Hadithi ya kusisimua- Mimba ya Jini

hadith yako ni nzur bg like!
 
Attachments

  • 1389061980472.jpg
    1389061980472.jpg
    59.3 KB · Views: 1,076
Hadithi ya kusisimuwa mimba ya jini-19-

ILIPOISHIA:

Niliyokuelekeza kama mkeo atajua basi mimi navunja mapenzi na wewe."

"Shehna sitaki kukupoteza," Mustafa alichanganywa na uzuri wa Shehna.

"Basi fanya hivyo."

"Nitafanya kwa ajili nakupenda."

Shehna alifurahi na kwenda kumkumbatia Mustafa na kumpiga mabusu.

SASA ENDELEA…

"Katika siku uliyonifurahisha leo imezidi siku zote, Mustafa ukizaa na mimi nitakupa zawadi kubwa ambayo hukuwahi kuiota maishani mwako."
"Nitashukuru."
"Kingine ulichonifurahisha kutengeneza uongo kwa mkeo juu yangu, imenifanya nizidi kukupenda."
"Lazima nifanye hivyo wewe ni mtu muhimu sana kwangu."
"Basi acha nikuache uendelee na kazi tutaonana usiku."

"Hakuna tatizo."
Shehna aliaga na kuondoka na kumuacha Mustafa akiendelea na kazi, baada ya muda Mustafa alitoka kufuata kitu kwenye gari. Alipofika mapokezi alishangaa kukuta rafiki yake kipenzi James akimsubiri.
"Ooh! James umefika zamani?"
"Kama nusu saa nimeambiwa una mgeni."

"Mbona ametoka muda mrefu."
"Bosi ametoka kapitia wapi?" Sara aliuliza.
"Jamani si hapa au ulipitiwa na usingizi?"
"Hatujamuona mtu, mgeni mwenyewe labda jini?"

Sara alisema jina ambalo siku zote lilikaa mdomoni kwake na kumchefua sana Shehna na kupanga kumkomesha na tabia yake ya kumwita jini. Alipanga usiku kabla ya kwenda kwa Mustafa aanzie kwa Sara ili kumkomesha aachane na kufuatilia mambo yake.
"Sara sitaki tena kusikia ukitamka jina hilo, siku hizi umenizoea sana eti eeh? Unasema lolote mdomoni mwako," Mustafa alimfokea Sara ilikuwa ni mara ya kwanza kukasirika toka aanze naye kazi miaka saba iliyopita.

"Samahani sana bosi," Sara alishtuka huku woga ukimtawala.
"Katika siku uliyoniudhi leo umeniudhi sana, una bahati nina mgeni ningekufukuza kazi sasa hivi," Mustafa alisema kwa hasira mpaka povu likamtoka mdomoni.
"Bosi nisamehe, nilisema kwa utani sikujua kama nitakuudhi kiasi hiki," Sara alijitetea.
"Nitamalizana na wewe baadaye ngoja nizungumze kwanza na mgeni wangu."

"Kwani tatizo nini mpaka ukwazike hivyo?" James aliuliza.
"James, tuzungumze yetu huyu nitamalizana naye."
James ilibidi anyamaze kwa vile hakujua chanzo cha Mustafa kukasirika vile kilitokana na nini, siku zote alimjua ni mkimya na mpole. Waliingia ofisini huku Mustafa akiwa bado ana hasira, kabla ya kuzungumza aliinama kwa muda kuonesha Sara amemuudhi sana.

"Kwani best kipi kimekukwaza hivyo?"
"U...u...u na..," Musfata alinyamaza baada ya simu yake kuita, alipoangalia aliiona inatoka kwa Shehna aliipokea.
"Haloo."
"Mustafa."
"Naam."
"Mbona kama haupo sawa?"

"Kwa nini?"
"Sauti yako inajieleza."
"Si huyu mshenzi leo atanitambua namfukuza kazi."
"Kwa nini?"
"Sikufurahia alivyokuita."
"Ananiitaje?" Shehna alijifanya hajui kitu.

"Eti anakufananisha na jini."
"Hapana mpenzi usimfukuze kazi."
"Kwa nini?"
"Ameropoka kwa bahati mbaya, sitaki mimi kuwa na wewe tuongeze maadui."
"Kwa hiyo?"
"Mpe onyo tu, hawezi kurudia."
"Ana bahati bila wewe ningemfukuza kazi sasa hivi."

"Msamehe kuanzia sasa fungua moyo wako zungumza na mgeni kwa uchangamfu."
"Sawa nitafanya hivyo."
"Naomba ucheke kidogo basi," Shehna alisema kwa sauti tamu iliyofanya Mustafa acheke.
"Haya mpenzi wangu kazi njema."
"Asante nawe siku njema."

Wakati huo Sara alikuwa kwenye hali mbaya kwa kujua siku ile ndiyo ya kufukuzwa, kazi ilimshinda, mapigo ya moyo yalimwenda mbio. Alijiinamia kwenye meza huku mkono mmoja ukiwa kifuani kuzuia mapigo ya moyo yaliyokuwa yakienda kwa kasi. Mustafa baada ya kuzungumza na mgeni wake alitoka kumsindikiza, alishangaa kumkuta Sara akiwa amejiinamia huku akilia kilio cha kwikwi.
"Sara una nini?"
"Sina kitu, nitafanya nini nawe hutaki kunisamehe?"
"Yale yameisha ila siku nyingine kuwa makini na kauli zako kwa wageni wangu hasa Shehna."
"A...a...sante bosi sirudii tena," Sara alitaka kumshika miguu, lakini Mustafa alimuwahi kumshika na kumnyanyua juu.

Itaendelea Kesho wakati kama huu....
 
Hadithi ya kusisimuwa mimba ya jini-20-

ILIPOISHIA JANA USIKU :
"A..a..sante bosi sirudii tena," Sara alitaka kumshika miguu, lakini Mustafa alimuwahi kumshika na kumnyanyua juu.
ENDELEA..

Majira ya usiku Mustafa alikumbuka maelekezo aliyopewa na Shehna, alimuacha mkewe atangulie kitandani na yeye kubaki sebuleni akijifanya kuwa bize na lap top yake. Mkewe alimshangaa mumewe siku ile kuwa bize vile wakati alimwambia hawezi kufanya kazi za ofisini akishafika nyumbani.

Baada ya kumsubiri mumewe kitandani kwa hamu kubwa, alishangaa kuona haji. Alitoka hadi sebuleni na kumkuta akijifanya yupo bize la Laptop yake.
"Mume wangu imeanza lini muda wa kulala uanze kazi?"
"Kuna kazi nilitakiwa lazima niifanye baada ya kufika, lakini nilisahau siwezi kulala bila kuifanya ili asubuhi nikifika kazini nifanye kazi nyingine," Mustafa alitengeneza uongo.
"Lakini si ni wewe uliyesema baada ya kazi ni nafasi yangu?" Husna alimuuliza mumewe huku amemkazia macho.
"Ni kweli mke wangu, lakini hii imetokea dharura."
"Mmh! Sawa, sasa mimi nina hamu na wewe itakuwaje?"
Kauli ile ilimchanganya sana Mustafa na kujiuliza itakuwaje kama mkewe atatangulia kukutana naye kimwili kabla ya Shehna, wakati alielezwa kukutana na mkewe mpaka mwezi upite. Alipata wazo la kumwambia asubiri ili avute muda wa kumfanya mkewe apitiwe na usingizi.
"Mke wangu hebu nivumilie kwa muda huu."
"Mmh! Sawa lakini kumbuka nilijiandaa leo kwa ajili yako."
"Najua mke wangu, kuwa na subra namalizia nakuja sasa hivi."
"Basi na mimi nitakaa hapa nikusubiri mpaka akimaliza tutakale," Husna alisema huku akikaa kwenye kochi.
"Mke wangu imeanza lini kulindana kama kibaka na polisi?"
"Yaani leo sijijui, natamani tukae pamoja mpaka umalize kufanya kazi zako, kitanda leo nimekiona kichungu bila wewe mume wangu."
"Mmh! Sawa," Mustafa alikubali kwa shingo upande.
Mkewe alijilaza kwenye kochi na kutazama mumewe aliyekuwa akijifanya yupo bize huku kichwa kikimuwanga kutokana mkewe kuonekana kama anajua nini kinatakiwa kufanyika. Muda ulikatika bila mkewe kuonesha dalili za kulala, alijiuliza atafanyaje ili mkewe alale na Shehna aje ndani.
Alipoangalia saa ya ukutani ndiyo ulikuwa saa sita kasoro za usiku,alijikuta alikosa raha kabisa. Alijikuta akitamani kulala kwani na yeye kichwa kilianza kuwa kizito kwa usingizi. Wakati akiwaka yale mkewe macho yalikuwa makavu hakuonesha dalili zozote za kulala huku macho yakiwa kwenye Runinga.
Alijifanya kutoka nje kumtazama Shehna kama atakuja ili amuwahi na kumueleza kuwa siku ile hali ilikuwa mbaya wafanye kesho japokuwa alijua atakuwa amemuharibia dozi. Aliamini zoezi alilolitaka Shehna alilikuwa ngumu kutekelezeka hasa kulifanyia nyumbani kwake chumbani kwake na kitandani anapolala na mkewe na mkewe akiwepo kilikuwa kitu kisichowezekana kwa akili ya kawaida.
Aliifunga Laptop yake na kunyanyuka huku akijinyoosha kidogo na kumfanya mkewe aseme.
"Dah! Afadhali umemaliza yaani leo hata sijielewi jinsi nilivyo na hamu na wewe imekuwa kama siku ya fungate," Husna alisema huku akijiweka vizuri kwenye kochi ili anyanyuke.
"Nakuja," Mustafa alisema huku akielekea nje.
"Usiku wote huu unakwenda nje kufanya nini?"
"Mke wangu maswali gani hayo?" Mustafa alisema kwa ukali kidogo.
"Mume wangu kukuuliza ni ubaya gani mimi mkeo nina haki ya kukuuliza chochote."
"Nakuja," Mustafa alisema huku akifungua mlango na kutoka nje na kumuacha mkewe akirudi kujilaza kwenye kochi kumsubiri mumewe.
Mustafa siku ile alimshangaa mkewe kuwa vile na kujiuliza labda amejua nini kinaendelea usiku ule. Alitoka nje kwa kuamini lazima kwa muda ule Shehna atakuwa amefika nje.
Wakati akiwaza hayo Shehna alikuwa amefika muda mrefu, aliyaona yote yaliyokuwa yakitendeka na jinsi Mustafa alivyokuwa akiteseka kwa jinsi mkewe alivyogoma kwenda kulala na jinsi ya kuyashinda masharti ya kukutana kimwili na mkewe ambaye siku ile alionesha kumtaka sana.
Alijifikiria jinsi ya kumsaidia Mustafa kwa kumfanya mkewe alale kwa hiyari yake bila kulazimishwa. Shehna alifurahi baada ya kumuona Mustafa akitoka nje alijua ametoka kumtafuta ili kumpa hali halisi ya ndani. Alimuacha atoke nje kisha alimsogelea Husna mke wa Mustafa na kumpuliza usoni na kukaa pembeni.
Husna alijikuta akisikia usingizi mkali bila kujielewa usingizi mzito ulimpitia. Mustafa baada ya kumtafuta Shehna kwa kuzunguka nyumba bila kumuona, alisogea mpaka mbele ya nyumba labda yupo barabarani lakini hakumuona. Baada ya kutomuona alisimama kwa muda kujiuliza atafanyaje ikiwa muda umekwenda na lazima akapande kitandani na ilikuwa lazima ampe mkewe haki yake ya ndoa kwa vile hakuwa na sababu ya kumnyima.

Itaendelea kesho wakati kama huu....
 
Hadithi ya kusisimuwa mimba ya jini-20-

ILIPOISHIA JANA USIKU :
“A..a..sante bosi sirudii tena,” Sara alitaka kumshika miguu, lakini Mustafa alimuwahi kumshika na kumnyanyua juu.
ENDELEA..

Majira ya usiku Mustafa alikumbuka maelekezo aliyopewa na Shehna, alimuacha mkewe atangulie kitandani na yeye kubaki sebuleni akijifanya kuwa bize na lap top yake. Mkewe alimshangaa mumewe siku ile kuwa bize vile wakati alimwambia hawezi kufanya kazi za ofisini akishafika nyumbani.

Baada ya kumsubiri mumewe kitandani kwa hamu kubwa, alishangaa kuona haji. Alitoka hadi sebuleni na kumkuta akijifanya yupo bize la Laptop yake.
“Mume wangu imeanza lini muda wa kulala uanze kazi?”
“Kuna kazi nilitakiwa lazima niifanye baada ya kufika, lakini nilisahau siwezi kulala bila kuifanya ili asubuhi nikifika kazini nifanye kazi nyingine,” Mustafa alitengeneza uongo.
“Lakini si ni wewe uliyesema baada ya kazi ni nafasi yangu?” Husna alimuuliza mumewe huku amemkazia macho.
“Ni kweli mke wangu, lakini hii imetokea dharura.”
“Mmh! Sawa, sasa mimi nina hamu na wewe itakuwaje?”
Kauli ile ilimchanganya sana Mustafa na kujiuliza itakuwaje kama mkewe atatangulia kukutana naye kimwili kabla ya Shehna, wakati alielezwa kukutana na mkewe mpaka mwezi upite. Alipata wazo la kumwambia asubiri ili avute muda wa kumfanya mkewe apitiwe na usingizi.
“Mke wangu hebu nivumilie kwa muda huu.”
“Mmh! Sawa lakini kumbuka nilijiandaa leo kwa ajili yako.”
“Najua mke wangu, kuwa na subra namalizia nakuja sasa hivi.”
“Basi na mimi nitakaa hapa nikusubiri mpaka akimaliza tutakale,” Husna alisema huku akikaa kwenye kochi.
“Mke wangu imeanza lini kulindana kama kibaka na polisi?”
“Yaani leo sijijui, natamani tukae pamoja mpaka umalize kufanya kazi zako, kitanda leo nimekiona kichungu bila wewe mume wangu.”
“Mmh! Sawa,” Mustafa alikubali kwa shingo upande.
Mkewe alijilaza kwenye kochi na kutazama mumewe aliyekuwa akijifanya yupo bize huku kichwa kikimuwanga kutokana mkewe kuonekana kama anajua nini kinatakiwa kufanyika. Muda ulikatika bila mkewe kuonesha dalili za kulala, alijiuliza atafanyaje ili mkewe alale na Shehna aje ndani.
Alipoangalia saa ya ukutani ndiyo ulikuwa saa sita kasoro za usiku,alijikuta alikosa raha kabisa. Alijikuta akitamani kulala kwani na yeye kichwa kilianza kuwa kizito kwa usingizi. Wakati akiwaka yale mkewe macho yalikuwa makavu hakuonesha dalili zozote za kulala huku macho yakiwa kwenye Runinga.
Alijifanya kutoka nje kumtazama Shehna kama atakuja ili amuwahi na kumueleza kuwa siku ile hali ilikuwa mbaya wafanye kesho japokuwa alijua atakuwa amemuharibia dozi. Aliamini zoezi alilolitaka Shehna alilikuwa ngumu kutekelezeka hasa kulifanyia nyumbani kwake chumbani kwake na kitandani anapolala na mkewe na mkewe akiwepo kilikuwa kitu kisichowezekana kwa akili ya kawaida.
Aliifunga Laptop yake na kunyanyuka huku akijinyoosha kidogo na kumfanya mkewe aseme.
“Dah! Afadhali umemaliza yaani leo hata sijielewi jinsi nilivyo na hamu na wewe imekuwa kama siku ya fungate,” Husna alisema huku akijiweka vizuri kwenye kochi ili anyanyuke.
“Nakuja,” Mustafa alisema huku akielekea nje.
“Usiku wote huu unakwenda nje kufanya nini?”
“Mke wangu maswali gani hayo?” Mustafa alisema kwa ukali kidogo.
“Mume wangu kukuuliza ni ubaya gani mimi mkeo nina haki ya kukuuliza chochote.”
“Nakuja,” Mustafa alisema huku akifungua mlango na kutoka nje na kumuacha mkewe akirudi kujilaza kwenye kochi kumsubiri mumewe.
Mustafa siku ile alimshangaa mkewe kuwa vile na kujiuliza labda amejua nini kinaendelea usiku ule. Alitoka nje kwa kuamini lazima kwa muda ule Shehna atakuwa amefika nje.
Wakati akiwaza hayo Shehna alikuwa amefika muda mrefu, aliyaona yote yaliyokuwa yakitendeka na jinsi Mustafa alivyokuwa akiteseka kwa jinsi mkewe alivyogoma kwenda kulala na jinsi ya kuyashinda masharti ya kukutana kimwili na mkewe ambaye siku ile alionesha kumtaka sana.
Alijifikiria jinsi ya kumsaidia Mustafa kwa kumfanya mkewe alale kwa hiyari yake bila kulazimishwa. Shehna alifurahi baada ya kumuona Mustafa akitoka nje alijua ametoka kumtafuta ili kumpa hali halisi ya ndani. Alimuacha atoke nje kisha alimsogelea Husna mke wa Mustafa na kumpuliza usoni na kukaa pembeni.
Husna alijikuta akisikia usingizi mkali bila kujielewa usingizi mzito ulimpitia. Mustafa baada ya kumtafuta Shehna kwa kuzunguka nyumba bila kumuona, alisogea mpaka mbele ya nyumba labda yupo barabarani lakini hakumuona. Baada ya kutomuona alisimama kwa muda kujiuliza atafanyaje ikiwa muda umekwenda na lazima akapande kitandani na ilikuwa lazima ampe mkewe haki yake ya ndoa kwa vile hakuwa na sababu ya kumnyima.

Itaendelea kesho wakati kama huu....

Not fair kuishia hapa
 
Back
Top Bottom