Haijalishi tumekosea wapi turudi tujipange!

Chiwa

JF-Expert Member
Apr 17, 2008
4,079
4,924
ifike wakati tutazame upya safari tuliyoianza kuikomboa nchi yetu katika kusimamisha uchumi imara na kuendelea kuwa na nchi yenye amani na mafanikio. tumekuwa watu wa kulalamika mno naogopa kusema kama wanawake! lakni hili ndio kweli. wachache wanaojitoa kwa bidii kwa ajiri ya taifa na jamii yetu kwa ujumla.

wengi tunafanya shughuli zetu si kwa zaidi ya 30% ya uwezo tulionao na tumekubali kufanya hivyo eti tumekata tamaa. wanasiasa tuliowategemea watangulize bendera yetu nao wengi hawawajiki tulivyotegemea wamekuwa watu wa mihemko!tunashindwa kuona kweli ndani yao wamekuwa watu wa kutetea maovu ilimradi kuna shibe!

Nafikiri na natamani tuangalie nini cha kufanya ikiwa ni kuielewesha jamii na sio kuilewesha kama ilivyofanywa sasa na ikiwezekana tutazame nchi yetu kwa miaka hamsini ijayo na tuwe tayari kujitoa hata kama sisi hatutapata maslahi yake kwa sasa. tutumie taaluma zetu na ikiweza tuungane tujue kila mmoja anaweza nini na mchango wake unaweza kuwa nini kwa jamii ili tuweze kwenda tunakutaka kufika.

ifike wakati kila mtu aone kunasehemu hakuwajibika ipasavyo na mchangiaji mkubwa kwa mzembe uliopo na sasa ameamua kubadilika! tukilifanya hili kwa dhamira zetu za ndani tunaweza kwenda kwa kujitazama kuanzia mimi mwenyewe, familia , jirani, mtaa,kata,tarafa ,wilaya ,mkoa na kisha taifa.
 
Back
Top Bottom