Hadithi ya kweli ya maisha yangu

Ajali ilikua moja au ajali mbili tofauti? Ukiacha miguu walipata shida nyingine?

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
Poleni asee, ilkua ajal ya familia?
 
Leo tunaanza upya nimeisoma yote kwa siku tatu nalala saa nane usiku ww ulietolewa bikra na jimama leta mambo acha niende kwa kigogo nikaone ana jipya gan
 
Duh wape pole sana wadogo zetu. Mungu ni mwema atawaponya
 
story ya dogo wako kunyuti shule umenikumbusha mbali sana bro πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Aisee.
Mungu awarehemu madogo.
Poleni sana Kwa hii changamoto.
 
Story sasa imekuwa chai

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Inaendelea


Ok ngoja nieleze sasa jinsi nilivyo shikwa kizembe.

Kabla muda wa kuhama hujafika kuna ajali fulani ilitokea ya pikipiki na mtembea miguu.

Boda alikua yuko race vbaya mno sasa alikosa balance akamgonga mtembea kwa miguu wote waliumia ila sio sana.

Huyo boda alikua amepakia ndoo zile za rangi zilikua ziko 16 sasa kipindi watu wamejaa barabarani kuangalia ajali, hizo ndoo zilikua zimeangukia mbali kidogo na majeruhi walipo, me niliziona zinazagaa tu nikaamua nimsaidia hyo boda kuzichukua na kumpa dogo aendee nazo home kuzificha ili tusimpe dereva presha sana ya kuzitafuta.


Na kweli nilizichukua wakat bado watu wakiwa bize kuona majeruhi wanavyotoa damu, nilimpa dogo nikamwambia "kimbia nazo home uzifiche sehemu nzuri"....baada ya tukio kuisha nilienda home nikazihesabu nikakuta zipo 16 nikasema angalau nimepata ka hela ka bundle ( Mb )...siku hyo niliuza kwanza ndoo tatu kwa kila moja sh 3000 nyingine nilipanga kuziua mdogomdogo, kumbe yule bro wangu nae alizipenda hizo zilizobaki akaniibia na yeye, ziliniuma utadhani kama zilikua zangu vile.

Nilijua kuwa yeye ndo aliiba kwa sababu kuna siku alikuja mchana pale home akakaa mpk jioni na ndo siku ndoo zilipotea, nilizikuta kwake nikajua tu ndo zile ndoo zangu.


Basi cku za kuhama ilibaki kama siku tatu muda wa kuhama ufike.Hao wenye nyumba safari hii walidhamilia kabisa kuwa ni must tuhame pale kwao.Mzee wangu sio kwamba alkua hana nyumba laaah....alikua ana nyukba tena kubwa tu sema ni uzembe wake kuimalizia hyo nyumba yake.

Mzee wangu ni member humu Jf najua kama ikitokea akausoma huu uzi ataelewa tu kuwa ni mimi na id yake naijua vizur sana.

Nasema tena Mzee wangu hakujali maisha ya wanawe hata ada kutulipia alitulipia tukiwa form one tu miaka mingine alikua hana habare na sisi yaani tushukuru Ndugu zetu.Kuna kipindi alikopa hela 5 million eti kwa kigezo cha ada za watoto lakn hakuna mtoto ata mmoja alie lipiwa ada ( nilisoma huo mktaba wa mkopo ) hela zilikua zinaishia kwa wapambe na mademu bila kusahau pombe, yaani alikua akitupatia 100k kila mtoto basi imeisha hyo.

Simsemi eti kisa na mchukia no..namkubali kinoma mzee wangu maana kaniokoa sana kwenye misala yangu mimi na familia yangu.Nitaendelea kuelezea vingine mbele ya safari.

Basi Mzee alikua anahangaika kutafuta nyumba ya kuhamia mpk nikawa namuonea huruma, yaan kila sehem amna nyumba.

Siki yenyewe ya kuhama ilivyofika kuna nyumba aliibahatisha ilikua ni nzur sana ina vyumba sita umeme kasoro Maji tu.

Mzee alitupatia maelekezo tu kuwa tukaisafishe ili jioni tuhame yeye alikua yupo misele yake.

Tena siku hyo Baba yake na huyo jamaa ( Mwenye nyumba og ) alikuaja kuhakikisha tuna hama kwake.

Siku hyo nilikua napenda isifike lakin tena nilikua napenda ifike maana nilikuwa nasubir tu tukihama ni mfanyie jamaa ( mtoto wa mwenye nyumba ) kitendo ambacho hata sahau kwenye maisha yake.

Niliindaa kisu vizur tu nikakificha chini ya godoro ilikua ni nife au afe ( lengo langu ni ilikua zile nguo ambazo alizichukua kuwa ni zake, nilikua nataka anipe au nimue )


Baada ya kutoka kusafisha ile nyumba mpya basi tulirud home kuanza kukusanya vitu ili jioni gari likja tupakie tusepe zetu.

Huyo jamaa alikua bado yeye yupo kazini kwake ko pale alikuepo huyo baba ake na wale wanae wengine walikuepo pale.Yule demu nilie kuwa na mgonga yeye alikua tu anasikitika sisi kuonda lakin lile li bonge lenyewe lina roho mbaya tu.

Jioni ilifika kwenye saa kumi na moja gari lilifika tukaanza kupakia vitu, wakati huo na msubir yule jamaaa atoke kazini aje nimzingue.Tulipakia vitu gari ilienda trip mbili ikawa imebakiza trp moja imalizie kusomba vitu.Huyo jamaa na kweli alitokea, nikawaambia madogo hili bifu ni langu pekee sitaki kuwaona mkiingilia.

Sijui hata nilikua na mdudu gani kichwani na bangi nilisha stafu kuvuta kitambo.Nilichukua kile kisu nikakiweka kiuononi, nikawa na msubir tu huyo jamaa aingie ndani nimtoke kwa nyuma nimzingue.

kama nilivyopanga utadhani movie vile [emoji23][emoji23] jamaa alitupita pale akatupa hi alafu akaelekea ndani.Nilikua natetemeka sio kawaida, nilimvizia kwa nyuma mpaka alivyofika korido nikamuwai shingoni kwa roba kali mpk tukadondoka...lakini sikumuachia nilikua na mwambia tu nguo zangu unanipa au hunipi wakati huo kisu kiko shingoni mwake jamaa alipiga kelele ( jamaa licha ya ukubwa wake lkn ni muoga hatare )...lile bonge mdo lilikua la kwanza kufika hapo korido lili ni nyang'anya kisu kwanza lkn shingo ya yule jamaa nilikua bado nimeikaba kisawasawa.

Alikuja na huyo Mzee wake walinivuta huku huyo bonge akinipa mingumi ili ni muachie, nilimuacha baada ya ngumi ya pua kuuma ( ngumi ya puani inauma jamaani [emoji23][emoji23][emoji23] mpk chozi lilitoka jicho moja )..bonge ndo alinipandisha hasira nilimfuata nikampa ngumi na yeye za puani mpk ikaangua kwenye cement zilikua hapo korido.Jamaa nae alikuja na kile kisu nikamuwai teke la mguu alianguka na nikashika kisu sasa kumchoma yule bonge maana ndo alikua ana kiherehere sana.

Nashindwa kuelezea kiukweli maana jamaa niliwamudu sema yule bab ao alinipiga makofi mpk akili ilikaa sawa wakanishika wakapeleka chumbani mwao yule demu eti nae akawa ananitukana, na nilikua nime taitiwa kisawasawa jamaa alipiga simu police.

Kwanza alikuja jamaa mmoja akasema waniachie alitoa kitambulisho kunionesha eti kuwa ni police, nilimpa na yeye ngumi nika mgeukia tena bonge, huyo police alinipiga vibaya mpk nikakaa chini mwenyewe.akanambia nianze kutoa maelezo.nilisema jamaa ana nguo zangu me namuomba yeye anazingua kunipa.

Mzee wao akasema kabla nguo hazijaja ( maana zilikuepo mulemule ndani ) mwenyekiti wa mtaa aitwe ili maelezo yaende vizur.Mwenyekiti alikuja kwanza hakuamin kukuta eti ni mimi ndo niko pale ( anajua me ni mstarabu ). Basi huyo kamaa na yeye alitoa maelezo yake kuanzia hela zske kupotea mpk nguo, aliita mpk mtu ambae anamuuzia nguo na risiti juu.

Sema kama kitu sio chako inaonekana sio chako kesho narud kuendelea.
 
[emoji23] Ngumi za pua na usoni tu kiujumla sio poa.. Ukipigwa kisawa sawa ikaingia unaweza kuuliza watu "Hivi nimejifungua mtoto gani? Wakati huo wewe ni mwanaume"

Halafu kuna boya from no where tu linasema eti mapenzi yanauma.. Hivi ushawahi kula ngumi ya uso, unaweza kusahau hata jinsia yako kwa muda

[emoji125][emoji125][emoji125]
 
🀣🀣🀣 aisee acha tu yaani pua linauma aisee kuliko mapenzi ubongo nilihisi umekuja puani
 
kwanini mkuu lbda nilichanganya tu siwez kutoa story ya uongo c unajua kwenye uandish kuchanganya hua sio ajabu.

sorry kwa hilo mkuu
Nimekukumbusha mkuu toka mwanzo tuko na hili story ila kutoka hapo kwa mtu aliyekuwa anafuatilia maudhui yote yamepotea

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
kwanini mkuu lbda nilichanganya tu siwez kutoa story ya uongo c unajua kwenye uandish kuchanganya hua sio ajabu.

sorry kwa hilo mkuu
Hata hivyo unajitahidi kukumbuka matukio yote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…