Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 7,194
- 12,689
Mwandishi: Hans Christian Andersen, 1837
Kimetafsiriwa na Pictuss.
Email: pictuspublishers@gmail.com.
Pictuss2021.
Haki zote zimehifadhiwa. Hakuna sehemu yoyote ya tafsiri hii inayoweza kunakiliwa, kutolewa kivuli(photocopy), kuhamishwa, kurekodiwa au kutolewa kwa namna yeyote bila ya taarifa ya awali ya kimaandishi ya mtafsiri.
VAZI JIPYA LA MFALME
Hapo zamani za kale kulikuwa na mfalme aliyependa sana mavazi na kuvaa. Alitumia pesa zake zote kununulia nguo. Hakujali kuhusu wanajeshi wake wala kwenda kwenye matamasha ya maonyesho kama wafalme wengine. Alienda iwapo tu alikuwa na nguo mpya za kuonyesha kwa watu.
Alivaa nguo tofauti kila saa ya siku. Wafalme wengi walitumia muda wao mwingi kwenye mabaraza ya kuhukumu na kushauriana lakini yeye almu ya ikuwa akishinda kwenye kabati la nguo.
Siku moja matapeli wawili wakijiita washonaji waliingia kwenye nchi hiyo. Walisema wanaweza kushona nguo nzuri yenye rangi na mapambo ya kupendeza sana.
Walisema nguo hiyo itatengenezwa na kitambaa ambacho hakitaonekana na yeyote yule aliye mjinga au asiyefaa kitu. Kifupi, mtu mwenye uelewa mdogo asingeweza kuiona nguo hiyo.
" Bila shaka itakuwa nguo nzuri sana" aliwaza mfalme.
" Kama nikiwa na nguo kama hiyo nitajua mara moja watu gani hawanifai kwenye uongozi wangu. Nitakuwa na uwezo wa kutofautisha wajinga na werevu, inabidi nishonewe nguo hii mara moja".
Akawaita wale washonaji na kuwapa pesa nyingi sana ili wamshonee nguo ile mara moja.
Wale matapeli wakaunganisha mashine ya kufumia vitambaa mara moja. Walifanya kazi kwa bidii sana, japo kiukweli walikuwa hawafanyi kazi yeyote. Waliomba kupewa nyuzi bora za hariri na nyuzi bora za dhahabu. Wakaziweka kwenye mikoba yao.
Wakaendelea kufanya kazi kwenye vmashine ya kufumia usiku na mchana lakini hakukuwa na nyuzi zozote kwenye machine.
"Nahitaji kujua wale mafundi wamefikia wapi na nguo yangu" alijisemea mfalme siku moja.
Akakumbuka kuwa mtu mwenye uelewa mdogo au ambaye hafai hawezi kuona kitambaa hicho, akaanza kuwa na wasiwasi. Lakini akajipa moyo kuwa haiwezekani yeye akawa mjinga na mtu asiyefaa kitu, pamoja na hilo akaona ni salama akimtuma mtu mwingine.
Watu wote kwenye ufalme ule walikuwa wamesikia kuhusu nguo yenye kitambaa cha ajabu. Wote walisubiri kwa hamu kujua iwapo majirani zao ni werevu au wajinga.
"Nitamtuma mtu wangu muaminifu na mwenye busara kwa wafumaji" mfalme alisema peke yake."
Huyu ni mtu mwerevu na hakuna anayeweza kufanya kazi kwa ufanisi kama yeye".
Kwahiyo huyu mzee wa busara akatumwa kwa wale mafundi matapeli ambao walikuwa wakifanya kazi kwa bidii kwenye mashine ya kufumia isiyo na nyuzi hata moja.
Alipofika alipatwa na mshangao mkubwa. " Hii inamaanisha nini!?" Aliwaza yule mzee huku macho yakimtoka. " Siwezi kuona hata nyuzi moja!" Hata hivyo hakusema mawazo yake kwa sauti.
Wale matapeli wakamkaribisha kwa bashasha akaribie mashine ya kufumia. Baada ya kukaribia wakamuuliza iwapo amependezwa na kitambaa kinachofumwa?
Wakamuuliza iwapo rangi zinapendeza huku wakimuelekeza kwa vidole sehemu tupu za mashine ya kufumia. Mzee yule alijitahidi kuangalia lakini hakuona kitu.
"Hiki nini!" Akawaza " kuna uwezekano mimi ni mjinga! Sijawahi fikiria hilo! Mtu yeyote hatakiwi kujua kuwa mimi ni mjinga na sifai kitu".
"Hapana, hapana, mfalme hapaswi kujua hili, sitamwambia yeyote kwamba siwezi kuona kitambaa kinachofumwa"
"Mzee haujatuambia iwapo umeridhika na kitambaa hiki?" aliuliza mfumaji mmoja huku akijidai kufanya kazi ya kufuma kwa bidii.
"Oh! Ni kizuri sana" alijibu yule mzee huku akiangalia mashine ya kufumia.
" Rangi na urembo vinavutia, nitaenda kumjulisha mfalme mara moja jinsi kilivyo kizuri".
" Tutashukuru sana" walisema wale matapeli. Wakaanza kumuelezea kuhusu rangi na urembo huku wakimuonyeshea kwenye kitambaa ambacho hakipo.
Mzee yule alisikiliza kwa makini maelezo yao ili aweze kumueleza mfalme. Wale matapeli wakaagiza waongezewe dhahabu na hariri ili waweze kukamilisha kazi yao.
Walipopewa, vyote wakaweka kwenye mikoba yao kisha wakaendelea kufanya kazi kwa bidii kwenye mashine tupu ya kufumia.