Ndagullachrles
Senior Member
- Jun 20, 2023
- 198
- 209
Hadithi ya Barnaba Tillya aliyempoteza mke wake kipenzi,Irene Tillya wakati akijifungua katika Hospital ya Marangu juni 4 mwaka huu inaumiza sana.
Ndiyo ni hadithi inayoumiza unapoanza kuhadithiwa kuanzia mke wake anapoondoka nyumbani hadi anafika Hospital na madhila aliyoyapata kuanzia wodi ya wazazi hadi chumba cha upasuaji.
Tillya anaishi Kitongoji cha Kouri kilichopo Kijiji cha Lekura kata ya Mamba wilaya ya Moshi Vijijini na alibahatika kupata watoto wawili na marehemu mke wake Irene Tillya.
hii hapa hadithi ya Barnaba.
"Asubuhi mke wangu aliamka salama akaenda sokoni kukusanya ndizi na akarudi nyumbani akiwa salama na kuingia jikoni kupika chakula lakini jioni akaanza kusikia uchungu"
"Aliwasiliana na daktari ambaye alikuwa akimhudumia mara kwa mara akiwa kliniki kwamba muda wa kujifungua umefika na anaelekea hospital"
"Daktari alichelewa sana kujibu sms ya mke wangu na alipomjibu alimwambia ameshapata taarifa na atajifungua kwa njia ya kawaida na si kwa upasuaji na akampa hongera"
"Lakini mwanzo daktari huyo alimwambia mke wangu atajifungua kwa oparesheni kwa sababu amekaa muda mrefu bila kubeba mimba lakini baadae wakabadilisha "
"Wakati anaondoka hakuweza kula chakula na aliniambia niweke chakula kwenye friji kesho akirudi atakila lakini ndiyo hivyo amerudi akiwa kwenye jeneza"
"Nilianza kuandaa vitu na baadae nikaondoka na mimi kwenda Hopsital nilipofika muda wa saa mbili nikiwa karibu na mlango wa wodi ya wazazi nikaanza kusikia mtu analia na kupiga kilele akiomba msaada kusogea zaidi nikajua ni mke wangu"
"Aliendelea kupiga kelele huku akiomba msaada lakini hakuna aliyemsaidia mpaka nikaomba niingie ndani nijue shida yake lakini wauguzi walinuzuia wakisema hakuna sheria inayoruhusu mwanaume kuingia wodi ya wazazi"
"Kelele hizo ziliwashtua mpaka wagonjwa wengine wakatoka nje na kuuliza kulikoni na wengine wakiomba ahudumiwe huyo mgonjwa"
"Kelele ziliendelea hadi saa saba usiku baadae nikaona wanamtoa kwa machela kutoka wodi ya wazazi kwenda chumba cha upasuaji lakini alikuwa amechoka sana lakini muunguzi mmoja alinidokeza kuwa ameshajifungua lakini mtoto ameshakufa na damu zilimtoka nyingi sana,niliumia sana".
"Baada ya muda daktari aliyekataa kunipa ushirikiano alitoka na kuanza kuniuliza 'wewe na mke wako mna watoto wangapi?",nikahoji kwa nini unaniuliza hivyo,alichonijibu ni kwamba mama na mtoto hawapo duniani tena"
"Nilianza kuangua kilio na hao madaktari na wauguzi wakaanza kunikimbia,niliona michilizi ya damu ikitoka chumba cha upasuaji,kwa kweli nilichanganyikiwa ,watu wengi walitoka na kuanza kulaani kitendo hicho"
"Ndugu zangu ambao walifika hapa Hospitalini nao walishuhudia tukio hilo na ilipofika asubuhi niliondoka na mabegi ya nguo za mke wangu na za mtoto na kurudi nyumbani"
Je unajua uongozi wa Hospitali ulitoa mchango gani kwa mfiwa?,walishiriki mazishi?,walitoa pole?,fuatilia mkasa huu hapa kesho
hapa chini kama unavyoona Tilya akiwa ameshika makaburi ya wapendwa wake,kushoto ni kaburi la mtoto wake na kulia ni kaburi la mke wake