Hadithi ya kweli ya maisha yangu

Daaaaah....uchawi mbaya sn nimejitahidi kupita kimya kimya nikashindwa nikasema ngoja nidondoshe hizo thanks (likes) tu ila bado kanafsi kakawa kananisuta nipunguze uchawi imenibidi tu niandike. Itoshe tu kusema mkuu umeshindikana
 
kwa sisi tuliokulia dar es salaam uswahilini, tandale, manzese, keko, mwananyama, mbagala, mabibo, nk nimeshuhudia matukio ila wewe ulikuwa kiboko mkuu
 
Dadeq ........ww jamaa ni mafia[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mzee endeleeaa
 
Nilitaka kupita kimya kimya bila comment, hii episode imefanya nicheke sana maana hiyo ngumi ya pua ni shida. Umenikumbusha mbali sana ha ha..

Ila jamaa ulikua na matukio sio mchezo,,eti mnasemaje sasa,, hajakaa sawa ngumi [emoji109] ya pua.. anyway story nzuri sana.
 
Inaendelea

Samahani sana kwa kuchelewa kupost...tanesco sio watu.


Tuendeleee....


Baada ya kuwa tunakosa hela kwa yule jamaa pindi tukiingia kuzisaka ilibidi tuhamie kwenye nguo zake, jamaa alikua na nguo nyingi alafu mpya mpya vi kadeti,staff jeans na vishat vizur vizur...

Nilikua nikiviiba tu naenda kuviuza chapu kwa wadau wangu.bro wangu ( mtoto wa bamkubwa ) ndo alikua muda mwingine ananitafutia wateja.

Kuna fundi fulani hivi alitaka kunidhurumu hela ya nguo nilizomuuzia nilimuashia moto kazini kwake hatokuja kusahau..

Kuna siku moja Jamaa angu mmoja hivi Baba ake alikua ataka kuoa ( kwa sherehe ya harusi ).sasa huyo jamaa angu Baba ake alimpa tenda kuwa atafute vijana Watatu kwa ajili ya kulinda Eneo ambalo sherehe ilitakiwa kufanyika ( Ukumbi mmoja unaitwa Eva Green upo karibia na Tembo beach )...tulipatikana mimi na washkaj zangu wawili mmoja ni yule rafiki angu tuliyekuwa tunauza nae dawa visiwani.

Jumla tulikua tunao linda ni wanne, yule jamaa ambae baba ndo mwenye shughuli na sisi watatu.

Huyo mzee alituahidi kutulipa 30k kila mtu baada ya sherehe kuisha..tuliikubali hyo tenda chapu na tulitakiwa tulinde kwa siku nne, ilikua ni pamoja na kufanya usafi kwenye huo ukumbi.

Sehemu niliyokua naishi mimi ni mbali na hao washkaji zangu ko ilikua ikifika saa nne usiku walikua wananipitia home na gari ( Bwana harusi ndo alikua ni dereva ).

Siku ya jumamosi usikusasa nyumban kwa Bwana harusi kulikua na Muziki ( mkesha japokua ni wasabato ila walifanya kibishi ).siku hyo hawakuja kunipitia home ilibid mimi ndo niwafuate huko kwenye mkesha wa harusi.

Yule Manzi angu nae ni jirani na huyo mshkaji wangu ( baba ake anae oa ) basi nilivyofika kwenye mkesha nilimuona manz angu kakaa nje kwao nikamuita kumuomba papa akanibania eti yupo mwezini alitaka nimshike ni hakikishe me nikapotezea.


Tulikaa kwenye mkesha mpaka kwenye saa sita hivi tukaondoka kuelekea Lindoni.kwa vile tulikua wengi tuliamua kutembea miguu.Wale washkaji wangu ni waoga ila wana mikwara hatari usiombe waanzishe ugomvi wewe upo utapigana pekee yako.

Tulipitia ile barabara ya kwa Mkuu wa Mkoa..tulipofika hapo sasa kwa mkuu wa mkoa tulisimamishwa na fenda imejaa mapolisi walio kuwa Doria...walituuliza " Mnatoka wapi na mna kwenda wapi"...wale jamaa zangu ni waoga ( japokua me nae muoga lkn hao ni balaa )..nilimjibu yule afande alie uliza swali kuwa "Tunatoka road na kwenda Tembo"..walisema kufanya nini nikawaambia kuwa sisi tunalinda ukumbi walitwambia tu "Usiku huu kuweni makini" kisha wakasepa.

Jirani na hapo kwa mkuu wa mkoa kuna Ukumbi mmoja unaitwa Musoma club.Siku hyo kulikua na harusi hapo.Maafande walivyo sepa zao tukaamua kuingia kwanza hapo kwenye harusi kuiba vinywaji ( me nilkua na begi alafu nilikua nimevaa kihuni kishenzi ).tukifika kwenye harusi tulikuta ndo inaisha vinywaji havikua vingi sana tukatoka.tukaamua kuitafuta harusi moja ilikua inasikika tu kwa mbali.Tuliifatilia mpaka kuipata, kumbe ilikua iko pale Ukumbi wa Dayosisi jirani na Tanesco.

Kuingia ilikua tabu maana mlinz aligoma tusiingie ndani mpk tumuonyeshe kadi.tulileta noma pale mlangoni mpk mlinzi akaturuhusu mwenyewe kuingia.Tulivyofika ndani sasa tulikuta napo harusi ndo inaelekea kuisha ila watu walikua wana serebuka na muziki alafu mezan kuna vinywaji tulianza kupita navyo tukiviweka kwenye begi langu...tamu zangu zilikuja mara baada kumuona Mama alikua anaweka vinywaji kwenye mkoba ( vinywaji vilikua vipo chini ko alikua amekaa na muda mwingi aliutumia kuangalia chini badala ya kuangalia mbele.


Mezani niliona simu nikasema hik lazima nichkue nisepe nayo bila rafiki zangu kujua.wakati yule mama anaendelea na zoezi lake la kuweka vinywaji kwenye mkoba wake..nilipitia ile simu ya yule Mama nikatoka nayo nje ya ukumbi spidi kama vile sio mimi.

Niliondoka eneo lile na kukimbia kuelekea Line Police...nilitoa betri kwenye ile simu ( tecno smart phone L6) pamoja na kutupa line zilikua kwenye simu.

Niliamua kuelekea Lindo kuwa subiri wale washkaj waje wanipe habari, walivyo kuja hata hawakujua kuwa me nimepiga tukio.

Kesho yake ilifika siku ya harusi tulienda kujiandaa kwa ajili ya kutoa huduma ya uimbaji ( Maana wote tulikua ni waimbaji wa choir )...baadae sana ndo niliwaambia kuwa siku ile niliiba kisimu cha tecno nikawaonyesha.Walitaka niuze alafu tugawane hela wote. kuna fundi simu ndo nilimuuzia bei ya kutupa tu 70k nikawagawia 30k wale jamaa na mi nikabak na 40k ya bure bure.

Nitaendelea tena kesho.
 
Umenikumbusha tecno l6 kangu kalikua kanakaa na chaji balaa hadi siku 3-5 kinachaji tu
 
Nakufatilia sana wewe jamaa inabidi tukulete NJIA PANDA na Dokta Issac marlaw CLOUDS story yako itabamba ile mbaya
 
Wewe ulikuwa ni mwizi sugu bila shaka utakuwa unaendelea na wizi ila kimya kimya mngetembelea mitaa nilipokuwa naishi na hakika sasa hivi ungekuwa kuzimu una busu miguu ya shetani..
Hahhahahhaah,usijivune bro huenda ungefanywa mbaya tu vilevile
 
Inaendelea


Harakati za kuiba na Kusali ziliendelea kama kawaida...kuna kipindi nilichalala vibaya mno nikawa nawaza napataje pesa sasa...sikumbuki ilikua ni juma ngapi? ila ilikua ni September.....niliamua kwenda mitaa fulani hivi lbd nitakutana zari huko njiani lakini hakukua na zari la maana nililokutana nalo...niliudhika sana nikawa narud home, mara nikakutana na wale wanaonunua vyuma chakavu, walikua ni wababa wawili wako na baiskeli wana piga promo biashara yao "* tunanunua vyuma chakavu..tunanunua vyuma chakavu*"..basi nikawaita waje ( home kulikua kuna bomba flani hivi refu la chuma la yule yule Jamaa nae mwibia ).....niliwaambia nina mali kama vipi twendeni mkaione tupande bei....wakakubali tukaanza safari kwenda home, kufika nikawaonyesha mzigo ulikua tu hapo nje...


Hao wanunua vyuma waliliona ila wakasema kuwa hilo chuma ni refu sana na wao hawajatembea na msumeno wa kukatia ko labda waende kuchukua msumeno ndo warudi...ilikua mida ya saa saba kuelekea saa nane...niliwaza sasa hawa waje waende tena warudi c kushikwa nitakua nimeshikwa na jamaa kama akirudi ghafla...

Niliwaza nikakumbuka kuwa mle chumbani kwa yule jamaa huwa kuna machuma matatu yapo kwenye kabati la ukutani...nilisema yes hayo ndo nachukua moja nawapa hao wakuda.

Yalikua ni machuma yale ya kwenye Mashine za ku pampu maji ziwani....niliwaza hapa nitakua na 40k kuendelea...hilo chuma ni zito mtu mmoja hulibebi..

Niliwaambia wale wakuda wanisubir niwaletee mali, nikaangia chumban kwa jamaa na gunia ili nilibebe lakin lilinishinda..nikawaita madogo wanisaidie, yule ambae sio mwizi alkua ana shangaa ana leta usabato wake pale eti kuwa mnachokifanya sio kizur...nilimwambia tu hela ninazokupa unafikir hua zinatoka wapi?..ila alisema sio poa ninayo fanya, siku mjali nilimwambia beba mzigo.

Kwenye ile harakati ya kunyanyua lile chuma maana tulikua tumeshalitoa kabatini, lilituteleza tukiwa tumelinyanyua bahati mbaya likatua kwenye mguu wangu wa kulia. hayo maumivu yasikie tu kwa jirani, nilivumilia kiume tukalitoa hivyo hivyo kibishi mpaka nje kwa wale wakuda ( nawaita wakuda kwa sababu ni Wakuda kweli )... tulivyolifikisha wakaliangalia mmoja akacheka na kusema eti hili ni chuma DONGO [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]...( hivi kweli kuna chuma dongo )...nilishangaa kusika chuma * dongo* ndo chuma gani hilo.

Walisema hua hayana thamani yale na walivyoniua nguvu ni baada ya kulipima wakakuta ni kg 33 [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] aisee kuna vitu vinafurahisha...niliwaambia kuwa hawako serious na kazi za watu yaani chuma tuna beba watu watatu tena kwa shida eti liwe kg 33.walitoa 6k kunipa eti ndo lina thamani ya bei hyo...niliwaangalia vbya wakati huo nasikilizia maumivu ya mguu, niliwaambia madogo tulibebe tulirudishe ndani...lakin hao wakuda waliniuliza " unataka sh ngap dogo tukupe "...niliwaambia 50k wakasema hilo chuma halina thamani lbda tukupe 20k...niliona hawa wakuda ni matapeli tu hawako serious tulilibeba chuma kurudisha ndani.

Wakuda wakaanza ku toa matusi eti nimewapotezea muda wao...tulivyo rudisha chuma ndani ilibidi niwarudie hao wakuda ili wanitukane vizur niwasikie.Nilikua nimekaa kwenye ngazi za mlangoni nasikiliza tu matusi yao...mdogo wangu wa kike alikua ndo anatoka shule muda huo ko alikuta hako ka mzozo.

Niliona wavuka mipaka sasa na matusi yao nilimwambia huyo dogo langu aingie chumban kwangu aniletee kilichopo chini ya Uvungu ( alikua anakijua nachokitaka )....alikuja na Panga ( lile lile ambalo mzee alitaka kumkata nalo Mama 2013 )..nililipokea nikawafuata hao wakuda japo na maumivu ya mguu lkn nilikua siyasikii sana.

Walivyoona hivyo walibaa na huku ni wakubwa kwangu walishindwa cha kufanya, niliwafuata nikiwa nime kunjia sura sicheki wala nini..mbona walilala mbele wakaacha baiskeli yao na kilo yao [emoji23][emoji23][emoji23] na ningewapiga bapa sema walikimbia.


Nilichukua baiskeli nikawatupia na ka kilo kao nikawaambia wasepe kabla sijawaua ( nilikua sitaki waendelee kubaki pale maana kama yule jamaa angetokea ingekuwa shida kwangu ).

Wakuda walisepa madogo wakabak wanacheka tu huku wakinambia "holy holm we ni nyokoo ".

Nilirudi chumban kwa yule jamaa hata nijipooze na ka kinywaji ( vilikua kwenye fridge yake ) nilichukua Alvaro mbili moja nikampa dogo langu wa kike na moja nikanywa, pia nilikuta vi Apple nikachukua kamoja ile namkatia dogo langu Kisu kilikua ni kikali kisenge kikapita na mimi kwenye kidole cha mkono wa kushoto, maumivu ya kidole na mguu yasikie tu....nilijiaulumu kwann nimefanya kile kitendo nilimuomba Mungu anisamehe tu.

Niliuguuza majeraha yangu tena nilichoma sindano ya tetenasi kabisa...mambo yalizidi kwenda na siku zangu zilikua zinahesabika kwa kweli.

Nitarudi tena kuendelea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…