Story za nguate
Member
- Mar 20, 2022
- 27
- 46
Hadithi: TEARS IN MY HEART {Machozi moyoni mwangu}
Mtunzi: SALUM SAID NGUATE
Simu:0784989666
Sehemu ya KWANZA
Nadhani alikua muhanga wa MOYO wake mwenyewe. MOYO wake unamnisaliti kila iitwapo leo. Kwa kumtia majaribuni na kumfanya hata hapoteze matumaini na kiungo hiki adhimu kwenye mwili wa binadamu.
Matatizo mengi aliosababishiwa ni makubwa na mazito kuvumilika na kumshinda na kukipa kiungo kingine fadhaa na hamaniko kiss kiungo hiko.
Kwa sababu yake macho yake yalivimba kila wakati huku yakipoteza nuru yake na kuuvaa wekundu ambao hata alishanapo na wapita njia wanahofia macho yake.
Kisa MOYO wake Hadi asifiwi Tena na apitapo huko mitaani kama zamani alivyokua anasifiwa na kua kivutio kwa kila wamuangaliae na kumtazama.
Alikua na macho mazuri ya kupendeza huku mboni zake na ukubwa wake ukiwavutia watazamaji.
Uzuri wote na muonekano wake wote mzuri umetoweka kwa sababu ya kiungo hicho. Ajiuuliza maswali mengi mengi Sana bila kua na jibu sahihi la swali yake hivyo akawa wa kulia muda wote.
Kwanini uliambatana na yeye? Ulikuja kwake kwake ili uwe kilio chake? Kwanini usingetolewa labda ukaja MOYO mpya na kuandamana nae?
Nakumbuka zamani sana nisikia kua eti "MOYO WA MTU KICHAKA"Utakua vipi kichaka ilihali unaumiza nq kutesa watu namna hii. Utafananishwaje na KICHAKA ilihali unaumiza na kuliza. Kivipi wakati hauna uwezo wowote wa kulingana nao?
Kichaka kibebacho nyasi na miti midogo kwa mikubwa kitafanana vipi na MOYO hapana.
Kichaka kiwezacho kubeba nyoka wakubwa kwa wadogo na wadudu wa kila aina hakiwezi kufanana na moyo.
Je, MOYO unaweza?
Unawezaje kubeba miiba mikali na yenye sumu wakati hata ngozi tu iwezayo kuufanya upambane na jua hauna? Miiba ikija kwake SI lazima utoboke na kupata majeraha makubwa kutibika
Hakuamini Kama unaweza kua mmiliki wa sifa zile. Akawaza Sana na kwenda mbali hadi pale ulipoitwa
MOYO WA MWANAUME MGUMU
Mmmmh unaanzaje kua mgumu na kwa sifa hii ya ubaguzi kwanini au wanawake wao hawana MOYO au ya kwao Ni milaini Kama wake?
Maana yeye pia Ni MWANAUME na haoni ugumu wa MOYo wake.
Hauwezi hata kuuzidi ugumu wa jiwe na miamba pengine hata saruji tu igandayo hailingani kwa ugumu.
Siyo Kama aliudhalilisha MOYo la hasha bali aliuambia ukweli kua ulimkosea na umeendelea kumkosea kila leo.
Aliendelea kujilaumu peke yake pasi na msaada wowote wa mawazo wala ushauri hii Ni kutokana na kua mwenyewe muda mwingi na mawazo haya yamtesayo.
Alilaani na kulaani sifa zote hupewazo MOYO kila leo kwa kusema kua hazikua stahili kwa MOYO huu umtesao na kumuumiza.
Aliamini kua wahenga hawakua sahihi pale walipoupa MOYO MOYO sifa nyingi na kemkem.
Hakuutamani Tena MOYo wake Kama angeweza Basi angeutoa na kubaki hana MOYo ili tuu aishi kwa amani pengine ulikua ndo sababu kuu ya kufanya awe katika Hali ile.
Kiukweli aliumia Sana zaidi ya Sana na kila alitae eneo lile alimuonea huruma kubwa huku yeye akiendelea kulia kwa sauti bila kujali Kama macho mengi yapo kwake au jinsia yake ilivyo na mawazi aliovaa.
Wahenga walisema ukiona mtu mzima analia ujue kuna jambo Basi ulitimia mchana ule wa jua kali huku mliaji akiwa peku miguuni na bila kujali Hali hiyo imesababisha usugu na mipasuko ya miguu yake.
JE, NI NANI HUYO NA KIPI KIMEMFIKA
USIKOSE SEHEMU YA PILI