Hadithi ya kusisimua- Mimba ya Jini

Hadithi ya kusisimua- Mimba ya Jini

Niwawekeeni hadithi Mnashindwa hata kuweka (Like) ? Munapenda vya bure tu acheni Roho mbaya hizo.

Ila kwl hadithi zako tunasoma wengi sn ila ht ku-like tunaona kazi lkn tunalalama kana kwamba ww hautumii muda wako mi ntaendelea kuzimimina likes haahaa km vp tuanze kusimuliana kwa PM kwa wale "likers" mmmh wataniua mnafiki mie.
 
Hadithi ya kusisimuwa mimba ya jini-5-

ILIPOISHIA:
“Niliwaambia mfanye mapenzi saa ngapi?”
“Saa nne.”
“Ndiyo muda uliofanya?”
“Hapana lakini haikuvuka sana.”
“Mustafa niliwaeleza saa nne kamili lakini mmevuka muda kwa nini umepuuza maagizo yangu?”
“Samahani kwa hilo.”
SASA ENDELEA..

“
Mmh! Sijui...halafu kwa nini hukufurahia uamuzi wa mkeo?”
“Nimefurahi ndiyo maana tumekubaliana kutanguliza mtoto wa kike.”
“Si kweli Mustafa, moyoni hujafurahia uamuzi wa mkeo kwa kulazimisha kutangulia mtoto wa kike kitu kitakachompa matatizo mtoto atakayezaliwa.”
“Kwa nini?” Mustafa alishtuka.
“Kuukunja moyo wako wakati wa tendo la ndoa tofauti na siku zote. Mimba iliyoingia umeitia sumu.”
“Sumu?” Mustafa alishtuka.
“Ndiyo, ili kuiondoa unatakiwa kuukunjua moyo wako bila hivyo mtoto atakuwa na matatizo.”
“Nimekuelewa.”
“Basi mi nikuache ufanye kazi.”
“Nashukuru ila nilikuwa na hamu sana ya kuonana na wewe.”
“Usiwe na wasi Mustafa utaniona mpaka utanichoka kwanza tumalize tatizo linalowakosesha raha kwa muda mrefu.”
“Asante, nitakusuburi.”
Mustafa alikata simu na kujikuta akiwa katika mawazo mengi juu ya mtu anayejiita Shehna. Alijiuliza ni nani mtu anayeyajua maisha yake kiundani pia kujua hata mambo yaliyojificha bila kumwambia.
“Huyu mwanamke atakuwa nani...mmh! au...ha...hapana siyo lazima atakuwa mganga tu siyo jini.”
Mustafa aliendelea kuwaza juu ya kauli tata za Shehna ambazo hakuelewa nini hatima yake. Alijiuliza alijuaje kama kitendo cha mkewe kulazimisha mtoto wa kike wakati yeye alitaka wa kiume kitu ambacho alimkubalia kwa shingo upande yeye alifanya siri lakini Shehna alitambua na kumtisha kuhusu ujauzito ambao yeye alisema uliingia siku ile usiku.
Alijiuliza sumu hiyo ni sumu gani ambayo inaweza kuleta matatizo katika ujauzito ule na moyo wake ataunyoosha vipi. Kuingia kwa sekretari wake kulimkatisha mawazo yake.
“Bosi vipi naona upo mbali?” Sara alisema akiwa ameshika faili mkononi.
“Kawaida tu.”
Sara alimpa kazi aliyomuagiza kuifanya, baada ya kumpa alimuuliza.
“Jana nilisahau kukuuliza mlikwenda Mbagala?”
“Sara tumetoka hapa saa ngapi?”
“Kweli, jana kazi zilitushika, kwa hiyo wifi alienda peke yake?”
“Hakwenda ila mwisho wa wiki atakwenda.”
Sara alitoka na kumuacha Mustafa akiwaza na kuwazua aliyoelezwa na Shehna.
****
Jioni wakati Mustafa anajiandaa kurudi nyumbani alipokea simu toka kwa mkewe.
“Haloo mpenzi,” alipokea kwa madaha kama kawaida yake anapopigiwa na mkewe.
“Mume wangu yupo wapi?” mkewe alizungumza sauti ya mtu anayeumwa sana.
“Mke wangu mbona unaongea hivyo?” sauti ya mkewe ilimshtua.
“Na...na...u...mwa.”
“Nini?” Mustafa alitaharuki.
“Na...na...,” sauti ilinyamaza ghafla na kusikia kishindo upande wa pili.
Mustafa alijikuta akitaharuki na kutoka mbio ofisini kuelekea nje kwenye gari lake ili awahi nyumbani kujua mkewe alipatwa na nini. Alimpita sekretari wake aliyekuwa katika maandalizi ya kuzima vyombo vya umeme ili watoke na bosi wake.
Alishangaa bosi wake akitoka mbio kuelekea nje bila kumsemesha, Sara aliacha kazi na kumfuata ili ajue kulikoni. Alimuona akielekea kwenye gari lake akiwa kama amechanganyikiwa, alimkimbilia na kumuuliza:
“Bosi vipi?”
“Sara hebu subiri,” alisema huku akiwasha gari.
“Bosi kuna nini mbona mbiombio kwenye gari au kuna kitu cha kutisha kimetokea ofisini?” Sara alizidi kuhoji.
“Sara niache kwanza,” Mustafa alisema huku akiwasha gari na kuliondoa kwa kasi kuelekea getini na kumpigia kelele mlinzi afungue.
Mlinzi alifungua haraka, Mustafa alilitoa gari kwa kasi kwa kuliingiza barabarani bila kuangalia na kuelekea nyumbani.
Mlinzi alimfuata Sara na kumuuliza:
“Vipi! Kuna nini?”
“Hata najua! Nimemuona akitoka ofisini mbio hata sijui kapatwa na nini?” Sara naye alikuwa amepatwa na mshangao.
“Hukumuuliza?”
“Majibu yake hayaeleweki! Kila nilipomuuliza majibu anajua mwenyewe, kaacha vitu vyake vyote vya muhimu koti, lap top.”
“Mmh! Basi kuna kitu kimempata si bure.”
“Nina wasiwasi kuna kitu kimemtokea ofisini.”
“Twende tukaangalie.”
“Nani aingie ofisini? Toka juzi Bosi simwelewi mambo yake, nina wasiwasi bosi anataka kurukwa na akili,” Sara alisema.
“Mmh! Hapana, asingeweza kuendesha gari vile.”
Wakati wakijadiliana yaliyomtokea bosi wao, Mustafa alikuwa akiwaza nyumbani na kushindwa kuelewa nini kilimpata mkewe ambaye muda mfupi uliopita alizungumza naye akiwa katika afya njema.
Alipofika nyumbani kwake alisimamisha gari lake nje ya nyumba yao na kukimbilia ndani bila kufunga mlango wa gari. Alipoingia ndani alishtuka kumkuta mkewe amelala chini akiwa amepoteza fahamu.
Alijaribu kumwita lakini hakuitikia, alimbeba na kutoka naye nje ili amuwahishe hospitali, alimuweka siti ya nyuma ya gari na kufunga mlango.
Naye alizunguka upande wa pili na kuingia ndani ya gari. Alipowasha gari liligoma kuwaka, alishangaa. Alipoangalia kwenye geji ya mafuta ilimshtua kuona mafuta yalikwisha.
“Shit,” alisema kwa sauti huku akipaga ngumi kwenye gari.
Mara simu yake iliitaka, huku akivuja jasho kutokana na tatizo la mkewe. Alijifuta kwa shati jasho lililokuwa likimvuja kama maji kisha aliitazama simu na kuona aliyepiga ni Shehna.
“Haloo,” alipokea pumzi zikiwa juu.
“Mbona hivyo?” sauti ya Shehna ilionesha kushtuka.
“Nina tatizo.”
“Tatizo gani tena Mustafa?”
“Mke wangu yupo hoi hata sijui anaumwa nini?”
“Mmh! Isiwe mimba?”
“Mimba?” Mustafa alishtuka.
“Eeeh, unashtuka nini?”
“Mimba hiyo imeingia lini?”
“Jana.”
“Acha utani, hakuna mimba inayoweza kuingia mara moja na kuanza kumsumbua mtu.”
“Mustafa kila mimba ina uingiaji wake.”
“Basi yote nitayajua hospitali.”
“Unampeleka hospitali ili iweje?”
“Ana hali mbaya sana, kwanza sijui kama mzima.”
Kauli ile ilimfanya Shehna aangue kicheko kitu kilichomshtua Mustafa na kuhoji.
“Mbona unacheka?”
“Nani alikuambia mimba ugonjwa?”
“Shehna una uhakika gani kama ni mimba?”
“Uhakika ninao, mrudishe mkeo ndani kwa vile haumwi.”
“Hapana siwezi kufanya hivyo lazima nimpeleke hospitali.”
“Haya fanya unavyotaka, lakini usinitafute wala tusilaumiane,” Shehna alitoa kauli ya kitisho.
Kauli ile ilimshtua Mustafa na kumfanya ajiulize Shehna ana maana gani.
“Shehna ulikuwa unataka nifanyeje?” ilibidi awe mpole.
“Mrudishe kwanza ndani.”
“Kisha?”
“Mrudishe kwanza.”
“Sawa.”
Mustafa alimchukua mkewe na kumrudisha ndani akiwa katika hali ileile ya kupoteza fahamu. Baada ya kumlaza kwenye kochi alichukua simu ili kuwasiliana na Shehna.
Alipochukua simu alikuta bado ipo hewani aliita.
“Haloo Shehna.”
“Abee Mustafa.”
“Tayari.”
“Kile kichupa cha manukato kipo?”
“Sijui.”
“Kiangalie kama kipo kisha chukua maji kwenye sahani ya bati nyeupe kiweke kisha mpake kichwani. Akiamka mpe anywe na mengine mpake tumboni.


Itaendelea kesho jioni...
 
Hadithi ya kusisimuwa mimba ya jini-5-

ILIPOISHIA:

“Kiangalie kama kipo kisha chukua maji kwenye sahani ya bati nyeupe kiweke kisha mpake kichwani. Akiamka mpe anywe na mengine mpake tumboni.


Itaendelea kesho jioni...

Mkuu afadhal mie nmeisoma leo maana kesho jion mbalii ningeisoma jana sijui ingekuaje
 
Hadithi ya kusisimuwa mimba ya jini-6-

ILIPOISHIA:
Mustafa alimchukua mkewe na kumrudisha ndani akiwa katika hali ileile ya kupoteza fahamu. Baada ya kumlaza kwenye kochi alichukua simu ili kuwasiliana na Shehna.
Alipochukua simu alikuta bado ipo hewani aliita.

"Haloo Shehna."
"Abee Mustafa."
"Tayari."
"Kile kichupa cha manukato kipo?"

"Sijui."
"Kiangalie kama kipo chukua maji kwenye sahani ya bati nyeupe kiweke kisha chukua maji yale mpake kichwani. Akiamka mpe anywe na mengine mpake tumboni.
SASA ENDELEA...

Mustafa alikwenda chumbani na kukikuta kichupa juu ya meza ya kujipodolea. Alikichukua na kwenda kwenye kabati na kuchukua sahani ya bati nyeupe ambayo aliiweka maji na kukiweka kile kichupa na kufanya maji yale kunukia.
Alifanya kama alivyoelekezwa kwa kumpa maji kichwani. Ghafla mkewe alifumbua macho.
"Husna," alimwita kwa sauti ya chini.
"Abee mume wangu," aliitika kwa sauti ya chini huku akipepesa macho.

"Vipi?"
"Safi," alijibu kwa sauti ya chini huku akikaa kitako.
"Unajisikiaje?"
"Mmh! Sijambo."
"Kwani ilikuwaje?"

"Yaani nilikuwa natoka chumbani ghafla nikaanza kujisikia vibaya..yaani vibaya sana. Nikapata wazo la kukupigia simu, nilijitahidi kukujulisha lakini ghafla kilikuja kiza kizito kilichoendelea sikujua."
Mustafa alimpa maji anywe, lakini mkewe alihoji.
"Ya nini?"
"We kunywa."
Mkewe alikunywa, yaliyobaki alimpaka tumboni.

"Mume wangu mbona sikuelewi?"
"Ndiyo tiba yako."
"Kwa nini tusiende hospitali."
"Shehna amekataa."
"Alikuja."

"Ndiyo," Mustafa alimdanganya mkewe.
"Jamani mbona hakukaa ili nimuone, yaani yule dada anaonekana mwema sana. Kwani anasema hali hii inatokana na nini?"
"Mimba."
"Mimbaa!" Husna alishtuka.
"Ndiyo, anasema imeingia kwa mtindo huo."

"Ndiyo nasikia leo mimba ikiingia mara moja mtu unaona mabadiliko makali."
"Basi mke wangu inaonekana mambo ya jana mimba imeingia."
"Siwezi kuamini mpaka nikapime."
"Duka la dawa lipo jirani kanunue kipimo."

Snura alinyanyuka ili atoke nje, mara simu yake iliita. Alirudi kwenye kochi na kuichukua ilikuwa inatoka kwa Shehna.
"Asalam aleykum," alipokea Husna.
"Waleykumu salam," aliitikia Shehna kwa lafudhi ya mwambao.
"Niambie shoga yangu, yaani umeniudhi kweli."
"Kwa nini tena shoga?"

"Yaani kumbe jana umekuja hata kusubiri tuonane?"
"Nilikuwa na haraka, la muhimu afya mengine majaaliwa tutaonana tu."
"Naona umenipigia simu una lipi shoga yangu?"
"Vipi unaendeleaje?"
"Mmh! Namshukuru Mungu."

"Mambo ya kawaida, siku zote mimba zina ujaji wake kwa vile ni mara ya kwanza lazima imekusumbua."
"Shoga hii siyo mimba, mimba gani ya siku moja?"
"Husna acha ubishi, mimi ndiye najua."
"Kwanza shoga, wewe ni nani mganga au ji.." Husna alikata maneno.
"Malizia tu si ulitaka kusema mimi jini siyo?"
"Hapana shoga."

"Utanijua tu muda si mrefu kama mimi mtu, jini, mganga au mchawi," Shehna alisema kwa sauti kali kidogo.
"Samahani shoga sikuwa na maana hiyo bali kukujua tu," Husna alijitetea.
"Si nimekueleza utanijua wasiwasi wako nini."
"Kuhusu ujauzito siwezi kuamini japokuwa nina dalili zote za ujauzito huenda ni malaria mi nataka kupima ili nihakikishe."
"Husna naomba suala lako usichanganye na masuala ya kizungu," Shehna alimpa onyo mke wa Mustafa.

Itaendelea Usiku Mwingi
 
.........
“Kuhusu ujauzito siwezi kuamini japokuwa nina dalili zote za ujauzito huenda ni malaria mi nataka kupima ili nihakikishe.”
“Husna naomba suala lako usichanganye na masuala ya kizungu,” Shehna alimpa onyo mke wa Mustafa.
[/FONT][/COLOR]
Itaendelea Usiku Mwingi


Ya sasa mbna fupi
 
Hadithi ya kusisimuwa mimba ya jini-7-

ILIPOISHIA:
"Samahani shoga sikuwa na maana hiyo bali kukujua tu," Husna alijitetea.
"Si nimekueleza utanijua wasiwasi wako nini?"

"Kuhusu ujauzito siwezi kuamini japokuwa nina dalili zote za ujauzito huenda ni malaria, mi nataka kupima ili nihakikishe."
"Husna naomba suala lako usilichanganye na masuala ya Kizungu," Shehna alimpa onyo mke wa Mustafa.
SASA ENDELEA...


"Sawa nimekuelewa shoga."

"Najua majibu yako yamejaa unafiki sasa ukienda kinyume tusilaumiane."
"Nimekuelewa shoga."
"Nataka hili umweleze na mumeo, sawa?" Shehna alisema kwa sauti kali.
"Sawa."

Simu ilikatika na kumfanya Husna arudi kwenye kochi na kukaa, safari ya kwenda duka la dawa baridi ikakatika ghafla. Mustafa alishtuka na kumuuliza mkewe.
"Vipi mbona huendi dukani?"
"Shehna amekataa."
"Amekataa nini?"

"Nisiende kununua kipimo cha mimba wala nisikitumie."
"Amejuaje unataka kwenda kununua?"
"Nimemwambia nataka kuhakikisha kama kweli nina ujauzito nakwenda kununua kipimo cha mimba."
"We unasemaje?"

"Niseme nini? Mmh! Ipo kazi."
"Kwa hiyo huendi?"
"Amesema suala la ujauzito wangu tusichanganye na mambo ya Kizungu."
"Kwa hiyo hata ukiumwa?"

"Sijui muulize wewe."
"Mmh! Sawa."
Walikubaliana kutotumia dawa za Kizungu kipindi chote cha ujauzito japokuwa Husna moyoni hakuamini kama alikuwa mjamzito na kutaka kufanya kwa siri ili kupata uhakika.

***
Sara baada ya bosi wake kuondoka katika mazingira tata alifunga ofisi na kuchukua vitu vya bosi wake ampelekee nyumbani ikiwa pamoja na kwenda kujua nini kilimsibu.
Alikodi gari na kuelekea kwa bosi wake, akiwa njiani ghafla usingizi ulimpitia. Ajabu aliposhtuka alijikuta kitandani kwake akiwa amelala na mizigo ya bosi wake ameishikilia mkononi.

Alipopepesa macho alishangaa kuona jua kama la asubuhi. Alinyanyuka kitandani na kushangaa kukuta mlango ukiwa wazi.
Aliweka vitu kwenye kochi na kuangalia saa ya mkononi iliyomuonesha ni saa mbili asubuhi. Alishangaa kujiona akiwa nyumbani amelala na vitu alivyokuwa akimpelekea bosi wake.

Alijawa na mawazo na kujiuliza alipotoka kazini na kukodi gari alimwambia dereva ampeleke kwa bosi wake au nyumbani kwake? Akakumbuka alimwambia ampeleke kwa bosi na si nyumbani.
Alijiuliza kama alikwenda nyumbani kipi kilimsibu mpaka akalala na nguo zake bila kuvua viatu na mkoba wenye ‘laptop' na koti la bosi wake. Bado alikuwa njia panda kuhusiana na kurudi nyumbani na kulala bila kula wala kufunga mlango.
Mara simu iliita ilikuwa ya bosi wake, aliipokea.

"Haloo bosi."
"Sara upo wapi?"
"Nyumbani."
"Unaumwa?"
"Hata siumwi."

"Mbona hujafika kazini?"
"Bosi hata sijui niseme nini?"
"Basi wahi ofisini huwezi kuamini nina nusu saa nipo nje ofisi imefungwa."
"Mungu wangu, jana nilijisahau na kuondoka na funguo."
"Basi wahi."

Sara alioga haraka na kubadili nguo kisha alikodi bodaboda kuwahi kazini huku akimuhimiza dereva akimbize pikipiki.
Alifika ofisini baada ya dakika tano, Sara alimsalimia bosi wake na kufungua ofisi, Mustafa akaingia ndani.
Alimkabidhi vitu vyake na kurudi kwenye eneo lake la kazi kumalizia kiporo ndipo amuuliza bosi wake jana ilikuwaje na kumweleza yaliyomtokea.
***
Husna mke wa Mustafa akiwa nyumbani peke yake moyo ulimsukasuka juu ya hali aliyonayo ambayo alielezwa ni ujauzito lakini alikatazwa kutumia kipimo cha Kizungu kutambua kama ni mimba.

Alijiuliza kama akikitumia nini kitakuwa, alimtuma mtoto dawa katika duka la dawa baridi akamletee kipimo kile. Baada ya kuletewa alikwenda msalani na kujisaidia haja ndogo na kuiweka kwenye kikopo kisafi na kurudi nacho chumbani.

Itaendelea Leo jioni....
 
Hadithi ya kusisimuwa mimba ya jini-8-


ILIPOISHIA:
Alijiuliza kama akikitumia nini kitakuwa, alimtuma mtoto duka la dawa baridi akamletee kipimo kile. Baada ya kuletewa alikwenda msalani na kujisaidia haja ndogo na kuiweka kwenye kikopo kisafi na kurudi nacho chumbani.

SASA ENDELEA...
Alikiweka kile kikopo chini na kukichukua kipimo, alikifungua ili akitie kwenye kikopo chenye haja ndogo. Mara simu yake iliita alipoitazama ilikuwa inatoka kwa Shehna.
Aliipuuza na kukiweka kile kipimo kwenye haja ndogo ili kuhakikisha kama ana mimba kweli. Kilipogusa tu kwenye haja ndogo, alihisi kama tumbo limechafuka ghafla. Ajabu nyingine haja ndogo iliyokuwemo kwenye kikopo iligeuka damu mbichi iliyotoa harufu kali. Alishtuka akiwa anashangaa hali ile, alizidi kushtuka kusikia hali ya majimaji ukimtoka chini kama ya kuziona siku zake. Alipoangalia alishtuka kuona nguo yote umetota kwa damu. Chini damu ilitengeneza michirizi aliyotapakaa sehemu kubwa kuonesha ametokwa na damu nyingi.
Kizunguzungu kilikuwa kikali alijitahidi kunyanyuka kwa kujilazimisha na kufanikiwa kuishika simu yake. Aliitafuta namba ya mume wake kwa shida na kupiga na kupokelewa upande wa pili.
"Haloo," Mustafa alipokea.
"Mu..mu..me wangu na..na ..ku..fa," baada ya kusema vile simu ilimponyoka na yeye akajitupa chini kama mzigo na kupoteza fahamu.
Mustafa alishtuka na kujiuliza mke wake amepatwa na nini tena. Hakutaka kutoka kama jana yake kwa kumshtua sekretari wake, alimuaga kwa sauti ya kawaida iliyoficha siri nzito ndani.
"Sara nafika nyumbani mara moja."
"Mbona hivyo kuna usalama?"
"Kawada tu."
Alitoka hadi kwenye gari lake na kuwasha kuwahi nyumbani huku akijiuliza mkewe amepatwa na nini. Aliendesha gari kwa mwendo wa kasi hadi nyumbani, baada ya kusimamisha gari alikimbilia ndani.
Alipoingia ndani alishtuka kukuta damu imetapakaa chumba kizima. Alishtuka kuona kikopo kikiwa na damu na ndani yake kuna kipomo cha mimba.
"Mungu wangu mke wangu kafanya nini?" Mustafa alishika mikono kichwani.
Alimshika mkewe aliyekuwa amelala sakafuni ambaye alionekana kapoteza fahamu huku akiwa ametokwa damu nyingi. Alijikuta akishindwa afanye nini baada ya kujua mkewe kafanya kosa kwenda kinyume na maelekezo ya Shehna.
Alimnyanyua na kumpeleka bafuni ambako alimfanyia usafi na kumrudisha kitandani, lakini wakati huo bado alikuwa amepoteza fahamu. Alibaki njia panda asijue ampeleke hospitali au afanye nini. Akiwa katika taharuki simu yake iliita, alipoangalia ilikuwa inatoka kwa Shehna, aliipokea haraka.
"Haloo Shehna."
"Haloo Mustafa, vipi mbona kama una tatizo?"
"Ndiyo, mke wangu ana matatizo."
"Matatizo gani tena?"
"Yaani hata sijui, anatokwa damu."
"Kwanza upo wapi?"
"Nipo nyumbani."
"Ha! Umeondoka sangapi wakati nimeingia nimeliona gari lako."
"Sasa hivi."
"Basi mi nipo ofisini kwako, utawahi kurudi?"
"Shehna, yaani matatizo ya mke wangu unayaona madogo?"
"Siyo madogo ya kujitakia."
"Sasa unanishauri nini?"
"Kuhusu nini?"
"Tatizo la mke wangu."
"Ulikuwa unahitaji msaada wangu ipi?"
"Wa ushauri wako."
"Mpeleke hospitali."
"Si ulitukataza?"
"Lakini mkafanya."
"Siyo mimi ni mke wangu."
"Basi mpeleke hospitali kwa hilo sina msaada wowote kwako lipo nje ya uwezo wangu."
"Haina tatizo kwenda hospitali?"
"Mustafa mi siyo mganga, wahi hospitali utampoteza mkeo," Shehna alisema kwa sauti kali kidogo.
"Sawa nimekuelewa."
"Sasa unarudi saa ngapi?"
"Sijajua."
"Ukimpeleka hospitali lazima atapata kitanda, nitakusubiri ukichelewa nitaondoka."
"Sawa."
Baada ya kukata simu Mustafa alimchukua mkewe na kumuwahisha hospitali. Alipofika alipokelewa na wauguzi na kukimbizwa wadini na kumuacha Mustafa nje akisuburi.
Baada ya vipimo majibu yalionesha ujauzito umetoka. Mganga alimwita ofisini na kumweleza tatizo la mkewe.
"Vipimo vinaonesha ujauzito umetoka."
"He! Kweli alikuwa na mimba?" Mustafa alishtuka.
"Ndiyo kwani ulikuwa hujui?"
"Ha..ha....ndiyo."
"Vipi Bwana Mustafa mbona unababaika?"
"Kulikuwa na dalili lakini hatukuwa na uhakika."
"Aah! Bwana Mustafa, unaniangusha siku hizi suala la ujauzito si la kusumbuka kwa vile mkiwa na wasiwasi mnakwenda duka la dawa baridi ambalo nina imani siku hizi lipo kila kona, unanunua kipimo na kupata uhakika."
"Na..na sababu ya kutoka ujauzito?"
"Inawezekana alianguka na kulilalia tumbo."
"Duh! Sasa itakuaje?"
"Atafanyiwa usafi na kuongezwa damu kutokana na kupoteza damu nyingi kisha tutaangalia hali yake kwa kesho, ikiendelea vizuri tutamruhusu."
"Kwa hiyo naweza kumsubiri?"
"Hapana kaendelee na majukumu ya ujenzi wa taifa ila acha namba yako ya simu tutakujulisha hali ya mkeo, yangu utaangalia katika business card yangu," Daktari alimkabidhi kadi Mustafa.
"Nashukuru, lakini tatizo siyo kubwa?"
"Siyo kubwa, damu ndiyo iliyopotea nyingi, lakini jioni ya leo atakuwa vizuri."
"Nashukuru dokta."
Mustafa alitoka na kurudi nyumbani kufanya usafi wa damu iliyomtoka mkewe. Lakini alishtuka kukuta nyumba ipo katika hali ya usafi hakuna hata na chembe ya damu sehemu.


Itaendelea Usiku Mwingi.....
 
Hadithi ya kusisimuwa Mimba ya Jini-9-

ILIPOISHIA:.

“Nashukuru, lakini tatizo siyo kubwa?”
“Siyo kubwa, damu ndiyo iliyopotea nyingi, lakini jioni ya leo atakuwa vizuri.”
“Nashukuru dokta.”

Mustafa alitoka na kurudi nyumbani kufanya usafi wa damu iliyomtoka mkewe. Lakini alishtuka kukuta nyumba ipo katika hali ya usafi, hakukuwa na hata chembe ya damu.

SASA ENDELEA...


Hakutaka kuwaza sana aliwasha gari na kurudi kazini, alipofika alishtuka kukutana na manukato makali ambayo aliamini ni ya Shehna. Alipoingia tu Sara alimwambia.
“Bosi hukupishana na mwanamke mwenye hijabu hapo mlangoni?”
“Hapana.”
“Mmh! Kapitia wapi? Sasa hivi katoka.”

“Basi sijamuona.”
“Yaani sasa hivi hata dakika haijafika, nina imani hata getini hajafika.”
“Amesemaje?”
“Anashida na wewe.”
“Hakutaja jina lake?”
“Amesema ukifika niseme sijui Shena.”

“Shena au Shehna.”
“Shehna, unajua tena lafudhi ya Kimwambao.”
“Duh!” Mustafa alisema huku akigeuka na kukimbilia nje amuwahi mgeni wake.
Mpaka anafika getini hakumuona mtu yeyote, alimfuata mlinzi na kumuuliza.
“Shabani kuna mgeni amepita hapa?”

“Ndiyo.”
“Mwanamke au mwanaume?”
“Mwanamke aliyevaa hijabu.”
“Ameenda wapi?”
“Baada ya kutoka nje lilipita gari ambalo lilimchukua.”
“Duh! Yaani alipotoka tu gari lilipita?”

“Amesimama barabarani kama dakika mbili hivi akisubiri, baada ya muda gari lilisimama na yeye kuondoka.”
“Atakuwa ameenda wapi, kwa nini hakunisubiri?”
“Kwani bosi hukuonana naye?”
“Sikuonana naye.”
“Yaani mmepishana, baada ya wewe kuingia na yeye akatoka.”

“Mungu wangu sasa nimepishana naye wapi?” Mustafa alijilaumu kwani alikuwa ana hamu ya kumuona Shehna kwa macho baada ya kuvutiwa na sauti yake iliyomfanya aamini ni mwanamke mzuri.
“Yupo vipi?”
“Kwa kweli umbile kalificha na vazi alilovaa ni mweupe, kwa lafudhi yake anaonekana kama Mpemba vile. Ila yule mwana mke ana umbile la utata. ”
“Kwa nini unasema hivyo?”

“Toka anaingia na kutoka, upepo ulikuwa ukiisukuma nguo yake na kuonekana ramani ya umbile lake na kuonesha mwanamke mzuri sana. Kwani bosi hujawahi kuonana naye?”
“Sijawahi.”
“Mbona alivyokuuliza kama mnajuana sana?”
“Kwenye simu si kwa kuonana.”
“Labda atarudi.”

“Mmh! Sidhani.”
Mustafa aligeuka na kurudi ofisini, alipofika kwa msaidizi wake Sara alimuuliza.
“Vipi bosi umemuona?”
“Walaa.”
“Anapaa?”
“Hapana nimekuta ameisha panda gari na kuondoka.”

“Bosi nilipokueleza ungetoka ungemuwahi.”
“Labda atarudi.”
“Nina imani atarudi amekusuburi sana.”
“Sijui atarudi?”
“Yaani unatoka tu yeye akaingia kama mmepishana mlangoni, nilimweleza akuwahi akasema atakusubiri. Baada ya kuchoka alitaka kuondoka nilimsihi akusubiri, akakubali. Nilikutafuta kwenye simu lakini haukuwa hewani.”

“Mbona simu yangu sijazima?”
“Yaani kila nikipiga inakata.”
“Labda mawasiliano.”
Mustafa alipotaka kuingia ofisini Sara alikumbuka kitu.
“Bosi.”
“Unasemaje?”

“Ha...halafu mbona manukato ya yule mwanamke yanafanana na yale ya siku ile tuliyoyakuta ofisini kwako?”
“Hata mimi nayasikia, yupo vipi?”
“Kwa kweli sikumuona mwili mzima ila ni mrembo sana mrefu tena anayejijali sana.”
“Poa, akirudi nitamuona,” Mustafa alijibu huku akienda ofisini kwake.
Alipofika alikaa kwenye kiti na kutulia kwa muda kabla ya kuanza kazi, aliwaza kuhusu hali ya mke wake na yaliyomtokea.

Itaendelea leo jioni.......
 
Hadithi ya kusisimuwa mimba ya jini-10-

ILIPOISHIA:

"Poa, akirudi nitamuona," Mustafa alijibu huku akienda ofisini kwake.

Alipofika, alikaa kwenye kiti na kutulia kwa muda kabla ya kuanza kazi, aliwaza kuhusu hali ya mke wake na yaliyomtokea.

SASA ENDELEA..
.


Alishangaa kiburi cha mkewe kukaidi amri ya Shehna kwa kutumia kipimo cha mimba wakati alikatazwa. Alijikuta akimlaumu mkewe kwa ukaidi alioufanya kufikia hatua ya kupoteza ujauzito.

Pia hali aliyoikuta nyumbani kwake ilimtisha sana na kushangazwa kukuta kumesafishwa, hakuna dalili za damu kumwagika. Alijikuta akijiuliza nani aliyefanya usafi ule wakati anaondoka nyumbani hakukuwa na mtu yeyote lakini aliporudi alikuta pamefasafishwa.
Wazo lake lilikuwa labda shoga yake alipita kumsalimia na kukuta hali ile na kuamua kufanya usafi. Lakini kilichomshtua ni sehemu yenyewe ya tukio kuwa chumbani kwake na kushangaa kama shoga yake aliingia chumbani na kufanya usafi.
Aliamini kama ni shoga yake lazima atapiga simu kuuliza kilichotokea. Mustafa akiwa katikati ya mawazo, Sara aliingia na faili la kazi na kushangaa kumkuta bosi wake amezama kwenye dimbwi la mawazo.
"Bosi vipi?"
"Poa," Mustafa alijibu huku akinyanyua uso kumtazama Sara.
"Upo sawa?"
"Kiasi."
"Mmh! Bosi basi jana hata sielewi kilichonitokea!"
"Kitu gani Sara?"
Basi bosi baada ya wewe kuondoka, ghafla nilichukua vitu vyak..."
Kabla Sara hajaendelea kumhadithia, alinyamaza baada ya kusikia sauti ya mtu mapokezi.
Alitoka kwenda kumuangalia, alipofika alishtuka kutomkuta mtu. Lakini ghafla alishangaa kusikia kizunguzungu, alikwenda kwenye kiti chake na kukaa.
Baada ya kukaa alisikia usingizi mzito, alipojaribu kujiepesha, usingizi ulimpitia. Sara aliposhtuka alijikuta amelala kwenye kochi nyumbani kwake akiwa na nguo zake za kazini.
Alishtuka na kujiuliza kinachomtokea ni kweli au anaota, alikumbuka tukio kama hilo lilimtokea jana yake wakati akimpelekea bosi wake vitu vyake baada ya kutoa mbio na kuviacha ofisini.
Baada ya kukodi gari ambalo aliingia na kumweleza dereva ampeleke anapokaa Mustafa na kushangaa kujikuta amelala nyumbani akiwa na vitu vya bosi wake.
Alijiuliza ni kitu gani huwa kinamtokea na kujikuta kwenye hali ile ambayo ilianza kumtisha.
Kwa vile muda ulikuwa umekwenda baada ya kuangalia saa na kumuonesha ni saa mbili usiku, alikwenda kununua chipsi na soda kisha akapanda kitandani kuitafuta siku ya pili.
***
Mustafa baada ya kutoka kazini, alipitia hospitali kuangalia hali ya mkewe inaendeleaje. Alimkuta hajambo kiasi ila mwili ndiyo haukuwa na nguvu hivyo kuendelea kuwepo hospitali mpaka siku ya pili.
Hakutaka kumuulizia ilikuwaje mkewe akakaidi amri ya Shehna na kufanya aliyvotaka. Aliamini sehemu nzuri ya kulizungumza suala hilo ni nyumbani hasa baada ya kuhakikishiwa na daktari kuwa kesho yake angetoka.
Hakutaka kumsumbua mkewe, alimuacha apumzike na yeye kurudi nyumbani. Alipita kwenye mgahawa na kuchukua chakula cha kubeba ili akalie nyumbani. Alipofika nyumbani, alioga na kupata chakula kisha alichukua ‘laptop' yake na kucheza gemu ya magari ili kuutafuta usingizi.
Akiwa katikati ya mchezo, alisikia mlango ukigongwa huku akiitwa jina lake, aliacha kucheza gemu na kutoka sebuleni. Alitulia kabla ya kufungua mlango kusikilizia ni nani anayegonga usiku ule.
"Nani?" aliuliza kwa sauti ya juu kidogo.
"Mimi," sauti ya kike ilijibu ambayo haikuwa ngeni masikioni mwake lakini hakuikumbuka ni ya nani.
"Wewe nani?"
"Shehna."
"Ka..ka..ribu," Mustafa alishtuka na kupata kigugumizi cha ghafla baada ya kusikia jina la Shehna.
Alifungua mlango na kulakiwa na harufu nzurii ya manukato, ilikuwa tofauti na aliyoizoea siku zote, ilikuwa nzuri zaidi. Mbele yake alikuwa amesimama mwanamke mzuri sana aliyekuwa amevalia vazi refu la gauni la kumeremeta lililoacha mabega wazi na kufunikwa na mtandio.
Chini alivaa viatu virefu, alipoangalia nje hakuona gari lolote lililopaki jirani. Kutokana na viatu vile venye kisigino kirefu, aliamini asingeweza kutembea kwa miguu umbali mrefu.
"Karibu ndani."
"Asante," Shehna alisema huku akiingia ndani na kulinyanyua juu gauni lake lililokuwa linaguza chini.
Shehna alikwenda kukaa kwenye kochi na kutulia, Mustafa baada ya kufunga mlango alirudi kukaa kwenye kochi lingine.
"Karibu sana," Mustafa alimkaribisha tena.
"Asante za hapa?"
"Mmh! Nzuri kiasi," Mustafa alijibu huku akimuibia Shehna kumtazama kutokana na uzuri wake, kitu alichokigundua Shehna na kusema huku akiondoa mtandio kichwani na kuziacha nywele zake ndefu nyeusi zionekane vizuri.
Aliachia tabasamu kama ua la mchana linavyochanya, macho yake makubwa kidogo yaliyopakwa wanja yaliongeza uzuri wake. Yalioneka yameumbwa kwa mahaba tu.
"Mustafa usipate shida ya kuhangaika kunitazama, una uhuru wa kunitazama upendavyo wala usiniogope."
"Ha..ha..una..na," kutokana na kushindwa kujiamini maneno yalipandana.
Mustafa kwa mara ya kwanza alimuona mwanamke mzuri katika maisha yake. Hakugundua kasoro yoyote kwa Shehna, kumbukumbu zake zilimkumbusha ndiye mwanamke aliyefanya naye mapenzi katika ndoto.
"Mustafa mimi mtu wa kawaida najua uzuri wangu utakubabaisha, nione kama nyama yoyote isiyo na mfupa kwenye kisu kikali."
"Unatu..tumia kinywaji gani?" Mustafa alijikaza na kumuuliza.
"Kwa leo sihitaji kitu nataka tuzungumze kitu ili niondoke zangu."
"Kitu gani?"
"Mustafa unakumbuka nilikuahidi nini?"


Usikose kusoma usiku mwingi
 
Hadithi ya kusisimuwa mimba ya jini-10-

ILIPOISHIA:

“Poa, akirudi nitamuona,” Mustafa alijibu huku akienda ofisini kwake.

Alipofika, alikaa kwenye kiti na kutulia kwa muda kabla ya kuanza kazi, aliwaza kuhusu hali ya mke wake na yaliyomtokea.

SASA ENDELEA..
.


Alishangaa kiburi cha mkewe kukaidi amri ya Shehna kwa kutumia kipimo cha mimba wakati alikatazwa. Alijikuta akimlaumu mkewe kwa ukaidi alioufanya kufikia hatua ya kupoteza ujauzito.

Pia hali aliyoikuta nyumbani kwake ilimtisha sana na kushangazwa kukuta kumesafishwa, hakuna dalili za damu kumwagika. Alijikuta akijiuliza nani aliyefanya usafi ule wakati anaondoka nyumbani hakukuwa na mtu yeyote lakini aliporudi alikuta pamefasafishwa.
Wazo lake lilikuwa labda shoga yake alipita kumsalimia na kukuta hali ile na kuamua kufanya usafi. Lakini kilichomshtua ni sehemu yenyewe ya tukio kuwa chumbani kwake na kushangaa kama shoga yake aliingia chumbani na kufanya usafi.
Aliamini kama ni shoga yake lazima atapiga simu kuuliza kilichotokea. Mustafa akiwa katikati ya mawazo, Sara aliingia na faili la kazi na kushangaa kumkuta bosi wake amezama kwenye dimbwi la mawazo.
“Bosi vipi?”
“Poa,” Mustafa alijibu huku akinyanyua uso kumtazama Sara.
“Upo sawa?”
“Kiasi.”
“Mmh! Bosi basi jana hata sielewi kilichonitokea!”
“Kitu gani Sara?”
Basi bosi baada ya wewe kuondoka, ghafla nilichukua vitu vyak...”
Kabla Sara hajaendelea kumhadithia, alinyamaza baada ya kusikia sauti ya mtu mapokezi.
Alitoka kwenda kumuangalia, alipofika alishtuka kutomkuta mtu. Lakini ghafla alishangaa kusikia kizunguzungu, alikwenda kwenye kiti chake na kukaa.
Baada ya kukaa alisikia usingizi mzito, alipojaribu kujiepesha, usingizi ulimpitia. Sara aliposhtuka alijikuta amelala kwenye kochi nyumbani kwake akiwa na nguo zake za kazini.
Alishtuka na kujiuliza kinachomtokea ni kweli au anaota, alikumbuka tukio kama hilo lilimtokea jana yake wakati akimpelekea bosi wake vitu vyake baada ya kutoa mbio na kuviacha ofisini.
Baada ya kukodi gari ambalo aliingia na kumweleza dereva ampeleke anapokaa Mustafa na kushangaa kujikuta amelala nyumbani akiwa na vitu vya bosi wake.
Alijiuliza ni kitu gani huwa kinamtokea na kujikuta kwenye hali ile ambayo ilianza kumtisha.
Kwa vile muda ulikuwa umekwenda baada ya kuangalia saa na kumuonesha ni saa mbili usiku, alikwenda kununua chipsi na soda kisha akapanda kitandani kuitafuta siku ya pili.
***
Mustafa baada ya kutoka kazini, alipitia hospitali kuangalia hali ya mkewe inaendeleaje. Alimkuta hajambo kiasi ila mwili ndiyo haukuwa na nguvu hivyo kuendelea kuwepo hospitali mpaka siku ya pili.
Hakutaka kumuulizia ilikuwaje mkewe akakaidi amri ya Shehna na kufanya aliyvotaka. Aliamini sehemu nzuri ya kulizungumza suala hilo ni nyumbani hasa baada ya kuhakikishiwa na daktari kuwa kesho yake angetoka.
Hakutaka kumsumbua mkewe, alimuacha apumzike na yeye kurudi nyumbani. Alipita kwenye mgahawa na kuchukua chakula cha kubeba ili akalie nyumbani. Alipofika nyumbani, alioga na kupata chakula kisha alichukua ‘laptop’ yake na kucheza gemu ya magari ili kuutafuta usingizi.
Akiwa katikati ya mchezo, alisikia mlango ukigongwa huku akiitwa jina lake, aliacha kucheza gemu na kutoka sebuleni. Alitulia kabla ya kufungua mlango kusikilizia ni nani anayegonga usiku ule.
“Nani?” aliuliza kwa sauti ya juu kidogo.
“Mimi,” sauti ya kike ilijibu ambayo haikuwa ngeni masikioni mwake lakini hakuikumbuka ni ya nani.
“Wewe nani?”
“Shehna.”
“Ka..ka..ribu,” Mustafa alishtuka na kupata kigugumizi cha ghafla baada ya kusikia jina la Shehna.
Alifungua mlango na kulakiwa na harufu nzurii ya manukato, ilikuwa tofauti na aliyoizoea siku zote, ilikuwa nzuri zaidi. Mbele yake alikuwa amesimama mwanamke mzuri sana aliyekuwa amevalia vazi refu la gauni la kumeremeta lililoacha mabega wazi na kufunikwa na mtandio.
Chini alivaa viatu virefu, alipoangalia nje hakuona gari lolote lililopaki jirani. Kutokana na viatu vile venye kisigino kirefu, aliamini asingeweza kutembea kwa miguu umbali mrefu.
“Karibu ndani.”
“Asante,” Shehna alisema huku akiingia ndani na kulinyanyua juu gauni lake lililokuwa linaguza chini.
Shehna alikwenda kukaa kwenye kochi na kutulia, Mustafa baada ya kufunga mlango alirudi kukaa kwenye kochi lingine.
“Karibu sana,” Mustafa alimkaribisha tena.
“Asante za hapa?”
“Mmh! Nzuri kiasi,” Mustafa alijibu huku akimuibia Shehna kumtazama kutokana na uzuri wake, kitu alichokigundua Shehna na kusema huku akiondoa mtandio kichwani na kuziacha nywele zake ndefu nyeusi zionekane vizuri.
Aliachia tabasamu kama ua la mchana linavyochanya, macho yake makubwa kidogo yaliyopakwa wanja yaliongeza uzuri wake. Yalioneka yameumbwa kwa mahaba tu.
“Mustafa usipate shida ya kuhangaika kunitazama, una uhuru wa kunitazama upendavyo wala usiniogope.”
“Ha..ha..una..na,” kutokana na kushindwa kujiamini maneno yalipandana.
Mustafa kwa mara ya kwanza alimuona mwanamke mzuri katika maisha yake. Hakugundua kasoro yoyote kwa Shehna, kumbukumbu zake zilimkumbusha ndiye mwanamke aliyefanya naye mapenzi katika ndoto.
“Mustafa mimi mtu wa kawaida najua uzuri wangu utakubabaisha, nione kama nyama yoyote isiyo na mfupa kwenye kisu kikali.”
“Unatu..tumia kinywaji gani?” Mustafa alijikaza na kumuuliza.
“Kwa leo sihitaji kitu nataka tuzungumze kitu ili niondoke zangu.”
“Kitu gani?”
“Mustafa unakumbuka nilikuahidi nini?”


Usikose kusoma usiku mwingi

Apa nakupa big LIKE
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom