Hadithi Muathirika Wa Ngono

SEHEMU YA 42

Johnson hakutaka kubaki nchini Marekani, ilikuwa ni lazima arudi nchini Tanzania kwa lengo la kumtafuta msichana Bhoke ambaye aliamini angeifanya kazi yake kama alivyotaka.

Aliukumbuka uzuri wa msichana yule, mchanganyikio wake wa rangi ambao uliwaacha watu wengi midomo wazi. Hakujua alipokuwa akiishi ila kitu ambacho alikikumbuka ni kwamba alikuwa Magomeni alipokuwa akiishi na mama yake.

Alipofika nchini Tanzania, akaanza kuelekea huko ambapo nao walihama na kuhamia Mikocheni B. Alipofika huko akaanza kumuulizia msichana huyo, kila mmoja hakujua mahali alipokuwa, mama yake alipofariki, naye hakukaa sana akaondoka, alipoondoka, hakuna aliyepafahamu.

Hilo likamuhuzunisha mno, kwake, huyo Bhoke alikuwa mtu muhimu kuliko yeyote yule. Ilikuwa ni lazima apambane kadiri alivyoweza lakini mwisho wa siku afanikiwe kuonana naye.

Kwa kuwa alikumbuka msichana huyo alikuwa na rafiki mahali hapo aliyeitwa Happiness, akamtafuta, alipomuona akaanza kuongea naye.

Msichana huyo ndiye ambaye alimwambia ukweli kuhusu Bhoke, kwamba alikuwa akijiuza kwa kusafiri kwenda sehemu mbalimbali kama kutanua soko lake. Johnson alivyosikia hivyo, hakuamini masikio yake, aliumia moyoni mwake lakini pia alikumbuka maisha ambayo aliishi Bhoke.

Yalikuwa maisha magumu mno, hakuwa na pesa za kutosha, alimtegemea mama yake ambaye baada ya kufariki, hakujua ni kwa namna gani angeweza kuyaendesha maisha hayo.

Hakutaka kumlaumu, kwa mtoto wa kike kama yeye ilikuwa ni lazima kuishi maisha hayo hivyo akapotezea na kumwambia Happiness kwamba alihitaji kuonana na msichana huyo.
“Nitakupa namba yake!” alisema Happy.
“Sawa.”

Akapewa namba ya Bhoke na kuanza kuwasiliana naye. Siku hiyo ndiyo kwamba msichana huyo alimaliza kufanya mapenzi na rais Edmund usiku uliopita, kitendo cha kupigiwa simu na Johnson kilimshtua kupita kawaida.

Ilipita miaka mingio, tangu mama yake alipofariki, alimpenda mno kijana huyo, alikumbuka jinsi alivyomjali katika kipindi cha nyuma, japokuwa hakuwa ameutoa usichana wake lakini kwake alikuwa mtu mwenye thamani kuliko mtu yeyote yule.
 
SEHEMU YA 43

Akamwambia kwamba alikuwa katika hoteli moja kubwa hivyo kama alihitaji kumuona ilikuwa ni lazima aelekee huko na kuongea naye.

Alipoambiwa hivyo, Johnson hakutaka kujiuliza mara mbilimbili, alipata majibu juu ya kile alichoambiwa.

Kulikuwa na wasichana wengi jijini Dar es Salaam ambao makazi yao yalikuwa ni hotelini tu.
Kila siku walikuwa huko ambapo waliwaita wateja wao waliogharamia kila kitu na kufanya mapenzi humohumo.

Aliyafahamu maisha hayo kwani yalikuwa yaleyale yaliyokuwa yakifanywa na wasichana wa aina hiyo nchini Marekani.

Kwa kuwa alikuwa na shida ya kuonana naye, hakutaka kusubiri, haraka sana akajiandaa na kuelekea huko. Alipofika, akaelekea mapokezi ambapo alizungumza na dada wa hapo ambaye alimwambia kwamba alikuwa na mgeni wake huko, akapigiwa simu na kumruhusu.

Akaelekea huko mpaka chumbani. Hakujua kama msichana huyo alikuwa akilindwa kwa kuwa alikuwa chakula cha rais lakini pia kulikuwa na kazi kubwa alitakiwa kuifanya.

Alipofika huko, akaingia ndani na kuonana na Bhoke. Akamsogelea na kumkumbatia. Joto la Johnson likamchanganya Bhoke, kifua chake kipana kiliufanya mwili wake kusisimka kupita kawaida.

Ghafla akabadilika na mwili wake kushikwa na kiu ya ajabu sana, alitamani kumvua nguo Johnson na kumwambia kwamba alimuhitaji, alihitaji kushikwa hapa na pale na hatimaye walale kitandani.

“John! Nimekukumbuka,” alisema msichana huyo kwa sauti ya mahaba huku wakiwa wamekumbatiana, katika sehemu kama hizo za kuupoza mwili wake hakutaka kusikia aibu, hapohapo akaanza kuilamba shingo ya Johnson kitu kilichomshtua mwanaume huyo.
“Bhoke....”

“Nimeshindwa kuvumilia Johnson, ninakuhitaji ukate kiu yangu,” alisema Bhoke kwa sauti ya mahaba.

Ilikuwa ni vigumu kwa Johnson, hakuwa mahali hapo kwa lengo la kufanya mapenzi na msichana huyo bali alikuwa hapo kwa kuwa kulikuwa na mambo walitakiwa kuzungumza wawili tu.

“Bhoke! Subiri kwanza,” alisema Johnson huku akimtoa msichana huyo mwilini mwake.

“Ninakuhitaji! Johnson!”
“Najua! Subiri kwanza,” alisema kijana huyo na kumtoa kabisa.
 
SEHEMU YA 44

Akamuweka kitandani, akaanza kumwangalia machoni mwake, kwa jinsi alivyoonekana tu, macho yake yalibadilika na kuwa na muonekano ulioonyesha ni kwa jinsi gani alizidiwa na alimuhitaji mwanaume huyo kitandani.

“Bhoke! Nimekuja kwa shida moja,” alisema Johnson.

“Shida gani?”
“Ninahitaji msaada wako wa ari na mali,” alisema Johnson huku akimwangalia msichana huyo.
“Msaada gani?”

Hapo ndipo alipoanza kumwambia kile alichokuwa akikihitaji, hakutaka kumficha, ilikuwa ni lazima kumuweka wazi kwani mbele yake kulikuwa na utajiri mkubwa mno.

Alimwambia kila kitu, Bhoke alibaki akimwangalia Johnson, hakuamini kama mwanaume huyo alikuwa akizungumzia trilioni za pesa, kwake, kile alichikisikia kilionekana kuwa kama ndoto.

“Unazungumzia dola bilioni tano!” alisema Bhoke huku akionekana kutokuamini kabisa.

“Ndiyo!”
“Ni trilioni zaidi ya kumi!”
“Kabisa!”

Akashusha pumzi tena, mhemko wa kufanya mapenzi na Johnson wote ukapotea ghafla, alifikiria pesa hizo, yaani kama angefanikiwa kuzipata basi angebadilisha maisha yake.

Isingekuwa kufanya mapenzi na wanaume hata ambao hakuwa akiwataka, angekuwa na uwezo wa kufanya mapenzi na mwanaume yeyote yule na kumlipa kiasi kizuri cha pesa.

Hakutaka kulemba, alimwambia kwamba alikuwa tayari ila kwa kuwa kulikuwa na kazi nyingine alitakiwa kufanya, alitakiwa kusubiri mpaka pale ambapo ingekamilika.
“Hakuna shida.”

Baada ya kumaliza mazungumzo yao, Johnson akatoka na kuelekea nje, moyo wake ulikuwa na furaha tena, hakuamini kama alifanikiwa kuonana na msichana huyo, akaongea naye na kubwa zaidi ni kuwa alikubaliana naye kwa kila kitu.

Uso wake ulikuwa na tabasamu pana. Pale nje alipofika, akachukua teksi na kuondoka hapo hotelini.

Walipokuwa njiani tu, ghafla gari moja aina ya Verrosa ikasimama mbele yao, wanaume wawili wakateremka, mikononi mwao walikuwa na bastole.

Watu waliokuwa maeneo hayo walishangaa, hawakujua kilichokuwa kikiendelea, huku wakijiuliza, risasi tatu zikapigwa hewani, kila mmoja aliyezisikia, hakutaka kubaki mahali hapo, akakimbia kuiokoa nafsi yake.
 
SEHEMU YA 45

Johnson hakuelewa kilichokuwa kikiendelea, yeye na dereva walibaki wakitetemeka tu.

Wanaume wale wakapiga hatua mpaka lilipokuwa gari lao, wakafungua mlango na kumteremsha Johnson huku wakimwambia anyamaze.
“Nimefanya nini jamani?”

aliuliza, swali lake hilo likajibiwa na kipigo kimoja cha kitako cha bunduki kisogoni, hapohapo akapoteza fahamu, hakujua ni kitu gani kiliendelea baada ya hapo.

Johnson alirudiwa na fahamu akiwa kwenye chumba kidogo kilichokuwa na giza totoro. Hakujua mahali hapo palikuwa wapi.

Kulikuwa na joto kali kupita kawaida na kila alipotaka kusimama alishindwa kwani aligundua miguuni mwake alifungwa kamba ngumu.
Kwa nyuma, kisogoni alikuwa na maumivu makali, alikaa kwa sekunde chake huku akitafakari mahali alipokuwa na kile kilichotokea ndipo akaanza kukumbuka kila kitu.

Mara ya mwisho alitoka hotelini, alipochukua teksi, kulikuwa na watu waliowasimamisha ambao walikuwa na bastola, waliwafuata na kumchukua yeye na kumpiga kitako cha bastola na baada ya hapo hakukumbuka ni kitu gani kilikuwa kimeendelea.

Kulikuwa na ukimya wa muda mrefu mahali hapo, harufu ya chumba kile haikuwa nzuri hata kidogo, ilikuwa ni harufu mbaya mno ya damu na hata aliposhika chini, aligundua kuugusa unyevuunyevu ambao alikuwa na uhakika ilikuwa ni damu.

Akaanza kuita kwa sauti, alihitaji msaada kutoka mahali hapo, hakujua kama watu waliomteka walikuwa humo au la, alichokihitaji ni kupata msaada kwani alihitaji kuendelea kuwa hai kwa kuwa kulikuwa na pesa nyingi alizokuwa akizihitaji kwa gharama yoyote ile.

“Nisaidieniiiiiii...” alipiga kelele kwa kuamini kungekuwa na watu ambao wangemsikia na kufika pale kumsaidia.
Baada ya dakika moja ya kupiga kelele, mlango ukafunguliwa na mwanaume mmoja kuingia na kuwasha taa.

Kwa jinsi mwanga wa ghafla ulivyommulika usoni mwake, akayafumba macho yake na kisha kuyafumbua kwa taadhari kubwa.
“Mbona unapiga kelele mwanaume wa Dar?” aliuliza jamaa huyo kwa sauti nzito.

“Bro! Nimefanya nini?” aliuliza Johnson huku akijitahidi kumwangalia mtu huyo aliyekuwa akiongea naye.
 
SEHEMU YA 46

Kwa muonekano wake tu, alitisha, alivalia suruali ya jinsi, ilionekana kama kuchoka, ilichanikachanika huku kwa juu akiwa na fulana nyekundu iliyoandikwa maneno yaliyosemeka vizuri machoni mwake, Gucci.

Chini alivalia raba nyeusi, mkononi alikuwa na saa moja iliyoonekana kuwa na gharama kubwa.

Alisimama imara huku akimwangalia Johnson ambaye muda wote huo alikuwa akitetemeka.
Swali ambalo aliuliza, hakujibiwa, mwanaume huyo akaondoka huku akiufunga mlango, na taa hakuizima.

Hapo ndipo macho ya Johnson yalipoanza kukiangalia chumba hicho.
Kilitisha, hakikuwa chumba cha kawaida hata kidogo.

Katika maisha yake aliwahi kuona filamu nyingi za kutisha ambazo watengenezaji waliamini kabisa watu wangeogopa mara baada ya kuzitazama, ila kwa vyumba vyote, mauaji yote yaliyokuwa yakitokea ilikuwa tofauti na chumba hicho.

Kilitisha kupita kawaida. Chini kulikuwa na damu, zilitapakaa kila eneo, kulikuwa na minyororo ya nguvu, kamba, mijeredi lakini pia kulikuwa chupa zilizokuwa zimepasuliwa, kichwani mwake kukamwambia chupa zile zilipasuliwa mwilini mwa mtu. Kwa kifupi chumba kile kilitisha sana.

Hakujua sababu iliyomfanya kuwa mahali hapo, hakufikiri hata kidogo kama Bhoke inawezekana alikuwa sababu, kitu ambacho kilikuja kichwani mwake ni jina moja la mwanaume aliyeitwa Thuram.
Alikuwa na mipango yake ya dhati, alijipanga kwa ajili ya kumgeuka mwanaume huyo.

Alimwambia kuhusu pesa zilizokuwa mahali fulani ambapo hakutaka ajue lakini ili kuzipata ilikuwa ni lazima kuzungumza na mwanaume alieitwa kwa jina la Bruce ambaye alifahamu kila kitu kuhusu pesa hizo.

Alihisi kabisa mwanaume huyo aligundua kwamba alikuwa akienda kusalitiwa na ndiyo maana aliamua kuwatuma watu kwa lengo la kwenda kummaliza.
Alijuta.

Alijilaumu mno kuingia mikononi mwa mwanaume huyo. Hakuona dalili za kupona tena, alijua kabisa huo ndiyo ungekuwa mwisho wake endapo tu mwanaume huyo angeagiza mara moja auawe hukohuko nchini Tanzania.
 
SEHEMU YA 46

Kwa muonekano wake tu, alitisha, alivalia suruali ya jinsi, ilionekana kama kuchoka, ilichanikachanika huku kwa juu akiwa na fulana nyekundu iliyoandikwa maneno yaliyosemeka vizuri machoni mwake, Gucci.

Chini alivalia raba nyeusi, mkononi alikuwa na saa moja iliyoonekana kuwa na gharama kubwa.

Alisimama imara huku akimwangalia Johnson ambaye muda wote huo alikuwa akitetemeka.
Swali ambalo aliuliza, hakujibiwa, mwanaume huyo akaondoka huku akiufunga mlango, na taa hakuizima.

Hapo ndipo macho ya Johnson yalipoanza kukiangalia chumba hicho.
Kilitisha, hakikuwa chumba cha kawaida hata kidogo.

Katika maisha yake aliwahi kuona filamu nyingi za kutisha ambazo watengenezaji waliamini kabisa watu wangeogopa mara baada ya kuzitazama, ila kwa vyumba vyote, mauaji yote yaliyokuwa yakitokea ilikuwa tofauti na chumba hicho.

Kilitisha kupita kawaida. Chini kulikuwa na damu, zilitapakaa kila eneo, kulikuwa na minyororo ya nguvu, kamba, mijeredi lakini pia kulikuwa chupa zilizokuwa zimepasuliwa, kichwani mwake kukamwambia chupa zile zilipasuliwa mwilini mwa mtu. Kwa kifupi chumba kile kilitisha sana.

Hakujua sababu iliyomfanya kuwa mahali hapo, hakufikiri hata kidogo kama Bhoke inawezekana alikuwa sababu, kitu ambacho kilikuja kichwani mwake ni jina moja la mwanaume aliyeitwa Thuram.
Alikuwa na mipango yake ya dhati, alijipanga kwa ajili ya kumgeuka mwanaume huyo.

Alimwambia kuhusu pesa zilizokuwa mahali fulani ambapo hakutaka ajue lakini ili kuzipata ilikuwa ni lazima kuzungumza na mwanaume alieitwa kwa jina la Bruce ambaye alifahamu kila kitu kuhusu pesa hizo.

Alihisi kabisa mwanaume huyo aligundua kwamba alikuwa akienda kusalitiwa na ndiyo maana aliamua kuwatuma watu kwa lengo la kwenda kummaliza.
Alijuta.

Alijilaumu mno kuingia mikononi mwa mwanaume huyo. Hakuona dalili za kupona tena, alijua kabisa huo ndiyo ungekuwa mwisho wake endapo tu mwanaume huyo angeagiza mara moja auawe hukohuko nchini Tanzania.
Thanks

Sent using Jamii Forums mobile app
 
SEHEMU YA 47

Aliendelea kulia zaidi mpaka baada ya saa tano ambapo mlango ukafunguliwa na kutolewa. Alipelekwa mpaka sebuleni ambapo hakukuwa na kitu chochote kile zaidi ya televisheni iliyopachikwa ukutani huku kukiwa na ndoo kama nne zilizojaa maji.

“Kaa hapo chini,” alisema mwanaume mmoja huku akimwangalia Johnson, haraka sana akatii na kukaa.

Alitulia tuli. Hakutakiwa kuzungumza kitu chochote kile. Muda wote huo mapigo ya moyo wake yalikuwa juu, alikuwa akitetemeka kupita kawaida na muda wote kijasho chembamba kilikuwa kikimtoka.

Aliambiwa kulikuwa na mtu ambaye angempigia simu, alihitaji kuzungumza naye, kulikuwa na mambo ambayo alihitaji kumwambia ambayo alitakiwa afanye kila liwezekanalo kuhakikisha linafanyika haraka sana.

Angepigiwa simu? Na nani? Ni huyo Thuram au alikuwa mtu mwingine. Alijiuliza maswali mengi ambayo hayakuwa na majibu kabisa. Baada ya dakika kadhaa, simu ya mezani ikaanza kuita, haraka sana mwanaume mmoja akaifuata na kuunyanyua mkonga wa simu na kuanza kuzungumza naye.

“Unaitwa nani?” aliuliza mwanaume aliyekuwa akisikika kutoka upande wa pili. Aliifahamu sauti, haikuwa ngeni masikioni mwake, aliwahi kuisikia mara kadhaa kwenye televisheni, huku akijiandaa kujibu, ubongo wake ulikuwa na harakati za kutaka kugundua ilikuwa ni sauti ya nani.

“Ni rais!” alijisemea moyoni kwa mshtuko.
“Naitwa Johnson!” alijibu huku akitetemeka.
“Ulikwenda kufanya nini hotelini?” aliuliza rais.

“Nilikwenda kuzungumza na rafiki yangu wa muda mrefu, anaitwa Bhoke,” alijibu.
“Muda mrefu! Unamaanisha nini?”
“Kwamba tangu tulipokuwa wadogo!”

“Na ulijuaje kama alikuwa humo?”
“Nilizungumza naye kwenye simu!”
“Sawa. Mlifanya mapenzi kwa dakika ngapi hotelini chumbani?” aliuliza rais, lilionekana kuwa kama swali la kijinga lakini alimaanisha sana.

“Hatukufanya mapenzi, nisingeweza kwa kuwa ninamuheshimu sana kama dada yangu,” alijibu Johnson.

“Kijana! Kamera zilikunasa ukibanjuka naye kitandani, halafu unabisha!”
“Hapana! Sikufanya naye! Haki ya Mungu!”

“Unajua unaongea na nani hapa?”
“Hapana!” alijibu.
 
SEHEMU YA 48

Alijua sana mtego wa swali hilo, kama angemwambia kuwa ni rais basi inawezekana kabisa mwanaume huyo angeagiza auawe kwa kuwa alihitaji iwe siri na ndiyo maana na yeye alimwambia kwamba hakumfahamu alikuwa nani.

Akaambiwa ampe simu mwanaume yeyote aliyekuwa hapo ambaye huyo akaambiwa amtoe Johnson kwani hakuwa na tatizo lolote lile, hivyo mwanaume huyo akaruhusiwa kuondoka zake.

Hilo likamfanya kumuogopa Bhoke, hakuwa mwanamke wa kawaida tena, aliwekewa ulinzi wa kila kona, alihitajika kwa udi na uvumba na hakukuwa na mtu yeyote ambaye angetamani kumsogelea kama tu ingegundulika mtu aliyekuwa nyuma yake.

Alikuwa na maswali mengi, alijiuliza kuhusu ukaribu wa watu hao, ulianzia wapi na ilikuwaje huyo Bhoke awe na ulinzi mkubwa kama huo kiasi cha mwanaume yeyote kutekwa na kupelekwa pasipopojulikana?

Alijiuliza hayo yote pasipo jibu lolote lile. Hapo ndani, akachukuliwa, akafumbwa macho yake na kuondolewa haraka sana kwa gari na baada ya nusu saa, gari likasimama maeneo ya Manzese na kuambiwa ateremke na kuelekea alipotaka kuelekea.

“Nashukuru sana wakuu,” alisema Johnson huku akionekana kuogopa. Hakuamini kama angeachwa hai.

Hapo, akaamua kuondoka zake. Bado maswali yalikuwa kichwani mwake. Bhoke alikuwa msaada mkubwa, mbele yake kulikuwa na pesa nyingi ambazo piga ua ilikuwa ni lazima azipate kwa staili yoyote ile.

Alichukua Bajaj, ndani bado aliendelea kujiuliza na kitu pekee kilichokuja kichwani mwake ni kuwa alitakiwa kupambana kuhakikisha anafanya kazi na msichana huyo.

Hakutaka kujali nyuma yake kulikuwa na nani! Kitu alichokuwa akijua ni kwamba Bhoke alikuwa pesa ndefu, kama angefanikiwa kumchukua na kuondoka naye kuelekea Marekani basi ilikuwa ni lazima afanikishe lile dili alilotaka kulifanya huko.

“Nitamrudia tena! Sikomi! Kwanza wanaume wa Dar kwenye ishu za wanawake huwa hatukomi! Labda utuambie twende shambani,” alisema Johnson.
 
SEHEMU YA 49

Rais alichanganyikiwa mno, hakutaka kuona akimpoteza msichana huyo mrembo. Alizungumza na walinzi wake na kuwaambia ni lazima Bhoke alindwe kwa nguvu zote kwa sababu tu alimfanya kuwa mwanaume aliyefaidi kuliko wanaume wote katika dunia hii.

Ulinzi wa chini kwa chini ulikuwa mkubwa hotelini, hakukuwa na mtu aliyekuwa akifahamu kitu chochote kile, kila mmoja aliwaona maofisa wa usalama wa taifa lakini hakukuwa na aliyejua kama watu hao walikuwa maofisa kutokana na namna walivyovaa.

Hata Johnson alipofika mahali hapo na kuelekea chumbani, walifahamu, walipewa taarifa na dada wa mapokezi na ndiyo maana alipotoka tu wakamteka huku wakimwambia rais kila kitu kilichotokea.

Wivu mkali ukamkamata rais, hakuamini kama Bhoke alithubutu kumuita mwanaume hotelini na kujifungia zao chumbani. Alikuwa na hasira, alipanga kumkaripia sana Bhoke, wambie kile alichokifanya hakikuwa sahihi na kama angemletea za kuleta basi angemuua.

Haraka sana huku akiwa na hasira zake, moyo wake ukiwa umevimba na ndita kuonekana usoni akachukua simu yake kwa lengo la kumpigia msichana huyo. Alipoiona namba tu, akampigia.
“Halo bebi!” aliita msichana huyo.

Alikuwa na hasira kali, moyo wake ulivimba lakini mara baada ya kuisikia sauti ya msichana huyo tu, akahisi hasira zote zilizokuwa moyoni mwake zikiondoka, ndita alizokuwa amekunja usoni mwake zikapotea na ghafla tabasamu pana kuonekana usoni mwake.

Sauti ya Bhoke ilikuwa dawa ya kila kitu, ilimuondolea matatizo yake na kumpa furaha na amani ya milele. Alipanga kumkaripia lakini baada ya kuisikia sauti hiyo, akajikuta akibadilika.

“Nimekukumbuka mpenzi,” alisema rais, hakuamini kama yeye ndiye ambaye aipoa vile.

“Nimekukumbuka mpenzi!” alisema Bhoke, tena alivyojua kuwatega wanaume kwa sauti yake, akaanza kuweka manjonjo yaliyomfanya rais huyo kuchanganyikiwa.

Wakaanza kuongea mambo mengi, aliyasahau kabisa mambo ya Johnson, alikuwa akizungumza vitu vingine kabisa. Baada ya nusu saa ndipo akakumbuka kwamba kulikuwa na jambo jingine alitakiwa kuzungumza na msichana huyo, akaanza kumuuliza.
 
SEHEMU YA 50

“Halafu bebi! Yule kijana aliyekuja hapo alikuwa nani?” aliuliza rais.
“Kijana yupi?”

“Jamani! Si huyo aliyefika muda si mrefu, anaitwa nani? Yaani umenifanya mpaka nimeumia mwenzako kwa ajili ya wivu,” alisema rais kwa upole kabisa.
“Ni rafiki yangu! Anaitwa Johnson, tulianzia mbali sana, tangu utotoni, alikuwa na shida ya kuongea nami!” alijibu Bhoke.

“Kuhusu nini jamani?”
“Maisha tu! Hatukuonana kwa miaka zaidi ya saba.”

“Duh! Kweli kipindi kirefu. Ila hamkufanya chochote?”
“Hapana! Ananichukulia kama dada yake!” “Sawa. Nashukuru bebi kwa kusikia sauti yako nyororo. Nakupenda sana mpenzi wangu,” alisema rais.

“Nakupenda pia baba watoto!”
Rais akakata simu. Akashusha pumzi ndefu, hakuamini alichokisikia. Moyo wake uliridhika kabisa hivyo kupiga simu huko alipohifadhiwa Johnson kwa lengo la kuongea naye kuhusu suala lake la kwenda huko hotelini saa kadhaa zilizopita.

Alijua kila kitu alichoambiwa hivyo alitaka kupima maongezi, ajue nani alikuwa mkweli na nani alidanganya, na alipojaribu kuzungumza na Johnson, kile alichoambiwa na Bhoke kilikuwa kilekile alichoambiwa na kijana huyo, amani na furaha moyoni mwake ikazidi kutawala.

“Mwachieni huyo kijana! Hana kosa lolote lile,” alisema rais na hivyo vijana wale kufanya kama walivyoambiwa pasipo kujua kwamba Johnson alitaka kufanya plan B, kwani alihisi kabisa kama angeibuka na Plan A ingeweza kufeli vibaya.

*** Bruce alikuwa dili kubwa, kila mtu alijua kuhusu mwanaume huyo kwamba alikamatwa baada ya kuzificha pesa kiasi cha dola bilioni tano sehemu.

Hakukuwa na mtu aliyekuwa akijua kuhusu pesa hizo, watu wengi walijifanya kuwa karibu naye huko jela ili lengo lao likiwa ni kutaka kujua ukweli lakini mwanaume huyo hakutaka kabisa kumwambia mtu yeyote yule.
Alikuwa kimya kabisa.

Askari wa magereza walijipendekeza kwake, walimpa maisha mazuri huku wakimpa kila kitu alichokuwa akihitaji kama njia mojawapo ya kumvutia lakini bado alikuwa mgumu kusema mahali pesa zilipokuwa.
 
SEHEMU YA 51

Alifungwa gerezani kifungo cha maisha, asingeweza kutoka, na kutokana na hilo, hakuwa tayari kusema mahali pesa zilipokuwa, alikuwa tayari kuona watu wakihangaika lakini si kutamka kwa mdomo wake.

Maofisa wa kijasusi wa FBI (Federal Bureau of Investigation) nao walizitolea macho pesa hizo, walizihitaji sana, walitaka kujua mahali zilipokuwa, walichokuwa wakitaka sana kuambiwa na Bruce ni mahali pesa hizo zilipokuwa.

Waliwatumia watu wengi, walifanya kazi kubwa ili kuambiwa lakini bado mwanaume huyo hakuwa tayari, alichowaambia ni kwamba alikuwa tayari kupoteza hata uhai wake lakini si kuona akimwambia mtu yeyote yule kuhusu pesa hizo.

Bado kulikuwa na wafungwa waliokuwa wakitumwa kwake, walijipendekeza kiasi kwamba ikawa kero sasa alichokifanya ni kuanza kuwapiga.

Kila mfungwa ambaye alianza kujipendekeza alianza kumpiga. Ugomvi wake ulikuwa mkubwa, kuna wengine walitolewa meno, walivunjwa kiasi kwamba hakukuwa na mtu yeyote yule aliyediriki kumsogelea.

Hayo ndiyo yalikuwa maisha pekee aliyokuwa akiyataka, hakutaka kuishi karibu na mtu yeyote yule, alihitaji kuwa peke yake mpaka pale ambapo angekufa na kuiacha Marekani ikiwa na kiulizo juu ya mahali pesa hizo zilipokuwa.

*** Dili aliloambiwa Bhoke lilimchanganya, hakuamini kama Johnson angemshirikisha katika dili kubwa na la maana kama hilo.

Hapo hotelini alikuwa akijifikiria ni kwa jinsi gani angeweza kuondoka na kuelekea nchini Marekani. Hakutaka tena kuishi Tanzania kwani aliamini kama angefanikiwa kwenda huko Marekani basi dili hilo lingeweza kutiki haraka sana.

Alitamani kuonana tena na Johnson, azungumze naye kuhusu dili hilo lakini hakuwa na nafasi hata kidogo. Aliwekewa ulinzi mkali, rais hakutaka msichana huyo aondoke kwenda sehemu yoyote ile bila ulinzi.

Kulikuwa na kazi nyingine ambayo alitakiwa kupewa lakini rais aliagiza hiyo kazi apewe mtu mwingine lakini si Bhoke, msichana ambaye alimfanya kuwa kimada wake.
 
SEHEMU YA 52

Kila siku usiku aliondoka ikulu na kwenda kuonana na msichana huyo hotelini. Walifanya mapenzi, Bhoke alitumia utundu wa kila aina kumchanganya mwanaume huyo kiasi kwamba kuna wakati alihisi kama msichana huyo alikuwa hatari kitandani kuliko wanawake wote.

“Nitamuacha mke wangu na kukuoa wewe, upo tayari/’ aliuliza rais huku akimwangalia Bhoke kitandani pale, alikuwa akikikuna kitambi chake.

“Haina shida. Ila Watanzania watasemaje?” aliuliza Bhoke.
“Haya ni maisha yangu! Siyo mambo ya kiserikali, itawabidi watulie tu,” alisema rais huyo.

“Sawa. Ninakubali mpenzi! Ila naomba unipe uhuru hata wa kwenda kumuona mama. Umenibana sana,’ alisema Bhoke, alichoka kubanwa, alihitaji kuonana na Johnson kwani alihisi lile dili aliloambiwa ilikuwa ni lazima lifanyike.

Rais Edmund hakuwa na jinsi, alimpenda sana msichana huyo na alihisi kama angekataa kumruhusu basi angemkasirisha kitu ambacho hakutaka kabisa kuona kikitokea.

Pamoja na ruhusa hiyo alimwambia kwamba kila sehemu ambayo angekuwepo, kungekuwa na ulinzi wake, alimpenda sana, hakutaka kuona mwanaume mwingine anakula tunda lake na ndiyo maana alitaka kuhakikisha anakuwa salama kila mahali atakapokuwa.

Hilo halikuwa tatizo kwa Bhoke, baada ya rais huyo kuondoka, akampigia simu Johnson na kumwambia hali halisi kwamba alikuwa akitembea na rais, ingekuwa vigumu sana kuonana naye waziwazi hivyo walitakiwa kufanya kitu ambacho kingewakutanisha na kuongea kidogo.
“Haina shida. Wewe utakuwa na ratiba gani?” aliuliza Johnson.

“Nimemdanganya naenda kumuona mama kesho!” alijibu.
“Wapi?”
“Magomeni!”

“Basi sawa. Naomba tuonane huko Magomeni kwenye mgahawa wa Virus,” alisema Johnson.
“Ila kutakuwa na ulinzi! Nitalindwa kila kona!”

“Hilo si tatizo! Hakikisha baada ya kufika hapo, unakwenda chooni, utanikuta huko!” alisema Johnson.

Walipanga na walipomaliza, Bhoke akalala na kesho mchana akaondoka na kuelekea huko Magomeni. Aliingia kwenye mgahawa huo, aliwaambia walinzi kwamba alihitaji kula kwanza halafu ndiyo aende kwa mama yake.
 
SEHEMU YA 53

Hapo mgahawani, alipeleka macho huku na kule, akamuona Johnson akiwa hapo huku akiwa na kofia kichwani. Alimjua, mwanaume huyo aliuchuna kana kwamba hawakuwa na appointment ya kuonana mahali hapo.

Baada ya dakika kadhaa, Johnson akainuka na kuelekea chooni, hakutoka huko, ndani ya dakika oja naye Bhoke akasimama na kuanza kuelekea huko, mlinzi mmoja akaanza kumfuata.

“Unataka kunifuata mpaka chooni? Unataka kunibaka?” alimuuliza mlinzi.
“Nataka kuhakikisha upo salama!”
“Samahani! Ila si mpaka chooni,” alisema Bhoke na kuondoka huku akimwacha mlinzi huyo mahali hapo.

Alipofika huko, akaelekea upande wa vyoo vya kume ambapo akamuona Johnson aliyemchukua na kumuingiza ndani kabisa. Wakaanz akuangaliana.

“Tunaondoka Tanzania! Nimeangalia uwezekano wa kuchukua viza, ni rahisi sana. Utatumiwa sponsorship na kutakiwa kwenda kusoma huko. Kuwa karibu na barua pepe yao,” alisema Johnso.
“Sawa.”

“Hakikisha unajaza kila kitu! Tutaondoka baada ya siku kadhaa,” alisema Johnson.
“Haina shida.”

Waliongea kwa dakika kadhaa tu na msichana huyo kutoka ndani ya choo hicho na kuelekea mgahawani na kuagiza chakula na kuanza kula, baada ya dakika kadhaa, Johnson akatoka na kuondoka zake.

Hiyo ilikuwa mbinu moja ambayo walitakiwa kuifanya kuhakikisha wanaondoka nchini Tanzania. Baada ya kumaliza akaondoka na kuelekea Magomeni kwa shoga yake na kukaa huko mpaka jioni.

Siku hiyo rais alimpigia simu na kumwambia kwamba alimuandalia nyumba ya kuishi iliyokuwa huko Sinza jijini Dar es Salaam.
 
SEHEMU YA 54

Alihitaji aende kuishi huko kwa kuwa ilionekana kuwa rahisi kwake kutokugundulika kuliko pale hotelini. Bhoke alifurahi, aliamini kwamba hiyo ndiyo ingekuwa nafasi ya yeye kutoroka na kwenda kufanya mambo yake mengine.

Akawa bize na barua pepe yake, alitumiwa link na Johnson na kumwambia kuomba udhamini wa kwenda kusomeshwa nchini Marekani.

Ni ndani ya saa kadhaa, akakubaliwa na hivyo kuandaliwa kila kitu. Hilo lilionekana kuwa jepesi kwake kwa kuwa Johnson aliratibu kila kitu.

Aliandaliwa kila alichokihitaji, ubalozi wa Marekani nchini Tanzania ukapewa taarifa kwamba msichana huyo alitakiwa kuondoka nchini baada ya siku mbili kuelekea nchini Marekani ambapo huko alitarajiwa kuanza masomo kwenye Chuo Kikuu cha Mississippi kilichokuwa katika jiji hilo.

“Bhoke! Kila kitu kipo tayari! Baada ya kupigiwa viza, nadhani tunatakiwa kuondoka haraka sana,” alisema Johnson.

“Na kama rais akijua, tutapitaje uwanja wa ndege?” aliuliza Bhoke huku akionekana kuogopa.
“Tutaondoka kwa kupitia Kenya!”
“Mh!”

“Ila ni endapo atagundua! Baada ya siku mbili utatakiwa kwenda ubalozini kugongewa viza, utanikuta huko,” alisema Johnson na kukata simu.
|
|
|

Je, nini kitaendelea?
Tukutane sehemu zijazo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom