X_INTELLIGENCE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2014
- 10,712
- 14,833
NILIKICHEKEA KIFO CHANGU no.1
mtunzi IDDY MHANDO
Nilikuwa safarini nikielekea sehemu nisipo pajua. ndani ya basi hilo tulikuwa abiria wengi lakini wote tulikuwa tumekaa kwenye siti hapakuwa na abiria ata mmoja aliyesimama. kabla ya safari hii nilipokea barua iliyonielekeza kupanda basi hilo linaloelekea Mwanza. hivyo sikuwa na jinsi kwani ilionyesha dhahiri aliyenipa amri hiyo hakuwa na chembe ya mzaha. safari ilikuwa nzuri japo nilipokuwa naelekea palikuwa pachungu na pabaya. pembeni ya kiti changu alikaa binti aliyekuwa makini na alichokuwa anakiandika kwenye simu yake. sikumbuki kama nilisalimiana nae binti huyu kipindi napanda hili basi. safari iliendelea hadi tulipofika Morogoro abiria tulishuka kwaajiri ya kuchangamsha mwili kununua vyakula pamoja na kupunguza mafuta mwilini. nami nilishuka nilinunua chakula pamoja na kinywaji. baada ya dakika kadhaa safari ilianza niliwaza mengi sana juu ya safari ile. niliwaza juu ya vitisho vya watu wale. niliwaza juu ya familia yangu niliyoiacha ikitaabika. lakini niliwahurumia sana wazazi wangu ambao bila wao leo hii nisingekuwa nasafiri. nilijikuta nikishindwa kuzuia hisia za uchungu, machozi yalitiririka kwenye milima ya mashavu yangu. ghafra nikashtushwa na sauti nyemba ya msichana aliekaa jirani yangu akihoji kwanini nilikuwa katika hali ile. nilishtuka sana dada yule alinionea huruma sana akaanza kunifuta machozi kwa kitambaa chake kilichokuwa kimepuliziwa marashi mazuri yaliyopenya ndani kabisa uvunguni mwa ubongo wangu.
dada: kuna nini kaka mbona unalia
mimi: hakuna kitu.
dada: naitwa RAYA naomba nikuache upumzike pengine baadaye tutazungumza kwa kirefu. RAYA alifungua kidogo dirisha la basi upepo mwanana ukawa unanipuliza nilihisi kama upepo ule unafika ndani kabisa ya ubongo nikahisi kama ubongo na mwili wangu umepoozwa mithiri ya kipande cha moto kilichochovywa kwenye maji ya baridi. nilijitahidi kuuvuta usingizi lakini ilishindikana.
URAFIKI WA EDDY NA RAYA WAANZA KUSTAWI
RAYA alijitahidi sana kuwa karibu yangu nadhani hakuwa na lengo baya nahisi kutokana na udhuni iliyoutawala uso wangu hivyo alipenda sana kujua nini kilichokuwa kimenisibu adi kuwa katika hali ile. palikuwa kimya sana ndani ya lile basi, zilisikika sauti za upepo na magari mengine tuliyokuwa tunapishana nayo. tulitembea kwa takribani masaa 9. hatimaye tulifika Singida. niliuvunja ukimya.
EDDY: ivi tupo wapi hapa?
RAYA: tupo Singida.
EDDY: naitwa EDDY nakumbuka kama ulinitajia jina lako ila limenitoka unaweza kunifanyia hisani ya kunitajia tena tafadhali?
RAYA: oh naitwa RAYA naelekea Mwanza vipi na wewe utakuwa safarini hadi Mwanza?
EDDY: ndio.
RAYA: ulinishitua sana nilipokuona unatokwa na machozi inaelekea kuna jambo zito sana linakukabiri.
{nilishindwa cha kumjibu RAYA . ni kweli nina matatizo lakini siwezi kuyaanika matatizo yangu kwa mtu niliyekutana naye juu juu}
EDDY: unajua muda mwingine akili huwa inachoshwa sana kutokana na kumbukumbu za mambo yaliyopita..
RAYA: pole sana ukiona mwanaume analia ujue kuna jambo kubwa linalomsumbua....lakini usijari kaka angu kila lenye mwanzo katika maisha huwa alikosi kuwa na mwisho. utaangaika, utapata tabu katika maisha ila kaa ukijua kuwa katikati ya shida na manyanyaso kuna njia ya mafanikio na furaha.
{maneno ya RAYA yalipenya kwenye fikra zangu yakanipa nguvu nikajiona shujaa} tuliendelea kuzungumza nikamuamini sana RAYA nilimuona ni miongoni mwa watu wachache sana ambao wapo teyari kujitoa kwa ajiri ya kusaidia wengine.
EDDY AFARIKI KWA AJARI SEKENKE.
safari iliendelea dereva alikuwa anaendesha mwendo makali tulipofika kwenye mteremko wa mlima Sekenke. gari ilimshinda maarifa dereva kwani alikuwa na mwendo mkali na alishindwa kuidhibiti huku mbele pakiwa na gari ndogo iliyokuwa imeharibika barabarani...katika jitihada za kuikwepa ile gari ndogo tulijikuta tunaporomoka. basi lilipondeka sana sizani kama kuna aliyepona ata mimi pia nilikufa.
nilishtuka nika piga kelele ahaaahaaahaa kumbe nilikuwa kwenye taswira aionayo mtu pindi awapo USINGIZINI sikutaka kuamini kuwa msichana RAYA nilikutana naye ndotoni nilitamani ingekuwa kweli lakini sikutamani matukio ya ajari ile.punde nesi aliyekuwa jirani yangu alianza kuita
"Dokta....dokta...dokta...mgonjwa ameinuka" nesi alikimbia huku akimwita DOKTA
nilijitazama nilikuwa nimezohofika sana, nimekonda mwili umeisha mkononi nikiwa nimepachikwa mrija wa kuongezea maji mwilini. sikuwa na nguvu ata za kuinua mkono wangu nguvu pekee nilizokuwa nazo muda ule ni za kupepesa tu kope zangu na kuchezesha macho...dokta alikuja tukawa tuna tizamana hakuniongeresha alinigusa macho yangu akaniangalia kisha akashusha pumzi ndefu.
DOKTA: pole sana EDDY hali yako inazidi kuwa nzuri naamini muda si mrefu utapona.
siku mjibu kitu yule dokta kwani ni kama akili zilikuwa azijanirudia vizuri.
EDDY AMLILIA aggyjay
nilipepesa macho huku na huko ndipo nilipo muona aggyjay moyo uliniuma sana nilitamani nipate nguvu niwe na uwezo nimuonyeshe mwanagu huyu upendo wa baba nilimpenda sana binti yangu aggyjay sikubahatika kumlea na amenisaidia nikiwa katika kipindi hiki kigumu. uchungu ulinishika nikajikuta nalia ...nikakumbuka maisha niliyopitia
kumbe kuna watu tumeumbwa tu sisi ni wa mateso tu hadi umauti, siku zote nilikuwa natabasamu usoni tu lakini moyo wangu uligubikwa na simanzi.
nilimuonea huruma aggyjay kwani nilijua muda si mrefu atanipoteza.
usikose kufuatilia simulizi hii ya kusisimua....