Hadithi -The girls in Island -06

chiqutitta

JF-Expert Member
Nov 13, 2015
1,160
3,124
SEHEMU YA SITA
THE GIRLS IN ISLAND 06



Baada ya mwendo mrefu, tuliona mwisho wa msitu huo na mbele yake kulikua na majani mafupi kama yaliyolimwa. Tukakazana mpaka tukafika eneo hilo. Hatukuamini macho yetu baada ya kufika eneo hilo. Tulizisikia kelele za watu na baada ya kusogea eneo hilo tuliona viumbe wa ajabu wakiwa uchi huku maziwa na nyeti zao ziikionyesha kuwa walikua jinsia ya kike.

Walikua wanawavua nguo watu waliowakamata na kuwarusha kwenye sufuria kubwa sana lilikua na uwezo wa kuigia hata watu kumi na tano. Lilikua na maji ya moto yaliyochemka vibaya huku viumbe wengine wakiendelea kukoka moto kwa miti mikavu.



Hapo kila mmojaa alibaki ametoa macho huku mioyo yetu ikidunda kuliko kawaida. Bila hiyari yangu, nikajikuta mwili mzima umetokwa na vipele vya baridi na macho yangu yakiwa yanatoka machozi kutokana na mpasuko wa moyo niliokuwa nao baada ya kuona mtu akipikwa huku akiwa hai.

Hatukuweza kukaa na kuendelea kuangalia yale yanayofanyika pale. Tulitoka na kuondoka zetu huku kila mmoja akiwa hana imani kama tunaweza kusalimika na kutoka salama kwenye kisiwa kile.

Tulirudi tena kwenye lile pango na kuanza kutafuta mahala ambapo tulihisi kuna usalama na tukajibanza na kuanza kukaa humo.

Baada ya kutulia kwa muda, hapo njaa ndio ilinianza kuniuma. Nilipo watazama wenzangu, nao alikua wanalalamika kama mimi.

“huu ndio mwisho wetu jamani, maana kama hatujapikwa tukiwa hai basi tutakufa kwa njaa.” Aliongea Bokker na kutuangalia wote kwa zamu.



“usiwe na moyo wa kike wewe, kama jogoo hafi kwa utitiri basi hata wewe huwezi kufa kwa njaa ya siku moja au mbili.” Aliongea Saidi na wote tukamuunga mkono.



Baada ya muda, tulisikia vishindo vya miguu ikiwa inakuja upande tuliokuwepo. Hapo tulitawanyika huku kila mmoja akijibanza mahala ambapo kulikua na giza kidogo. Walipita wasichana wazuri sana ambao walivalia vibwaya peke yake huku maziwa yao yakiwa hayajafunikwa na kitu chochote.

Hatukuweza kuwatambua kwa haraka walikua na asili gani kwakua walikua weupe lakini wakiwa na maumbile ya kibantu. Walikua na nywele ndefu kama wahindi na matumbo yao yalikua madogo yaliyovutia sana. Lakini hakuna ambaye alishawishika na uzuri wa wasichana hao kwakua kila mmoja alikua na hofu ya usalama wa maisha yake.



Baada ya kundi hilo la wasichana wapatao sabini kupita maeneo hayo, hali ilitulia tena mpaka tulipoona miale ya jua la asubuhi. Hakuna ambaye alipata hata lepe la usingizi kati yetu. Hata kama alikuwepo, basi alilala wima hapo hapo alipojificha.



“mnaonaje kama tukitoka na kwenda kutafuta chakula?” aliongea Philipo baada ya kukaa kimya kama masaa mawili bila mtu yeyote kuongea kitu asubuhi hiyo.

“hata mimi naona ni wazo jema jamani, maana kufa njaa ni kufa kizembe.” Niliongea maneno ya kishujaa yaliyo pitishwa na kila mmoja aliyekuwa pale.

Tulitoka na kupiga moyo konde huku mimi nikiomba dua kwa Mungu wangu anilinde na majini wale wala watu.



Tulihangaika sana bila kufanikiwa hata kupata mti wenye matunda. Baada ya muda, tuliona miti ambayo ilikua na matunda ya zaituni. Tulifika na kuanaza kuyatupia mawe yale matunda na kufanikiwa kuyachuma kwa wingi sana. Tulikula mpaka matumbo yakatuuma.



Kiu kikaja kuwa kikwazo kingine. Hapo hatukua na jinsi, tulianza kuyasaka maji huku kila mmoja wetu akiwa tayari kwa lolote. Maana uwezekano wa kutoka pale hakuna aliyekua ameliweka katika kichwa chake.



Baada ya kutalii kwa muda msituni humo, tulifanikiwa kuona bwawa lililokuwa na maji masafi sana. Tulipoangalia vizuri, kwa mbali tuliona wasichana wakiwa uchi wakioga kwenye bwawa hilo.

Hakika tulisahau matatizo kwa muda kwa kucheki movie ile ya wasichana ambao walikua na uzuri na mvuto ambao naamini katika dunia hii walikua wanaongoza. Tuliwaangalia mpaka walipomaliza kuoga na kwenda kuvaa nguo zao na kuondoka.



Hapo ndio tulipata muda wa kusogea kwenye lile bwawa na sisi tukapata kukata kiu yetu kwa kuyafakamia maji.

“manaonaje kama tukiweka kambi karibu na hapa?” aliuliza Booker.

“nani asiyekujua kuwa wewe ni mzee wa mademu, yaani hukuona sehemu yoyote zaidi ya hapa ambapo kuna wasichana wanaoga… acha tamaa zako Bokker.” Nilimchana live na hakuweza kuongea lolote tena. Wenzangu wote wakabaki wanacheka na kumfanya Bokker naye atabasamu.



Tulisogea pembeni kidogo ya lile bwawa na kukuta baadhi ya miti ikiwa imeanguka. Hapo wazo la kujenga nyumba ya miti likaja. Tukashirikiana wote kwa pamoja na kufanikiwa kujenga nyumba na kumaliza usiku ambapo tulillala kama tumekufa kwa jinsi tulivyokua tumejawa na uchovu pamoja na usingizi wa siku mbili..



Tuliamka salama asubuhi na kurudi kule kwenye mizaituni. Tulichuma matunda mengi na kurudi nayo kwenye kijumba chetu tulichokijenga na kuyajaza humo angalau yatusukume angalau siku tatu.



Baada ya hapo, tulienda kwenye bwawa na kukuta maji yametulia huku hakuna hata mtu mmoja anayeonekana maeneo ya karibu na hapo.

Tuliingia na kuana kuoga huku kila mmoja akiwa anayasifia maji hayo kutokana na utamu na ubaridi wake mdogo uliokua unatupa burudani.



Hatukujua kua tumetumia muda gani kwenye lile bwawa. Ila tulioga mpaka tukajisahau kabisa kama tupo kwenye matatizo.

Baada ya kumaliza kuoga, tulitoka nje ya bwawa pamoja na kuangaza nje ya lile bwawa. Hatukuamini baada ya kuona tumezungukwa na warembo waliokua wanatushangaa. Kila niliyemtupia jicho alikua ananikonyeza na kung`ata meno kama ishara ya kunitambani. Tulitazamana huku tukiwa tumepigwa na bumbuwazi. Hatukujua tuchukue uamuzi gani kwa wakati huo.

Kabla hata akili hazijachekecha na kutuambia tutumie njia gani katika kuwakabili wale warembo waliokuja kuoga. Tulishangaa kuona wote wakianza kusaula nguo zao huku wakiwa wanatabasamu na kutuonyesha meno yao yaliyojipanga vizuri na kuongeza uzuri katika muonekano wa sura zao.



Hisia za uoga ziliniondoka kwa kasi na moyo wa kishujaa ukanipanda. Ukijumlisha na ukame wa kutokutana kimwili na msichana siku nyingi ndio kabisaa. Nilijipa moyo kuwachangamkia vizuri tu kama wakijilengesha kwangu na kuhitaji wajumuike na mimi. Mawazo hayo hayakua kwenye kichwa changu tu, wote tulikua na mawazo hayo hasa hasa Bokker ambaye yeye akiona upaja tu basi anachanganyikiwa. Sasa leo ndio kakutana na warembo ambao hajawahi hata kuwaota halafu ndio wanamchekea na kumvulia nguo.

Niligeuza shingo yangu na kuwaangalia wenzangu ambao walikua wanatabasamu huku wakijilamba kama nyoka kwa uchu.



Kwa mapozi ya ajabu na catwerk za kimisi, wale warembo wapatao kumi walianza kutufuata huku wakiwa kama walivyozaliwa na kuingia kwenye lile bwawa tulilokuwemo.

Wakati nimebung`aa, nilishtukia tu mkono wa mtoto mmoja ambaye niliishiwa pozi nilipotazama macho yake ya mahaba yaliyolegea utadhani amekula kungu.

Kabla sijakaa sawa, alinyanyua mguu wake na kunibana usawa wa kiuno changu na kunifanya nianze kusikia vitu vinagombana huko kwenye boxer niliyovaa.



Nilipiga chabo kwa wenzangu na kuwakuta saa nyingi walishaanza kupiga vitu vyao. Nilibaki mimi tu ambaye nilijifanya mgumu huku kiukweli hali yangu ilikua mbaya wakati huo.

Nilishtushwa na ulimi wa mrembo mwingine ulionitambalia kama shoti ya umeme ukipitishwa kwenye sikio langu. Hapo nilitoa mhemo wa ajabu uliomfanya yule mrembo mwengine kuzidisha sifa kwa kuanza kutalii kwa ulimi wake kwenye shingo yangu. Walinichangia warembo hao na kunifanya nibaki nyang`a nyang`a kabisa.

Mpaka hapo, nikawa kama ngamia aliyekubali kuelekea kibla tayari kwa kuchinjwa. Hata sikuelewa boxer yangu ilivuka saa ngapi, nami nikajikuta nipo kama nilivyozaliwa.



“BAINA NA KELI”



Ilisikika sauti kutoka nje ya lile bwawa. Nikashangaa kuona wale wasichana wakiniachilia haraka na kusimama kikakamavu. Nilipotupa macho yangu mbele, niliona kundi la wasichana wazuri lakini wakiwa wamejazia kama wale wanaonyanyua vitu vizito.

Katikati nilimuona msichana mzuri aliyevalia nguo ndefu kama ya kihindi hivi lakini alipokua anapiga hatua zake kuja tulipokua, niliona mpasuo mkubwa sana uliosogea mpaka kwenye paja lake.

Juu alivaa taji kama la kimisi hivi huku sura yake ikipambwa na urembo mbali mbali uliomfanya azidi kuwa mzuri. Niliwatazama wenzangu waliokua kama wamelewa kwa jinsi walivyoshughulikiwa na wale mabinti.

Mimi nilitulia na kumuangalia yule dada aliyekua anatamba na kunyenyekewa. Hapo ndio akili yangu iliponisomea kua yule dada atakua ndio kiongozi wa wale wasichana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom