Hadithi ya kweli ya maisha yangu

Kwahyo huyo manzi wa karatu, yuko msoma hadi Leo mkuu??
 
mkuu ni app gani unatumia kutengeneza beats
 
inaendelea


Hatimaye cku zangu za kuishi na kupiga kazi zilifika tamati mwez wa 11 mwanzoni kabisa yani nilikua nasubir tarehe ya mshahara tarh 08 nichukue mshara wangu.

Siku hyo ilikua jumapili niliwai kiwandani mpk idarani kwangu nikakabidhiwa machine na operator ( alikua mdada bonge ) sasa nilianza kufuma vitambaa vya mifuko kama kawaida mpk kwenye saa tatu asubui wakaja ma in charge wawili pamoja na mwalimu wetu alie tufundisha.

Sijui walkua wanakagua nini ila alivyofika kwangu wakanambia kuwa kama nimesoma ratiba vizur nikasema ndio....wakanambia kaisome tena.Niliisoma duh nikakuta kumbe cku hyo nilikua naingia shift ya usiku ( ratiba ilibadilishwa maana ilikua ni mwanzo wa mwezi )...walinambia niache mashine nirud home kujiandaa na shift ya usiku.

Niliacha nikarud home kulala, saa kumi na 11 jioni nilijiandaa fresh tu afu nikaelelekea kiwandani.Kwa vile nilikua nimewai niliamua kusikilizia kwanza nje ya get kusubir saa kumi na mbili ili niingie idarani.

Hatimaye niliingia idarani lakini siku hyo kwenye line yangu machine zilikua zimejaa, yaani nilikosa machine cku hyo, nikamfuata fundi wa hyo line nikamwambia kuwa sina machine akanambia niende kwenye line namba 4 ( me nilikua line namba 5 ).....kwenda huko line no 4 nako kulikua kumejaa ko nikarudi tena kwenye line yangu nikawa napiga story na operator mmoja hivi nilikua nimepanga nae sehem moja.

Alikuja meneja wa sections yetu akaniona napiga story akaniita kuniuliza mbn sifanyi kazi nikamwambia nimekosa machine.

Kila operators lazima aendeshe machine tatu kama tu amemaliza mwezi mmoja toka aajiriwe, machine mbili ukiwa umemaliza zile siku kumi za kufundishwa na machine moja ndani ya zile siku kumi.

Manager alinambia nimfuate ko tulienda kutafuta nae line ambayo machine zipo tu tukakosa akanambia iki nisikae bure aliniomba niwe dereva boy ( delivery boy ) niwe nasambaza zile cone ( Nyuzi ) kwa ma operator...nilkubali nikaanza kusambaza hizo cone me najamaa mmoja ni Bubu tokea saa 1 jioni nilikua nasambaza hizo koni mpk saa nne ambapo in charge aliiniita akanambia kwanini nafanya kaz isiyo nihusu..nilimwambia akataka niache alafu akanipeleka kwenye machine line namba 1 nikapewa machine tatu.

Hizo machine zilikua ni mbovu hatari alafu cone zake ni clearly ( yaani ile mifuko ambayo rangi yake ni kama silver hivi ).. hizo cone za clear usiku zinasumbua hatar kutokana na hyo rangi yake, pale unapochomeka uxi kwenye matundu ya mikanda ya machine usipokua makini unaweza ukatoa Reject ( mfuko kuwa hauna ubora ).

Machine hzo nilizopewa zilikua zina speed ndogo ko ili niweze kutoboa lengo langu zilitakiwa ziwake bila kuzima mpk asubui, lakin kutona na kuwa mbovu yaani niliteseka nazo sana nikawa namuita fundi anatengeneza lakin wapi zikawa bado ni mbovu tu.

Kama nilivyowaambia kwenye section yetu kulikua na machine za aina nne na kila machine ilikua na speed yake na lengo lake.Ile line namba tano niliyowekwa ilikua machine zske ni nzur mpk raha kuziendesha speed nzuri sana.

Sasa hizi nilizopewa cku hyo 😂😂 kwanza speed ilikua ndogo lengo kubwa.nilipambana siku hyo ( Mungu na ma operator waliokuepo ni mashahidi )

Ilifika saa nane za usiku machine bado zilikua zinasumbua ssna.nikiona wenzangu wana mita za vitambaa karbia 900 eti me ndo machine iliyokua na mita nyingi ni moja ilikus na mita 205....niliamua kuziacha hizo machine bila kutoa taarifa ( nilikua cjui kama ni kosa ) basi kulikua na machine zilikua hazitumiki kwenye hyo hyo line nikaziwasha nikaanza kupiga kazi.

Hizo machine zilikua nzur mpk nikawa nasema kwann nilipoteza muda bure kuhangaika na yale machine mabovu.

Nilipiga kazi sana na huyo fund alkua anakuja kwenye hizo machine ana cheka huku anasema umeamua kuchukua machine nyingine huku anssema piga kaz kijana pambana sanaa.

Asubui ilifika saa kumi na mbili nilikabidhi machine kwa operator aliyekuja kunipokea alafu me nikaenda zangu chooni kunawa ili nisubir kad yangu nisepe.

Wakat nasubir kadi nilishangaa naitwa na madamu mmoja hivi kuwa niende kwa in charge nahitajika.Sikuia na wasiwasi wowote nilienda mpk kwenye kiofisi cha in charge.

In charge aliniuliza kama me ndo niliendesha machine fulan nikasemas ndio ila niliziacha kutokana ubovu wake nikaamua kuendesha nyingine.

Kumbe yule fundi alikua ni mnafki mkubwa, yeye ndo alimwambia in charge kuwa niliacha machine nikaenda kulala 😂😂😂😂😂 ...sasa pale idaran ungelala wap na huku makelele ya machine ni 24/7...nilijieleza kuwa niliona machine ni mbovu nikaamua kuchukua nyingine ili lengo langu litimie, lakin in charge alinambia hataki kuniona tena pale ( akawa kanifukuza kazi ) nilimwambia fresh tu nikawa naondoka kutoka idaran.

Lakin kuna madam mmoja hivi alinifuata akanambia nikaombe msamaha hata kama sina kosa.nilimsikiliza yule madamu nikarud tena kwa in charge ili nimuombe msamaha lakin wapi alinitolea lugha chafu sana mbele za watu mok akawa anamuita KK aje anitoe kwa nguvu..

Kwa vile kulikua na makele sana Kk alikua mbali na hakusikia saut ya in charge kwa huo muda.

Nilivyoona in charge hana hata dalili za kunielewa niliamua kwenda tena choon kunawa sasa kipind narud ili nitoke nje in charge aliniona akanambia kwa ukali ngoja ni mnukuu "wee **** c nimekwambia utoke nje huelewei nini wewe nimesema toka nje sitaki kukuona hapa"....nilimwambia dharau aache kusema hivyo napo ikawa ni kosa, alinitukana sana nikaona huyu boya anijui.

Kulikua kuna ndoo ilikua karbu na machine line namba 4 ilikua ni ya rangi zile za machine ya printers...ilikua ni nzito nzito niliichukua nikampiga nayo huyo in charge shavuni mwake, mpk alidondoka chini, ashukuru sana mafund ndo waliwai kunishika.

Nilipelekwa stoo mimi na huyo in charge ( kueleza mashitaka )...tulivyofika huko sikua na mtetez zaid ya yule madamu mpole.in charge alitaka niondoke na nisirud tena pale idaran nikasema poa tu hakuna shida ila nilimwambia dharau me sipendi.

KK alikuja kunitoa nje, kadi yangu huyo in charge aliichana chana ko tulitoka nje na yule KK akawa anasema ndo maisha hayo dogo pia akanambia niende kwa ma HR ilinipatee msaada zaidi.

Kazi kweli nilikua naipenda sana maana nilikua nshaizoea ila ckua na namba niliona niiache tu pengine ckupangiwa kuifanya na Mwenyezi Mungu.

Niliumia sana nikaenda geto nilifika nikamjulisha kwanza sister kuwa nimefukuzwa kaz kisha pia wengine wafuata.

Mzee alinambia nirud musoma haraka nikaish na yule manzi wa karatu.Manz mwenyew nilimwambia kuwa nimefukuzwa kazi itabid arud kwao tu lakin aliktaa alisema hawez kurud kwao.

Sikuondoka mwez huo nilikaa kwanza nikawa na muwinda yule in charge ili nimpige alafu ndo nisepe zangu na ana bahati sana sikumpata kabisa.Nilikua namuwinda pale nje ya geti sema tu ndo walikua wanachelewa kutoka ila ningemshika nilikua namchana na wembe usoni.

Niliamua kuuza baadh ya vitu kwa washkaj zangu vingine niligawa bure na hata kodi ya nyumba ilikua bado haijaisha ko nilimpa jamaa mmoja aimalizie me ilivyofika mwez wa kumi na mbili niliamua kurud musoma.

nitarejea tena.
 
Na app gan ya piano kwenye simu unaikubali na huwa unaitumia zaidi?
Natumia perfect piano kwa ajili ya kupiga piano na ORG 21 kupiga beats sema haina mambo mengi sana tu hua napiga beat kwenye kinanda
 
Hongera kwa kupata mke, nakumbuka mke wangu naye nilimpata kwa staili inayofanana.... Demu alileta bag akakomaa haondoki huku alisisitiza yeye ndio mke Mungu kanipa😅, nikawa mkali nikampa mateso yote aliyashinda🙌
Duh aiseeeeeee
 
Hongera kwa kupata mke, nakumbuka mke wangu naye nilimpata kwa staili inayofanana.... Demu alileta bag akakomaa haondoki huku alisisitiza yeye ndio mke Mungu kanipa[emoji28], nikawa mkali nikampa mateso yote aliyashinda[emoji119]

Kaka bora uishi ndan na mwanamke anaekupenda kuliko asiekupenda alaf ww unampenda ni zaid ya mateso,komaa nae huyo ndio chaguo lako mzee
 
Hongera kwa kupata mke, nakumbuka mke wangu naye nilimpata kwa staili inayofanana.... Demu alileta bag akakomaa haondoki huku alisisitiza yeye ndio mke Mungu kanipa😅, nikawa mkali nikampa mateso yote aliyashinda🙌
hongera pia mkuu...huyu mwanamke wangu nacho mpendea ni heshima aliyonayo kwangu na kwa wazazi.Tayar na ndoto nae ni yeye ndo aje azingue
 
hongera pia mkuu...huyu mwanamke wangu nacho mpendea ni heshima aliyonayo kwangu na kwa wazazi.Tayar na ndoto nae ni yeye ndo aje azingue
Ila maisha ni safar ndefu sana yan wakati uko musoma pamoja na kua na mademu wengi hukubahatisha kumpata wa kukufaa mpaka ulipotimba arusha utakutana na mkaratu

Mpenzi sahihi anakuja kwenye maisha yako pasivo ww kutegemea wala hakuna sababu ya kulazimisha vitu

Hii story ina vitu vingi sana vya kujifunza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…