Hadithi : Suprise Ya Ajabu

Hadithi : Suprise Ya Ajabu

HADITHI: Surprise ya Aibu
SEHEMU: 20
MTUNZI: DR AMBE
SIMU: 0713646500

ILIPOISHIA:
Mmh! Mtoto wa kike nilianza kuamini kauli za Side Butamu kwamba yeye kaumwa kwa viungo vyote vitamu duniani. Japokuwa niliinjoi mapenzi kwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu. Lakini niliona fedheha kushindwa na kinyangarakata kama Side ambacho hata mkononi hakijai. Mpaka tunakwenda mapumziko Side alikuwa anaongoza tena kwa pointi nyingi.
SASA ENDELEA...
Niliamini nilimdharau na tamaa zangu za mwili ndizo zilizofanya nifanye mapenzi na mtu asiye na hadhi kama Side Butamu kama alivyojinadi. Kwanza alikuwa maskini pili alikuwa mlemavu wa miguu iliyolemaa na kutembea kwa kujivuta kwa makalio.
Nilimuangalia Side Butamu aliyekuwa amejilaza pembeni yangu kama kifurushi cha mzigo akiangalia juu kwenye dali bila wasi kuonesha hakubahatisha.
“Side ni kweli au umenibahatisha?”
“Mara nyingi ukisema kilicho ndani ya uwezo wangu, siwezi kukuhonga pesa ila nina uwezo wa kukupa penzi la kweli. Na leo ni woga kama tupo sehemu tulivu mbona leo ungeomba talaka kwa mumeo,” Side alijitapa.
“Utani huo Side?”
“We mwenyewe si umeuona muziki usio zima kwa umeme wa mgao?”
Mmh! Side jamani alinitisha kwa majingambo yake, lakini sikuwa wa kukubali kushindwa kirahisi. Baada ya mapumziko mafupi tulirudi kwenye ungwe ya pili. Kama kawaida Side alianza kwa kasi ile ile ya mwanzo na kuzidi kuniweka katika wakati mgumu.
Nami sikutaka kurudi nyuma tukakutana wote katikati ya uwanja ikawa piganikupige, Side alikuja juu nami nilimfuata hukohuko. Nilijikuta nikimwaga chozi mtoto wa kike kwa penzi tamu la Side Butamu. Mtoto wa kike wazimu wa mapenzi ulinipanda na kujituma vilivyo kulinda hadhi yangu.
Sikuamini mtu kama yule mlemavu asiye na hadhi yoyote kunipeleka puta kama gari kwenye njia mbovu. Katika ya mpambayo nilishangaa kumuona Side akitulia na kuanza kutokwa povu zito mdomoni. Macho yalimbadilika na kutazama juu kama ugonjwa wa kifafa.
Mungu wangu! Nilijua nimeishaua kumzidishia dozi kaka wa watu, yeye mapenzi starehe mwenzie sehemu ya maisha yangu kama kuvuta pumzi.
Nilishtuka na kuruka pembeni na kuanza kumwita.
“Side...Side.. Side Buta..”
Side hakuitikia zaidi ya kukoroma huku povu likimtoka, tumbo lilikuwa limerudi ndani kidogo likutane na mgongo. Wakati nimepagawa nafikiria jinsi ya kumsaidia Side, mlango uligongwa kwa nje. Sauti ya mume wangu ilizidi kunichanya na kujiona nimekwisha mtoto wa kike.
Nilijiuliza imeanza lini mume wangu kurudi bila kunijulisha, niliona nimeumbuka mchana kweupe. Talaka niliiona mbele ya sura yangu, wazo la haraka lilinituma nikamfiche Side bafuni. nilimbeba kama furushi na kwenda kumbwaga bafuni kisha nguo zake nilizificha chini ya uvungu.
Muda wote huo mume wangu alikuwa akigonga mlango huku akiniita kwa jina langu.
Nilijifuta jasho lililokuwa likimwagika kama maji, kisha nilifungua mlango na kukutana na mume wangu aliyekuwa amefura kwa hasira.
“Imeanza lini kujifungia mlango kwa ndani?” mzee Kupe alifoka.
“Nawe imeanza lini kurudi bila kunijulisha?” badala ya kumjibu nami nilimbana kwa swali.
“Nimekupigia simu hupokei, nimetuma mtu hufungui ulitaka nisifanye kazi zangu, nimeamua kuja mwenyewe. Mbona kama ulikuwa una...!!” Moyo ulipasuka pa! nikajua nimeumbuka mtoto wa kike, lakini niliwahi kumkata kauli.
“Nafanya nini? si nilikuwa nimelala.”
“Mbona mwili unatoka jasho?” akiniuliza huku akinichunguza.
“Niliota ndoto mbaya sana.”
“Ndo utoke jasho namna hiyo kama ulikuwa unacheza mieleka?”
“Mume wangu hata sijui ni nini, kama jinamizi lilinikaba na kuteseka kwa muda huku jasho likinitoka. Yaani kugonga kwako mlango ndio kumenitoa kwenye ndoto hiyo sijui ungechelewa ingekuwaje labda ungekuta mkeo nimekufa,” nilitengeneza uongo huku nikijifuta jasho ambalo bado liliendelea kutoka japo chumba kilikuwa na kiyoyozi.
Mume wangu alinipita na kuelekea msalani, nilitaka kumzuia lakini nilijiuliza atanielewaje ikiwa sijawahi kufanya kitendo kama kile hata siku moja. Nilijikuta nikisimama kama sanamu na kumsindikiza kwa macho. Nilijiuliza mlango wa bafuni niliufunga au la, niliamini kwa mchecheto niliokuwa nao sikukumbuka kuufunga.
Nilimuomba Mungu asimuone kwani ilikuwa aibu kubwa kukutwa na mwanaume nikifanya mapenzi wenye kitanda chake kibaya zaidi mlemavu. Nikiwa naomba dua kimoyomoyo, haikuzuia chochote. Dua langu halikufika popote nilisikia sauti kali ya mume wangu ikiniita.
“Mooreen hiki nini?”
Mara alitoka na Side akimburuza kwa kukishika kiguu chake kimoja.
“Moureen mke wangu ni uchafu gani unafanya? Unadiliki kufanya mapenzi na mlemavu, ni aibu gani hii?” Mzee Kupe alianza kulia.
“Nisamehe mume wangu ni shetani tu kanipitia,” nilijitetea huku nikipiga magoti mbele yake.
“Sawa kakupitia, lakini si kwa mlemavu kama huyu mke wangu aibu gani hii. Umelazimisha tumpe nafasi afanye kazi kumbe mwanaume wako?” Mzee Kupe alisema kwa hasira.
Mume wangu angejua wala asingesema kauli ile, Side alikuwa zaidi ya wale wanaovaa masuti na miili mikubwa ya mazoezi. Kwangu Side ndiye niliyemuoina mwanaume wangu wa shoka.
“Kweli ni mlemavu, lakini yote umeyataka wewe,” mtoto wa kike baada ya kuona maji yapo shingoni nilimtolea uvivu kwa kumwaga mchele mbele ya kuku.
“Yapi hayo?” nilimuona akishtuka macho yamemtoka pima.
“Unikidhi haja zangu muhimu umekuwa ukinipaka shombo tu kila siku.”
“Kwa mtindo huo utaniua kwa ukimwi.”
“Kwa hiyo unaamua nini?” Nilimuuliza nikiwa nimemshikia kiuno nilijua kama mbwai, mbwai tu.
“Kila mtu achukue chake, nitaendelea kuchukua Changudoa kama zamani nijue moja kuliko kufuga changudoa mama huruma.”
“Vyovyote vile, hata mimi nimechoka kupakwa shombo, mwili huu unatakiwa kutumiwa na wanaume wenye nguvu sio wewe kibabu. Kwanza shukuru nimekuvumilia muda wote lakini nimekuwa nikiteseka kila kukicha,” nilijua chakula hakiliki tena kwa vile Mzee Kupe alikuwa amemwaga ugali nami nikamalizia kwa kumwaga mboga.
“Kabla ya yote uondoe uchafu wako mbele ya macho yangu.”
Muda huo Side alikuwa amerudiwa na hali yake ya kawaida, kutokana na woga uliomtawala haja ilimtoka pale chini. Nilimtolea nguo zake chini ya uvungu na kumpa, kutokana na kuchanganyikiwa Side alijikuta akivaa kaptula yake kichwani.
Nilijikuta nikitaka kucheka, lakini nilimuonea huruma nilimsaidia kuvaa nguo zake na kumruhusu aondoke. Niliamini Side hakuamini jinsi alivyoachwa bila kuguswa. Baada ya kuondoka vita ikabakia kwangu, mume wangu aliamua tuachane.
“Mi nafikiri tumeshindwana, siwezi kutunza uchafu ndani mwangu.”
“Nami siwezi kukaa na mwanaume mchelemchele.”
“Ndiyo nini, unanitukana?”
“Sikutukani, ukweli ndiyo huo.”
“Sawa hata ukinitukana, lakini kama nilivyosema kila mtu achukue ustaarabu wake kwa vile wewe ni kunguru hufugiki.”
“Poa, mi’ kunguru nawe nyoka mtembelea tumbo unayetaka kukimbia wakati miguu huna, unataka wanawake vijana wakati mwenyewe nguvu za kupepea, utaliwa mali zako kila siku.”

Nini kitaendelea?
 
HADITHI: Surprise ya Aibu
SEHEMU: 21
MTUNZI: DR AMBE
SIMU: 0713646500

ILIPOISHIA:
“Nami siwezi kukaa na mwanaume mchelemchele.”
“Ndiyo nini, unanitukana?”
“Sikutukani, ukweli ndiyo huo.”
“Sawa hata ukinitukana, lakini kama nilivyosema kila mtu achukue ustaarabu wake kwa vile wewe ni kunguru hufugiki.”
“Poa, mi’ kunguru nawe nyoka mtembelea tumbo unayetaka kukimbia wakati miguu huna, unataka wanawake vijana wakati mwenyewe nguvu za kupepea, utaliwa mali zako kila siku.”
SASA ENDELEA...
“Maliza matusi yote, leo ndiyo mwisho wa kufanya uchafu kwenye nyumba hii.”
“Hii nayo nyumba wakiitwa wenye nyumba utapita wewe?” niliendelea kumpa makavu.
Sikumlazimisha tulikwenda kwa mwana sheria na kugawana mali. Alinipa nyumba mbili za nguvu magari mawili na pesa za kuanzia maisha.
Mtoto wa kike baada ya talaka, chaguo langu la kwanza lilikuwa Side Butamu mwanaume aliyenigusa nikagusika. Japokuwa nilitaka kumtoa roho baada ya kichaa cha mapenzi kunipanda. Nilimtafuta Side ambaye alikuwa amehama kufanyia kazi nje ya jumba la mtalaka wangu kuhofia usalama wa maisha yake.
Baada ya kumpata niliushangaza ulimwengu kwa kuolewa na Side Butamu, hakika alinipa utamu usio niisha hamu. Kila nilipokuwa Side alikuwa pembeni yangu, japo wanaume wenye pesa zao waliniijia na dau kubwa kutaka kunitoa mikononi mwa Side.
Kutokana na mapenzi mazito aliyonipa Side Butamu nilijikuta nikimuamini kupita kiasi. Niliyabadili maisha ya Side na kumfanya aishi kama mfalme kushona na kuweka viraka viatu vya wanaume wenzake akasahau. Kumbe mwanaume yule japokuwa mlemavu alikuwa na roho mbaya kuliko ya nyoka.
Kumuamini kote na kumhurumia alitumia nafasi ile kunitapeli na kuchukua sehemu kubwa ya mali yangu, kitu kilichonifanya nichanganyikiwe na kuuza zilizobaki kisha kurudi kwangu.
Baada ya kurudi nyumbani wanangu mliendelea kusoma kama kawaida kwa vile sehemu kubwa ya fedha yangu niliiwekeza kwenye elimu yenu. Baada ya kutendwa na Side Butamu ambaye wakati huo alikuwa amechukuliwa na shoga yangu, niliondoka huku nikijipanga kumfanyia kitendo kibaya.
Kwa kweli Mungu atanisamehe Side Butamu nilimuua kifo kibaya sana. Niliwatuma watu wakamkamata na kumleta. Nilimtia kwenye gunia na kumpiga mpaka akapoteza fahamu kisha nilimmwagia petrol dumu la lita tano lote na kumtia kiberiti.
Sikuondoka mpaka mwili ulipobakia majivu, alikufa kifo kibaya sana kwa kweli. Yale yalikuwa malipo ya usaliti baada ya kuyabadili maisha yake, lakini kumbe nilikuwa nafuga nyoka aliyekuwa na kunimeza. Baada ya kifo cha Side nilitimkia Mwanza ili kutuliza akili yangu kwa muda.
Kama kawaida nilifikia hoteli niliyokaa siku za nyuma, fedha zilipoanza kuniishia nilirudi kwenye kazi yangu ya ukahaba kwa vile nilijiamini mtaji ulikuwa mwili wangu. Nilikuwa nikitoka usiku na kwenda kwenye hoteli za kifahari na kununua kinywaji kisha baada ya muda nilielekea msalani ili kuwakonga wanaume wakwale. Kutokana na umbile nililojaaliwa midume mikwale alinitolea macho na kurusha ndoano.
Niliporudi ofa zilimiminika, niliangalia mwenye kisu kikali ndiye niliyetoka naye. Kwa vile nilirudi upya baada ya kulelewa na mzee Kupe, maisha ya ndoa yana raha zake niliamini kweli mimi kunguru sifugiki kwa kuyakataa maisha ya raha kama yale.
Nilivyokuwa nimenawili na kupendeza kwenye macho ya wanaume nilijikuta nikiwaokota kama senene. Nakumbuka vizuri ilikuwa siku ya jumapili nikiwa hoteli ya Kapil Cabana, kama kawaida yangu niliagiza pombe ya bei mbaya na kunywa kidogo kisha nilikwenda msalani. Baada ya muda alikuja Mzungu kwenye meza yangu ambaye alijipendekeza kunilipia kisha aliomba usiku wa siku ile tuwe pamoja.
"Upo peke yako au una mtu?" aliniuliza.
"Nipo peke yangu."
"Tunaweza kwenda?"
"Bila wasi."
Baada ya kinywaji niliongozana naye kwenye gari lake, tuliondoka hadi hotelini alipopanga. Ilionekana ni wale wataalamu kutoka nje ya nchi waliokuja kwenye miradi ambao hawajapata nyumba wanaishi hotelini. Alikuwa amepanga High Clasic Hotel. Kama kawaida usiku nilimpa mshikemshike na kumpa penzi zito lililomrusha akili.
Tulijikuta tunafanya mapenzi kwa nguvu hadi kufikia hatua ya kuchoka wote kama majogoo yaliyochoka kupigana na kila mmoja usingizi ulimpitia. Niliwahi kushtuka na kumkuta bado akikoroma, saa ya ukutani ilinionyesha ni saa kumi na moja kasoro.
Nilijikuta napata wazo la zamani la wizi japokuwa sikulipenda kwa kuhofia akiamka anaweza kunikamata na kunipiga kisha kuninyang'anya dola mia mbili alizonipa. Lakini roho nyingine iliniambia liwalo na liwe biashara ina kanuni mbili faida na hasara.
Nilijinyanyua kitandani taratibu na huku nikimuacha Mzungu aliyenitajia jina lake Mr Hourison akiwa anakoroma. Huku nikitetemeka nilinyata taratibu hadi kwenye kabati na kuanza kupekua. Nilikutana na mkoba mdogo, nilipokifungua sikuamini macho yangu. Zilikuwa dola tupu kwa uoga haja ndogo nilishindwa kuizuia.
Sikuwa na haja ya kuzihesabu nilizibeba zote, huku nikiwa natetemeka nilimuomba Mungu Mzungu asiamke. Nilivaa nguo zangu harakaharaka na kuupakatia ule mkoba kwa ustadi mkubwa.
Nilipofika getini kidogo mlinzi anizuie hapo nilijua nimekwisha, nilimpa dola kumi na kuniachia nitoke. Nilipotoka getini tu, nilipata teksi mpaka hotelini. Niliingia chumbani kwangu nikiwa siamini, baada ya kufunga mlango nilizimwaga zile dola juu ya kitanda. Kwa furaha nilizichota na kujimwagia. Nilikwenda kuoga kisha nilianza kuzihesabu, mmh! Sikuamini zilikuwa dola elfu ishilini na tano. Niliona umasikini umenitoka na wanangu mtaendelea kusoma shule muda wote wa uhai wangu hata kama nitatangulia mbele ya haki.
Sikutoka mbali ya hoteli kwa muda wa wiki nzima, wakati huo taarifa za kuibiwa Mzungu na changudoa zilizagaa jiji la Mwanza na msako mkali uliendelea.
Baada la tukio lile nilitoroka na kurudi tena Dar kwa vile Sibe Butamu hakujulikana amepotelea wapi. Nilitulia nyumbani kwa muda wa mwaka mzima. Lakini bado nilikuwa siwezi kuvumilia japokuwa nilipata bwana lakini tabia yake ya kunipiga kila akilewa ilinifanya niachane naye. Niliamua kupumzika tena nyumbani. Lakini siku moja mojamoja nakwenda viwanja ili nipate mwanaume kwa dau dogo. Nilikuwa kama mvuta sigara bila kupata hata pafu moja nilikuwa silali.
Miaka ilikatika na wanangu mlisoma na kupata mafanikio makubwa kwa kwenda nje kusoma masomo zaidi na kufanikiwa kupata kazi nzuri.
Wanangu wote kwa pamoja mlinijengea jumba kama kasri ya mfalme. Pamoja na maisha mazuri mliyokuwa nayo mlitaka kumjua baba yenu. Lakini kupitia maelezo yangu ya kina kila mmoja amejifahamu sidhani kama kuna mtu ataniuliza juu ya baba yake.
Najua mwanzo niliwadanganya kuwa baba yenu alinikimbia na kuniachia watoto, lakini siri yangu ilikuwa moyoni. Kwa vile leo kila kitu kipo wazi ni wewe Martin pekee baba yako anajulikana ni Shauri Kati mchora Katuni.
Pamoja na wanangu kunifanya niishi maisha kama nipo peponi, lakini damu ya ukahaba bado ilikuwa mwilini na kutoka siku mojamoja kwa siri. Sio siri ule usemi siku ya kwenda uchi ndiyo siku ya kukutana na mkwewe ilijidhihirisha.
Kama kawaida nilitoka mara nyingi na kurudi usiku, nikichelewa sana nilirudi kabla ya alfajiri. Nilikuwa na wanaume zangu watano ambao yeyote aliyeniwahi aliondoka na mimi. Na ratiba yangu waliijua ilikuwa siku ya jumatano, jumamosi na jumapili.
Siku hiyo kama kawaida nilikutana na mmoja wa wateja wangu kumbuka nilikuwa sifanyii hiki bali hobi. Tukiwa tunapata nyama choma na mtu wangu ili twende kwenye shughuli si ndio wakatokea wanawake zaidi ya watatu wakisema nimezoea kuwachukulia bwana yao na kuanza kunipa kipigo mpaka nikapoteza fahamu na kujikuta nipo hospitali.
Kwa kuwa maumivu hayakuwa makubwa niliruhusiwa asubuhi na kuamua kurudi nyumbani. Kumbe ndiyo siku ya kuumbuka mbele ya wanangu, hii wanangu ni Surprise ya aibu.”
****
Baada ya maelezo marefu yaliyo watoa machozi watoto wake Moureen aliwapigia magoti wanaye wamsamehe kwa aibu waliyoiona. Wote walisimama na kumnyanyua mama yao na kumketisha kwenye kiti.
"Mama huna kosa mbele yetu najua tabu zote ulizozipata ni kwa ajili yetu, sisi kama wanao tumekusamehe ila tunaomba msamaha. Tunaomba utusamehe kwa kuja bila kukutaarifu ni sawa kuingia chumbani kwako bila hodi. Lazima hali hii ingejitokeza.
“Mama tusamehe sana kwa yote uliyosema imeonyesha jinsi gani ulivyokuwa na mapenzi mazito kwetu na kupitia mitihani mizito lakini ulisimama kidete kututafutia maisha mazuri wanao. Mama sisi wanao hatuna la ziada ila tunaomba tena utusamehe si wewe utuombe msamaha mkubwa hakosi," Martin mwanaye mkubwa alisema kwa niaba ya wadogo zake.
Maneno yale yalimfanya mama yao abubujikwe na machozi huku akisema:
"Wanangu najua leo ndiyo siku Mungu alifanya hivi kwa makusudio makubwa kama ingeendelea kuwa siri nami ningeendelea kufanya uchafu na kumkosea Muumba wetu. Najua wanangu mlitaka kunifanyia mama yenu Surprise lakini limegeuka aibu kwangu na kuumbuka mama yenu. Leo hii naahidi kuachana na mambo yote machafu na Mungu anitie nguvu, nasema ukahaba basi."
Moureen alikumbatiana na wanaye kwa furaha na kusahau yote yaliyopita huku akiamini kuanzia pale amekuwa kiumbe mpya. Tokea siku ile Moureen aliachana na ukahaba na kumtafuta mzee mwenzie na kufunga ndoa ya uzeeni. Moureen mpaka anakufa hata sahau Surprise ya aibu iliyomkuta na mambo yake yote kuwa hadharani.
MWISHO!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom