Hadithi ya kweli.

Hadithi ya kweli.

Jaguar

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2011
Posts
3,440
Reaction score
1,029
Ni kutoka iringa-Tanzania.Baba mmoja wa kihehe akiwa na mwanawe wakitoka machungani walikuwa wanajaribu kuwavusha ng'ombe wawili (mama ng'ombe na ndama) kukatisha mto.Kila yule mzee alipojaribu kumvusha yule mama ng'ombe,aligoma.Yule baba alihangaika sana bila mafanikio.Mwishowe mtoto wa huyu baba wa kihehe akampa wazo babake kwamba watangulie kumvusha ndama then mama ng'ombe atafuata mwenyewe.Baba mtu kwa kinyongo alijaribu mbinu hiyo na ikafanikiwa kwa urahisi saana.Baba mtu alimwambia mwanawe atangulie na ng'ombe nyumbani,yeye atakuja baadaye.Yule baba hakuonekana nyumbani mpaka kesho yake walipomkuta ananing'inia mtini i.e kajinyonga. Mfukoni alikuwa na karatasi imeandikwa,'SIWEZI KUVUMILIA,MWANANGU KANIZIDI AKILI'.Wahehe punguzeni hasira!
 
nyela!! yenyewe isenga hiyo na mtoto wake ndio imesababisha baba ajinyonge ayaaaaaa watani ndauli????
 
Hao tushawazoea kujinyonga kwao ni ufahali
ufahari gani..wakati ndo ameshaondoka, ataonaje na kujisikia huo ufahari alioupata wakati umeshakufa.. watani zangu wahaya ndo wanajua kuonyesha ufahari... iwe nina madigrii matano toka bostoni
 
Ni hadith ya kweli/stori ya kweli? Naomba ufafanue ninamatazo juu lugha ya Kiswahili!
 
Ni hadith ya kweli/stori ya kweli? Naomba ufafanue ninamatazo juu lugha ya Kiswahili!
Kwenye kamusi ya kiswahili hakuna neno stori ila kuna neno hadithi.Hadithi>(kiswahili),story>(kiingereza).
 
kwakweli tungekuwa na viongozi katika nchi hii wenye staili ya kihehe, mambo ingekuwa mswano, akifanya upumbavu mkimvalia njuga tu anajiuzulu.
 
Back
Top Bottom