Habari zenu wanaJamii.. Nina imani mko Salama kabisa..
Kwa mara nyengine tena nimekuja na story hii.. inayohusu, ni namna gani nilivyouanza na kuumaliza mwaka wa 2018.
Nirudishe Historia nyuma kidogo mpaka mwaka 2017, ambapo kuanzia mwezi wa 9 mpaka wa 11, niliachana na mabinti wanne ambao nilikuwa nao kwenye mahusiano.. Na mwezi wa 12 nikapata binti mwengine.. ambaye huyu mahusiano yake kidogo yalikuwa serious, kwa maana pia alisisitiza kunipeleka mpaka kwao na alinitambulisha.
Maisha yakaenda na Mwezi ukafika Mwishoni.. Yaani kuukaribisha mwaka 2018 sasa.
Kama ishara ya shukrani na Upendo nikaamua kujitutumua nikamnunulia yule binti simu flani kali ili akaribishie mwaka.. ingawa sikuwa nimemkabidhi
Usiku wake nikaenda mpaka Chuo alichokuwa anasoma.. Nikapaki ndinga nikawa nimekaa naye hapo huku tukisubiri mwaka mpya uingie.. Sasa ile saa tano na nusu inafika.. kidogo wakaja jamaa wawili waliovalia nguo za kiaskari na wakapiga lock Gari yangu, na kuanza kunizingua vibaya, hadi yule binti akaanza kupata wasiwasi.. ila mimi nikawa nawajibu kawaida tuu, na nikafunga gari ..nikasepa zangu kwenye kituo chao kidogo cha polisi ili niepushe utata nikiwa na yule Binti wa watu..
Tuliyazungumza yakaisha na hapo ndipo nilipopata nafasi ya kwenda kutoa gari yangu na kuagana na yule binti mida ya saa 6 na nusu.. yaani mwaka mpya 2018.
Ule mwaka ukawa umeingia kwa style hiyo ya shari.. na yule binti kiukweli alionekana amechukizwa, hivyo hakutaka kuzungumzia jambo lolote na hata zawadi yake hakutaka kuipokea.. basi nikaamua kumpeleka hadi kwenye malazi yake na kumwacha hapo nikiwa bado nambembeleza..
Cha kushangaza kesho yake naamka asubuhi mida ya saa 3 napokea Text inasema ..PLEASE CAN WE END THIS AND JUST BE FRIENDS.. nilishangaa sana na kuishia kucheka tuu.. na nilishukuru kwa upande mwengine kwa maana Simu yangu aina ya iPhone 6s ilipona.. maana sikutaka kubembelezana naye..
Ila nahisi lilikuwa Gundu, kwa maana tangu pale.. sikupata binti hadi mwaka huu tarehe 2 mwezi wa 1..
Karibuni.
Sent using Jamii Forums mobile app
Life is not fair,mi wangu sijawahi kumnunulia hata pipi,ila haniachi
Sent using Jamii Forums mobile app
Afu kaandika ndinga pale nikatamani aweke picha ya ndinga lake apo isije kuwa ni ivi vi raum, ist, passo, sjui ka vits mara sjui CarinaπππNeno gari limetawala sana kwenye uzi wako kamanda
By the way, Hongera kwa kumiliki gari !
Sent using Jamii Forums mobile app
hahaha ndinga ni ndiga tu Mkuu haijalishi,wengine kama Mimi hapa hata lile gutta lakuchulia mizigo pale mabibo sokoni limekuwa mtihaniAfu kaandika ndinga pale nikatamani aweke picha ya ndinga lake apo isije kuwa ni ivi vi raum, ist, passo, sjui ka vits mara sjui Carinaπππ
Afu kaandika ndinga pale nikatamani aweke picha ya ndinga lake apo isije kuwa ni ivi vi raum, ist, passo, sjui ka vits mara sjui Carinaπππ
Kuna gari za kuita ndinga mkuu na kuna gari za kuita usafiri...unakuta njemba miraba minne limetuna kwenye ist utafikiri yuko kwene baby walkerπππ afu akishuka ananing'iniza funguo kiunoni kabisa iyo nayo eti iitwe ndingaπππ uwezi chukua 80mil na 10 mil ukazipaki apo afu zote zikaitwa ndingahahaha ndinga ni ndiga tu Mkuu haijalishi,wengine kama Mimi hapa hata lile gutta lakuchulia mizigo pale mabibo sokoni limekuwa mtihani
game's up ..besides ndo nipo kwenye edge ya huo umriYaani mzee una ndinga na una uwezo wa kuhonga simu ya laki tisa halafu unakaa mwaka mzima huna demu!
Raise up your game bro.
Sent using Jamii Forums mobile app
ndo huyohuyo kiongozi.. ila nimeupgrade.. sasa story yake ukiisikia ndo utachekaUliyempata mwaka huu ndiyo huyo ulieachana nae jana?
daah aisee umeiweka kitaalamu sanaDaaaaah kaka kwa ulivyojieleza hakukuwa na sababu ya msingi ya huyo binti kukuacha,ila kwa kuwa una gari na good life yawezekana ndo kilimvuta kwako,unaweza ukampata unaempenda ila ukakosa ataekupenda ila ukapata ataependa ulichonacho,kingine ujue maisha n magumu hususan vyuoni,kama madada wanaweza kujiuza ili kujikimu vyuon watashindwaje kuwa na wew ili wapone,kingne jitathmin kitandan ukoje(simaanishi ukilala unakoroma au laaa),maana mwanamke anaweza akakuacha na gari na zawad yako ya iphone akaenda kwa mwenye baiskeli na zawadi ya mahindi choma,namaanisha huyo jamaa anajitahd kitandan,
USHAURI
Kama utataka demu wa kick and run(yaan wa kutolea maganda meupe tuu),show how capable you are in life kama hvyo unamsimamisha ukiwa na ndinga but ukitaka mke show less of your wealth,paki gari nyumban panda daladala au boda mfate,hapo utapendwa wew na utapata real love,ila ukienda na ndinga litapendwa ndinga huku ukihis umependwa wew
hahahah vivo hivyo ..au ndo mchonga mchongo[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] maana anaonekana either anayajua sana, au yeye alikuwa miongoni mwa wale askari au alikuwa yule demu wako
aah ile nilimpa bimkubwa kiongoziHiyo iphone bado ipo mkuu?, nikucheki pm [emoji3] [emoji3] [emoji3]
Sent using Jamii Forums mobile app
daah acha kabisaLife is not fair,mi wangu sijawahi kumnunulia hata pipi,ila haniachi
Sent using Jamii Forums mobile app
hapana.. ni Nissan PatrolAfu kaandika ndinga pale nikatamani aweke picha ya ndinga lake apo isije kuwa ni ivi vi raum, ist, passo, sjui ka vits mara sjui Carinaπππ
hahahah.. mwambiehahaha ndinga ni ndiga tu Mkuu haijalishi,wengine kama Mimi hapa hata lile gutta lakuchulia mizigo pale mabibo sokoni limekuwa mtihani
point yako nimeipataKuna gari za kuita ndinga mkuu na kuna gari za kuita usafiri...unakuta njemba miraba minne limetuna kwenye ist utafikiri yuko kwene baby walkerπππ afu akishuka ananing'iniza funguo kiunoni kabisa iyo nayo eti iitwe ndingaπππ uwezi chukua 80mil na 10 mil ukazipaki apo afu zote zikaitwa ndinga
PassoAfu kaandika ndinga pale nikatamani aweke picha ya ndinga lake apo isije kuwa ni ivi vi raum, ist, passo, sjui ka vits mara sjui Carinaπππ