Hadithi : Muhanga Wa Mapenzi

Hadithi : Muhanga Wa Mapenzi

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,746
Reaction score
25,662
Image may contain: 1 person, text


Love Stori: Muhanga wa mapenzi
Sehemu: 01
Mtunzi: Ally Mbetu
SIMU: 0713646500
Athumani alijikuta akiwa njia panda asijue aelekee upande gani, ilikuwa ni baada ya kumsindikiza rafiki yake aliyekuwa amekuja kunitembelea. Hii yote ilitokana na kuwa mgeni maeneo yale , akiwa amekuja kwa kaka yake ambaye alikuwa amekwenda masomoni nje ya nchi na muda huo alikuwa bado hajaoa.
Hivyo kumuita kumlindia nyumba yake, japokuwa alikuwa mgeni maeneo yale lakini hakupenda aonekane si mwenyeji wa maeneo lile. Kwa kuwa vile alipitia njia ndefu wakati wa kusindikiza aliamua apitie njia ya mkato ili niwahi nyumbani.
Cha ajabu baada ya kuingia uchochoro mmoja alijikuta nimetokea mbele ya jumba moja la kifahari. Ilimchanganya kidogo asijue nielekee upande gani . Alijiuliza nirudi au atafute kichochoro apenye. Wakati akiwa katika kujishauri mara gari la kifahari Toyota VX V8 NEW Model lilisimama mbele yake baada ya muda kidogo mlango ulifunguliwa.
Ulitangulia mguu mmoja ambao olionesha raba aina ya NIKE kisha supu ya mguu ilionesha kinachotemka si kitu cha kawaida. Naam kitu kilichoteremka si cha kawaida. Alikuwa binti mmoja mweupe akiwa katulia katika vazi la shule siketi yake iliyombana na kuonesha makalio yalivyotulia si masihara. Binti alikuwa amepewa upendelea na muumba. Baada ya kuteremka alifunga mlango wa gari na gari kuondoka.
Baada ya gari kuondoka binti yule alielekea ndani ya jumba lile la kifahari, Ahumani alionelea ni vizuri amuulize njia ya kutokea barabarani. Kabla ya kuingia getini alimwita lakini hakumjali alichepua mwendo kuingia ndani. Alifikiria labda hajamsikia. Alichapulisha mwendo na kumwahi kabla hajagusa kengele ya getini. Alipomgusa tu yule msichana alimkalipia.
“We kaka umerogwa … Usinishike wewe una hadhi ya kunishika mtu kama mimi,” alimjibu huku alijifuta sehemu aliyomshika kwa kitambaa cha mkononi.
“ Samahani sister nilikuwa nataka kukuliza,“ Athumani alisema kwa upole.
“ Uniulize uliniona na nafanya kazi mapokezi?” alimjibu kwa nyodo.
“ Samahani,” Athumani alimuomba msamaha msichana aliyeonekana ana dharau sana.
“Ninyi ndio vibaka achana na mimi.”
Mabishanoyao yalisababisha askari wa getini afungue mlango na kuhoji.
“Rachel vipi ?“ Aliuliza askari.
“ Si hili libaba eti linataka kuliuliza kama sio likibaka linataka kuniibia.”
Ilibidi mlinzi aingilie kati na kumwambia Rachel aingie ndani na kuniuliza shida yangu. Alimweleza hali halisi mlinzi alimuelewa na kumuonyesha njia ya mkato.
Baada ya kuachana na yule msichana alirudi nyumbani kuendelea na shughuli zake, maneno ya yule binti hakuyatilia maanani hasa akizingatia watoto wa kubwa. Wengi wametawaliwa na dharau
RACHEL
Rachel msichana aliyeubwa akaumbika mtoto wa tajiri mmoja jijini anayetambuliwa kwa jina la John Mulisa. Pamoja na uzuri wake alikuwa ni binti anayejiona sana si nyumbani hata shuleni alichagua rafiki wa kuzungumza naye wengi walipenda kumwita mama mashauzi.
Siku moja Rachel chumbani kwake baada ya kutoka shule jicho lake lilikuwa barabarani sehemu kulikokuwepo dirisha lake. Jicho lake lilitua kwa mvulana mmoja aliyekuwa akipita katika vazi la kuvutia pia mwili wake ulijengeka kiume hasa.
Mvulana yule alikuwa mgeni machoni kwake, alijikuta akimpenda ghafla ya kutamani siku moja awe wake. Rachel alimsindikiza kwa macho hadi alipopotea machoni kwake. Alijikuta akijiuliza kijana mzuri kama yule anakaa wapi na atawezaje kumpata mtoto wa kike. Alijukuta akiuvaa ugonjwa usio na dawa ya kumeza wala kupaka.
Alijikuta akiwa katika ugonjwa wa kupenda bila ampendaye kujua. Akiwa shule alijikuta yupo katika kipindi kigumu darasani masomo yalikuwa kero kwake baada ya muda mwingi kuutumia kumuwaza mtu asiyemjua.
************
Rachel baada ya kutoka shule alikuwa chumbani kwake alibadili nguo akiwa mbele ya dressing table iliyokuwa karibu na dirisha ambalo lipo upande wa barabarani alivutiwa na kijana mmoja aliyekuwa anapiti sawa na dirisha lake ambaye alikuwa akimuona kwa mara ya pili mfururizo .
Bila kujielewa alijikuta akipenda kila kitu alichokuwa nacho yule mvulana . kuanzia mavazi yake mwendo wake, umbo lake na sura yake . Aliacha shughuli ya kubadili nguo alinyanyuka dirisha ili aliweze kumuona vyema yule kijana wa kiume.
“Ama kweli kuna vijana wa kiume walioumbwa wakaumbika hata ukipita mbele ya watu wanakuonea wivu “ alijikuta akijisemea mwenyewe.
Baada ya yule kijana kupita alimwacha Rachel katika lindi la mawazo juu ya kijana yule na kujiuliza sijui kama atamtia tena machoni . Rachal baadaya kubadili nguo na kuvaa nguo za kupendeza alisimama mbele ya kioo na kujisifia jinsi alivyo mzuri na jinsi alivyopendeza . Alijikumbatia mwenyewe huku akisema:
“ Jinsi alivyopendeza halafu nipate kijana mzuri kama niliyemwona muda ule mbona dunia nitaisanifu.“
Rachal alizivua zile nguo na kubakia na nguo ya ndani na kujitupa katika kitanda cha sita kwa sita na kujipindua kitanda kizima huku akimuwaza yule kijana ambaye ameuteka moyo wake kwa ghafla.
Nini Kitaendelea?
 
Love Stori: Muhanga wa mapenzi
Sehemu: 02
Mtunzi: Ally Mbetu
SIMU: 0713646500

ILIPOISHIA:
Baada ya yule kijana kupita alimwacha Rachel katika lindi la mawazo juu ya kijana yule na kujiuliza sijui kama atamtia tena machoni . Rachal baadaya kubadili nguo na kuvaa nguo za kupendeza alisimama mbele ya kioo na kujisifia jinsi alivyo mzuri na jinsi alivyopendeza . Alijikumbatia mwenyewe huku akisema:
“ Jinsi alivyopendeza halafu nipate kijana mzuri kama niliyemwona muda ule mbona dunia nitaisanifu.“
Rachal alizivua zile nguo na kubakia na nguo ya ndani na kujitupa katika kitanda cha sita kwa sita na kujipindua kitanda kizima huku akimuwaza yule kijana ambaye ameuteka moyo wake kwa ghafla.
SASA ENDELEA...
Rachel alijikuta kwenye wakati mgumu wa kuugua homa ya mapenzi huku akimuogopa kumweleza muhusika kutokana na dharau alizomfanyia alijuuuta kumdharau asiyemjua. Hali ile ilimfanya awe mwingi wa mawazo muda wote kila alipokuwa akimuona yule kijana akipita moyo wake ulimlipuka na kujikuta kwenye wakati mgumu.
Muda mwingi alikuwa mtu wa mawazo kipindi kitu kilichopelekea kumshtua kila mmoja kuanzia wazazi wake , walimu hata rafiki yake mkubwa Joyce .
“Rachel vipi mbona siku hizi mbili unaonekana una mawazo mengi,“ Joyce alimuuliza.
“Joyce ni kweli kuna kitu kimenisibu lakini si leo, ila ipo siku nitakuelezea ili unisaidie, “ alimjibu rafiki yake kwa sauti ya unyonge.
“Hapana Rachel wewe ni rafiki yangu na siri zetu hatufichani naomba uniambie huenda nikakusaidia hata kimawazo.”
Rachel ilibidi amueleze ukweli Joy jinsi anavyompenda mtu asiyejua mapenzi yake kwake.
“ Kwanini uutese moyo wako wakati mtu mwenyewe hayupo mbali mueleze ukweli ujue moja siku zote kwenye maumivu ya moyo unatakiwa kujitoa muhanga kwa kujiweka wazi mbele ya yule umpendaye.”
Rachel aliahidi kuyafanyia kazi yale aliyoelezwa na shogae Joyce .
***
Kutokana na gari linalomfuata kumchukua shule kuchelewa Rachel aliomba lift kwenye gari la kina Joyce ambalo lilimshushia karibia na kwao. Baada ya kuteremka katika gari aliagana na Joyce wakati anageuka ili aondoke nusra aanguke kwa mshtuko pale alipokutana uso kwa uso na mtu ambaye alimuona hana hadhi ya kuzungumza naye lakini akatokea kuwa ugonjwa wa mahaba yake.
Kutokana na tabia yake ya nyodo hata kumueleza alishindwa alibakia kumsindikiza kwa macho tu na kuingia ndani mwao huku moyo wake ukizidi kutaabika juu ya mapenzi.
Siku iliyofuata baada ya kutoka shule na kuingia chumbani kwake alielekea dirishani ili afungue pazia atazame nje wapita njia. Hakuamini macho yake pale alipomwona tena yule kijana akipita. Safari hii alifurahi zaidi kwani alikuwa amesimama akizungumza na mtu na alipomwangalia vizuri alimtambua kuwa ni yule kijana aliyemzodoa siku moja akiwa katika mavazi ya kawaida.
“ Dah! Kumbe bonge la hand some boy, ni kijana mzuri sana tena sana …. Mmh, maskini sijui kama atanielewa nikimweleza nampenda wakati niliisha mtoa nishai,” Rachel aliwaza peke yake bila kupata jibu kitu kilicho mnyima raha.
****

Athuman akiwa anatoka katika shughuli zake, alijirudisha nyumbani kwa mwendo wa taratibu mara alishtushwa na sauti ya mtoto mdogo wa kiume ikimwita kwa nyuma.
“Kaka ……kaka.”
Athuman aligeuka na kumtazama yule mtoto na kumuuliza.
“Unasemaje?”
“Kuna barua yako, “ alisema yule mtoto huku akinyoosha mkono kumpa barua.
“Inatoka kwa nani?” aliuliza huku akiipokea.
“Yule.”
Alimuonesha binti Rachel aliye juu katika jumba la kifahari ambalo anakaa tajiri mmoja John Mulisa. Alimuangalia yule binti ambaye alikuwa amesimama mbele ya kibaraza. Alipomwangalia vizuri ili amtambue alijificha kwa aibu, lakini Athuman alimkumbuka ndiye aliyenitoa nishai siku moja.
Aliifungua ile barua na kuisoma palepale maneno niliyoyakuta yalimshtua kidogo nakumchanganya. Eti anamtesa moyo wake, yeye ndiye mwokozi wake na anasubiri jibu kama wokovu barua yenye maneno machache ilimalizia kwa manane: deep love Rachel.
Athuman alicheka kidogo kisha alinyanyua tena macho na kumwangalia kama mwanzo alijificha tena . Alijiuliza ni yeye au kuna mtu mwingine aliyempelekea ile barua mwenye hadhi ya kuzungumza naye . Athuman aliamini ile barua si yake mtumwaji atakuwa amekosea.
Aliachana na ile barua na kutupa vipande vyake vilivyo peperushwa na upepo kisha alipiga hatua kuondoka eneo lile. Rachel alimfaidi Athuman kwa kumuona vizuri tena kwa ukaribu zaidi.
Wakati Athuman anasoma ile barua Rachel alikuwa amefumba macho huku amejikumbatia kwa mikono yake miwili. Lakini moyo ulipasuka baada ya kushuhudia barua yake ikichanwa na kalatasi kutupwa barabarani. Kitendo cha Athuman kuichana barua yake kilikuwa kama kuuchana moyo wake.
Alijikuta akilia kwa uchungu huku akikimbilia kitandani na kuukumbatia mto huku akiendelea kulia na kulitaja jina la yule mvulana baada ya kulitambua jina lake kutokana na kusikia akikitwa na mtu.
“Athuman mpenzi kwa nini umeuchana moyo wangu, kwa nini huna huruma na mateso yangu ya moyo? Athuman nisamehe sikujua nitendalo lilikuwa sawa na kuupasua moyo wangu kwa kisu kisicho na makali bila ganzi. Hebu fikiria ni maumivu gani moyoni mwangu?”
Rachel alijizungumza huku akilia kwa sauti ya chini, mama Rachel alikuwa akiingia chumbani kwa mwanaye ili kumwita kwa ajili ya chakula cha mchana. Sauti ya kilio cha kulalamika kilimshtua na kuingia ndani taratibu ili ajue kuna nini. Alishangaa kumkuta akiwa amekumbatia mtu kitandani peke yake huku akizungumza kama anazungumza na mtu. Alipomwita aligundua mwanaye yupo usingizini.
Alitoka huku akijiuliza Athuman ni nani anayemsumbua mwanaye na kumuingiza kwenye dunia mbaya ya mateso ya nafsi ya mapenzi. Moyoni aliapa kumsikisha adabu huyu kijana anayeitwa Athuman.

Nini kitaendelea?
 
Love Stori: Muhanga wa mapenzi
Sehemu: 03
Mtunzi: Ally Mbetu
SIMU: 0713646500

ILIPOISHIA:
Rachel alijizungumza huku akilia kwa sauti ya chini, mama Rachel alikuwa akiingia chumbani kwa mwanaye ili kumwita kwa ajili ya chakula cha mchana. Sauti ya kilio cha kulalamika kilimshtua na kuingia ndani taratibu ili ajue kuna nini. Alishangaa kumkuta akiwa amekumbatia mtu kitandani peke yake huku akizungumza kama anazungumza na mtu. Alipomwita aligundua mwanaye yupo usingizini.
Alitoka huku akijiuliza Athuman ni nani anayemsumbua mwanaye na kumuingiza kwenye dunia mbaya ya mateso ya nafsi ya mapenzi. Moyoni aliapa kumsikisha adabu huyu kijana anayeitwa Athuman.
SASA ENDELEA...
****
Siku ya pili Rachel akiwa ndani ya gari akirudishwa shuleni alimuona Athuman akipita karibu na kwao kama ilivyokuwa kawaida yake. Alijikuta mapigo ya moyo yakimwenda kasi. Alijikuta akikosa uvumilivu na kujikuta akimwambia dereva wao.
“Peter naomba uniteremshe hapa.”
“Kwa nini?’
“Nimekueleza niteremshe hapa,” Rachel alisema kwa sauti ya ukali.
Dereva hakubisha alisimamisha gari, Rachel aliteremka haraka na kumkimbilia Athuman aliyekuwa ameanza kulipita jengo la jumba lao.
“Kaka..kaka,” alimwita huku akimkimbilia.
Athuman aligeuka baada ya kujiona eneo lile yupo peke yake, alishika kifuniani na kuuliza.
“Mimi?”
“Ndiyo.”
Alisimama kumsubiri Rachel, baada ya kufika alimuomba samahani.
“Samahani kaka,” Rachel alisema huku akihema kutokana na kuja mbio.
“Bila samahani.”
“Naomba kwanza uniache kidogo nipumue, unajua nimekuja nakimbia.”
“Hakuna tatizo.”
Wakati Rachel akivuta pumzi na kujenga ujasiri ya kuzungumza na Athuman, baba yake mzee John Mulisa alikuwa akirudi na kumuona binti yake akizungumza na mwanaume. Alisimamisha gari na kuteremka na kwenda kwa kasi alipokuwa amesimama binti yake na Athuman.
Alipofika bila kuuliza alianza kuangusha kipigo kwa Athuman ambaye alipigwa butwaa. Athuman alijikuta njia panda na kushindwa kuelewa kinachoendelea. Mama mmoja mwenye mwili mkubwa alimshika yule mzee ili asiendelee kumsuburu Athuman aliyekuwa amepigwa butwaa.
“Baba Rachel hebu mwache mtoto wa watu utamuumiza bure.”
Yule mzee alimwachilia Athuman na kumfanya aondoke na wakati huo watu walianza kukusanyika na kuanza kumuuliza maswali.
“Vipi mshikaji, mbona dingi anakupa maumivu bila kumpa dispirin,” kijana mmoja alimuuliza.
“Achana naye si unajua watu wengine wanatafuta sababu.”
Athuman alijibu huku akiondoka eneo la tukio na kuelekea nyumbani. Alifikiria mengi juu ya binti yule hakujua nia yake, alijiuliza kweli anampenda au ana sababu zake.
***
Athuman akiwa sebuleni amejipumzisha kwenye kochi baada ya chakula huku akitazama tivii, alishtushwa na sauti ya kengere mlangoni. Iliyomuashiria kuna mtu mlangoni, alikwenda hadi mlangoni na kufungua mlango.
Hakuhamini macho yake, aliyekuwa mbele yake hakuwa mwingine ila Rachel mtoto wa tajiri John Mulisa.
“Athuman mbona unanishangaa? Nikalibishe ndani basi,” Rachael alisema huku akiachia tabasamu pana.
“Sishangai ila siamini kama wewe, pia umenitia wasiwasi juu ya mzazi wako pale tu kunikuta barabarani nusra anitoe roho. Kama akikukuta huku si atanitoa roho kabisa?” Athuman alisema huku akimkaribisha Rachel ndani.
“Athuman ukufikiria hivyo basi wazazi wasinge jifungua kwa uchungu.”
Alimkaribisha Rachel ndani baada ya kukaa kwenye kochi alimuuliza.
“Mrembo unatumia kinywaji gani?”
“Nipatie maji ya matunda” Rachel alijibu huku akitabasamu.
“Mbona sina, kuna soda tu.”
“Yoyote upendayo mpenzi,” kauli ile ilimshtua Athuman na kujifikiria alichokisikia ni kweli au masikio yake.
“Mmh! Nimeisha kuwa mpenzi wake? Wacha tuone mwisho wake,” Athuman aliwaza moyoni.
Wakati Athuman akijiandaa kumfungulia Rachel soda kengele ya mlango ililia na kumfanya Athuman aache kufungua soda. Aliiweka juu ya meza na kwenda kuufungua mlango.
He! Baada ya kufungua mlango Nusra Athuman azimie na kutamani ardhi ipasuke na kummeza. Aliyekuwa mbele yake amesimama hakuwa mwingine ila mzee John Mulisa, baba yake Rachel. Kama umeme alimvamia na kuanza kunishushia kipigo kingine akisaidiana na askari alikwendanao, mkongoto aliopata ulisababishia apoteze fahamu.
Alipozinduka alijikuta akiwa amelazwa hospitari huku akiwa nimefungwa kitu kama chuma mkononi. Baaada ya kupata uelewa aligundua mkononi alikuwa amefungwa pingu mkono mmoja. Pembeni kulikuwa na askari akinilinda kama vile ameua.Nini kitaendelea?
 
Love Stori: Muhanga wa mapenzi
Sehemu: 04
Mtunzi: Ally Mbetu
SIMU: 0713646500

ILIPOISHIA:
Wakati Athuman akijiandaa kumfungulia Rachel soda kengele ya mlango ililia na kumfanya Athuman aache kufungua soda. Aliiweka juu ya meza na kwenda kuufungua mlango.
He! Baada ya kufungua mlango nusra Athuman azimie na kutamani ardhi ipasuke na kummeza. Aliyekuwa mbele yake amesimama hakuwa mwingine ila mzee John Mulisa, baba yake Rachel. Kama umeme alimvamia na kuanza kunishushia kipigo kingine akisaidiana na askari alikwendanao, mkongoto aliopata ulisababishia apoteze fahamu.
Alipozinduka alijikuta akiwa amelazwa hospitari huku akiwa nimefungwa kitu kama chuma mkononi. Baaada ya kupata uelewa aligundua mkononi alikuwa amefungwa pingu mkono mmoja. Pembeni kulikuwa na askari akinilinda kama vile ameua.
SASA ENDELEA...
Ilikuwa nivigumu kutathimini nini kilichomkuta hadi kufikia hatua kujeruhiwa hivyo bila sababu ya yeye kuhukumiwa vile. Athuman hakujua binti yule alikuwa na ajenda gani yeye na baba yake.
Mara ya kwanza amepigwa bila kosa mara ya pili amepigwa mpaka akapoteza fahamu na kujeruhiwa hata bila kuulizwa. Alishangaa kuvishwa pingu bila kosa. Alijikuta akiwaza au ndiyo ule useme mwenye pesa hana kosa ila mlala hoi hawana haki hata kama umeonewa?
Akiwa bado yupo katika windi la mawazo alishutushwa na kundi la watu wasiopungua watano mmoja alimtambua alikuwa mkuu wa polisi wa mkoa RPC pamoja na daktari, walisogea hadi kitandani kwake.
“Mkuu kijana mwenyewe ndio huyu,” daktari alimsonta kidole Athuman aliyekuwa amelala kitandani. Mkuu wa polisi alikwenda hadi pale kitandani na kumsemesha.
“ Kijana unajisikiaje hali yako?” alimuuliza Athuman kwa upole.
“Sijambo kidogo mzee, Shikamoo.”
“Marahaba,” Mkuu wa polisi aliitikia kisha alitaka maelezo ya Athuman kuwa pale.
Athuman alimpa kisa kizima bila kuacha hata neno moja, mkuu wa polisi baada ya kumsikiliza alimpa pole.
“Pole sana kijana kama ni hivyo, lakini bado tunaendelea na uchunguzi. Hivyo utakuwa chini ya polisi mpaka tupate ushahidi wa kutosha wa pande zote.”
Baada ya mazungumzo yasiyo na msaada kwa Athuman, mkuu wa polisi aliondoka. Baadaye Athuman alichukuliwa na kupelekwa mahabusu . Akiwa mahabusu aliona bado anaonewa kama ukweli amesema bado anawekwa rumande. Aliamini pesa na ubabe ndivyo vilivyotawala haki za wanyonge siku zote.
***
Rachel alijawa na simanzi mkubwa moyoni mwake baada ya kufumaniwa ndani kwa Athuman pia alijilaumu kuchelewa kumwelezea ukweli kuwa anampenda hata kama akifungwa angejua amefungwa kwa kosa gani. Yote yale ilikuwa sababu za mapenzi yake ya dhati kwa yule kijana .
Kukosa raha kulimfanya mama yake kuyaona mabadiliko ya mwanaye, alimfuata na kumtuliza kwa kumwambia:
“Mwanangu wewe huna kosa ila tunataka kumfunza adabu huyo mwana haramu anayetaka kukuharibia masomo.”
“Mama yule kijana hana kosa mwenye makosa ni mimi,” Rachel alimtetea Athuman.
“Hata ukimtetea vipi lazima atujue sisi ni kina nani na lazima aozee gerezani gerezani hata kwa kesi ya kichwa tutampa.”
“Mamaaa!” Rachel alishtuka.
“Unashtuka nini? Tena ondoka hapa usichefue nitakugeuzia kibao sasa hivi,” mama Rachel alimchumba mkwala mwanaye.
Rachel alikuwa mpole, lakini alimdadisi mama yake kuhusu hali ya Athuman huko mahabusu, mama alisema hajui kitu labda amsubiri baba yake atakaporudi. Mara aliingia Mzee John Mulisa, mkewe alimpokea mkoba. Baada ya kutulia alitaka kujua juu ya yule kijana aliyefumwa na binti yao.
“Mume wangu vipi kuhusu yule kijana?”
“Mama Rachel yule kijana lazima nimwonyeshe mimi ni nani, lazima itakuwa fundisho kwa yeyote atakayetaka kuchezea anga zangu,” Mzee John Mulisa alijigamba mbele ya mkewe.
Rachel aliyekuwa amejificha nyuma ya mlango aliyasikia yote yaliyosemwa na baba yake, alitulia tuli ili asikie mwisho wake.
” Lazima tuonyeshe sisi ni wazazi wenye uchungu na mtoto wetu, hawezi kutaka kumuharibia masomo yake hivihivi halafu tumchekee,” mama Rachel aliunga mkono.
“ Ile kazi hiyo nimempa mkuu wa polisi aishughulikie nasuburi taarifa yake.”
‘Mume wangu lazima uhakikishe anafungwa mwana Hizaya yule tena ikiwezekana maisha.”
Kauli ile ilizidi kumuumiza roho Rachel ambaye alizidi kumuonea huruma Athuman kwa vile yeye ndiye aliye muingiza kwenye matatizo.
“Mke wangu nina imani unanijua vizuri, yule nani kwangu, wacha kufungwa maisha hata nikitaka kuyongwa haitashindikana kwangu,” mzee John Mulisa alizidi kujitapa mbele ya mkewe.
“ Aah! Baba afungwe kwa kosa gani? Mbona mna roho mbaya, mnataka kumwonea mtoto wa watu. Nakuhakikishieni hafungwi kwa hali na mali, acheni roho mbaya,” Rachel alitoka nyuma ya mlango na kuwakata kauli wazazi wake baada ya maneno yao kumchoma moyo.
Maneno yale yaliwafanya wazazi wake washikwe na bumbuazi, hawakutegemea kusikia maneno makali kama yale toka kwa mtoto wao. Mzee John Mulisa, alicheka kicheko cha kivivu na kusema:
“Mama Rachel, maneno ya mtoto ni ya kitoto achana naye tuendelee na maongezi yatu...” Rachel alimkata kauli baba yake.
“Mnafanya mzaha eeh! Nasema msipomwachia mtanijua mimi ni nani? Kwa nini hamuachi kumfuatafuta mtoto wa watu amewalia nini? Japokuwa ninyi ni wazazi wangu msije mkajilaumu baadaye,” Rachel alizidi kuwapandishia wazazi wake.
Kitendo kile cha Rachel kukosa adabu mbele ya wazazi wake, baba yake mzee John Mulisa alinyanyuka na kwenda kumzaba vibao. Rachel alikimbilia chumbani kwake na kujitupa kitandani na kuanza kulia kwa sauti. Mama yake huruma ilimwingia na kumfuata kumbembeleza bila mafanikio.

Nini kiatendelea?
 
Love Stori: Muhanga wa mapenzi
Sehemu: 05
Mtunzi: Ally Mbetu
SIMU: 0713646500...

ILIPOISHIA:
Maneno yale yaliwafanya wazazi wake washikwe na bumbuazi, hawakutegemea kusikia maneno makali kama yale toka kwa mtoto wao. Mzee John Mulisa, alicheka kicheko cha kivivu na kusema:
“Mama Rachel, maneno ya mtoto ni ya kitoto achana naye tuendelee na maongezi yatu...” Rachel alimkata kauli baba yake.
“Mnafanya mzaha eeh! Nasema msipomwachia mtanijua mimi ni nani? Kwa nini hamuachi kumfuatafuta mtoto wa watu amewalia nini? Japokuwa ninyi ni wazazi wangu msije mkajilaumu baadaye,” Rachel alizidi kuwapandishia wazazi wake.
SASA ENDELEA...
Kitendo kile cha Rachel kukosa adabu mbele ya wazazi wake, baba yake mzee John Mulisa alinyanyuka na kwenda kumzaba vibao. Rachel alikimbilia chumbani kwake na kujitupa kitandani na kuanza kulia kwa sauti. Mama yake huruma ilimwingia na kumfuata kumbembeleza bila mafanikio.
*****
Usiku ulikuwa ni mrefu kwa Athuman alikosa kabisa usingizi kwa mawazo, alijiona naonewa bila kosa lolote. Alijua ni yote sababu ya jeuri ya fedha, Alijiuliza kuhusu ujio wa yule binti anayedai ananipenda, ni kweli alikuwa na mapenzi ya kweli au alitumwa na baba yake kumuingia matatizoni ili wanifunge.
Hakujua kosa lake nini alilowakosea hata hata yule binti mwenyewe hakuwa amemfanya kitu chochote cha kumfanya afikie hatua ile. Alikumbuka hata siku ya kwanza alipokutana naye hakumjibu lolote pamoja na kukashifiwa.
Akiwa katikati ya wimbi la mawazo alishtuliwa na sauti ikimwita.
“Athuman ndiye nani?” Ilikuwa sauti ya askari, kabla ya kuitika kwanza Athuman alijiuliza ni nani anayemuita au ndiyo kwenye mahojiano mengine na mkuu wa polisi.
“Nipo afande,” Athuman aliitikia
”Unaitwa nje.”
Mlango ulifunguliwa na Athuman alitoka nje ili akamuone anayeniita. Alitoka hadi nje ya jengo, ilikuwa tofauti na wengi huishia kaunta na kuzungumza na wageni wao. Alijiuliza nani aliyekuwa akimwita.
Nilipotoka nje alishtuka kumkuta ni Rachel, bila aibu mtoto wa kike alimkimbilia na kumkumbatia. Kitu kile kilichowashangaza askari wote waliokuwa pale kituoni.
” Pole sana mpenzi, vyote ni vizingiti vya penzi letu, lakini tutavivuka, “ Rachel alisema akiwa bado amemkumbatia. Athuman hakujibu kitu alitulia tuli ili ajue nini nitachoendelea.
“Athuman mpenzi tunaweza kwenda, nimeisha kuwekea dhamana.”
Alisema Rachel huku akijitoa kifuani na kumshika mkono, waliongozana hadi katika BMW aliyokuja nao Rachel alimfungulia mlango kwa heshima. Athuman aliingia kisha Rachel naye alizunguka upande wa pili na kuingia.
Baada ya kila mmoja kufunga mkanda safari ilianza ya kumrudisha nyumbani.
Njiani Rachel alimpa pole nyingi Athuman na kumuomba msamaha kwa yote yaliyonitokea.
“Mpenzi pole sana, lakini usijali.”
“Asante Rachel,” Athuman alijibu kwa upole.
“Athuman mapenzi yangu ni mazito kwako nakuahidi kukulinda kwa nguvu zangu zote,” Rachel alijisahau kama anaendesha gari na kuanza kunitomasa Athuman nusra wapate ajali.
Wakiwa njiani Rachel aliliona gari la baba yake likija kwa mbele alimuamulisha Athuman alale chini.
“Athuman lala chini baba huyo!”
Athuman aliona bwawa limeingia luba, moyo ulimpasuka pa! alijua shughuli imeiva . Aliamini kama Baba Rachel akiniona tena yupo na mwanaye angemfanya kitu kibaya hata kumpiga risasi.
Alitii amri kwa kufungua mkanda haraka na kuinama chini mara Rachel aliaimamisha gari ili kuzumngumza baba yake aliyemuwashia taa asimame.
“Vipi unatoka wapi saa hizi?” Ilikuwa sauti ya mzee Mulisa.
“ Natoka kwa shoga yangu Joyce,” Rachel alijibu kwa kujiamini.
“Mbona hukuaga, mama yako alikuwa anakutafuta wahi nyumbani… Pia nilisahau kamwambie leo naweza kuchelewa kurudi.”
“Baba naye yaani umeshindwa kumpigia mama simu?” Rachel alimwambia baba yake.
“Nitafanya hivyo ila na wewe fikisha ujumbe.”
“Sawa baba.”
Rachel aliagana na baba yake na kukanyaga mafuta.
“Nyanyuka mpenzi, pole kwa usumbufu pia naomba univumilie kwa yote yaliyokutokea au yatakayokutokea.”
“Nimekuelewa mpenzi.”
Athuman muda wote alijikuta akijiuliza maswali mengi juu ya yote yaliyomtokea na jinsi Rachel alivyomtoa polisi na hatima ya penzi lao ambalo kwake aliiona hatari mbele yake.
Rachel alisimamisha gari mbele ya nyumba anayoishi Athuman, waliteremka pamoja na kuingia ndani. Baada ya muda Rachel aliniaga na kuondoka na kumuhaidi atampitia jioni ili waende sehemu tulivu kwa maongezi zaidi. Athuman alishindwa kumkatalia alimkubalia.
******
Kengele ya mlangoni ilimuashilia Athuman nje kuna mtu, alisogea hadi mlangoni na kufungua hakuwa mwingine ila Rachel alikuwa amependeza sana . Kwa vile naye alikuwa tayari amejiandaa waliongozana hadi katika gari moja la kifahari la wazi na kuelekea pembeni ya bahari ya Hindi.
Athuman na Rachel walielekea ufukweni, walipofika hawakutelemka haraka ndani ya gari. Upepo mwanana wa bahari uliwalipepea, Rachel alifungua kifuko kidogo na kutoa soda mbili za kopo pamoja na sambusa ambazo ambazo alizinunua kwa ajili ya kutafuna wakati wa maongezi.

Nini kiatendelea?
 
Love Stori: Muhanga wa mapenzi
Sehemu: 06
Mtunzi: Ally Mbetu
SIMU: 0713646500......
ILIPOISHIA:

Kengele ya mlangoni ilimuashilia Athuman nje kuna mtu, alisogea hadi mlangoni na kufungua hakuwa mwingine ila Rachel alikuwa amependeza sana . Kwa vile naye alikuwa tayari amejiandaa waliongozana hadi katika gari moja la kifahari la wazi na kuelekea pembeni ya bahari ya Hindi.
Athuman na Rachel walielekea ufukweni, walipofika hawakutelemka haraka ndani ya gari. Upepo mwanana wa bahari uliwalipepea, Rachel alifungua kifuko kidogo na kutoa soda mbili za kopo pamoja na sambusa ambazo ambazo alizinunua kwa ajili ya kutafuna wakati wa maongezi.
SASA ENDELEA...

Rachel, pamoja wa ugeni kwa Athuman hakuonyesha woga wowote kama ilikuwa siku yao ya kwanza kuwa karibu na kwa nafasi kama ile. Alipitishia mkono shingoni huku ukitetemeka ikionesha hajiamini Athuman alitulia tuli alimwacha afanye atakacho.
“Athuman vipi, mbona huoneshi kama tupo pamoja au bado unawaza ya baba?” Rachel alimuuliza Athuman huku akimtazama usoni.
“Nikweli Rachel hata kama nitaonyesha mapenzi juu yako ni kazi bure,” Athuman alijibu kwa sauti ya upole.
“Aah! Kwanini unasema hivyo ?“Rachel aliuliza akionesha ameshtuka sana kutokana na kauli ya Athuman.
“Rachel wewe ni mtoto wa tajiri hivyo sina ubavu wa kushindana na baba yako.”
“Ni kweli usemayo lakini penzi halifundishwi shule wala toka kwa wazazi , ni upendo unaotoka ndani ya moyo wa watu wawili walio shibana. Hivyo msimamo wetu ndio siraha pekee ya kuwafanya wazee wangu kulikubali matakwa yetu, nami nipo radhi kwa hali na mali kuona penzi letu linadumu milele,” Rachel alisema huku machozi yakimtoka.
“Usemayo ni kweli, kumbuka baba yako ana uwezo wa kunifanya chochote ili kuhakikisha ananishikisha adabu. “
“ Athuman mpenzi, kumbuka mimi ni mtoto wa tajiri ambaye napata kila kitu ninachotaka kwa wazazi wangu. Na wazazi wangu wananipenda sana vyote wanaweza kunipa sio mapenzi,” Rachel alisema huku akimtazama Athumani kwa jicho la huruma.
“Rachel hakuna kinachokosekana kwa wazazi hata mapenzi ukifika muda wake utayapata.”
“Penzi nilipate vipi kwa wazazi wangu, sasa Athuman naona tumechokana kwa muda mfupi,” jibu la Athuman lilimkwaza Rachel.
“ Samahani Rachel naona hujanielewa vizuri, sina maana unayofikiria. Maana yangu kutapata mchumba ambaye atapokelewa na wazazi wako bila vikwazo,” Athuman alitetea hoja yake.
“Aah! Lakini anaweza kuwa sio chaguo langu siku zote ndege hutua mti aupendao, nami tayari nilishatua kwako.”
Maneno mazito yale yalimfanya Athuman akose cha kuzungumza na kubakia akimkazia macho Rachel ambaye macho yake yataka ujabari kumtazama yalijaa majaribu matupu.
“Athuman japo mimi ni mtoto wa tajiri lakini nipo kizuizini na mkombozi wangu ni wewe, nimeukabidhi moyo wangu mikononi mwako tafadhari nipokee nipo chini ya miguu yako.”
Rache aliliomba penzi la Athuman kwa sauti tamu ya kinanda
ya kubembeleza huku machozi yakiweka michirizi juu ya mashavu.
“Rachel siwezi toa jibu haraka kutokana na kichwa changu kutingwa na mambo mengi, nipe muda,” Athuman alijibu kwa sauti ya upole.
“Jamani Athuman, kwanini usiseme tu upo tayari kunipokea ili niwe wako. Kama mimi nilivyojitolea juu yako?”
Hali aliyokuwa nayo Rachel ilimtia huzuni Athuman, kama kawaida yake machozi yalizidi kumtoka.
“Rachel mpenzi nami nipo radhi kukupokea ili uwe wangu,” Athuman alijikuta akisema bila kutambua nazungumza nini.
“Waaaooo! Kweli Athuman?” Rachel alimkumbatia kwa furaha na kujikuta wakigusanisha midomo yao katika mapenzi mazito.
Walifungua vinywaji vyao huku wakigonganisha kopo zao, walikunywa huku wakinyweshana na kulishana keki kwa mdomo kama ndege na kinda lake. Rachel aliniona ni kiumbe kilichozaliwa upya katika ulimwengu wa wapendanao, kila mmoja alilifurahia penzi lile jipya.

*****
Mzee John Mulisa na mkewe mama Rachel wakiwa sebuleni waliendelea na mazungumzo yao, baba Rachel alimuuliza mkewe:
“Mama Rachel huyu mtoto mbona simuoni amekwenda wapi?”
“Amekwenda kwa shoga yake Joyce,” Mama Rachel alijibu bila wasiwasi wowote.
“Mbona leo amechelewa sana kurudi?”
“Sijui nini kimemchelewesha, ningekuwa na wasiwasi kama yule mwanarahamu angekuwa nje... Tena kweli baba Rachel umefikia wapi na yule fisadi?”
“Kwa kweli leo nilikuwa bize lakini mwache apate adabu, wiki ijayo lazima afikishwe mahakamani na hukumu siku hiyo hiyo tena ngoja niwasiliane na mkuu wa kituo cha polisi nijue amefikia wapi,” Mzee Mulisa alichikua simu ya mkononi na kubonyeza namba za kituo cha polisi, haikuita muda mrefu simu ilipokewa.
“Haloo kituo cha polisi makao makuu hapa, tukusaidie nini?”
“ Mulisa naongea.”
“Ahaa! Mzee shikamoo kumbe wewe, “ mkuu wa kituo alijibu kwa adabu.
“Ndiyo mimi, vipi ile shughuli mmefikia wapi?”
“Mzee ile shughuli tuliona haina umuhimu wowote kwa hiyo hatukuishughulikia.”
“Kwa nini useme hivyo?” Mzee Mulisa aliuliza.
“Tutafanyaje wakati mtu mwenyewe yupo nje.”
“Yupo nje? Mbona sikuelewi ina maana mmekaidi amri yangu?” Aliuliza kwa ukali.
“Sio sisi mzee ni mwanao ndiyo kaja kumtoa leo asubuhi,” mkuu wa kituo alijitetea.
“Kwa nini mmemruhusu amtoe?” Alizidi kupamba moto.
“Sio sisi ila ni wewe mzee ulishasema tusiikatalie lolote familia yako hata mbwa wako.”
Kauli ile ilimfanya Mzee Mulisa ashushe pumzi ndefu kama mtu aliyetua mzigo mzito na kumshtua mkewe aliyekuwa akifuatilia mazungumzo yale.
“Mume wangu mbona hivyo?”

Nini kitaendelea?
 
Love Stori: Muhanga wa mapenzi
Sehemu: 07
Mtunzi: Ally Mbetu
SIMU: 0713646500......

ILIPOISHIA:
“Mzee ile shughuli tuliona haina umuhimu wowote kwa hiyo hatukuishughulikia.”
“Kwa nini useme hivyo?” Mzee Mulisa aliuliza.
“Tutafanyaje wakati mtu mwenyewe yupo nje.”
“Yupo nje? Mbona sikuelewi ina maana mmekaidi amri yangu?” Aliuliza kwa ukali.
“Sio sisi mzee ni mwanao ndiyo kaja kumtoa leo asubuhi,” mkuu wa kituo alijitetea.
“Kwa nini mmemruhusu amtoe?” Alizidi kupamba moto.
“Sio sisi ila ni wewe mzee ulishasema tusiikatalie lolote familia yako hata mbwa wako.”
Kauli ile ilimfanya Mzee Mulisa ashushe pumzi ndefu kama mtu aliyetua mzigo mzito na kumshtua mkewe aliyekuwa akifuatilia mazungumzo yale.
“Mume wangu mbona hivyo?”
SASA ENDELEA...
“Tunafanya kazi ya bure kubeba maji kwenye gunia.”
“Kwa nini mume wangu?”
“Yaani Rachel anavunja amri yangu?”
“Kafanya nini?”
“Amemtoa yule kijana, leo akirudi atanitambua na huyo kijana atajuta kuzaliwa,”Mzee Mulisa alisema kwa hasira.
“Basi inawezekana hata kwa huyo Joyce hakwenda yupo na huyo kijana, kuna umuhimu wa kupiga simu kwa kina Joyce ili kupata ukweli wa mambo.”
“Sawa,” Mzee Mulisa aliitikia kwa unyonge hata nguvu hakuwa nazo tena. Mama Rachel aliamua kupiga simu ili kupata ukweli. Baada ya simu kuita kwa muda ilipokelewa upande wa pili na mama Joyce.
“Haloo naomba kuzungumza na Joyce mimi mama Rachel.”
Baada ya muda Joyce alikuwa katika simu.
“Haloo mama shikamoo.”
“Marahaba mwanangu, eti Rachel leo amefika huko?”
Wakati huo Rachel alikuwa ndio kwanza anaingia sebuleni kwao, swali alilisikia kabla Joyce hajajibu kitu aliiwahi simu ya mama yake na kuikata.
“Rachel kwa nini uikata simu?”
“Simu ya nini wakati mimi mwenyewe nimekwisha ingia,” alijibu kwa kujiamini.
Mama yake alishindwa kuzungumza chochote na kumtazama mwanaye. Mzee Mulisa alishtuka pale kwenye kochi baada ya kupitiwa na usingizi. Alinyanyuka kwa hasira alimshika mwanaye na kumuuliza.
“Wewe mwana haramu kwa nini umemtoa yule shetani polisi? ”
“Lazima nimtoe kosa lake nini? Kama mwenye makosa ni mimi nifungeni mimi sio mtoto wa watu asiye na hatia, “ jibu lilikuwa kama kufuli katika mdomo wa Mzee Mulisa na kuzidi kumchosha zaidi baada ya kuyasema yale Rachel alikwenda chumbani kwake kulala na kuwaacha wazazi wake wakiwa vinywa wazi.
“Mke wangu kuna umuhimu wa kumdhibiti yule kijana.”
“Kuna haja ya kufanya hivyo.”
***
Siku ya pili Rachel alikutana na Joyce shuleni, wakati wa mapumziko shoga yake alitaka kujua sababu ya mama yake kukata simu. Rachel alimpa stori kamili juu ya kufanikiwa kumpata Athuman.

“ Hongera shoga, mambo si hayo ulikuwa unaogopa nini, lakini ipo kazi kati yako na Mzee Mulisa.”
“Atatuliza boli tu,” Rachel alisema kwa kujiamini.
“Ehe! Tuachane na hayo vipi kuhusu pepa, maana imebakia wiki, sijui umejiandaa vipi?” Joyce alimuuliza shoga yake.
“Sio siri toka Athuman aingie akilini, sikupata tena muda wa kusoma zaidi ya kumuwaza yeye.”
“Sasa ndiyo itakuwaje?”
“Joyce mtihani wangu mkubwa maishani mwangu naamini ulikuwa kumpata Athuman, kwa vile nimefauru sina tena haja ya mtihani mwingine.”
“Ina maana hufanyi tena hata huo mtihani?” Joy alishtuka.
“Nitafanya kutimiza wajibu lakini sitegemei kwenda popote zaidi ya ndoa yangu na Athuman.”
“Shoga una makubwa, mara hii mipango ya ndoa?”
“Yote tuna kamilisha kesho tena shoga nitakualika ili ushuhudie tukivalishana pete ya uchumba lazima uwepo kupiga picha.”
Muda wa kutoka shule ilipotimu Toyota VX V8 ili simama mbele ya shule na kuwachukua Rachel na Joyce.
***
Athuman alijikuta katika kipindi kigumu cha kulikubali penzi na mtoto wa tajiri, wakati baba yake anawaka mithili ya moto wa tiper. Alijiuliza ni kweli akishilikiana na Rachel wataweza kuuzima moto wa mzee Mulisa mtu mwenye pesa kama mchanga. Alijikuta akipiga moyo konde na kuwa radhi kukabiliana na ushindani toka kwa mzee Muliza kutokana na mapenzi ya dhati Rachel aliyoonesha kwake.
Vilevile alijua kwa kipindi kile Rachel angemsaidia kutatua matatizo yake kwa kumweleza matatizo yake ambayo yote yalitatuliwa na Rachel ambaye alimuahidi kumfanya aishi maisha ambayo kwake mwanzo aliona ni njozi.
*****
Kwa vile mtoto wao alikuwa karibu na kufanya mtihani wa mwisho wa kidato cha nne, Mzee Mulisa na mkewe walionelea lazima awekwe chini ya ulinzi mkali ili ajiandae vizuri na mtihani. Walimuhamisha chumba chake na kumuhamishia chumba cha self conteiner ili ashinde ndani akijisomea baada ya muda wa shule.
Pamoja na hatua waliyofikia ya kumdhibiti vile ili ajiandae na masomo hilo halikumfanya Rachel asimuwaze Athuman. Rachel aliwaomba wazazi wake awe karibu na Joyce ili wasaidiane kusoma, hawakumkatalia. Joyce aliombewa ruhusa kwa wazazi wake na kukubaliwa na kuhamia nyumbani kwao Rachel kwa kipindi kile cha maandalizi ya mtihani.

Wito ule ulimfanya Joyce ashangae jinsi Rachel alivyobadilika kuonesha mabadiliko ya maandalizi ya mtihani alijiuliza ni kweli Rachel ameamua kujikita kwenye masomo. Lakini kumbe ilikuwa tofauti, ilipotimu usiku Rachel hakuwa katika masomo zaidi ya kumpa shoga yake story za mapenzi hasa zaidi za Athuman. Ikawa mara aibusu picha kubwa ya Athuman ya passport size.
“Rachel bora niendoke zangu nyumbani sina muda wa story zaidi ya kujisomea,” Joy alishtuka na tabia za shoga yake.
“Joy usiwe hivyo shoga yangu unajua saa hizi nipo kizuizini nina hamu ya kumuuona mpenzi wangu Athuman.
“Sasa mmi uliniitia nini, si bora ungeniacha nyumbani nijisomee mwenyewe,” Joy alimlalamikia Rachel.
“Joyce hiyo ilikuwa kuwafunga macho wazee, muda si mrefu nitatoka kwenda kwa Athuman,” Rachel alionekana kutojali chochote zaidi ya kuzama katika mapenzi kuliko masomo.
“Kwenda kwa Athuman! Usiku wote huu?” Joy alishtuka.
“Eeh, kipi cha ajabu.”
“Rachel usiku wote huu anafuata nini? Baba yako akija nitamjibu nini?”
“Hakuna mtu wa kuja muda huu wakilala wamelala”
“Kwanza utapitia wapi milango yote imefungwa?”
“Nitapitia dirishani.”
“Rachel mbona una makubwa! Utateremkaje toka hapa hadi chini?” Joy alizidi kumshangaa shoga yake.

Nini kitaendelea?
 
Love Stori: Muhanga wa mapenzi
Sehemu: 08
Mtunzi: Ally Mbetu
SIMU: 0713646500......
...
ILIPOISHIA:.
“Joyce hiyo ilikuwa kuwafunga macho wazee, muda si mrefu nitatoka kwenda kwa Athuman,” Rachel alionekana kutojali chochote zaidi ya kuzama katika mapenzi kuliko masomo.
“Kwenda kwa Athuman! Usiku wote huu?” Joy alishtuka.
“Eeh, kipi cha ajabu.”
“Rachel usiku wote huu anafuata nini? Baba yako akija nitamjibu nini?”
“Hakuna mtu wa kuja muda huu wakilala wamelala”
“Kwanza utapitia wapi milango yote imefungwa?”
“Nitapitia dirishani.”
“Rachel mbona una makubwa! Utateremkaje toka hapa hadi chini?” Joy alizidi kumshangaa shoga yake.
SASA ENDELEA...

“Nina kamba nimeshaiandaa na kuifanyia mazoezi.”
“Mmh, hayaa,” Joy hakuwa na la kusema.
Ilipotimu saa tano na nusu usiku Rachel alitoka kupitia dirishani kwa kutumia kamba. Kabla ya kuondoka Joy alimbembeleza asifanye hivyo kwani aliogopa atawajibu nini wazazi wake pindi wajapo na kutomkuta.
“Joy asikuambie mtu kupenda ugonjwa nimekuwa mtumwa wa penzi la Athuman, wiki sasa sijamwona machoni mpenzi wangu.”
***
Kwa Athuman alijikuta katika kipindi kigumu pale alipomkosa kumtia machoni Rachel. Kila alipojipitisha kwao hakufanikiwa kumuona alimanusra aende kuulizia lango kuu la nyumba ya Mzee Mulisa, lakini wazo hilo hakuliafiki. Siku zote usiku kwake ulikuwa mrefu kwa ajili ya kumuwaza Rachel mtoto wa tajiri.
Kila mawazo yalipozidi aliichukua picha ya Rachel aliyokuwa ameiweka chini ya mto na kuibusu kisha aliizima taa yenye mwanga mkali na kuwasha taa ya rangi ya kijani na kupunguza sauti ya muziki mololo kwa kutumia limoti uliutafuta usingizi kwa kubembelezwa na kibao laini my heart will go on kilichoimbwa Celine Dion.
Sauti ya kengele ya mlangoni ilimshitua Athuman toka katika usingizi ulioanza kumchukua. Alijiuliza atakuwa nani wote ule, saa ya ukutani ilimuonesha saa sita kasoro usiku.
Alinyanyuka kitandani na kwenda hadi mlango kabla ya kufungua mlango aliuliza.
“Nani?”
“Mimi,” sauti ile ilimshtua ilikuwa inafanana na ya mpenzi wake Rachel, akilini hakufikiria kama angeweza kuja usiku ule. Rachel alipaza sauti ya juu
yenye kuchanyanganyika na ukali ilikuwa kama inamzindua usingizini.
Athuman hakuamini masikio yake baada ya sauti ile kuwa kweli ya Rachel. Kabla hajajua nini kinaendelea, Rachel alisema kwa hasira:
“Athuman kufungua imekuwa mwaka, hunipendi au una mtu mwingine na mimi napoteza muda wangu kukupenda basi mimi naondoka.”
Alipofungua mlango mbele ya macho yake hakuamini kumkuta Rachel peke yake usiku ule. Alitaka kujua Rachel amefikaje pale, wasiwasi wake huenda ule ulikuwa mtego mwingine.
Lakini alipiga moyo konde na kumkaribisha ndani, baada ya kumuingiza ndani alitaka kujua amefikaje pale. Rachel alimpa picha kamili jinsi alivyo toroka kwao.
“Sasa wakija chumbani kwako na kukukosa itakuwaje?” Athuman alimuuliza Rachel.
“Hata siku moja hawawezi kqka chumbani kwangu usiku ndio maana wakanitafutia chumba cha self container.”
Athuman hakupoteza muda alimpokea Rachel , kwake ilikuwa kama majibu ya maumivu ya kumkosa mpenzi wake kwa wiki nzima.Twisheni! aliyoitoa kwa Rachel katika masuala ya mapenzi ilizidi kumchanganya mtoto wa watu, kutokakana na kuwa mgeni katika medani ile.
Lakini yalianza kutoa matunda naye Rachel aliweza kwenda naye sambamba katika medani ile huku akifurahia mapenzi. Baada ya kutwanga na kupepeta wote walikuwa hoi bin taabani.
Lakini Rachel ndiye alikuwa hoi zaidi, kutokana na muda kuwa umekwenda Athuman alimuomba Rachel arudi kwao kabla ya kupambazuka Lakini Rachel alikataa na kusema atalala mpaka asubuhi. Athuman alimbembeleza sana na kumkubalia kurudi kwao kwa shingo upande.
Alimsindikiza hadi kwao muda huo ulikuwa majira saa kumi alfajiri, baada ya kuhakikisha ameshaingii ndani ya uzio wa nyumba yao Athuman alirudi zake kuendelea na usingizi.
***
Rachel alipoingia chumbani kwake alijitupa kitandani bila kubadili nguo zake na kujilaza kutokana na mwili wote kuwa umenyong’onyea kwa mikiki mizito ya Athuman na kupitiwa usingizi mzito. Ilipotimu muda wa kwenda shule Rachel alikuwa bado amejawa na usingizi na mwili ulikuwa nyang’anyang’a hata nguvu za kunyanyuka kitandani hakuwa nazo.
Joy alipomuamsha waende shule, shoga yake alimwomba aende peke yake kwa vile alikuwa bado na usingizi mzito pia mwili haukuwa na nguvu. Joy alimbeleza waende shule, bado alishikilia msimamo wake wa kuendelea kulala. Mama Rachel alimuuliza Joy kuhusu Rachel ilibidi atengeneze uongo kuwa shoga alisoma sana mpaka alfajiri na kumfanya azidiwe na usingizi. Mama Rachel alikubaliana na uongo wa Joy na kumuacha Rachel aendelee kulala.
***
Siku ya pili kama kawaida ilipofika muda wake Richel alikwenda kwa Athuman na kumuacha Joy akijisomea na kurudi saa tisa usiku akiwa hoi na kushindwa tena kuamka asubuhi. Lakini Joy alimwambia kama hata kwenda shule basi siku ile angerudi kwao.
Rachel alijilazimisha kwenda ili kufanya rafiki yake aendelee kuwepo kwao ili kuzidi kuficha siri yake. Rachel alionekana amechoka na mama yake kuhoji hali ile.
“Vipi maendeleo yake kimasomo?” alimuuliza Joy
“Yanaridhisha.”
“Vipi na leo umekesha unasoma?”
“Ndiyo mama.”
“Na kweli maana inaonesha leo hakulala kwa kijisomea, “ kauli ile Rachel alichekelea chini chini kama wazazi wake wangeujua ukweli wangeua mtu.
Rachel shuleni alishinda akisinzia, muda wote alifikiria mchezo uliomrusha akili kama sio kumpangawisha na kuona kusoma ni kupoteza muda bora aolewe na Athuman ambaye ndiye aliyemuingiza katika ulimwengu wa wapendanao.
Rachel alikuwa tayari kufanya lolote kuliko kumkosa Athuman mwanaume aliyeyateka mawazo yake na kumuwaza muda wote na kuyaona masomo hayana nafasi akilini mwake.
Siku ambayo hakwenda kwa Athuman muda wa kujisomea usiku aliutumia kumuwaza huku akikumbatia mto muda wote na kujisahau kuwa anatakiwa kusoma na aliposhtuka ilikuwa tayari kumepambazuka. Siku ya pili alipokwenda shuleni mtindo ulikuwa uleule wa kusinzia darasani. Mwalimu alimuona na kumfuata.
“Rachel vipi?”
“Maandalizi ya mtihani mwalimu.”
“Ooh! Pole sana kwa vile toka uingie unasinzia bora ukalale nyumbani upunguze usingizi.”
Rachel alipata nafasi ya kurudi nyumbani, hakwenda nyumbani alikwenda moja kwa moja kwa Athuman. Alimkuta mwenye mawazo mengi kitu ambacho hakupenda kukiona kikimtokea mpenzi wake.
“Vipi mpenzi mbona hivyo?” Rachel alimuuliza Athuman.
“Nina shida,” Athuman alijibu kiunyonge.
“Athuman, kwa shinda yako nipo radhi hata kumuua hata baba yangu ili kuhakikisha unapata furaha ya maisha yako.”

Nini kitaendelea?
 
Love Stori: Muhanga wa mapenzi
Sehemu: 09
Mtunzi: Ally Mbetu
SIMU: 0713646500......

ILIPOISHIA:
Siku ambayo hakwenda kwa Athuman muda wa kujisomea usiku aliutumia kumuwaza huku akikumbatia mto muda wote na kujisahau kuwa anatakiwa kusoma na aliposhtuka ilikuwa tayari kumepambazuka. Siku ya pili alipokwenda shuleni mtindo ulikuwa uleule wa kusinzia darasani. Mwalimu alimuona na kumfuata.
“Rachel vipi?”
“Maandalizi ya mtihani mwalimu.”
“Ooh! Pole sana kwa vile toka uingie unasinzia bora ukalale nyumbani upunguze usingizi.”
Rachel alipata nafasi ya kurudi nyumbani, hakwenda nyumbani alikwenda moja kwa moja kwa Athuman. Alimkuta mwenye mawazo mengi kitu ambacho hakupenda kukiona kikimtokea mpenzi wake.
“Vipi mpenzi mbona hivyo?” Rachel alimuuliza Athuman.
“Nina shida,” Athuman alijibu kiunyonge.
“Athuman, kwa shinda yako nipo radhi hata kumuua hata baba yangu ili kuhakikisha unapata furaha ya maisha yako.”
SASA ENDELEA...
“Hivi mpenzi maisha haya mpaka lini? Kaka akirudi nitakuwa wapi, pia hatutakuwa na nafasi ya kuinjoi mapenzi yetu.”
“Athuman ulikuwa anatakaje?” Rachel alimuuliza huku akichezea bustani la kifuani.
“Ungenipangia nyumba ili kaka akirudi tuendelee na raha zetu.”
“Athuman mbona hilo dogo ulikuwa anataka lini?”
“Kwa vile kaka amebakiza miezi miwili arudi ingekuwa vizuri mwezi mmoja kabla ya kurudi.”
“Basi hiyo kazi niachie unataka sehemu gani?”
”Yenye hadhi na sisi.”
“Hilo umepata omba jingine.”
Mara nyingi Rachel alikuwa akiiba ATM Card na kuchukua kiasi cha pesa kutumia lakini kupitia ombi la mpenziwe alipanga kuchota pesa nyingi hata milioni kumi kwenye card ya baba na mama yake.
*****
Mzee Mulisa na mkewe walikuwa wamesahau ya Athuman na kuelekeza nguvu zao kwa mtoto wao ili kuhakikisha anafanya vizuri katika mitihani wa kidato cha nne kwa kumpatia kila alichokitaka ili kuhakikisha anafanya vizuri. Kwao ilikuwa sawa na kutwanga maji katika kinu au kubeba maji kwenye gunia kutokana na mtoto wao kuhamishia mawazo kwa Athuman na si katika masomo.
“Mama Rachel siamini kama mtoto wetu angetulia kiasi hiki, alitaka kuchanganyikiwa bila kumbana na kumuahamishia kule sijui kama tungemuweza,” Mzee Muliza alimwambia mkewe.
“Lakini baba Rachel yote umeyataka wewe ulimdekeza hata mimi ulinizuia nisimkanye eti kipenzi chako, kwa vile mtoto wa tajiri atakiwi kukosa raha. Haya sasa kumdekeza kwako kidogo kututumbukie nyongo.”
Wakiwa katikati ya maongezi mara Rachel aliingia ndani.
“Vipi mama mbona hivyo unaumwa?”
“Hapana baba siku hizi nasoma sana usiku muda mwingi nikiwa shuleni nasinzia,” Rachel alitengeneza uongo.
“Punguza kusoma sana usiku,” Mzee Mulisa alisema.
“Lakini si ninyi mmenitia kizuizini ili nisome, tatizo nini?”
“Soma mama, lakini vipi maendeleo yako?” mama yake alimuuliza.
“Sio mabaya sana nina uhakika wa kufanya vizuri.”
“Nakuahidi ukifanya vizuri nitakutafutia zawadi mkubwa, kwanza nitakununulia gari la kifahari la kuendea shuleni,” baba yake alimtia moyo.
“Nitashukuru baba.”
Rachel aliagana na wazazi wake na kwenda zake kulala, ama kweli usilolijua sawa na usiku wa kiza. Kama wangejua usingizi ule mtoto wao unatokana na nini wangemmwaga mtu ubongo.
***
Rachel kila usiku masomo yake aliyasomea kwa Athuman kwa muda wote wa kujiandaa na mtihani. Familia mbili ya wazazi wa Rachel na Joyce ziliungana pamoja kuwafanyia watoto wao sherehe ndogo ili kuwapa moyo ili wajitayarishe vizuri na mtihani wa kidato cha nne.
Ilikuwa ni sherehe iliyoandaliwa katika Jumba la mzee Mulisa na wazazi wa Joyce, wazazi wote waliwahidi watoto wao zawadi nyingi pindi watakapofanya vizuri au kupata alama za kuridhisha katika matokeo yao.
Sherehe ile pamoja na kuwa ya kupendeza kati ya familia mbili lakini ilikuwa kero kwa Rachel ambaye alikuwa kama bugudha kwake akili yake ilikuwa haiwazi mtihani zaidi ya penzi tamu kwa Athuman. Baada ya sherehe kwisha wazazi wake walimuweka chini ili kuongeza ahadi nzito.
“Mwanangu Rachel nakuahidi ukifanya vizuri katika masomo yako nitakununulia ndege kwa ajili ya kukupaleka shule,” Mzee Mulisa alimuahidi Rachel na mkewe kila mmoja aliahidi zawadi yake.
“Mwanangu ukipata division 1 kama alivyosema baba yako tunakununulia ndege na kuwa mwanafunzi wa kwanza Afrika kumiliki ndege na ukipata 2 mimi mama yako nitakununulia gari lolote la kifahari ulitakalo.”
“Sitawangusha wazazi wangu.”
Kama wazazi wa Rachel wangeingia moyoni kwa mtoto wao basi zawadi kubwa kuliko yote mtoto wao angetaka kuolewa na Athuman.
“Wangesema kama ni ningepata alama za kuridhisha ningeolewa na Athuman mbona ningesoma kama mwendawazimu. Lakini shule sina hata hamu nayo bora siku zifike nipunguze bugudha za wazazi, “ Rachel alijifikiria na kuona wazazi wake kama wanacheza makidamakida.
Alipokuwa shuleni alinielezea yote yaliyoahidiwa siku ya sherehe.
“Joy bora tumalize ili nipate muda wa kukutana na sweet heart wangu.”
“Lakini Ray jitahidi basi shoga katika mtihani usipate ziro,” Joy alimbembeleza rafiki yake ili afanye vizuri kwenye mtihani kuliko kuhamishia mawazo yake kwa Athuman.
“Ina maana kupata ziro itasababisha nimkose Athuman?” Rachel alimuuliza huku ameshikilia mkono kiunoni.
“Siyo hivyo Ray wazazi watajisikia vibaya.”
“Vibaya kama nilikaa nyumbani bila kuolewa.”
***
Siku ya kufanya mtihani ilipofika Rachel hakuisumbua akili yake zaidi ya kufanya yale anayoyaweza na kuyaacha asiyoyaweza wala hakutaka kuumiza ubongo wake. Cha ajabu siku ya mwisho ya mtihani alishangilia kitu kilichomshangaza kila mmoja wengi walikuwa na wasiwasi labda ana uhakika na alichokifanya katika mtihani au alikuwa na majibu hasa wakizingatia ni mtoto wa tajiri.
Wangejua anachoshangilia wala isingewasumbua akili yao , wazazi nao walimpongeza mtoto wao kwa kumaliza salama mtihani wake. Rachel alipofika nyumbani hakuwa na muda wa kupoteza zaidi ya kuomba ruhusa kwa wazazi wake anakwenda kwa Joyce.
“Wazazi wangu naomba nifike kwa Joy kuna vitu vyangu nilivisahau ni muhimu sana.”
“Nenda lakini uwahi kupumzika si unajua baada ya kazi nzito ya mtihani unatakiwa kupumzika” alisema mama yake.
“Sawa mama sitachelewa.”
Wazazi wake walimuomba aende upesi ili awahi kurudi walipotaka kumpa gari ili awahi alikataa alisema atachukua Teksi.
“Chukua gari uwahi,” mama yake alisema.
“Hapana mama nitachukua teksi tu.”
“Haya basi nenda uwahi kupimzika.”
“Sawa mama.”
Alitoka nje na kuchukua teksi hadi kwa mpenzi wake huku wazazi wake wakiamini kabisa mtoto wao amekwenda kwa shoga yake Joy.

Nini kitaendelea?
 
Love Stori: Muhanga wa mapenzi
Sehemu: 10
Mtunzi: Ally Mbetu
SIMU: 0713646500......

ILIPOISHIA:
“Wazazi wangu naomba nifike kwa Joy kuna vitu vyangu nilivisahau ni muhimu sana.”
“Nenda lakini uwahi kupumzika si unajua baada ya kazi nzito ya mtihani unatakiwa kupumzika” alisema mama yake.
“Sawa mama sitachelewa.”
Wazazi wake walimuomba aende upesi ili awahi kurudi walipotaka kumpa gari ili awahi alikataa alisema atachukua Teksi.
“Chukua gari uwahi,” mama yake alisema.
“Hapana mama nitachukua teksi tu.”
“Haya basi nenda uwahi kupimzika.”
“Sawa mama.”
Alitoka nje na kuchukua teksi hadi kwa mpenzi wake huku wazazi wake wakiamini kabisa mtoto wao amekwenda kwa shoga yake Joy.
SASA ENDELEA…

Alipofika alimkuta ametulia sebuleni akiangalia tivii. Hata bila ya salamu alimvamia kwenye kochi huku akisema:
“Darling, mambo safi sasa hivi ushindwe mwanyewe.”
Alimkumbatia kwa furaha baada ya kuamini kamba iliyokuwa imemfunga imefunguka. Siku hiyo walifanya sherehe ambayo walipanga kuifanya atakapomaliza mtihani wa mwisho.
Walijikuta wakifanya sherehe ya wawili na kujikuta wakitumia hata vinywaji ambavyo hawajavizoea kwa kunywa pombe ambayo Rachel alijifanya mzoefu kumbe wapi. Alikunywa pombe zilizomzidi na kulala fofofo. Muda ulizidi kukatika bila Rachel kuonesha dalili zozote za kupata unafuu wa pombe. Athuman alijikuta akichanganyikiwa na kujiuliza atamwambia nini baba yake kama akitokea kama sio kuozea gerezani au kufa kwa kipigo au kuhukumiwa bila kupelekwa Mahakamani.
****
Mzee Mulisa alipotoka katika shughuli zake majira ya saa tatu na nusu usiku, alipoingia ndani kitu cha kwanza alitaka kuonana na mwanaye na ili ampe tathimini nzima ya mtihani na kujua nini matumaini katika mtihani ule.
“Mama Rachel hebu niitie huyo mwanao ili atupe picha ya mtihani kaonaje ili tumuandalie zawadi mapema,” Mzee Mulisa alisema huku akimpatia koti mkewe.
“Mbona mwanao toka alipotoka hajarudi.”
“Yaani mpaka saa hizi?”
“Si alishamaliza mtihani sijui kama atashikika.”
“Hayo siyo majibu mke wangu …hebu nipe hiyo simu yangu nimuulizie shoga yake.”
Mama Rachel alimpa mumewe simu baada ya kubonyeza za nyumbani kwao Joyce haikuchukua muda mrefu iliita na kupokelewa.
“Haloo nani ninayeongea naye?” Mzee Mulisa aliuliza.
“Mimi mama Joy,” sauti upande wa pili ilijibu.
“Ni Mzee Mulisa hapa.”
“Aah, shemeji, vipi leo maajabu kupiga simu.”
“Shemeji mbona Rachel amechelewa kurudi nyumbani mwambie awahi kurudi.”
“Shemeji mbona leo sijamwona Rachel?”
“Hujamwona vipi naye ameaga majira ya alasiri anakuja kwa Joyce.”
“Kwa kweli sijamwona labda nimuulize shoga yake.” Mama joyce alimwita joyce, baada ya kufika alipewa simu aongee na mzee Mulisa.
“Shikamoo baba,” Joy alimuamkia Mzee Mulisa.
“Aah! Joyce, marahaba mama hujambo?”
“Sijambo baba.”
“Eti shoga yako yupo wapi?”
“Toka tuachane shuleni sijaonana naye tena.”
“Etiii! Unasema hujamwona mbona sikuelewi atakuwa amekwenda wapi?” Mzee Mulisa nusra azirai kwa mshtuko.
*****
Wakati huo Rachel akiwa kwa Athuman hakuonesha
dalili zozote za kurudiwa na nguvu, Athuman alizidi kuchanganyikiwa kila alipouangalia muda ulizidi kukimbia saa ilionesha saa mbili usiku.
Alijikuta akichanganyikiwa asijue afanye nini, mapigo ya moyo yalimwenda kwa kasi woga ulitanda na kushindwa kujua afanye nini. Aliamua kumbeba Rachel hadi bafuni huku akionesha hajiwezi, alimvua nguo na kumwagia maji ya baridi ambayo kidogo yalimsaidia kupata nguvu kidogo.
“Rachel mpenzi wangu jikaze uende nyumbani,” Athuman alimbembeleza Rachel.
“Athuman usiniudhi hapa nimefika siondoki,” Rachel alisema kwa sauti ya kilevi.
“Hapa Rachel utaniingiza matatizoni baba yako atanila nyama.”
“Hawezi kwani kupenda mtu ni utashi wa mtu na si wazazi kama mtihani nimemaliza.”
Athuman alijitahidi kumbembeleza kumpeleka kwao alikubali japo kwa shingo upande. Alimkodia gari mpaka karibia na kwao, alipokaribia alishangaa kuona nje ya nyumba ya Mzee Mulisa kuna gari la polisi.
Baada ya muda gari la Mzee Mulisa ilitoka na kufuatiwa na magari mawili ya polisi. Athuman alimuomba dereva asimamishe gari mbali kidogo na nyumba ya mzee Mulisa.
Gari la mzee Mulisa liliwapita likiongoza msafara wa magari mawili ya polisi. Baada ya kuhakikisha yamepita alimwomba Rachel aende kwao mwenyewe . Aliteremka na kwenda kwao huku akipepesuka kidogo, alipohakikisha ameisha vuka geti lao aliondoka.
***
Baada ya majibu ya Joy, Mzee Mulisa alijikuta amesimama kama amepigwa na shoti ya umeme kitu kilichomshtua mkewe na kumuuliza.
“Vipi wanasemaje?” Mama Rachel alimuuliza mumewe aliyekuwa ameganda kama kapigwa na shoti ya umeme.
“Inasemekana hajafika nyumbani kwa kina Joyce.”
“Hajafika? Mbona sikuelewi, kama hajafika kaelekea wapi sasa, au kapata ajali. Baba Rachel tupeleke taarifa polisi ili tujue kama kuna ajali iliyotokea leo jijini,” mama Rachel alichanganyikiwa.
“Mama Rachel isiwe amekwenda kwa yule mwanaharamu wake?”
“Kweli mume wangu inawezekana, kabla ya kwenda huko lazima tuitaalifu polisi ili tukafanye msako kwa yule kijana,” mama Rache alitoa wazo.
“Nikimkuta nitaua mtu leo.”
Mzee Mulisa alipiga simu polisi kwa mkuu wa kituo wa polisi wa mkoa, mkuu alimuahidi kumpa ushirikiano. Alileta gari mbili lililojaa polisi, gari lilisimamishwa mbele ya nyumba ya mzee Mulisa.
Mzee Mulisa aliongozana na polisi hadi sehemu anayoishi Athuman nyumba ilizingilwa kama kuna gaidi aliyejificha ndani ya nyumba akiwa na bomu. Polisi waligonga mlango kwa nguvu bila kupata jibu. Wakati huo Athuman alikuwa amekwisha rudi na kuelekea nyumbani kwake.
Alipokaribia kwake alishangaa kuwaona askari wakigonga mlango wake, walipoanza kugonga kwa nguvu alijitokeza.
“Jamani mna shida gani mbona mnataka kunivunjia mlango?” wote waligeuka.
“Si huyu hapa,” Mzee Mulisa alisema kwea sauti ya mshtuko baada ya kumuona Athuman.
“Vipi wazee mbona mnavamia nyumba kama kuna jambazi lililokimbilia ndani?”
Mzee Mulisa alizidi kuchanganyanyikiwa baada ya kuufungulia mlango, waliingia ndani na kufanya upekezi wa nguvu. Baada ya pekua bila kuona mtu chochote, nilimshuru Mungu kimoyomoyo. Nilijiona nimecheza kama pele la sivyo ningesahaulika gerezani
****
Baada ya kumkosa ndani walimuuliza kwa vitisho lakini Athuman alionesha msimamo wa kutomtatambua Rachel. Baada ya kukosa ushahidi mzee Mulisa aliaga na kuondoka na kikosi cha polisi waliokuja na kazi moja. Athuman alimshukuru Mungu jinsi alivyokuta na jinsi walivyovamia na kumkosa Rechel.

Nini kitaendelea?
 
Love Stori: Muhanga wa mapenzi
Sehemu: 11
Mtunzi: Ally Mbetu
SIMU: 0713646500......

ILIPOISHIA:
Baada ya kumkosa ndani walimuuliza kwa vitisho lakini Athuman alionesha msimamo wa kutomtatambua Rachel. Baada ya kukosa ushahidi mzee Mulisa aliaga na kuondoka na kikosi cha polisi waliokuja na kazi moja. Athuman alimshukuru Mungu jinsi alivyokuta na jinsi walivyovamia na kumkosa Rechel.
SASA ENDELEA....
Aliamini kabisa kama wangemkuta na hali aliyokuwa nayo lazima polisi wangemuulia ndani au mzee Mulisa angemuua kwa risasi. Baada ya kuondoka Athuman alipigwa na butwaa baada ya kugundua juu ya kitanda kulikuwa na nguo ya ndani ya Rachel, aliamini kama mzee Mulisa angeiona lazima angeitambua kutokana na yeye kumnunulia kila kitu binti yake. Aliitoa pale na kuificha kisha alizima taa na kujilaza.
Usiku mzima alijiuliza Rachel akiulizwa na wazazi wake alikuwa wapi atawajibu nini. Lakini alimuamini Rachel alikuwa msichana msiri tena mwenye msimamo. Usingizi ulimpitia bila kujijua na kujikuta ameamka siku ya pili.
******
Majira ya saa nne asubuhi mlango uligongwa Athuman alikwenda kufungua, alipofungua alivamiwa na Rachel kwa furaha.
“Wawooo my husband to be.”
“Rachel vipi! Za toka jana?”
“Zipo bomba ile mbaya.”
“Mmh! Vipi jana ilikuwaje?”
“Hakuna kitu chochote.”
“Rachel, hukuulizwa ulikuwa wapi na wazazi wako?”
“Aah, mama aliniuliza.”
“Ulimjibu nini?”
“Nilimjibu nimeisha maliza mtihani.”
“Yeye akasemaje?”
“Anijibu nini kwani mi mtoto mdogo?”
“Basi jana baada ya kukufikisha tu na kurudi nyumbani nimemkuta baba yako.”
”Mzee Mulisa?” Rachel alishtuka.
“Ndiyo.”
“Wapi?”
“Kwangu.”
“Kwako anafanya nini?”
“Alikuwa amekuja kufumania?”
“Serious?”
“Kweli kabisa, tena alikuja na jeshi utafikiri wamegundua Osama kajificha hapa.”
“My Jesus.”
“Kweli kabisa elewa kabisa siku ambayo baba yako atanifumania nipo na wewe uhai wangu utakuwa mikononi mwake.”
”Akikuua wewe aniue na mimi.”
“Rachel unajua kuwepo kwako hapa nikunitia matatani?”
“Matatani kivipi, hivi Athuman mimi siyapendi maisha yako?”
“Rachel, kuja na gari la kwenu ni kidhibiti tosha hata mtu akipita na kuliona lazima atajua wewe upo hapa.”
“Kumbe wasiwasi wako ni huo, kwa taarifa yako baba ameondoka amekwenda Marekani na kurudi hadi mwezi mmoja ukatike.”
“Usiniambie! Na mama je?”
“Mama hana noma mnoko huwa baba siku zote.”
“Ooh! Kidogo moyo umetulia hukujua hali yangu ya mapigo ya moyo yalivyokuwa ikikimbia.”
Athuman alisema huku akishusha pumzi ndefu na kujasho chembamba kikimtoka.
“Pole sana mpenzi wangu kwani mimi siwaogopi wazazi wangu, nawaogopa lakini wewe nakupenda zaidi sipendi uumie kwa ajili yangu,” Rachel alimtoa hofu Athuman.
“ Asante kwa hilo. ”
Athuman alimbeba juu juu Rachel hadi juu ya kochi, kweli paka akitoka panya alikuwa na uhuru mkubwa wa kufanya atakalo bila woga wowote.
“Mmhu, ulikuwa unasemaje?”
“Leo nataka twende Bagamoyo tukapumzike ikiwezekana turudi baada ya siku tatu.”
“Na mama yako je?”
“Mama anajua mimi mtu mzima hawezi kufanya lolote.”
“Hapana Rachel japokuwa mama si mkali, lazima naye tumuheshimu ili siku likitokea upate wa kukutetea.”
“Basi tutarudi kesho.”
“Hapo kidogo sio mbaya sana.”
Athuman alijiandaa baada ya muda walielekea Bagamoyo kwenye hoteli ya kitalii kujirusha na mpenziwe.
********
Mzee Mulisa kabla ya kuondoka aliwaita vijana wake na kuwaeleza wamlinde Rachel na kumfuatilia kila kona atakayo kwenda kwa kupigwa picha za video na za kawaida ili akirudi awe na ushahidi kamili.
Vijana wa mzee Mulisa waliifanya kazi ile kwa kufuatilia kila kona ya Rachel atakapo kwenda. Rachel alipotoka asubuhi walimfuatilia bila yeye kujijua huku wakimpiga picha za kawaida na video.
Rachel mpaka anaingia kwa Athumani na kutoka kuelekea Bagamoyo, hakujua kama kuna watu wanamfuatilia yeye. Hotel aliyopanga vilevile nao walipanga na kuendelea kumpiga picha za ushahidi kwa siri. Kila kona aliyokwenda Rachel na Athuman walikuwa ubavuni kwao bila kujua na kuzidi kuwapiga picha za ushahidi.
****
Ilikuwa ni siku ya furaha kwa wapenzi wawili ambao siku hiyo walijirusha kila kona katika mapenzi mazito nao watu waliotumwa walifuatilia kila kona na kupiga picha za ushahidi walizotumwa na mzee Mulisa.
Baada ya kujirusha majini walipumzika mchangani kisha waliingia chumbani kwao, ile kidogo iliwapa ugumu watu waliokuwa wakiwafuatilia kwa kuzikosa picha za ndani kutokana na mazingira.
Ilibidi wawasiliane na Mzee Mulisa aliyekuwa Marekani jinsi mchakato ulivyokuwa ukiendelea.
“Mzee hapa tupo Bagamoyo Rachel yupo na yule kijana uliyemweka ndani kipindi kile wapo katika starehe za hali ya juu.”
“Aisee, basi mfuatilieni kila kona ili nikirudi nipate ushahidi wa kumshikisha adabu huyo mshenzi.”
“Lakini kwa nini mzee tusimshikisha adabu?”
“Hapana najua kunaweza kutokea makosa ya kusababisha mwanangu apate matatizo kitu ambacho sitaki kitokee. Endeleeni tu kumfatilia kazi zingine nisubirini nikirudi.”
“Sawa mzee.”
Muda huo wakiwasiliana na mzee Mulisa, Athuman na Rachel walikuwa wamejipumzisha ufukweni baada ya kuingia ndani na kujikuta wakikosa picha zingine za ushahidi. Ilibidi waende hadi mapokezi ili kujua kama wamechukua chumba muda au wanalala palepale.

Nini kitaendelea?
 
Love Stori: Muhanga wa mapenzi
Sehemu: 12
Mtunzi: Ally Mbetu
SIMU: 0713646500......

ILIPOISHIA:
“Mzee hapa tupo Bagamoyo Rachel yupo na yule kijana uliyemweka ndani kipindi kile wapo katika starehe za hali ya juu.”
“Aisee, basi mfuatilieni kila kona ili nikirudi nipate ushahidi wa kumshikisha adabu huyo mshenzi.”
“Lakini kwa nini mzee tusimshikisha adabu?”
“Hapana najua kunaweza kutokea makosa ya kusababisha mwanangu apate matatizo kitu ambacho sitaki kitokee. Endeleeni tu kumfatilia kazi zingine nisubirini nikirudi.”
“Sawa mzee.”
Muda huo wakiwasiliana na mzee Mulisa, Athuman na Rachel walikuwa wamejipumzisha ufukweni baada ya kuingia ndani na kujikuta wakikosa picha zingine za ushahidi. Ilibidi waende hadi mapokezi ili kujua kama wamechukua chumba muda au wanalala palepale.
SASA ENDELEA...
Walipofika mapokezi walimuulizia muhudumu aliyekuwa mwanamke.
“Samahani dada eti Athuman na Rachel wanalala au wanaondoka?”
“Ndio kina nani hao?”
“Wale vijana wawili wa kike na kiume.”
“Ooh! Wale ngoja niangalie,” baada ya muda alisema.
“Wamechukua chumba kwa siku mbili.”
“Wapo chumba namba ngapi?”
“111”
“Tunaomba chumba cha jirani na wao.”
“Chukueni 112.”
“Tupe hicho.”
Walichukua chumba namba 112 jirani na chumba walichopanga Rachel na Athuman ili waweze kuwa karibu nao. Walikwenda katika chumba walicho panga na kutumia muda mwingi kuwavizia huenda watatoka, lakini baada ya kuingia hawakutoka tena zaidi ya kupata kila kitu wakiwa ndani.
Kila mmoja alikuwa na hamu na mwenzake hakuna aliyekubali kuwa mbali na mwenzake hasa siku adimu kama ile. Baada ya kusubiri kwa muda ili wapate picha zingine kwa kuwa karibu ya mlango wa chumba cha Rachel bila mafanikio na muda nao ulikuwa ukiwatupa mkono walimpigia simu tena mzee Mulisa kumweleza mambo yaliyokuwa yakiendelea.
“Mzee hapa wamepanga chumba na kupanga kutoka baada ya siku pili.”
“Ina maana mama yake anafanya nini, okay kazi hiyo niachie mimi.”
Mzee Mulisa alimpigia simu mkewe ambaye aliipokea.
“Mhu! Mume wangu za huko?”
“Mbaya.”
“Kivipi tena mume wangu?”
“Rachel yupo wapi?”
“Ametoka.”
“Amekwenda wapi?”
“Mmh, sijajua huenda yupo kwa kina Joy”
“Una uhakika?”
“Mimi nitajuaje mume wangu sitembei nae.”
“Kwa taarifa yako Rachel yupo Bagamoyo na yule kijana.”
“Muongo! Umejuaje nawe haupo nchini?”
“Kuna watu niliwapa kazi ya kumfuatilia Bagamoyo nasikia amepanga chumba kwa siku mbili.”
“Mungu wangu Rachel huyu ana nini mwanangu? Huyu kijana kamlambisha kitu gani kinachomfanya asione wala kusikia. Sasa itakuwaje mume wangu?”
“Fanya hivi nitamtuma mkuu wa polisi aende kumchukua Rachel na kumuweka ndani kisha yule kijana wampe kipigo kitakatifu nikimkuta nimkute amevunjika kila kona ya mwili hata wakumuua sio tatizo.”
“Mmh! Mume wangu sasa hivi hunipeleki Bagamoyo kilichopo mtume huyo mkuu wa polisi akamkamate na kumuweka ndani mimi nitakwenda kesho.”
“Okay wacha niwaliane naye, lazima nimtie adabu yule kijana hawezi kunichezea kiasi hicho,” Mzee Mulisa alisema kwa hasira.
Mzee Mulisa akiwa amefura kama amekula amira alimpigia simu mkuu wa polisi aliyekuwa ameishalala.
“Sawa mzee nimekusikia niwatuma vijana wangu.”
“Siyo vijana wako nataka uende wewe,” alisema kwa kufoka kama anasema na mtoto wake.
“Sawa mzee.”
Ilibidi mkuu wa polisi aamke usiku ule aongozane na vijana wake mpaka Bagamoyo hoteli waliyoelekezwa. Askari walivamia hoteli kama kuna gaidi na kwenda hadi kwenye chumba alichopanga Rachel na Athuman na kugonga kwa nguvu.
Baada ya kugonga kwa nguvu Rachel alikwenda kufungua akiwa amejifunga shuka, alikutana uso na mkuu wa polisi. Lakini hakuonesha kushtuka cha kwanza alikunja uso na kumfokea.
“Ni ustaarabu gani kuja kuwaamsha watu usiku ndiyo mafunzo uliyojifunza katika chuo chenu cha polisi? Hivi mzee huna kazi za kufanya? Huwezi kupumzika na mkeo unafuatilia upumbavu huu? Hivi kwa nini lakini kila ninachokifanya mnanifuatilia. Nanyonya? Bado nasoma? Lakini kwa nini lakini?”
Rachel alimfokea mkuu wa polisi kama mtoto mdogo, mkuu wa polisi alipigwa na butwaa asijue afanye nini nguvu zilimuishia. Rachel aliwageukia polisi waliongozana na mkuu wa polisi waliokuwa na bunduki mkononi.
“Hivi nanyi hamna kazi za kufanya, ni matukio mangapi yametokea ya ujambazi hamjaenda mnakuja kwa watu wanaostarehe. Bila aibu watu mnakuja na bunduki kuna jambazi mbona kwenye majambazi mnakwenda baada ya masaa sita baada ya tukio?
“Sasa nasema hivi kama kuna mwanaume wa kweli aingine ndani amkamate mpenzi wangu nasema hivi, japokuwa mnaniona mdogo lakini chochote mtakacho kifanya tutafikishana mbali.
“ Ninyi si mnamuona baba ndiye kila kitu sasa mguseni mpenzi wangu nitakufa na mtu, nimechoka kufuatwa kama mkia na kiuno” Rachel alifoka huku machozi yakimtoka alijua ni baba yake tu ndiye aliye watuma mama yake asingefanya mjinga kama ule.
Wote waliokuja kumkatata hata wapelelezi wa mzee Mulisa waliosogea eneo la tukio kuchukua picha walibakia vinywa wazi. Rachel hakutaka kuendelea kuzungumza alirudi ndani na kufunga mlango kwa komeo huku akisema
“Mwenye nguvu avunje.”
Mkuu wa polisi alisimama kama dakika tano akitafakari maneno ya Rachel kisha aliwaeleza vijana wake.
“Twendeni zetu.”
Vijana wake waligeuka na kuondoka njiani kila mmoja alisema lake.
“Mzee mimi nilifikiri tunakuja kuvamia jambazi kumbe ni starehe za watu, ona tulivyo dhalilishwa, mzee vitu vingine fikiria kabla ya kufanya.”
Mkuu hakujibu kitu alijikuta akipandwa na hasira na kumpigia simu mzee Mulisa.
“Baada ya kumpigia simu mzee Mulisa alipokea na kuuliza.
“Halo mmefikia wapi?”
“Nasema hivi kuanzia leo usinitume upumbavu wako na mwanao.”
“Mkuu unadiriki kunitamkia hivyo?”
”Nimesema hivyo siwezi kudhalilishwa na mtoto yule mdogo wa kumzaa.”
“Ooh! Basi thamahani, lakini yule kijana mmemkamata?”
“Nasema hivi sitaki tena kusiki issue yeyote ya mwanao.”
Baada ya kusema vile alikata simu.

Nini kitaendelea?
 
Love Stori: Muhanga wa mapenzi
Sehemu: 13
Mtunzi: Ally Mbetu
SIMU: 0713646500......

ILIPOISHIA:
Mkuu hakujibu kitu alijikuta akipandwa na hasira na kumpigia simu mzee Mulisa.
“Baada ya kumpigia simu mzee Mulisa alipokea na kuuliza.
“Halo mmefikia wapi?”
“Nasema hivi kuanzia leo usinitume upumbavu wako na mwanao.”
“Mkuu unadiriki kunitamkia hivyo?”
”Nimesema hivyo siwezi kudhalilishwa na mtoto yule mdogo wa kumzaa.”
“Ooh! Basi thamahani, lakini yule kijana mmemkamata?”
“Nasema hivi sitaki tena kusiki issue yeyote ya mwanao.”
Baada ya kusema vile alikata simu.
SASA ENDELEA...
***
Baada ya mkuu wa polisi kuondoka Rachel alifunga mlango na kusimama nyuma ya mlango na kupumua pumzi ndefu akiwa ameuegemea mlango, kisha alitoka taratibu hadi kitandani ambako palikuwa patupu. Aliamini Athuman akijificha bafuni kwa woga wa kukamatwa.
Lakini hakumuona ilibidi amwite.
“Sweet upo wapi?”
Lakini hakukuwa na jibu alijiuliza Athuman atakwenda wapi au ameruka dirishani bado hakuamini kutokana na dirisha kuwa limefungwa kwa ndani. Alizidi kuita huku akimtoa hofu mpenzi wake.
“Sweetie hakuna tatizo upo wapi?”
Athuman alitoka uvunguni akiwa ametokwa na haja ndogo bila kujielewa, Rachel baada ya kumuona Athuman kwenye hali ile aliangua kicheko.
“Athuman mpenzi wangu ni uoga gani huo?”
“Rachel we sema tu, ungejua kipigo walichonipiga siku ile ya kwanza kukuta nyumbani kwangu asingesubutu kunicheka badala ya kunionea huruma. Wale watu wanapigia sifa utafikiri wanaua nyoka, basi tu nakupenda lakini kwa kipigo cha siku ile hata kukusogelea nisingekusolegea wacha leo tunalala kitanda kimoja.”
“Kwa taarifa yako leo nimewatolea uvivu sijui kama watatufuata tena mkuu wa polisi nimempa makavu anashindwa kumlaza mkewe anafuata kuharibu starehe za watu,” Rachel alisema kwa kujiamini.
“Nimekusikia lakini nilidhani watakupiga.”
“Waanzie wapi, kwa taarifa yako hakuna mtu wa kutugusa hata tukifanya kosa.”
“Mmh, sawa lakini baba yako akirudi si ataniua?”
“Hawezi, nitapambana naye mpaka atua ya mwisho.”
“Lakini kumbuka yule ni baba yako?”
”Athuman hebu tuachana na wajinga wale tule raha zetu,” Rachel alibadili mazungumzo.
Walizima taa yenye mwanga mkali na kuwasha yenye mwanga hafifu, Rachel alimvutia kifuani Athuman taratibu walilala pamoja.

***
Mzee Mulisa baada ya mkuu wa polisi kukata simu aliwapigia vijana wake kuwauliza nini kimetokea.
“Eti kuna nini, mbona mkuu wa polisi kanijibu maneno mazito?”
“Bosi weee acha tu, mwanao mkorofi sana kamtukana mtu mzima kama mtoto mdogo hata maneno ambayo hakutakiwa kuyasema kwa kweli kamdhalilisha sana.”
“Mmh!” mzee Mulisa aliguna.
“Kibaya zaidi kamtishia kazi yake na kumwambia kama atamkamata mpenzi wake watafikishana mbali.”
“Ni kweli kasema hivyo?”
“Ndiyo mzee.”
“Amekuoneni?”
“Hapana, kwa nini mzee tusimfanyie huyo kijana kwani kuna nini kumpoteza katika ramani ya dunia?”
“Nooo, waacheni wala usimgumse namjua vizuri mwanangu anaweza kuwaweka katika wakati mgumu. Huyu mtoto sasa ameshindikana, sasa fanye hivi ondokeni hapo mara moja kabla hajawaona,” Mzee Mulisa aliwataka vijana aliowatuma waondoke mara moja eneo lile.
“Kwa nini mzee tuondoke tutaweza kufanya mambo kitaalamu bila yeye kujua,” vijana walitoa ushauri.
“Hata kama mtafanya kitaalamu kiasi gani lazima atajua ni mkuu wa polisi anaweza kwenda mbele zaidi na kuwafanya muwe kwenye wakati mgumu.”
“Sawa mzee kwa vile tumeisha lipia tutaondoka kesho asubuhi.”
“Nimesema ondokeni muda huu sitaki kubishana na mbwa,” mzee Mulisa alifoka. Ilibidi watu aliowatuma waondoke usiku ule ule japokuwa muda ulikuwa umekwenda sana.
********
Rachel alirudi nyumbani kwao siku ya pili majira ya saa tano asubuhi, alipoingia alimkuta mama yake amekaa sebuleni, alipita na kumsalimia kisha alielekea chumbani kwake. Alipopiga hatua mbili mama yake alimwita.
“Rachel.”
“Yes mamy.”
“Unatoka wapi?”
“Tulikwenda Bagamoyo rafiki zangu tukalala hukohuko kutokana na muda kwenda.”
“Rachel usinifanye mtoto mdogo, niambie ukweli jana ulikuwa wapi?”
“Bagamoyo mama.”
“Ulikuwa unafanya nini?”
“Nilikuwa kwenye pati na wanafunzi wenzangu,” Rachel alikuwa akidanganya kitoto.
“Joy alikuwepo?”
“Hakuwepo.”
“Pati ile anaijua?”
“Haijui.”
“Unajua habari zako nimezipata toka kwa baba yako kuwa ulikuwa na mwanaume Bagamoyo.”
“Yule ni rafiki yangu ambaye baadaye atakuwa mume wangu,” Rachel alijibu kwa kujiamini.
“Rachel unajua unazungumza na nini?”
“Na mama yangu mzazi.”
“Kwa nini sasa unakosa adabu?”
“Mama sio kukosa adabu bali kukueleza ukweli ulivyo au ulitaka nikudanganye?”
“Si unajua baba yako hataki tabia hizo?”
“Ni kweli kwa vile nimemaliza mtihani nimechagua kuolewa badala ya kuendelea kusoma.”
“Rachel baba yako atakuua akisikia upuuzi huo,” mama yake alimtaadhalisha.
“Aniue kwa lipi, la kukataa kusoma na kuolewa si ni yeye alisema mtu akitimiza miaka 18 ana haki ya kujichagulia maisha kwa vile ana umri wa mtu mzima mwenye kutambua mazuri na mabaya?” Rachel alitetea hoja yake.
“Yote haya niliyajua, baba yako aliyataka kwa kukudekeza kama yai na kutaka maisha ya kizungu, mimi tena simo mtajuana na baba yako,” mama Rachel alijitoa.
Rachel hakusubiri mama yake azungumze mengine aligeuka na kuelekea chumbani kwake akimuacha mama yake kashika tama.

Nini kitaendelea?
 
Love Stori: Muhanga wa mapenzi
Sehemu: 14
Mtunzi: Ally Mbetu
SIMU: 0713646500......

ILIPOISHIA:
“Rachel baba yako atakuua akisikia upuuzi huo,” mama yake alimtaadhalisha.
“Aniue kwa lipi, la kukataa kusoma na kuolewa si ni yeye alisema mtu akitimiza miaka 18 ana haki ya kujichagulia maisha kwa vile ana umri wa mtu mzima mwenye kutambua mazuri na mabaya?” Rachel alitetea hoja yake.
“Yote haya niliyajua, baba yako aliyataka kwa kukudekeza kama yai na kutaka maisha ya kizungu, mimi tena simo mtajuana na baba yako,” mama Rachel alijitoa.
Rachel hakusubiri mama yake azungumze mengine aligeuka na kuelekea chumbani kwake akimuacha mama yake kashika tama.
SASA ENDELEA...

Siku zote mzee Mulisa baba yake Rachel alikuwa akitaka mwanaye aishi maisha ya kizungu hata kuvaa nguo za nusu uchi ambazo mama yake alimkanya lakini baba yake alimkataza mkewe kuingilia uhuru wa mtoto wa vile ameisha kuwa mtu mzima. Maneno yale yalimpa kichwa Rachel kufanya mambo yake bila mama yake kumuingilia huku baba yake akichelelea na kumuona mtoto wao yupo sawa.
Hali ile ilimweka mama Rachel kwenye wakati mguymu wa kumuonya mtoto wao kutokana na kupewa uhuru na baba yake. Siku zote baba Rachel alipokuwa akitoka Rachel alifanya mambo yake bila woga kwa kujua mama yake hawezi kumwambia chochote.
Mzee Mulisa alikuwa akimpenda sana mwanaye ambaye alikuwa wa pekee kuhakikisha utajiri alionao aishi nusu ya maisha ya peponi.
****

Baada ya wiki mbili mzee Mulisa alirudi toka katika safari zake, bahati mbaya hakumkuta Rachel alikuwa Mikumi na Athuman katika mbuga za wanyama. Vijana wake walimjulisha yupo wapi, kwa hasira baada ya kutua alikodi ndege hadi mbuga ya Mikumi alipofika alikwenda hadi mapokezi na kumuulizia Rachel.
Alielekezwa yupo mbugani anaangalia wanyama na mpenzi wake, hakuwa na haraka alisubiri kwa muda wa masaa mnne akiwa amefura kama kaumuliwa na amila.
Majira ya saa kumi na mbili walirudi kutoka mbugani, baada ya kuteremka kwenye gari walishikana kimahaba kielekea hotelini walipopanga kwa mapumziko ya siku mbili.
Mzee Mulisa aliwaona wakiteremka kwenye gari wakiwa wamekumbatiana, hasira zilimpanda alitamani akamrukie Athuman na kumtafuna mbichi. Walipokaribia mlango wa kuingia hotelini Athuman alikuwa wa kwanza kumwona mzee Mulisa alitaka kutimua mbio lakini alishindwa kujitoa kwenye mikono yaRachel aliyekuwa amemkumbatia kwa nguvu kiunoni akiwa amemlalia kifuani.
Mzee Mulisa nguvu zilimuishia na kubakia akitumbua macho, kitendo cha Athuman miguu yake kuwa mizito na kushindwa kutembea kilimshtua Rachel na kutaka kujua kulikoni kuwa katika hali ile.
“Athuman vipi mbona hutembei umechoka nini?” alimuuliza huku akimtazama usoni.
Athuman alimjibu kwa macho kumuonesha alipokuwa amejaa tele mzee Mulisa kama Malaika mtoa roho. Rachel alishtuka kumuona baba yake kitu ambacho hakukitegemea.
Alimuachia Athuman na kumkimbia baba yake na kwenda kumrukia.
“Ooh, Dady siamini hii ni surprise kwangu, umerudi lini Dady?”
Mzee Mulisa alibakia kimya akikapua macho kama kafumaniwa akifanya mapenzi na mnyama. Hali ile ilimshtua Rachel kutokana na hali aliyoonesha baba yake.
Wakati huo Athuman haja ndogo na kubwa zilitaka kutoka kwa pamoja kwa kuamini kile kilikuwa kiama chake kama amekutwa live akiwa na mtoto wa tajiri aliyetishia maisha yake. Watu alioongozana nao walimfanya awe kwenye hali ngumu kutokana na kuwa na miili mikubwa ya mazoezi.
Rachel alijua Athuman yupo kwenye hali gani pia alijua hata baba yake alikuja kule baada ya kusikia yupo na Athuman aliamini kama atakaa kimya atakuwa katika wakati mgumu.
Alijitoa muhanga kwa baba yake ili kujionesha alichokifanya akikuwa siri au kumvizia baba yake asafiri.
“Sweetie njoo uonane na baba yangu mzazi.”
Athuman alibakia bado amesimama kama amebandikwa gundi kwa woga wa kumuogopa mzee Mulisa baba yake Rachel. Mzee Mulisa bila kusema neno alimshika mkono mwanaye na kuelekea kwenye ndege ili waondoke.
“Baba na rafiki yangu?” Rachel alimuuliza baba yake.
Baba yake hakumjibu alimshika mkono hadi ndege ilipopakiwa na kumuingiza kisha walinzi wake na ndege kuondolewa kurudi Dar wakiumuacha Athuman peke yake ambaye aliona ajabu baba Rachel kuondoka bila kumfanya chochote.
Kama kungekuwa na sehemu ya kuruka toka kwenye ndege basi Rachel angeruka kurudi kwa Athuman, kitendo kila kilimuudhi sana na kuanza kulia safari nzima.
Walipofika walielekea nyumbani mara moja na kutolewa amri Rachel hatakiwi kutoka nje ya nyumbani kwao.
Athuman alirudi hadi hotelini akiwa hajiamini kuachwa salama bila hata kupigwa kibao aliona maajabu. Siku ile alilala pale na siku ya pili alirudi jijini Dar huku akijiuliza nini hatima ya maisha yake na mapenzi yake na Rachel.
Wakati huo mpenzi wake Rachel aliwekewa mlinzi kwa kutembea naye sehemu zote ambazo atakazo elekezwa, kitendo kile kilimuudhi sana Rachel na kupanga mpango kabambe wa kukutana na Athuman.
Mzee Mulisa alipanga mpango wa kumpoteza Athuman bila mtu yeyote kujua kifo chake kiwe cha kawaida, aliwaita vijana wake na kuwaeleza watafute njia ya kumpoteza Athuman bila mtu yeyote kutilia mashaka kifo chake.
Rachel kama kawaida yake kila siku usiku alitoroka na kwenda kwa Athuman na kula raha zao mpaka usiku wa manane urudi kwao. Mtindo ule uliendelea bila wazazi wake kujua.
Vijana wa mzee Mulisa walipanga kumchukua Athuman usiku wa manane na kwenda kumuulia pembeni ya bahari ili ionekane kama amekufa maji. Majira ya saa sita usiku wakiwa wapo karibu ya nyumba anayoishi Athuman tayari kuvamia. Waliona teksi ikisimama mbele ya nyumba ya Athuman.
Walipoangalia vizuri hawakuamini macho yao kumuona mtoto wa bosi wao Rachel akiteremka kwenye teksi ile baada ya kulipa nauli gari iliondoka na yeye kuingia mule ndani, kila mmoja alimtazama mwenzake. Ilibidi mmoja aulize.
“Jamani yule si mtoto wa bosi?”

Nini kitaendelea?
 
Love Stori: Muhanga wa mapenzi
Sehemu: 15
Mtunzi: Ally Mbetu
SIMU: 0713646500......
ILIPOISHIA:
Walipoangalia vizuri hawakuamini macho yao kumuona mtoto wa bosi wao Rachel akiteremka kwenye teksi ile baada ya kulipa nauli gari iliondoka na yeye kuingia mule ndani, kila mmoja alimtazama mwenzake. Ilibidi mmoja aulize.
“Jamani yule si mtoto wa bosi?”
SASA ENDELEA...

“Ndie yeye.”
“Sasa jamani hii si picha ya Kihindi, bosi si alituhakikishia amemwekea ulinzi mkali?”
“Hata mimi nashangaa.”
“Sasa tutafanyaje kazi? Si unajua akishuhudia tunamteka anaweza kuharibu kila kitu.”
“Joe hukuwepo Mikumi yule mtoto balaa ni mkorofi sana, kibaya baba yake anampenda sana. Si tulikwenda mbuga ya Mikumi kumfuata mshikaji, kabla ya kuwaona mzee aliapa kummwaga ubongo jamaa lakini alipotokea na binti yake aliishiwa nguvu kwa binti kumtambulisha jamaa kwa mzee.”
“Patamu hapo, ikawaje?” Jamaa walijikuta wakitaka stori kwanza badala ya kufanya kazi iliyo wapeleka.
“Mzee alimshika mkono binti yake na kumpeleka kwenye ndege na kuondoka naye.”
“Na jamaa?”
“Tulimuacha hukohuko.”
“Hayo nimeyasikia, sasa ya hapa itakuwaje?”
“Hapa hakuna ujanja ni kumjulisha mnene tujue tufanye nini si unajua mnene anataka tumalize kazi hii kabla ya kuondoka tuwe tumempoteza huyo kinyago kwenye sura ya dunia.”
“Na kweli unajua jibu atakalotoa litatuisaidia tufanye nini, si unajua hataki binti yake tumguse.”
Waliamua kumpigia simu bosi wao mzee Mulisa kumjulisha Rachel ameonekana akiingia kwa Athuman. Mzee Mulisa aliyekuwa usingizini na kuamshwa na simu yake, hakuamini alichosikia kabla ya yote alinyanyuka kitandani kwake na kwenda chumba cha mwanaye ili ajue kuna ukweli gani na aliyoambiwa na vijana wake.
Mlango ulikuwa umefungwa kwa ndani, alijaribu kugonga kwa nguvu hakukuwa na jibu lolote toka ndani. Alitoka hadi nje na kumuomba mlinzi apande juu na kuingilia dirishani apate uhakika kama kweli Rachel hayumo ndani.
Mlinzi alirudisha jibu kuwa ndani hakuna mtu, aliufungua mlango kwa ndani kumfanya mzee Mulisa kuweza kuingia chumbani kwa Rachel, naye alizunguka kila kona hakumuona. Alikubaliana na vijana wake huenda kweli Rachel yupo kwa Athuman.
Alirudi hadi chumbani kwake na kumuasha mkewe ambaye alishangaa kusikia Rachel hayupo.
“Jamani mbona huyu mtoto ana balaa,” mama Rachel alishangaa.
“Yaani huyu kijana sijui nimfanye nini?” mzee Mulisa aisema huku akibadili nguo.
Usiku ule ule waliondoka pamoja kuelekea anapokaa Athuman muda ulikuwa unakimbilia saa tisa za usiku. Waliongozana hadi nyumba aliyokuwa akikaa Athuman. Akiwa na vijana wake wa kazi waligonga mlango.
Rachel kabla ya kuitika alichungulia na kumuona baba na mama yake wakiwa na mmoja wa vijana ambao walikuja kwa kazi moja ya kumshikisha adabu Athuman. Kwanza alishtuka kwa kusema kwa sauti ya woga.
“Ha! Baba?”
“Mungu wangu leo nimekwisha.” Athuman alisema kwa hofu.
“Usihofu kazi yote niachie mimi, nitapambana nalo mpaka kieleweke,” Rachel alimtoa hofu mpenzi wake.
“Sasa itakuwaje?”
“Nawafungulia mlango,” Rachel alisema.
“Usifungue, wataniulia ndani,” Athuman alijitetea kwa kumuhofia mzee Mulisa.
“Haguswi mtu leo,” bado Rachel alijiweka mbele.
Baada ya kusema vile Rachel alifungua mlango na kukutana uso kwa uso, mama yake alishtuka kumuona mwanaye akitoka akiwa amejifunga upande wa kanga.
“Ha! Rachel?”
”Ni mimi mama karibuni,” Rachel alisema bila wasi.
“Haiwezekani lazima nimmwage ubongo mwanaharamu huyu.”
Mzee Mulisa alisema huku akitoa bastora mkononi na kutaka kuingia ndani kwa nguvu.
“Kabla ya kumuua mpenzi wangu niueni kwanza mimi,” Rachel alisimama mbele ya baba yake kumkinga Athuman.
“Mume wangu punguza hasira kama hasara tumeoshaipata, na siamini kama Rachel atasoma, kwa tukio la leo inaonesha kabisa mtoto wetu kakubuhu zaidi ya hapo ni kunitafutia matatizo makubwa.
Kwa ushauri wangu kama imefikia hatua ya kutoroka usiku wa manane hatuwezi kumdhibiti tena tumkubaliane na akitakacho,” mama Rachel alimwambia mumewe.
“Ina maana tumuoze kwa maskini huyu?” Mzee Mulisa alisema kwa hasira.
“Eeh, ndiyo mwanao kampenda, nina imani nyuma yao kuna matukio mengi ili kuyafunika na kuibariki ndoa yao, tukiyaacha yatatuchafua.”
Hakukuwa na jinsi mzee Mulisa ilibidi awe mpole kutokana na maelezo ya mke wake, walimchukua Rachel bila kufanya lolote na kurudi naye nyumbani kwao. Siku ya pili Rachel aliwekwa chini na wazazi wake na kukubalia kumtambua Athuman kama mkwe wao na kupanga siku ya kuja kutambuliwa na familia ya mzee Mulisa. Rachel alifurahi baada ya kuona ndoto yake imekuwa kweli.
***
Siku ya pili mzee Mulisa alifika nyumbani kwa Athuman na kumkuta ndio anajiandaa kutoka, hakuwa na wasiwasi tena baada ya kuhakikishiwa usalama wake kwa kuhurusiwa kumuoa Rachel.
“Karibuni,” Athumani alimkaribisha mzee Mulisa.
“Asante.”
“Shikamoo baba.”
“Marahaba za hapa?”
”Nzuri tu, Rachel hajambo?”
“Naimani hajambo.”
“Sijui baba mnatumia kinywaji gani?” Athuman alimuuliza mzee Mulisa.
“Asante tumetoka kunywa sasa hivi.”
“Ndio baba, naona asubuhi asubuhi.”
“Kuna kitu kimoja nataka kuzungumza na wewe.”
“Kitu gani hicho?”
“Kuhusu Rachel.”
“Amefanya nini?”
“Ni hivi kijana unajua nina malengo makubwa sana kwa binti yangu hasa katika elimu, sio kwamba nataka kuingilia mapenzi yenu bali nilikuwa nataka muda kidogo ili niweze kumsomesha kisha hapo ruksa kufunga naye ndoa nami nitaghalamikia kila kitu.”
“Kwa hilo baba, mimi sina pingamizi,” Athuman hakuwa na kipingamizi.
“Sasa nilikuwa naomba msaada wako mmoja na tukikubaliana sasa hivi nitakupa kiasi chochote cha pesa ukitakacho cha kuanzia nitakupa milioni 50 ukitaka zaidi nitakupa kwa vile fedha kwangu si tatizo.”
“Msaada gani huo baba?”
“Nataka uachane na Rachel kwa wewe kumkataa, ukifanikiwa kulivunja nitakuongezea ishirini zingine zifike milioni 70.“
Baada ya kusema vile alimtuma kijana mmoja kwenye gari lake na kurudi na pesa hizo, baada ya kupewa mzee Mulisa alimkabidhi Athuman na kumweleza.
“Nategemea msaada wako.”
Athuman hakusema kitu, baada ya kuzitoa milioni 50 mzee Mulisa aligeuka na kuondoka akimuacha Athuman amepigwa butwaa

Nini kitaendelea?
 
Love Stori: Muhanga wa mapenzi
Sehemu: 16
Mtunzi: Ally Mbetu
SIMU: 0713646500......

ILIPOISHIA:
“Nataka uachane na Rachel kwa wewe kumkataa, ukifanikiwa kulivunja nitakuongezea ishirini zingine zifike milioni 70.“
Baada ya kusema vile alimtuma kijana mmoja kwenye gari lake na kurudi na pesa hizo, baada ya kupewa mzee Mulisa alimkabidhi Athuman na kumweleza.
“Nategemea msaada wako.”
Athuman hakusema kitu, baada ya kuzitoa milioni 50 mzee Mulisa aligeuka na kuondoka akimuacha Athuman amepigwa butwaa.
SASA ENDELEA...
Athuman alijawa na mawazo mengi juu ya taarifa zile ambazo hakuzitegemea alijiuliza wazazi wa Rachel walikuwa na maana gani kufanya vile. Alijiuliza kama atakubali kuvunja uchumba na Rachel ambaye alijitoa kwake na kukubali kila kitu kwa wazazi wake ikiwa pamoja na kuwavunjia adabu.
Alijiuliza tena kuhusiana na pesa alizopewa milioni 50 kwa ajili ya kuvunja uchumba wake na Rachel ili aendelee kusoma. Aliamini kabisa Rachel asingesoma kama angemkataa zaidi ya kufanya jambo zito la kunywa sumu.
Alijua kabisa kama Rachel atajiua kwa ajili yake uhasama utakuwa mkubwa hata mzee Mulisa kumuua kwa risasi ili kulipa kisasi cha kifo cha mwanaye. Pia kukaidi amri ya mzee Mulisa ingemtia matatani hata kumsababishia kifo.
Kila alilolifikiria kwake lilikuwa zito aliamini wazo lile bora alifikishe kwa mama Rachel amsikilize na yeye anasemaje.
****
Siku ya pili alikwenda hadi nyumbani kwao Rachel bahari nzuri alimkuta mama peke yake, Rachel alifurahi kumuona kwao alinirukia na kunipiga mabusu mbele ya mama yake bila woga kuonesha jinsi gani mtoto wa kike alivyopagawa kwa Athuman.
“Karibu baba,” mama Rachel alimkaribisha Athuman kwa heshima zote.
“Asante, shikamoo mama za hapa?”
“Nzuri tu baba, Rachel mletee kinywaji mgeni.”
Rachel aliondoka na kufuata kinywaji bila kumuuliza mgeni ilibidi mama Rachel amuulize mwanaye.
“Rachel mbona umeondoka bila kumuuliza mgeni anatumia kinywaji gani?”
“Mama naye mtu na chake, nisipojua mimi nani mwingine atajua.”
“Haya wapendanao.”
Rachel alijibu huku akielekea kwenye friza, mama yake alitabasamu na kumgeukia Athuman na kumtania.
“Baba umemlisha nini mwanangu haoni asikii juu yako?”
“Nimlishe nini basi nyota zimeoana.”
“Mmh! Sawa.”
Baada ya muda Rachel alileta sinia la vinywaji iliyokuwa na glasi tatu, zilizojaa juice.
“Karibu mpenzi,” alipiga magoti mbele ya Athuman na kumfanya mama yake achekelee moyoni kwa kitendo kile cha heshima aliyopewa Athuman. Kwa mama yake alishangaa hakuwahi kukifanya kile hata kwa baba yake mzazi.
“Mmh! Mwanangu adabu ya woga hiyo.”
“Mamaa! Mume lazima aheshimiwe.”
“Mbona, baba yako hujamfanyia hivi?”
“Mama kwa Mungu anatambulika mume si baba, ndio maana walisema mwanamke ataachana na wazazi wake na kuambatana na mumewe ambaye ndiye wataungana na kuwa mwili mmoja,” Rachel alishusha mistali ya Biblia.
“Mmh! Sikuwezi.”
Baada ya kumgawia kila mmoja kinywaji chake Rachel alikaa pembeni ya Athuman na kuanza kumnywesha juisi.
“Rachel, tulia basi nizungumze na mgeni.”
“Sawa mama mkiona hivi basi muharakishe harusi mume mtamu mama.”
“Haya basi mpe nafasi nizungumze naye kisha nitakuacheni mmalize hamu zenu, mhu baba”
Athuman kabla ya kuzungumza alishusha pumzi na kuonekana kuna jambo linamtatiza, kitu alichokigundua mama Rachel.
“Baba kuna kitu najua unataka kuzungumza au cha wawili?”
“Ni kweli mama.”
“Athuman ni kitu gani mimi sitakiwi kukijua?” Rachel aliingilia kati mazungumzo yale.
“Hapana mpenzi kuna kitu nataka kuzungumza na mama kisha nitazungumza na wewe.”
“Sawa, mimi sifai” Rachel alisema huku akitaka kulia.
“Hapana Rachel, hebu muache mwenzio azungumze kisha nawe utaelezwa.”
Rachel aliondoka kwa shingo upande.
Baada ya kuondoka mama Rachel alimgeukia Athuman na kumuuliza kilichompeleka pale.
“Mhu, baba ulikuwa unasemaje?”
Baada ya kuvuta ujasiri alisema kwa sauti ya upole jinsi baba Rachel mzee Mulisa alivyompelekea milioni 50 ili aachane na Rachel.
“Mama, mimi naweza kufanya hivyo, si uamuzi wa kumwambia mimi na wewe basi, lakini mnajua madhara yake?”
“Mmh! Baba mimi ndio nasikia kwako, unayosema ni kweli?”
“Kweli kabisa mama.”
“Na hizo pesa zipo?”
“Zipo toka jana nilipopewa sijazigusa zimo ndani.”
“Mmh! Sasa shida yake nini?”
“Niachane na Rachel.”
“Mbona mume wangu ana mazito, hajui kama siku utakayo mtamkia Rachel basi ujue na uhai wake siku hiyo ndiyo utagota. Haya ninayo yaona kwa Rachel jinsi alivyochanganyikiwa kwako umwambie mwanangu humtaki si ndio kumpoteza.
Lakini kwa nini mume wangu ananila kisogo yote haya yamefika hapa kwa ajili yake bado anafanya kitu kujua.
“Baba nakuomba usimtamkie mwanangu neno hilo hata siku moja nipo radhi kukupa zaidi ya hizo kuhakikisha maisha ya mwanangu yanakuwa ya furaha.”
“Mama, pia naogopa pindi nitakapo kaidi amri ya mzee maisha yangu yatakuwa hatiani kwani nina imani hapendi mimi kuwa na Rachel. Nakuapia mama kama sio vitisho vya Rachel ningekwisha achana naye lakini amenionesha mapenzi ya kweli na kujitoa muhanga kwa ajili yangu leo hii nimtose, hata kidogo siwezi heri nife kuliko kumpoteza Rachel.”
“Ni kweli mwanangu siku zote sisi wanawake tuna roho kama ya kuku hatuwezi kuvumilia, uamuzi wetu siku zote ni kujiua kwani huamini ndio njia ya kutatua matatizo.”
“Basi mama huo ndio mtihani ulio mbele yangu, ningekuwa na tamaa mbona wala nisingekuja kuwaeleza ningechukua hela na kumueleza Rachel mimi na yeye basi angenilazimisha? Lakini naheshimu mapenzi yake kwangu pia uhai wake ni muhimu kuliko milioni 50.”
“Ni kweli baba, umeonesha jinsi gani ulivyoiva kiakili unamshinda hata baba yenu, milioni 50 zinatafutwa na kupatikana lakini si uhai wa mwanangu.”
“Sasa mama ulikuwa unanishauri nini?”
“Mwanangu nimekusikia kazi hiyo niachie mimi, hizo milioni 50 usizirudishe ni asante yako kwa moyo wako wa ujasiri angekuwa mwengine asingefanya haya. Ningempoteza mwanangu hivihivi, narudia nasema asante nenda kwa amani usihofu kitu chochote nakuahidi mimi kama mama yake Rachel lazima utamuoa kwa dini yeyote.”
Baada ya mazungumzo aliitwa Rachel ili aagane na Athuman, Rachel alitokea akiwa amevimba macho kwa kulia kitu kilichomshtua kila mmoja.
“Rachel mpenzi nini tena?”
“Mama ni jinsi gani wazazi wangu msivyo nipenda mnanunua uhai wangu kwa milioni 50, mama kweli kabisa mimi sina thamani kwenu, mnajifanya mnanipenda kumbe waongo...Siamini ...siamini,” Rachel alisema huku akilia kuonesha aliyasikia mazungumzo yale.

Nini kitaendelea?
 
Love Stori: Muhanga wa mapenzi
Sehemu: 17
Mtunzi: Ally Mbetu
SIMU: 0713646500......

ILIPOISHIA:
Baada ya mazungumzo aliitwa Rachel ili aagane na Athuman, Rachel alitokea akiwa amevimba macho kwa kulia kitu kilichomshtua kila mmoja.
“Rachel mpenzi nini tena?”
“Mama ni jinsi gani wazazi wangu msivyo nipenda mnanunua uhai wangu kwa milioni 50, mama kweli kabisa mimi sina thamani kwenu, mnajifanya mnanipenda kumbe waongo...Siamini ...siamini,” Rachel alisema huku akilia kuonesha aliyasikia mazungumzo yale.
SASA ENDELEA...

“Mwanangu hata mimi sipo tayari kukupoteza,” mama yake alijitetea.
“Athuman...Athuman mpenzi, leo ndio nimeamini kweli unanipenda na kujitoa muhanga kwa maisha yangu. Asante sana Athuman Mungu atakulipa hata nikifa nitendelea kukupenda na kuamini kweli wewe ulikuwa na mapenzi ya kweli na mimi.”
“Rachel nathamini upendo wako nilijiapiza moyo wangu toka nilipojua mapenzi yako kwangu ni ya kweli na kujitoa muhanga kwa ajili yangu. Nakuahidi kwa mara nyingine mbele ya mama, ni kifo pekee ndicho kitakacho tutenganisha si fitina za watu.”
Rachel alijitupa kifuani kwa Athuman kitu kilichomfanya mama Rachel kuwaacha wamalize hamu zao kwa upana zaidi. Baada ya kuondoka Rachel aliendelea kumshukuru Athuman.
“Athuman wewe ni mume niliyeshushiwa toka kwa Mungu, hakuna mwanaume mwingine atakaye pata nafasi moyoni mwangu. Kwa ulichokifanya juu yangu mimi nitafanya mara mbili yako. Asante Athuman nimeamini nilipoangukia sikukosea sikugusa chini,” Rachel aliendelea kumshukuru mpenzi wake.
“Rachel wewe ni mwanamke wa ajabu upendo wako umenifunduisha vitu vingi, upendo wako umenijaza ujasiri na kuweza kukabiliana na chochote kijacho mbele yangu. Wewe ni msichana wa ajabu wenye msimamo na mwenye kutetea hoja zako. Nakupenda sana Rachel.”
“Asante, hata mimi nakupenda, leo iwe isiwe lazima nije nilale kwako.”
Baada ya kupozana mioyo Athuman aliaga na kuondoka.
***
Mama Rachel alimsubiri mumewe kwa hamu kubwa ili amweleze sababu ya kutaka kusababisha mauti ya mtoto wao. Muda ulipotimu mumewe alirejea nyumbani kama kawaida ajabu aliikuta hali si ya kawaida. Mkewe hakuwa na furaha kama kawaida Rachel naye alionekana kama mgonjwa macho yalikuwa yamemvimba kwa kulia.
“Jamani kuna usalama, eti bebiii?” Alimgeukia mwanaye aliyekuwa amejilaza kwenye kochi, Rachel hakumjibu kitu alimuangalia bila kumsemesha wala kumjibu.
“Eti mke wangu, kuna nini?” Wazo lake lililenga huenda Athuman amemuacha Rachel, moyoni aliamini alichotaka kukifanya kimefanikiwa.
“Mmh, kawaida tu,” mkewe alijibu bila kuonesha uchangamfu.
“Lakini hapa kuna kitu si bure macho ya Rachel hayaoneshi dalili nzuri.”
“Si ndiyo uliyoyataka,” mama Rachel alijibu.
“Lakini mimi nafikiri kilichotokea ni kitu cha kawaida kinachotakiwa ni kwa Rachel kujikita kwenye elimu, nami nakuahidi mwanangu kukupatia kila utakacho.”
Mzee Mulisa alizungumza bila kuelewa alichokuwa akikizungumza, Rachel ambaye alikuiwa amejaa jazba alisema kwa hasira.
“Baba unajifanya unanipenda kumbe muongo mzandiki, unanunua uhai wangu kwa milioni 50?”
Kauli ile ilimshtua mzee Mulisa kwani hakutegemea Athuman kutoa siri ile kutokana na kumpa kiasi kikubwa cha pesa. Kabla ya kujibu mkewe aliongezea juu.
“Mume wangu kwa nini umefanya kitendo cha kinyama cha kutaka kuvunja mapenzi ya mwanao, tuliongea nini na umefanya nini? Hivi furaha yako umkute mwanao amekauka au una mpango wa kumla nyama?”
“Sivyo hivyo mke wangu bado siamini kama yule kijana ni saizi ya mwenetu, ni aibu kumuoza mtoto wetu atatupa nini? Nia yangu ni kuhakikisha mtoto wetu anaachana na yule kijana kisha anarudi shule.”
“Mimi na wewe tulizungumza nini tulipomkuta Rachel kwa yule kijana, tulikubaliana kwa vile yule kijana hana uwezo mkubwa lakini mtoto wetu kampenda tumwezeshe ili aweze kuishi na mtoto wetu bila matatizo.”
“Ni kweli mke wangu, lakini bado nafsi yangu haikubali, yule kijana hawezi kumuoa mwanangu.”
“Haya sasa hutaki mwanao kesha mpenda!”
“Kwanza habari hizi umezipata wapi?’
”Uliyemueleza, japokuwa kijana mdogo ameangalia mbali na kujua madhara ya kuvunja mahusiano yake na Rachel yangekuwa na madhara makubwa kuliko milioni 50 zako.”
“Mmh!” aliguna na kukosa neno la kusema.
“Kweli mume wangu una akili za kushikizwa kama umeweza kumpa milioni 50 na kumuahidi milioni 20 zaidi ili ziwe sabini kwa nini usimpe milioni mia moja afanye kazi yenye kuonekana ili aweze kumtunza mwanao? Lakini unatumia pesa nyingi kiasi hicho kutaka kuutoa uhai wa mwanao.”
“Mama wala baba asisumbuke si ananiona nimekuwa kero kwake, wala asitumie pesa zote hizo kununua uhai wangu. Basi wacha mimi ninywe sumu ya mia mbili ili nimpunguzie mzigo huenda kuwa kwangu humu ndani ni kero kwake,” Rachel aliingia kati mazumgumzo ya wazazi wake.
“Hapana Rachel nipo tayari kufanya chochote ili uolewe na Athuman, naomba mnisamehe kwa yote niliyotenda. Nimeamini Athuman anakupenda mapenzi ya dhati,” Mzee Mulisa aliomba radhi.
“Baba siwezi kukusamehe kwa vile ulichofanya ulifanya kwa siri kama Athuman asingekuwa na upendo wa kweli wa kurudisha milioni 50. Kama asingekuwa na mapenzi ya dhati kwangu ningeachwa kama kina la ndege kwenye upepo ukali na kufa kifo kibaya,” Rachel alimwambia baba yake huku akilia.
“Ni kweli nimefanya kosa mwanangu nisamehe sana mwanangu na mke wangu, nimekosa jamani, japo mi mkubwa lakini hutenda makosa na kuhitahi msamaha, aliye sahihi ni Mungu pekee.”
“Mimi nikusamehe kwa lipi nakuona upo sawa kwa kila ulilofanya, kwa vile umeweza kutoa mamilioni ya pesa ili kuhakikisha unaiua furaha yangu. Bado siamini kama wewe mwenyewe ulikubali kisha umenigeuka ..siamini ..siamini,” Rachel alizungumza kwa jazba huku akiendeleza kilio.
Mzee Mulisa aliona maji yamefuka shingoni na nguo imemvuka pabaya mbele za watu hakuwa na budi kuchutama kwa mara ya kwanza alimpigia magoti mtoto wake kumuomba radhi.
“Rachel mwanangu nilifanya yote yale si kwa nia mbaya bali kuyaokoa maisha yako, Athuman ni kijana maskini huwezi kuyatengeneza maisha yako.”
“Aaah! Unajua unanishangaza sana kama ulijua maskini na umeweza kumpa milioni 50 na ishirini ulitaka kumuongezea ili avunje penzi lake kwangu. Huoni huo ni utajiri tosha kwa nini hukutupa hata milioni 500 ili tuweze kuendeleza maisha yetu bila kukusumbua?” Rachel alimuuliza baba yake.

Nini kitaendelea?
 
Love Stori: Muhanga wa mapenzi
Sehemu: 18
Mtunzi: Ally Mbetu
SIMU: 0713646500......

ILIPOISHIA:
“Rachel mwanangu nilifanya yote yale si kwa nia mbaya bali kuyaokoa maisha yako, Athuman ni kijana maskini huwezi kuyatengeneza maisha yako.”
“Aaah! Unajua unanishangaza sana kama ulijua maskini na umeweza kumpa milioni 50 na ishirini ulitaka kumuongezea ili avunje penzi lake kwangu. Huoni huo ni utajiri tosha kwa nini hukutupa hata milioni 500 ili tuweze kuendeleza maisha yetu bila kukusumbua?” Rachel alimuuliza baba yake.
SASA ENDELEA...

“Kwa kweli mwanangu sikuwa na wazo hilo, ili kukuonesha nakupenda na vilevile nakuthamini, nakuahidi kukusimamia kwa kila kitu juu ya ndoa yako na Athuman.”
“Pamoja na kusema yote hayo bado sikuamini, nakuona unanipaka matope kwa mgongo wa chupa,” bado Rachel hakutaka kumuamini wala kumsamehe baba yake kwa kuamini kutoa milioni sabini ni dhahili alikuwa amedhamilia.”
“Nifanye nini ili mwanangu uamini nitafanya unacho kifikiria?”
“Chochote utakacho nifanyia siwezi kukuamini na siwezi kukuamini kamwe,” Rachel alimpa wakati mgumu baba yake ambaye kwa mara ya kwanza alijiona kiumbe mdogo asiyejaa mkononi kwa mwanaye.
“Mama Rachel mke wangu, naomba basi umueleze mwanao ili aniamini kama sitafanya upuuzi kama huu tena.”
“Mume wangu kwa kweli mpaka sasa sijapata jibu kwa kile ulichokifanya cha kutuzunguka kumbe una ajenda nzito, hivi unajua vizuri jinsi Rachel anavyo mpenda Athuman halafu leo uwaachanishe. Mume wangu kilio ulichotaka kukiiingiza ndani ungekinyamazisha kwa shilingi ngapi kama ulitaka kukiandaa kifo cha mwanao kwa milinini 70?”
“Mke wangu jamani mimi ndiye kiumbe cha kwanza kufanya makosa ambayo sisitahili kusamehewa? Hata mimi japo kichwa cha familia nahitaji kusamehewa kama viumbe wengine, natubu jamani nimekosa naomba msamaha wenu nipo chini ya miguu yenu.
Rachel mwanangu nisamehe mama....Mama Rachel mke wangu nisamehe mpenzi, kama hamtanisamehe basi heri ninywe sumu kuliko kuonekana kiumbe nisiye na thamani kwenu kwa kuniona nafaa wakati wa furaha wakati wa matatizo mnanipa kisogo,” Mzee Mulisa naye alichimba mkwala.
“Mume wangu kwa kweli ulichokifanya kilikuwa sawa na kufanya kipango ya mauaji ya mwanao bila kujua. Nakuapia kama si ujasiri wa Athuman sasa hivi Rachel tungempoteza japo wewe uliamini ndiyo tiba lakini ulikuwa umefanya mauaji ya bila kukusudia. Lakini hatuna budi kukusamehe kwa vile umetambua kosa lako. Rachel msamehe baba yako,” mama Rachel alimweleza mwanaye.
“Nimemsamehe,” Rachel alisema.
Rachel alikumbatiana na baba na mama yake wote kukumbatiana kwa kusameheana na kuyasahau yote yaliyopita.
***
Mzee Mulisa alikubali kwa shingo upande lakini moyoni alipanga kumfanyia kitu kibaya Athumani. Aliona kumuoza mwanaye kwa maskini kama yule ilikuwa sawa na kumpa nguruwe. Alimchukia moyoni kwa kuvuruka mipango yake juu ya mwanaye kwanza kamualibia masomo na kuharibu malengo yake ya kumsomesha mwanaye ili awe na digirii ya uchumi aweze kumkabidhi mali zake aziongoze pindi watakapo zeeka.
Siri ile aliipanga kuifanya baada ya mwaka mmoja wa ndoa ya mwanaye kwa kumuua Athumani kwa siri bila mwanaye kujua wakati huo akijifanya yupo karibu na familia ile na kutoa misaada mingi huku akipanga kushtuka akipewa taarifa ya kifo cha Athumani kwa kulia mpaka kuzirai ili mkewe ajua kile kifo hausiki nacho.
Pia alipanga kumpiga mwanaye sindano ya siri ya kuzuia kupata ujauzito ili kipindi chote cha mwaka mzima aweze kumrudisha shule ili afikie alichokipanga.
Siku ya pili alitumwa Rachel kumfuata Athuman ili aonane rasmi na mzee Mulisa kama mkwewe mtalajiwa. Rachel alimfuata Athumani nyumbani alimkuta amejipumzisha. Alipofika alimrukia huku akipiga kelele.
“Athumani Mungu mkubwa kasikia kilio chetu.”
“Vipi kuna nini? Naona una furaha usiyo ya kawaida.”
Rachel alimweleza yote yaliyojili mpaka kutumwa kumfuata.
“Rachel unamuamini baba yako?” Athumani alimuuliza mpenzi wake.
“Kwa mkwala niliompiga hawezi kufanya tena ujinga wake twende akakutambue na kupanga mipango ya ndoa.”
“Mmh! Kama ni hivyo lazima tumshukuru Mungu kwa kazi yake.”
“Yaani, naona kama vile tayari tumeisha kuwa mke na mume, Yaani sijui itakuwaje baada ya kufunga ndoa.”
“Tukipata na mtoto!”
“Yaani mwanangu nitamlea kama yai.”
Waliondoka pamoja mpaka nyumbani kwao, walipofika mzee Mulisa alimuomba msamaha Athumani mbele ya familia yake kwa yote yaliyotokea huku akiusifu ujasiri wake ambao aliamini ndiyo uliokoa maisha ya mwanaye kipenzi. Siku ile ilipangwa siku ya harusi.
Maandalizi yalikwenda vizuri ya harusi baada ya Rachel kusisitiza kubadili dini na wazazi wake kumkubalia. Lakini Athuman hakutaka kuwaudhi wazazi wa Rachel ndoa ilifungwa Bomani kwa kila mmoja kubakia na dini yake na baadaye kufanyika sherehe kubwa kwenye ukumbi.
Kutokana na kuijua thamani ya elimu Athumani baada ya mwezi alimuomba mzee Mulisa amtafutie mkewe shule ili aendeleze elimu yake na kufikia malengo yake. Mzee Mulisa alishtuka kusikia vile na kujiona mpumbavu kutaka kumtendea mabaya mkwewe ambaye kumbe ana mawazo ya kimaendeleo.
Mara moja alimtafutia Rachel shule na kuendelea na kidato cha tano, Athuman aliendelea kuwa karibu mkewe kwa kumpa moyo mpaka alipohitimu elimu ya chuo na kupata shahada ya uchumi. Siku ya mahafari ya mwanaye kupokea cheti cha kupata shahada ya kwanza ya uchumi mzee Mulisa alilia machozi na kukumbuka nia yake mbaya Athumani. Alijikuta akimpenda mkwewe na kutoa sehemu ya mali yake kwa mwanaye na mumewe.
Sasa hivi wanaendelea na maisha yao huku Rachel akiitafuta shahada ya pili, maisha ya mke na mume yenye upendo yakiendelea. Na kuendeleza miradi walio achiwa na wazazi wao. Walipanga watafute mtoto baada ya shahada ya pili.
MWISHO
 
Love Stori: Muhanga wa mapenzi
Sehemu: 18
Mtunzi: Ally Mbetu
SIMU: 0713646500......

ILIPOISHIA:
“Rachel mwanangu nilifanya yote yale si kwa nia mbaya bali kuyaokoa maisha yako, Athuman ni kijana maskini huwezi kuyatengeneza maisha yako.”
“Aaah! Unajua unanishangaza sana kama ulijua maskini na umeweza kumpa milioni 50 na ishirini ulitaka kumuongezea ili avunje penzi lake kwangu. Huoni huo ni utajiri tosha kwa nini hukutupa hata milioni 500 ili tuweze kuendeleza maisha yetu bila kukusumbua?” Rachel alimuuliza baba yake.
SASA ENDELEA...

“Kwa kweli mwanangu sikuwa na wazo hilo, ili kukuonesha nakupenda na vilevile nakuthamini, nakuahidi kukusimamia kwa kila kitu juu ya ndoa yako na Athuman.”
“Pamoja na kusema yote hayo bado sikuamini, nakuona unanipaka matope kwa mgongo wa chupa,” bado Rachel hakutaka kumuamini wala kumsamehe baba yake kwa kuamini kutoa milioni sabini ni dhahili alikuwa amedhamilia.”
“Nifanye nini ili mwanangu uamini nitafanya unacho kifikiria?”
“Chochote utakacho nifanyia siwezi kukuamini na siwezi kukuamini kamwe,” Rachel alimpa wakati mgumu baba yake ambaye kwa mara ya kwanza alijiona kiumbe mdogo asiyejaa mkononi kwa mwanaye.
“Mama Rachel mke wangu, naomba basi umueleze mwanao ili aniamini kama sitafanya upuuzi kama huu tena.”
“Mume wangu kwa kweli mpaka sasa sijapata jibu kwa kile ulichokifanya cha kutuzunguka kumbe una ajenda nzito, hivi unajua vizuri jinsi Rachel anavyo mpenda Athuman halafu leo uwaachanishe. Mume wangu kilio ulichotaka kukiiingiza ndani ungekinyamazisha kwa shilingi ngapi kama ulitaka kukiandaa kifo cha mwanao kwa milinini 70?”
“Mke wangu jamani mimi ndiye kiumbe cha kwanza kufanya makosa ambayo sisitahili kusamehewa? Hata mimi japo kichwa cha familia nahitaji kusamehewa kama viumbe wengine, natubu jamani nimekosa naomba msamaha wenu nipo chini ya miguu yenu.
Rachel mwanangu nisamehe mama....Mama Rachel mke wangu nisamehe mpenzi, kama hamtanisamehe basi heri ninywe sumu kuliko kuonekana kiumbe nisiye na thamani kwenu kwa kuniona nafaa wakati wa furaha wakati wa matatizo mnanipa kisogo,” Mzee Mulisa naye alichimba mkwala.
“Mume wangu kwa kweli ulichokifanya kilikuwa sawa na kufanya kipango ya mauaji ya mwanao bila kujua. Nakuapia kama si ujasiri wa Athuman sasa hivi Rachel tungempoteza japo wewe uliamini ndiyo tiba lakini ulikuwa umefanya mauaji ya bila kukusudia. Lakini hatuna budi kukusamehe kwa vile umetambua kosa lako. Rachel msamehe baba yako,” mama Rachel alimweleza mwanaye.
“Nimemsamehe,” Rachel alisema.
Rachel alikumbatiana na baba na mama yake wote kukumbatiana kwa kusameheana na kuyasahau yote yaliyopita.
***
Mzee Mulisa alikubali kwa shingo upande lakini moyoni alipanga kumfanyia kitu kibaya Athumani. Aliona kumuoza mwanaye kwa maskini kama yule ilikuwa sawa na kumpa nguruwe. Alimchukia moyoni kwa kuvuruka mipango yake juu ya mwanaye kwanza kamualibia masomo na kuharibu malengo yake ya kumsomesha mwanaye ili awe na digirii ya uchumi aweze kumkabidhi mali zake aziongoze pindi watakapo zeeka.
Siri ile aliipanga kuifanya baada ya mwaka mmoja wa ndoa ya mwanaye kwa kumuua Athumani kwa siri bila mwanaye kujua wakati huo akijifanya yupo karibu na familia ile na kutoa misaada mingi huku akipanga kushtuka akipewa taarifa ya kifo cha Athumani kwa kulia mpaka kuzirai ili mkewe ajua kile kifo hausiki nacho.
Pia alipanga kumpiga mwanaye sindano ya siri ya kuzuia kupata ujauzito ili kipindi chote cha mwaka mzima aweze kumrudisha shule ili afikie alichokipanga.
Siku ya pili alitumwa Rachel kumfuata Athuman ili aonane rasmi na mzee Mulisa kama mkwewe mtalajiwa. Rachel alimfuata Athumani nyumbani alimkuta amejipumzisha. Alipofika alimrukia huku akipiga kelele.
“Athumani Mungu mkubwa kasikia kilio chetu.”
“Vipi kuna nini? Naona una furaha usiyo ya kawaida.”
Rachel alimweleza yote yaliyojili mpaka kutumwa kumfuata.
“Rachel unamuamini baba yako?” Athumani alimuuliza mpenzi wake.
“Kwa mkwala niliompiga hawezi kufanya tena ujinga wake twende akakutambue na kupanga mipango ya ndoa.”
“Mmh! Kama ni hivyo lazima tumshukuru Mungu kwa kazi yake.”
“Yaani, naona kama vile tayari tumeisha kuwa mke na mume, Yaani sijui itakuwaje baada ya kufunga ndoa.”
“Tukipata na mtoto!”
“Yaani mwanangu nitamlea kama yai.”
Waliondoka pamoja mpaka nyumbani kwao, walipofika mzee Mulisa alimuomba msamaha Athumani mbele ya familia yake kwa yote yaliyotokea huku akiusifu ujasiri wake ambao aliamini ndiyo uliokoa maisha ya mwanaye kipenzi. Siku ile ilipangwa siku ya harusi.
Maandalizi yalikwenda vizuri ya harusi baada ya Rachel kusisitiza kubadili dini na wazazi wake kumkubalia. Lakini Athuman hakutaka kuwaudhi wazazi wa Rachel ndoa ilifungwa Bomani kwa kila mmoja kubakia na dini yake na baadaye kufanyika sherehe kubwa kwenye ukumbi.
Kutokana na kuijua thamani ya elimu Athumani baada ya mwezi alimuomba mzee Mulisa amtafutie mkewe shule ili aendeleze elimu yake na kufikia malengo yake. Mzee Mulisa alishtuka kusikia vile na kujiona mpumbavu kutaka kumtendea mabaya mkwewe ambaye kumbe ana mawazo ya kimaendeleo.
Mara moja alimtafutia Rachel shule na kuendelea na kidato cha tano, Athuman aliendelea kuwa karibu mkewe kwa kumpa moyo mpaka alipohitimu elimu ya chuo na kupata shahada ya uchumi. Siku ya mahafari ya mwanaye kupokea cheti cha kupata shahada ya kwanza ya uchumi mzee Mulisa alilia machozi na kukumbuka nia yake mbaya Athumani. Alijikuta akimpenda mkwewe na kutoa sehemu ya mali yake kwa mwanaye na mumewe.
Sasa hivi wanaendelea na maisha yao huku Rachel akiitafuta shahada ya pili, maisha ya mke na mume yenye upendo yakiendelea. Na kuendeleza miradi walio achiwa na wazazi wao. Walipanga watafute mtoto baada ya shahada ya pili.
MWISHO

Safi sana...

Athumani na Rachel wamepitia misukosuko mpaka huruma...


Chapter Closed...


Cc: mahondaw
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom