"wala mawazo yako tu mamy!" nilimjibu nikielekea moja kwa moja mpaka chumbani kwangu, mwanamama huyo akanitazama tu nilipokuwa naondoka, nilipofika chumbani kwangu nikaanza kupanga panga nguo zangu kwenye begi tayari ili nikirudi kwa mwanamama Hawa kule kwenye nyumba ya wageni nikae kae kidogo
"unaenda wapi kwani Frank?" mwanamama Penina aliniuliza akiwa amesimama mlangoni amenikuta
"nategemea kusafiri mda wowote kuanzia leo jioni!"
"unaenda wapi?" mwanamama huyo alinifuata na kunisukuma nikakaa kitako kisha nae akanikalia mapajani
"nitakuambia mamy rafiki yangu amepatwa na msiba wa baba yake ameniomba nimsindikize!"
"basi kabla hujaondoka nifanyie kitu basi moyo wangu ufurahi"
"baba yupo wapi?"
"ametoka sijui kaenda kutazama mpira sijui kufanyaje!"
"mh nikirudi, ni siku mbili tatu tu" nilizidi kumdanganya
"mbona nasikia mazungumzo huku, Frank umerudi saa ngapi na ulikuwa wapi ukashindwa kuaga?" baba aliufungua mlango wa chumba changu huku akiongea na kushtuka alipomkuta mwanamke wake akiwa amenikalia, nimempakata mapajani.....
Baba aliingia na kutukuta chumbani nikiwa nimempakata mchepuko wake huyo mapajani, tukibebishana, mzee wangu huyo hakuamini macho yake akabaki ametoa macho tu, mwanamama Penina akasimama haraka haraka akijishtukia
"ndo kinachoendelea humu hiki?" baba aliongea kwa hasira huku akiingia na kuurudisha mlango
"jamani mme wangu?" Mwanamama Penina alibaki akijikuna kuna na kujing'ata ng'ata vidole vyake kwa wasiwasi
"Frank unatembea na mama yako humu humu ndani kwangu, mwanamke wangu mimi unataka laana yangu saa hizi?"
"huyu siyo mama yangu mbona mama umemwacha nyumbani baba..."
"Frank nyamaza!" mwanamama Penina alijaribu kuninyamazisha
"hapana lazima nimwambie ukweli huyu mzee anachokifanya siyo"
"toka nyumbani kwangu tokaa!!"
"usimfanyie hivyo ni mtoto wako huyu jamani" mwanamama Penina alijaribu kumshika baba
"niache nawewe mpumbavu!" baba akamsukuma mwanamama huyo akaangukia kitandani mzima mzima
"naenda mzee usijali!" nilimjibu nikivaa begi langu taratibu na kumpita baba aliyekuwa amenikata jicho huku nikimuaga mwanamke wake huyo, mama wa kambo asiye rasmi, na baba akiwa na hasira akanifuata nyuma nyuma
"Frank!" akaniita tena
"naam" nikamgeukia kumtazama
"usimwambie mama yako sahau tu yote rudi tu ukae hapa!"
"hapana mzee mimi naenda zangu!" nilimjibu nikitoka taratibu ndani ya nyumba hiyo, sikuwa na wasiwasi tena maana sasa nina pesa ingawa sijazishika mkononi lakini zipo nina uhakika, kwa mwanamama Hawa, nilitoka nikichukua boda boda kutaka kurudi kule kule kwenye nyumba ya wageni niliyomwacha mwanamama Hawa na ndipo simu yangu ikaota kutazama alikuwa mwanamama huyo
"Frank mbona unachelewa uko wapi?" aliniuliza
"nachelewa tena jamani wakati nilikwambia narudi jioni mammy ila nimeshakumisi nipo njiani!"
"ila usije kwenye gesti ile njoo kwenye hoteli hii huku ya (...)" alinitajia jina
"hotelini tena jamani mamy?"
"ndiyo pesa si ipo wewe una shida gani kwani?"
"hamna sawa nakuja!"
Boda boda ilinifikisha mpaka mbele ya hoteli hiyo nzuri nikashuka na kumlipa dereva boda boda pesa yake wakati huohuo meseji ikaingia kwenye simu yangu mwanamama Hawa akinionyesha namba ya chumba na ghorofa ya ngapi kinapopatikana kwenye hoteli hiyo ya ghorofa zaidi ya kumi iliyopo mjini kabisa na maarufu, nikaingia mpaka kwenye lifti ya kunipeleka ghorofa ya juu kabisa nilipofika nikakitafuta chumba kwa namba yake kama alivyonielekeza kwa njia ya meseji, nilipofika kwenye mlango wa chumba husika nikakuta umerudishwa tu wala haujafungwa kabisa nikausukuma na kuzama ndani nikakutana na mishumaa myekundu kila kona ya chumba hicho cha hoteli na maua yamemwagwa yametapakaa chini kila sehemu lakini mwanamama Hawa sikumuona
"mamy mamy!!" nilimwita nikitazama tazama kulia na kushoto mpaka nikafungua chumba cha bafuni lakini sikumuona badala yake nililiona tu beseni kubwa la kuogea lenye maji yenye povu jingi likiwa halina mtu ndani yake, mara mkono ukanigusa begani nikashtuka na kugeuka na kumwona mwanamama hawa akiwa anatabasamu siyo yule wa