PSEUDOPODIA
JF-Expert Member
- Aug 9, 2020
- 376
- 735
Jana nilikuwa kijiwe kimoja hivi cha madalali wa nyumba na viwanja hapa Dar es Salaam.
Watu walikuwa wanajadili kwa kina maswala ya usajili ya vilabu vya simba na Yanga.
Ghafla mada ikabafilika ghafla baada ya mzee mmoja niliekuwa nnamfahamu ambaye ana bint yake aliyefaulu form 4 kwenda form 5.
Mada ilibafilika baada ya Mimi kumuuliza mzee bint yako alipangiwa kombi gani, mzee kwa kulalamika akajibu kuwa alifaulu sayansi ila wakampanhia HKL .
Mara jamaa mmoja akadakia, duuh anza kumtafutia mtaji kabisa akimaliza chuo aanze biashara. Maana siku hizi ajira hakuna. Mada ikakolea baada ya watu kuanza kumuhesabia magufuli miaka aliyobakiza hata kama atashinda tena. Ikaonekana yule mtoto paka amalize chuo magufuli atakuwa kashaondoka madarakani.
Fundi ujenzi mmoja akadakia kuwa, Huyu bwana safari hii hapiti, Amefanya maisha yamekuwa magumu kwelikweli. Kipindi cha Nyuma kazi zilikuwa nyingi paka tunazikimbia, leo zunguka mji wote huu utakuta sehemu zinazojengwa hazizidi hata tatu. Mimi 2015 nlimpigia kura ila mwaka huu simpigii.
Madalali nao wakadakia kuwa hata kwao hali ni hiyohiyo. Yaani huyu jamaa wakiskia ameshindwa watafurahi sana.
Nlichokiona Jana kwa hili kundi na makundi mengine ya Bodaboda, Mamantilie, Wajasiriamali wadogowadogo ni kuwa karibu wote wanata Magufuli aondoke. Yaani hata itokee tume ya uchaguzi waseme Uchaguzi ni kesho na hakuna kampeni Basi Magu anashindwa vibaya sana ingawa yeye kafanya kampeni karibu miaka mitano na bado zinafanyika juhudi za kutosha ili Lisu asisikike. Nilichokiona ni kuwa Lisu haitaji Kampeni wala habari zake ziwafikie watu. Ila watu wenyewe wapo tayari kumchagua bila hata kumsikia.
Ni hayo tu.