plus kubwa kwa wapinzani, hasa Chadema.

Tayari Ndugai kisha onyesha rangi zake halisi hata akiwa ndani ya yale majoho, kwani mavazi huwa hayabadilishi tabia ya mtu.

Nashangaa kwa nini CCM walimruhusu Ndugai kukubali kufanya ule mdahalo.

Yani kwa ujumla jana star Tv walipambanisha mlima kilimanjaro na kichuguu, Ngugai amedhihirisha kuwa ni layman.

Nafurahi kuwa watanzania wamegundua nani mapumba na nani nafaka.
 
Ni kweli kabisa walichemka,mie nawalaumu hata waandaaji pamoja na upeo mdogo wa Ndugae kushindwa kuelewa Role yake, maana mie naamini kabisa Ndugae alialikwa pale kama Naibu spika na sio kada wa chama au mnadhimu wa ccm badala yake alisahau nafasi yake kama naibu spika nakuonyesha maaba makubwa kwa ccm jambo lilonifanya binafsi nijihoji sana juu ya uelewa wake na uwezo wake wakufikiri nakujenga Hoja.

Waandaji wa Midahalo kama hii lazima wabalance wazungumzaji wakuu huwezi ukamweka mtu mmoja akaplay role mbili tofauti Ndugae upande mmoja naibu spika kiongozi wa Bunge kazi kubwa ya Bunge kuisimamia serikali upande huohuo anaitetea Serikali kwasababu inaongozwa na Chama chake so which is which!!
 
duuuuuuuuuu! wadau michango mizito nawashukuru mm mwenyewe nilishangaa sana badala ya ndugai kujibu hoja za msingi azungumzia magwanda
 
Kale kasafiri ka kwenda UK kalimpandisha chati ndani ya ccm na wakaona anafaa kusimama na TL, JN jana alisimama kama mbunge wa ccm na si spika wa BLJMT, kauli zake dhidi ya cdm zilikuwa zimejaa chuki na ni kama alikuwa akipanic na hivyo kushindwa kujibu hoja ama kusema yanayostahili.<br />
Kwa upande wa TL mwanzoni alitaka kujifagilia sana lkn baadae alirudi na kuwa objective sana na hii ilikuwa ni bonge la credit kwa cdm bungeni na kwake kama mnadhimu.<br />
Namna walivyohitimisha mjadala wao utagundua kuwa ushindi wote aliondokanao TL na aibu ya wazi ilikuwa kwa JN, siku nyingine anapaswa (JN) kuwa makini na kukontroo emotions zake hasa anaposimama kama n/spika lakini akisimama kama mbunge wa ccm hakuna shida kwani akili zao tunazijua.<br />
<font color="#008000"><font size="4"><span style="font-family: arial black"><b>ONYO: Usifikirie, kutenda na kuamua kama mbunge wa CCM</b></span></font></font>
Hilo onyo limekaa njema.
 
Hivi marudio ya kipindi hiki ni lini nasi tujionee au if recorded somewhere please rusheni tuone tuliopitwa na uhondo huu
 
Kwa maoni yangu naona haikuwa sahihi kumpambanisha Mnadhimu Mkuu wa Chadema Bungeni Tundu Lissu na Naibu Spika, Job Ndugai kwani nafasi zao hazilingani.

Ilitakiwa Lissu angepambanishwa na mwenzake katika nafasi kama yake Bungeni, yaani Mnadhimu wa CCM.

Kwa kuwapambanisha Lissu na Ndugai, wananchi tayari wameshaona kwa nini huyo Naibu Spika ana upendeleo kwa wana-CCM wenzake (wabunge wa CCM) ndani ya Bunge, kwani tayari kishaonyesha chuki za waziwazi dhidi ya chama hicho kama vile kuvaa kwao magwanda yanayoashiria shari na mapambano (kwa muono wake).

Kuanzia sasa Watanzania watakuwa na kila sababu ya kumuona naibu Spika huyo kuwa si mtu wa kutenda haki Bungeni, nah ii ni plus kubwa kwa wapinzani, hasa Chadema.

Tayari Ndugai kisha onyesha rangi zake halisi hata akiwa ndani ya yale majoho, kwani mavazi huwa hayabadilishi tabia ya mtu.

Nashangaa kwa nini CCM walimruhusu Ndugai kukubali kufanya ule mdahalo.

Ha ha haaaaaa huyu ndio kiboko yenu, aliwatoa wabunge wenu nje na akawavunjia heshima kweupeeeeeeeeeeeee
 
Kwa maoni yangu naona haikuwa sahihi kumpambanisha Mnadhimu Mkuu wa Chadema Bungeni Tundu Lissu na Naibu Spika, Job Ndugai kwani nafasi zao hazilingani.

Ilitakiwa Lissu angepambanishwa na mwenzake katika nafasi kama yake Bungeni, yaani Mnadhimu wa CCM.

Kwa kuwapambanisha Lissu na Ndugai, wananchi tayari wameshaona kwa nini huyo Naibu Spika ana upendeleo kwa wana-CCM wenzake (wabunge wa CCM) ndani ya Bunge, kwani tayari kishaonyesha chuki za waziwazi dhidi ya chama hicho kama vile kuvaa kwao magwanda yanayoashiria shari na mapambano (kwa muono wake).
Kuanzia sasa Watanzania watakuwa na kila sababu ya kumuona naibu Spika huyo kuwa si mtu wa kutenda haki Bungeni, nah ii ni plus kubwa kwa wapinzani, hasa Chadema.
Tayari Ndugai kisha onyesha rangi zake halisi hata akiwa ndani ya yale majoho, kwani mavazi huwa hayabadilishi tabia ya mtu.
Nashangaa kwa nini CCM walimruhusu Ndugai kukubali kufanya ule mdahalo.

Kweli mkuu...William Lukuvi ndie angepaswa kupambanishwa na Tundu Lissu...kama madhumuni ya mdahalo ni juu ya TZ yetu tunayoitaka- kutoka bungeni, mpambano wa Lissu na Lukuvi ungekua unafaa.

Kwa kumpambanisha Lissu na Ndugai, ni kuidhalilisha CCM, kwani Ndugai ingawa ni NS, lakini kwenye mdahalo alishindwa kusimama na kutoa hoja kama NS, bali alitoa hoja kama mbunge wa Kongwa kupitia CCM!

Kitu ambacho kilifanya macho ya waTZ yazidi kufunguka na kupambanua ukweli juu ya usawa na haki bungeni kati ya wabunge wa CCM na wapinzani (haswa CHADEMA).
 
MImi nilisha sema Ndugu gani ni mtupu na hata kumtuma kwenda UK kwa issue ta rada nilishangaa sana .Yaani yule naye eti wa maana .Ma CCM kwisha kizi yako uchi na hata hayana aliye nafuu maana wasomi ndani ya CCM wote ni wachumia chumvi mh
 
Back
Top Bottom