Hadithi ya kusisimua- Mimba ya Jini

Hadithi ya kusisimua- Mimba ya Jini

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,037
Reaction score
34,741
SAA mbili kasorobo, Mustafa baada ya kufika ofisini, kabla ya kuanza kazi haja ilimshika na kuelekea msalani.
Baada ya kumaliza kujisaidia alikwenda kwenye sinki la kusafishia mikono ili ajisafishe. Alivua pete ya ndoa na kuiweka juu ya sinki kisha alijimwagia sabuni ya maji mikononi na kuanza kunawa.


Simu iliyokuwa mfukoni ilianza kuita, kwa vile hakuweka mlio ilitetemeka kuonesha ilikuwa inaita. Hakuipokea kwa vile bado alikuwa na sabuni mikononi, hivyo alinawa haraka na kufuta mikono kwa taulo dogo ili apokee simu. Lakini kabla hajaipokea ilikuwa tayari imekatika.

Ingawa ilikuwa imekatika lakini aliitoa ili aangalie nani aliyekuwa akimpigia, kabla hajaangalia simu iliita tena, kwa vile ilikuwa mkononi aliangalia na kukuta jina la Shehna.

Japokuwa alishtuka kuona jina lile ambalo kwake lilikuwa geni. Aliamini kuzungumza na aliyepiga angemjua kwa vile jina lilikuwa kwenye simu yake.

Alibonyeza kitufe cha kupokelea na kusema:
"Haloo."
"Haloo Mustafa, asalam aleiykum," ilikuwa sauti ya lafudhi ya kimwambao.
"Waleiykum msalaam," Mustafa aliitikia huku akiifikiria sauti ile na kutaka kumjua aliyempigia ambaye jina na sauti yake vilikuwa vigeni akilini mwake.
"Upo wapi?" sauti ilimuuliza.
"Nipo ofisini."
"Nipo ofisini kwako muda tu, lakini mwenyeji wangu sikuoni."
"Nakuja basi."

"Fanya haraka kuna sehemu nawahi, nilipita ofisini kwako mara moja."
Mustafa alitoka haraka kumuwahi mgeni huyo, alimpita sekretari wake bila kumuuliza kitu japokuwa haikuwa utaratibu mzuri kumruhusu mgeni aingie ofisini bila mwenyewe kuwepo.

Mara zote sekretari wake alikuwa akimruhusu mtu kuingia pale aliporuhusiwa kufanya hivyo.
Lakini kwa kauli ya mgeni kuingia ofisini ilionesha ameruhusiwa bila ridhaa yake.
Alipoingia ndani alishtuka alipokuta hakuna mtu ofisini, lakini harufu ya manukato mazuri ilisambaa kila kona.

Alitoka haraka ili amuwahi kwa kuamini huenda aliamua kutoka baada ya kuchoka kumsubiri. Lakini aliamini hakutumia muda mrefu msalani.
Alikwenda hadi getini kwa mlinzi na kumuulizia.
"Eti kuna mgeni ametoka sasa hivi?"
"Mgeni! mgeni gani?" mlinzi ilionesha kushtuka.
"Mwanamke."
"Bosi, toka uingie wewe hajaingia mtu yeyote."

Itaendelea risasi Jumamosi.

"Hapana, labda ulitoka eneo la kazi, mgeni alikuwa ofisini kwangu sasa hivi."
"Bosi hakuna mgeni yeyote zaidi ya dada Sara ambaye alikutangulia kuingia kabla yako."
"Mmh! Hebu ngoja."
Mustafa alirudi hadi ofisini na kumuuliza Sara, sekretari wake akuyekuwa bize na kazi kwenye kompyuta.
"Sasa mgeni ametoka?"
"Mgeni gani?" Sara naye alionesha kushtuka.
"Aliyekuwa ofisini kwangu sasa hivi?"
"Bosi, hakuna mgeni yeyote aliyefika hapa, kwanza ilianza lini nimruhusu mgeni aingie ofisini kwako bila ruhusa yako?"
"Sasa huyu mgeni kaingiaje na kapitia wapi?"
"Bosi mgeni unayemsema umemuona wapi?"
"Hebu njoo ofisini."
Sara na Mustafa waliongozana hadi ofisini ambako harufu ya manukato makali ilikuwa bado ikinukia.
"Bosi pafyumu nzuri kama hii umeitoa wapi?" Sara alisema huku akinyanyua pua zake kuivuta.
"Sara, haya manukato nimeyakuta baada ya kurudi kutoka msalani."
"Muongo!" Sara alishangaa.
"Kweli kabisa, yanaonekana ni ya huyo mgeni aliyeingia ofisini kwangu."
"Sasa kapitia wapi?"
"Hebu subiri."
Mustafa alisema huku akichukua simu yake juu ya meza, aliangalia namba iliyoingia yenye jina la Shehna na kuipiga. Simu ilionekana kuwa bize inazungumza.
"Simu yake inaongea."
"Mmh! Si ulitoka nje, mlinzi anasema kuna mgeni aliingia?"
"Hata yeye anasema hajamuona."
"Mmh! Mtu gani tusimuone wote basi atakuwa jini."
"Hapana si jini, nitampigia tena."
Mustafa aliachana na mambo ya mgeni asiyeonekana, alikumbuka amesahau pete yake msalani wakati akimuwahi mgeni. Alikwenda hadi sehemu ya kunawia mkono, alishtuka kukutana tena na harufu ya manukato aliyokutana nayo ofisini kwake.
Alipoangalia juu sinki hakuiona pete yake.
Alishtuka na kuangalia chini labda imeanguka vilevile hakuiona, aliingia msalani kuitafuta pia huko hakuiona.
Akili yake ilimweleza kuwa pete ile aliivua wakati akitaka kunawa mikono. Alitoka hadi kwa Sara kumuulizia.
"Sara kuna mtu ameingia msalani wakati nlipoingia ofisini?"
"Hakuna."
"Unajua wakati nanawa niliweka pete yangu ya ndoa juu ya sinki, baada ya kuzungumza na simu niliwahi ofisini lakini ajabu nimerudi sijaikuta."
"Mmh! Umeangalia vizuri?"
"Nimeangalia, Sara au leo sikuja na pete?"
"Umekuja nayo, si unakumbuka nilikutania siku ukiipoteza utamwambia nini mkeo."
"Nakumbuka, sasa imekwenda wapi?"
"Mmh! Mbona mauzauza leo."
"Huwezi kuamini ile harufu ya manukato nimekutana nayo tena msalani."
"Wewe!" Sara alishangaa.
"Kweli Sara."
"Bosi, hebu tulia kwanza inawezekana leo umeamka na mawazo mengi kutokana na ishu ya wifi. Nilikueleza mkienda Mbagala kila kitu kitakuwa sawa, yule mama kawasaidia wengi. Sema bosi tatizo ulilificha sasa hivi ungekuwa na mtoto."
"Ni kweli, jana niliporudi nimemkuta wifi yako analia."
"Tatizo?"
"Lilelile la mtoto, anasema sijui kawasikia watu wakimsema kwa mafumbo kwamba yeye ni tasa."
"Hukumweleza tuliyozungumza jana?"
"Nimemweleza lakini anasema amechoka na uongo wa waganga, tangu tuanze kuhangaikia mtoto huu mwaka wa tano sasa."
"Mwaka wa tano?" Sara alishtuka.
"Ndiyo, na fedha tulizopoteza tungeweza kujenga nyumba kubwa na gari mbili."
"Bosi yule mama kiboko wapo waliokata tamaa kama yeye lakini walipotumia dawa zake walipata watoto."
"Mbona kuna sehemu tulikwenda na kuelezwa hivyohivyo mpaka waliopata watoto tuliwaona, lakini alipotumia hakupata kitu."
"Hebu nendeni Mbagala tuone."
"Alikubali kwa shingo upande, hivi namsubiri amesema atanipitia saa tano tuelekee huko Mbagala."
"Basi bosi kapumzishe akili labda baadaye utakumbuka ulipoiweka pete."
Mustafa alirudi ofisini kwake na kukaa kitini, alijitazama vidole vyake asiamini kama kweli hakuja na pete.
Akiwa bado anavishangaa vidole vyake simu yake iliita, alipoangalia alikutana na jina la Shehna. Aliipokea:

Itaendelea tu Mkuinipatia (Like) Zenu ninawangojea ...........................
 
Hadithi ya kusisimuwa Mimba ya Jini- 2


ILIPOISHIA:

Alitoka haraka ili amuwahi kwa kuamini huenda ameamua kutoka baada ya kuchoka kumsubiri. Lakini aliamini hakutumia muda mrefu msalani.
Alikwenda hadi getini kwa mlinzi na kuulizia.
"Eti kuna mgeni ametoka sasa hivi?"
"Mgeni! mgeni gani?" mlinzi ilionesha kushtuka.
"Mwanamke."
"Bosi, toka uingie wewe hajaingia mtu yeyote."

SASA ENDELEA...
"Hapana, labda ulitoka eneo la kazi, mgeni alikuwa ofisini kwangu sasa hivi."
"Bosi hakuna mgeni yeyote zaidi ya dada Sara ambaye alikutangulia kuingia kabla yako."
"Mmh! Hebu ngoja."
Mustafa alirudi hadi ofisini na kumuuliza Sara, sekretari wake aliyekuwa bize na kazi kwenye kompyuta.
"Sasa mgeni ametoka?"
"Mgeni gani?" Sara naye alionesha kushtuka.
"Aliyekuwa ofisini kwangu sasa hivi."
"Bosi, hakuna mgeni yeyote aliyefika hapa, kwanza ilianza lini kumruhusu mgeni aingie ofisini kwako bila ruhusa yako?"
"Sasa huyu mgeni kaingiaje na kapitia wapi?"
"Bosi mgeni unayemsema umemuona wapi?"
"Hebu njoo ofisini."
Sara na Mustafa waliongozana hadi ofisini ambako bado harufu ya manukato makali ilikuwa ikinukia.
"Bosi pafyumu nzuri kama hii umeitoa wapi?" Sara alisema huku akinyanyua pua zake kuivuta.
"Sara, haya manukato nimeyakuta baada ya kurudi kutoka msalani."
"Muongo!" Sara alishangaa.
"Kweli kabisa, yanaonekana ya huyo mgeni aliyeingia ofisini."
"Sasa kapitia wapi?"
"Hebu subiri."
Mustafa alisema huku akichukua simu yake juu ya meza, aliangalia namba iliyoingia yenye jina la Shehna na kuipiga. Simu ilionekana ipo bize inazungumza.
"Simu yake inaongea."
"Mmh! Si ulitoka nje, mlinzi anasema kuna mgeni aliingia?"
"Hata yeye anasema hajamuona."
"Mmh! Mtu gani tusimuone wote basi atakuwa jini."
"Hapana si jini, nitampigia tena."
Mustafa aliachana na mambo ya mgeni asiyeonekana, alikumbuka amesahau pete yake msalani kumuwahi mgeni. Alikwenda hadi sehemu ya kunawia mkono, alishtuka kukutana tena na harufu ya manukato aliyokutana nayo ofisini kwake. Lakini alipoangalia juu ya sinki hakuiona pete yake.
Alishtuka na kuangalia chini labda imeanguka vilevile hakuiona, aliingia msalani kuitafuta pia huko hakuiona. Akili yake ilimweleza kuwa pete ile iliivua wakati akitaka kunawa mikono. Alitoka hadi kwa Sara kumuulizia.
"Sara kuna mtu kaingia msalani wakati naingia ofisini?"
"Hakuna."
"Unajua wakati nanawa niliweka pete yangu ya ndoa juu ya sinki, baada ya kuzungumza na simu niliwahi ofisini lakini ajabu nimerudi sijaikuta."
"Mmh! Umeangalia vizuri?"
"Nimeangalia, au Sara, leo sikuja na pete?"
"Umekuja nayo, si unakumbuka nilikutania siku ukiipoteza utamwambia nini mkeo."
"Nakumbuka, sasa imekwenda wapi?"
"Mmh! Mbona leo mauzauza."
"Huwezi kuamini ile harufu ya manukato nimekutana nayo tena msalani."
"Wewe!" Sara alishangaa.
"Kweli Sara."
"Bosi, hebu tulia kwanza inawezekana leo umeamka na mawazo mengi kutokana na ishu ya wifi. Nilikueleza mkienda Mbagala kila kitu kitakuwa sawa, yule mama kawasaidia wengi. Sema bosi tatizo ulilificha sasa hivi ungekuwa na mtoto."
"Ni kweli, jana niliporudi nimemkuta wifi yako analia."
"Tatizo?"
"Lile lile la mtoto, anasema sijui kawasikia watu wakimsema kwa mafumbo kwamba tasa."
"Hukumweleza tuliyozungumza jana?"
"Nimemweleza lakini anasema amechoka na uongo wa waganga, toka tuanze kuhangaikia mtoto huu mwaka wa tano sasa."
"Mwaka wa tano?" Sara alishtuka.
"Ndiyo, na fedha tuliyopoteza tungeweza kujenga nyumba kubwa na gari mbili."
"Bosi yule mama kiboko wapo waliokata tamaa kama yeye lakini walipotumia dawa zake walipata watoto."
"Mbona kuna sehemu tulikwenda na kuelezwa hivyo hivyo mpaka waliopata watoto tuliwaona, lakini alipotumia hakupata kitu."
"Hebu nendeni Mbagala tuone."
"Alikubali kwa shingo upande, hivi namsubiri amesema atanipitia saa tano tuelekee huko mbagala."
"Basi bosi kapumzishe akili utajua pete umeiweka wapi."
Mustafa alirudi ofisini kwake na kukaa kitini, alijitazama vidole vyake asiamini kama kweli hakuja na pete. Akiwa bado anavishangaa vidole vyake simu yake iliita, alipoangalia alikuta ni Shehna. Aliipokea:
Itaendelea
 
Duh ile ishaisha tena mm nlikua wp ngoja niisake kwnz ndani ya jeneza duh huku kupeana assignment kiana MziziMkavu
 
Last edited by a moderator:
[h=1]Hadithi ya Kusisimuwa Mimba ya Jini- 3[/h]
ILIPOISHIA:
"Basi bosi kapumzishe akili utajua pete umeiweka wapi."
Mustafa alirudi ofisini kwake na kukaa kitini, alijitazama vidole vyake asiamini kama kweli hakuja na pete. Akiwa bado anavishangaa vidole vyake simu yake iliita, alipoangalia alikuta ni Shehna. Aliipokea: SASA ENDELEA..."

Haloo."
"Haloo Mustafa samahani, niliwahi kutoka kwa vile kuna sehemu nilitakiwa kuwahi."
"Umepitia wapi?"
"Jamani Mustafa kuna njia ngapi ya kuingia na kutokea ofisini kwako?"
"Moja."
"Basi ndiyo niliyopitia."
"Mbona sekretari wangu hajakuona?"
"Nimemkuta yupo bize ila sikutaka kumsumbua kwa vile mlango wako ulikuwa wazi."
"Huyo hajakuona, na mlinzi?"
"Sikumkuta inawezekana alikuwa msalani."
"Mmh!"
"Mustafa unaguna nini?"
"Aah! Basi yaani bado ujio wako umekuwa kitendawili, pete yangu umechukua?"
"Mustafaa! Niichukue ili iweje tuna uhusiano?"
"Hapana."
"Sasa pete yako niichukue vipi wakati hatuna uhusiano wa kimapenzi?"
"Nashangaa."
"Umemuuliza mkeo?"
"Nimuulize nini ikiwa nimeondoka nikiwa nimeivaa?"
"Mustafa acha ubishi, hebu muulize mkeo."
"Nitamuuliza."
"Muulize sasa hivi kisha nitakupigia," Shehna alisema na kukata simu.
Mustafa hakutaka kuendelea kubisha aliamua kumpigia simu mkewe lakini alijua ni kuchochea matatizo kwa vile alikumbuka aliondoka nyumbani na pete kidoleni. Baada ya simu kupokelewa upande wa pili alimuuliza mkewe;
"Samahani mke wangu eti pete nimeiacha nyumbani?"
"Ndiyo, nashangaa kuiona kwenye sinki la kunawia mikono msalani."
"Ooh! Afadhali," Mustafa alishusha pumzi ndefu.
"Mbona umeshusha pumzi ndefu?" mkewe alimuuliza.
"Yaani nimeitafuta kila kona ofisini nilidhania nimepoteza."
"Una tabia ya kuvua pete?" mkewe alimuuliza.
"Ninapotoka msalani sitaki ipate maji."
"Basi pole mume wangu uliisahau, mi namalizia kazi nakuja."
"Hakuna tatizo."
Mustafa alikata simu na kushusha tena pumzi na kuamini kabisa siku ile aliamka akiwa na mawazo mengi. Lakini kitu kingine kilichomshangaza harufu ya manukato aliyoyasikia ambayo hakuwahi kuyasikia maishani mwake. Simu yake iliita, ilikuwa ya Shehna.
Aliipokea:
"Haloo."
"Vipi, mkeo amesemaje?"
"Amesema niliisahau nyumbani."
"Sasa inakuwaje unanishushia lawama?"
"Samahani nilichanganyikiwa."
"Sasa kuna kitu muhimu kilinileta asubuhi ya leo ambacho kimekutesa kwa miaka mitano."
"Kitu gani hicho?" Mustafa alishtuka.
"Mtoto."
"Umejuaje?"
"Mustafa acha kujitoa akili, habari za mkeo kukosa mtoto kwa miaka mingi uliniambia mwenyewe na kuhangaika kwa waganga wa kila aina wa ndani na nje. Uliniambia umepoteza fedha nyingi lakini hakuna manufaa yoyote. Kutokana na kuhangaika sana imefikia hatua ya kukata tamaa japokuwa mnataka kwenda leo Mbagala kujaribu mara ya mwisho uongo kweli?"
"Kweli, nilikuambia lini?"
"Sasa inamaana ningejuaje bila wewe kuniambia?"
"Basi nimechanganyikiwa kiasi cha kusahau kama niliwahi kuzungumza na wewe ishu hiyo."
"Tuachane na hayo, Mustafa nataka nikusaidie mkeo kupata mtoto lakini naomba na wewe unisaidie shida yangu."
"Shida gani?"
"Kwanza nataka mkeo apate mtoto mengine yatafuata, ila naomba uniahidi mkeo akipata mtoto na mimi utanisaidia?"
"Nakuahidi ukinisaidia mke wangu kupata mtoto unachokitaka kama kimo ndani ya uwezo wangu nitakusaidia pia nitakupa zawadi kubwa sana."
"Basi naomba msiende kwa mganga dawa nitampelekea mimi."
"Nitaamini vipi kama utakayompa ni dawa?"
"Utaamini mkeo akishika ujauzito mwezi huu."
"Mmh! Sawa."
Baada ya mazungumzo alikata simu na kutulia akiwaza huku akiamini matatizo ya mkewe kuchelewa kupata mtoto yamemchanganya sana hasa baada ya familia yake kuingilia kati na kumtaka aoe mwanamke mwingine kutokana na sheria ya dini yake.
Siku zote hakutaka kuongeza mwanamke mwingine kwa kujua atakuwa hakumtendea haki mkewe pia kufanya vile ni kumnyanyapaa.
Kibaya zaidi alijua angemuumiza mkewe kama mwanamke aliyemuoa angepata mtoto ungekuwa ukatili mkubwa kwa sababu wote hawakuwa na tatizo la kiafya zaidi ya kuchelewa tu kupata mtoto.
Akiwa katika lindi la mawazo simu yake iliita, alipoangalia alikuwa mkewe, aliipokea:
"Haloo mke wangu."
"Mume wangu pole na kazi."
"Asante."
"Eti kuna dada mmoja anaitwa Shehna amenipigia simu na kunieleza matatizo yangu kama niliwahi kumweleza na kunieleza kuwa amezungumza na wewe kuhusu dawa ya matatizo yangu na kuniambia nisiende tena kwa waganga dawa atakayonipa itatoa majibu mwisho wa mwezi huu?"
"Hata mimi kaniambia hivyo... hebu subiri kuna mtu anagonga mlango."
"Sawa."
Baada ya dakika tatu mkewe alipiga tena simu ambayo aliipokea.
"Ehe, mke wangu."
"Kuna kijana kaleta kichupa kidogo chenye maandishi ya Kiarabu, kasema kapewa na dada mmoja ambaye hakumuona sura kutokana na kuvaa hijabu iliyomziba uso."
"Kwa hiyo tusiende Mbagala?"
"Hebu tuangalie na uongo wake."
Mustafa alikubaliana na mkewe wasiende tena kwa mganga, alimpigia simu Shehna kutaka kumshukuru. Lakini simu haikuwa hewani, aliachana naye na kuendelea na kazi zake.
***
Kutokana na wingi wa kazi, Mustafa alirudi nyumbani usiku na baada ya chakula walikwenda kuoga na kurudi kitandani.
"Mume wangu Shehna alisema tukutane kimwili saa nne kamili ili yai la uzazi lisipotee," mke wa Mustafa alimweleza mumewe.
"Alikupa maelekezo jinsi ya kutumia hii dawa?"
"Ooh! Nilisahau kumuuliza."
"Sasa tutafanyaje?"
"Namba yake si unayo mpigie."
Mustafa alinyanyuka kitandani na kwenda kuchukua simu, alitafuta jina la Shehna ili ampigie lakini ajabu halikuonekana.
"Mbona jina lake silioni kwenye simu?"
"Kwani alipokupigia hukusevu namba yake?"
"Namba yake ilikuwemo kwenye simu."
Mkewe naye alichukua simu yake kuangalia namba ya Shehna ambayo hakuiona.
"Hata kwangu siioni."
"Sasa tutafanyaje?"
"Yaani najilaumu kutomuuliza maelekezo ya dawa, sasa hatujui tumywe au tujipake."
"Heri maandishi yaliyoandikwa kwenye chupa yangekuwa ya Kingereza tungeweza kusoma maelekezo lakini Kiarabu siambui hata moja."
"Sasa tutafanyaje na muda unakaribia?"
"Hatuna jinsi kwa vile hakutupa maelekezo pia namba yake haipatikani,"
Mustafa alinyamaza baada ya simu yake kuita, aliichukua na kuitazama na kujikuta akitamka kwa sauti.

Je, kiliendelea nini? Usikose baadae
 
waiting.......

Duh ile ishaisha tena mm nlikua wp ngoja niisake kwnz ndani ya jeneza duh huku kupeana assignment kiana MziziMkavu

Ndugu Mzizimkavu unatuchosha na habari za kijuu juu na bora umalize mkasa wote

MziziMkavu nakushauri uwe unakusanya hadithi yote then uiweke hapa mara moja tu. Unatukatiza pataamu sana bhana!

Al haji mzizi vipi bwana stimu inakata.

Mzizimkavu unatisha tunasubira kifwatacho kwa hamu

Mr.dryroot!
Niwawekeeni hadithi Mnashindwa hata kuweka (Like) ? Munapenda vya bure tu acheni Roho mbaya hizo.
 
[h=2]Hadithi ya kusisimuwa mimba ya jini-4-[/h]
ILIPOISHIA:
"Sasa tutafanyaje na muda unakaribia?"
"Hatuna jinsi kwa vile hakutupa maelekezo pia namba yake haipatikani,"
Mustafa alinyamaza baada ya simu yake kuita, aliichukua na kuitazama na kujikuta akitamka kwa sauti.
SASA ENDELEA...

"Shehna."
"Amepiga?" mkewe aliuliza huku akinyanyuka kutaka kuona kwenye simu.
"Ndiyo."
"Pokea haraka kabla hajakata."
Mustafa alipokea simu.
"Haloo Shehna."
"Jamani mbona una pupa hivyo mwanaume wewe."
"Lazima niwe na pupa kutokana na muda kusogea bila kuwa na maelezo ya matumizi ya dawa uliyotupa."
"Ni kweli niligundua nilifanya kosa najua muda umekwenda sana, sasa chukua ndoo ya maji weka maji yaliyomo kwenye hicho kichupa nusu kisha mkaoge kwa vile muda utakuwa umekaribia baada ya kuoga jifuteni maji.
Kabla ya tendo, kila mmoja ajipake mafuta hayo sehemu zake za siri ndipo muingiliane baada ya tendo kila mmoja anywe kidogo kisha muonge tena kwa kuweka mafuta yaliyobakia kwenye chupa na kulala."
"Samahani Shehna."
"Bila samahani."
"Tunaweza kuoga na sabuni?"
"Hapana, mnaoga hivyo hivyo."
"Sawa nimekuelewa."
"Mlikuwa mnataka mtoto gani?"
"Ye yote."
"Mbona moyoni wewe unataka mtoto wa kiume?"
"Ni kweli lakini atakayepatikana nitampokea."
"Na mkeo?"
"Ye yote," alisema Mustafa.
"Mbona unamsemea."
"Yeyote tu ni mtoto," mke wa Mustafa alijibu kwa sauti.
"Mbona uliweka nadhili mtoto wa kwanza akiwa mwanamke utampa jina la mama yako?"
"Ni kweli, lakini atakayekuja nitampokea."
"Sasa mnaweza kukubaliana mnataka mtoto gani atangulie, kama wa kike mtakunywa hayo mafuta kabla ya tendo kama wa kiume, mtakunywa baada ya tendo."
"Tumekuelewa."
"Mna swali?" Shehna aliuliza.
"Hatuna."
"Haya usiku mwema."
"Na kwako pia."
Baada ya simu kukatika Mustafa alimgeukia mkewe na kumuuliza.
"Nina imani umesikia, unataka tutangulize mtoto gani?"
"Wa kike."
"Kwa nini asianze wa kiume?"
"Si umesema upo tayari kupokea mtoto yeyote."
"Naomba mke wangu unipe upendeleo kwa huyu wa kwanza."
"Umeshindwa vipi kunipa upendeleo mkeo wa pili awe wa kiume?"
Walijikuta wakisahau muda ulikuwa umekwisha hivyo walitakiwa kutekeleza walichoelekezwa. Mpaka wanakubaliana muda walioelekezwa ulikuwa umevuka zaidi ya dakika kumi na tano.
"Mke wangu tumevusha muda tulioambiwa tutafanyaje?"
"Kwani saa nne imevuka?"
"Lakini alisema saa nne juu ya alama."
"Ilikuwa kutufanya tuwe makini zaidi, lakini muda haujapita sana."
Walikwenda kuoga kwa kufuata maelekezo yote, baada ya kuoga walijipaka manukato na kunywa kwa vile walikubaliana kutanguliza mtoto wa kike. Baada ya hapo alikutana kimwili na baada ya tendo walikwenda kuoga na kurudi kitandani kulala.
***
Usiku, Mustafa aliota akifanya mapenzi na mwanamke nzuri wa kiarabu ambaye alimweleza anataka kuzaa naye. Siku ya pili aliamka amechoka sana kutokana na kutumika mara mbili kwanza na mkewe pili katika njozi.
Alipoamka hakumueleza mkewe alivyoota, alioga na kupata kifungua kinywa na kuwahi kazini. Mustafa akiwa kazini simu yake iliita, ilikuwa ya Shehna, aliipokea haraka.
"Haloo Shehna!"
"Aah! Mustafa, tanguliza asalamu aleykumu."
"Ooh! Samahani, asalamu aleykumu."
"Waleykumu salamu."
"Haya bibie niambie?"
"Nilitaka kukusalimia tu, pia kukueleza jinsi ulivyonifurahisha kwa kutunza siri zako."
"Siri gani?"
"Unajua wanaume wengi kila kinachotokea huwaeleza wake zao."
"Mimi kimenitokea nini?"
"Unakijua, lakini hukutaka kumwambia mkeo."
"We' umejuaje?"
"Mustafa tuachane na hayo, mbona jana umeniangusha?" Shehna alibadili mada.
"Kivipi?"
"Niliwaambia mfanye mapenzi saa ngapi?"
"Saa nne."
"Ndiyo muda uliofanya?"
"Hapana lakini haikuvuka sana."
"Mustafa niliwaeleza saa nne kamili lakini mmevuka muda, kwa nini umepuuza maagizo yangu?"
"Samahani kwa hilo."

Itaendelea
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom