Hadithi Muathirika Wa Ngono


Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2016
Messages
104,185
Likes
294,432
Points
280
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2016
104,185 294,432 280
SEHEMU YA 34

“Basi ni lazima nifanye naye mapenzi!”
“Ila si lazima!”

“Hapana! Lazima nifanye naye. Napenda mno kufanya mapenzi,” alisema Bhoke, alimaanisha alichokuwa akikizungumza kwani kwake, kufanya mapenzi ndiyo ilikuwa starehe yake kubwa kuliko hata kula.

Mambili hakuwa na shida na hilo, alichohitaji ni msichana huyo kufanya kazi yake tu. Kwa kuanzia, akampa kiasi cha milioni tatu na kumwambia mahali ambapo mwanaume huyo angekuwepo kwa ajili ya kuzungumza na wadau mbalimbali kama njia mojawapo ya kuanza kampeni zake.

Bhoke alipoondoka, haraka sana akawapigia simu viongozi wake na kuwaambia kuhusu msichana huyo kwamba alikubali kufanya kazi yake kwa malipo yaleyale waliyokuwa wamepanga.
“Na ni mzuri?” aliuliza waziri mmoja kwenye simu.

“Sanaaaa! Yaani isingekuwa hapa nyumbani, nadhani leo ningevunja naye amri ya sita,” alisema Mambili na kuanza kucheka.

Haraka sana taarifa zikatumwa mpaka kwa Rais Edmund Golam na kuambiwa kuwa msichana huyo alipatikana na tayari alianza kujipanga kwa ajili ya kufanya kazi hiyo kubwa iliyokuwa mbele yake.

Naye alipoambiwa hivyo, kama ilivyokuwa kwa waziri akaulizia uzuri wa Bhoke, akaambiwa kwamba alikuwa mrembo mno hivyo walikuwa na uhakika wa kufanikiwa kwa kile walichokuwa wamekipanga.

Rais Edmund aliposikia hivyo ni kama akili yake ilichanganyikiwa, akamwambia waziri kwamba kabla ya kazi hiyo kufanyika ilikuwa ni lazima aonane na msichana huyo ili ampe mbinu za kufanya katika kutekeleza mpango huo.

Hilo halikuwa tatizo, haraka sana simu ikapigwa mpaka kwa Mambili na kuambiwa kile alichokisema rais hivyo kama iliwezekana ilikuwa ni lazima ampigie simu Bhoke na kumwambia kuhusu kile alichoambiwa.

Halikuwa tatizo, akampigia simu msichana huyo na kumwambia kila kitu. Bhoke aliposikia, hakuamini masikio yake, katika maisha yake yote hakuwahi kufikiria hata mara moja kwamba angeingia ikulu hata kwa bahati mbaya.
 
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2016
Messages
104,185
Likes
294,432
Points
280
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2016
104,185 294,432 280
SEHEMU YA 35

Alimwambia Mambili jinsi alivyokuwa akiogopa, hakujiamini kwa sababu kila siku alijiona malaya ambaye hakutakiwa kuthaminika hata kidogo, sasa suala la kwenda huko alihisi kama angeweza kuichafua ikulu hasa baada ya waandishi wa habari kugundua.

“Hakuna atakayejua! Niamini!” alisema Mambili.

Bhoke akapangiwa chumba hotelini kwa siku ambazo alitakiwa kusubiri wito kutoka ikulu. Katika kipindi hicho hakutakiwa kujiuza, japokuwa ilikuwa vigumu lakini aliambiwa akae pasipo kufanya mapenzi na mtu yeyote yule.

Mwili wake uliwasha, huko chumbani hotelini hakutaka kukubali hata kidogo. Kulikuwa na walinzi waliokuwa wakimlinda kwa nje, kuhakikisha haingii mtu ndani ya hoteli ile na kwenda chumbani kwake.

Kwa kuwa alikuwa hajiwezi kabisa, alichokifanya ni kupiga simu mapokezi na kuongea na msichana wa hapo, alichomwambia ni kwamba alihitaji huduma ya kukandwa mwili wake.

“Sawa! Tunakuandalia mtu, unahitaji wa kike au wa kiume?” aliuliza dada wa mapokezi swali ambalo kwake lilikuwa ni la kijinga sana.

“Wa kiume.”
“Basi haina shida. Naomba uteremke mpaka kwenye chumba maalumu kwa kazi hiyo,” alisema msichana huyo.

“Na haiwezekani kufanyia chumbani?”
“Inawezekana! Ila wengi hawapendi kufanyia vyumbani mwao!”

“Basi mimi nataka!”
“Haina shida, atafika ndani ya dakika chache,” alisema msichana huyo na kukata simu.

Hilo ndilo alilolitaka, hakuweza kuwa na subira hata kidogo, kila alipokuwa mule chumbani alihisi kabisa kulikuwa na vijidudu vilikuwa vikitembea mwilini mwake na mwisho wa siku kwenda chini ya kitovu na kukaa hapo.

Aliteseka siku nzima, alijitahidi kujiridhisha yeye mwenyewe lakini alishindwa kabisa na ili aridhike, mwili wake uwe salama kabisa ilikuwa ni lazima atafute mwanaume wa kukata kiu yake.

Baada ya dakika ishirini, mlango ukaanza kugongwa, harakaharaka akaufuata huku akiwa na taulo na kuufungua. Macho yake yakatua kwa kijana mmoja aliyevalia fulana ambayo iliufanya mwili wake kuonekana vilivyo kabisa.
 
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2016
Messages
104,185
Likes
294,432
Points
280
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2016
104,185 294,432 280
SEHEMU YA 36

Alishika vifaa vyote na kumwambia Bhoke kwamba yeye ndiye alikuwa mtu wa kumkanda mwili wake na alifika mahali hapo kwa kazi hiyo kama alivyoagiza.

“Oh! Karibu sana,” alisema Bhoke huku akimshika mkono na kuupeleka kwenye kifua cha mwanaume huyo kitu kilichomfanya kushtuka.
“Nashukuru sana!”

Akaingia ndani, Bhoke akaelekea bafuni, akaoga huku kijana yule akibaki mahali pale peke yake. Yeye mwenyewe pale alipokuwa alichanganyikiwa, ni kweli kwenye maisha yake aliwahi kuwaona wanawake wazuri ile yule aliyemuona siku hiyo alikuwa balaa.

Bhoke alikuwa na uzuri wa asili, alikuwa na mwili mzuri na hata alipokuwa akitembea, huku kwa nyuma kulikuwa kunachezacheza kitu kilichomchanganya sana kijana huyo.

“Hivi ameniita kwa massage au kuna jingine?” alijiuliza kijana huyo, akaingiza mkono wake mfuko, akatoa pakti moja ya kujikunga ambazo alipenda sana kutembea nazo kwani kwa kazi aliyokuwa akiifanya, mara nyingi alipata vishawishi vikubwa na kujikuta akilala na wanawake aliokuwa akiwafanyia kazi hiyo.

“Zipo! Hizi tatu zinatosha kutumika kama tu atachanganyikiwa na massage yangu,” alisema kijana huyo, baada ya dakika kadhaa, Bhoke akatoka bafuni na taulo lake, akawekwa juu ya meza ndogo ya kufanyiwa massage na kuliweka taulo lake pembeni, akabaki kama alivyozaliwa. Hayo yote aliyafanya ili kukata kiu yake ya muda mrefu. Pepo la ngono lilimsumbua mno.
|
|
|


Je, nini kitaendelea?
 
Smart911

Smart911

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2014
Messages
22,189
Likes
20,630
Points
280
Smart911

Smart911

JF-Expert Member
Joined Jan 3, 2014
22,189 20,630 280
Addiction ya Bhoke ni mbaya sana...

Starehe sasa imekua karaha, adhabu...


Cc: mahondaw
 
Reptilia

Reptilia

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2018
Messages
453
Likes
160
Points
60
Reptilia

Reptilia

JF-Expert Member
Joined Feb 21, 2018
453 160 60
dah lini tena duh inasisimua
 
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2016
Messages
104,185
Likes
294,432
Points
280
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2016
104,185 294,432 280
SEHEMU YA 37

Rais Edmund alikuwa ikulu, kama ilivyokuwa kwa Bhoke kuwashwa na mwili wake na kupenda sana ngono ndivyo ilivyokuwa hata kwa rais huyo.

Alikuwa ikulu lakini mara kwa mara alikuwa akiondoka usiku na kwenda mitaani kuonana na michepuko yake.
Alihusudu ngono kuliko kitu chochote kile.
Kila alipokuwa akifanya ziara nchi mbalimbali, aliwapigia simu wanawake wake na kuonana nao huko na kufanya nao mapenzi. Kila siku mke wake alikuwa mtu wa kulalamika, alimwambia mume wake abadilike lakini hakusikia kabisa.

Kila mrembo wa Tanzania alitembea naye, waigizaji wa maigizo kwenye runinga alitembea nao, kila mwanamke ambaye alipata kiki, alitembea naye kitu kilichoonyesha ni kwa jinsi gani alihusudu sana kufanya mapenzi kuliko kufanya kazi aliyopewa na wananchi.

Muda huo kichwa chake kilikuwa kikimfikiria Bhoke tu, aliambiwa kuhusu msichana huyo, alikuwa mrembo mno, kusingekuwa na mwanaume yeyote ambaye angemkataa kama tu angesimama mbele yake.

Alipewa sifa nyingi za msichana huyo na hivyo alihitaji kujionea kwa macho yake ili auone uzuri huo, alifanaje, aliumbikaje na ni kwa jinsi gani alikuwa mzuri kitandani.
Pale alipokuwa kila wakati alitamani kuwasiliana naye, alizungumza na Mambili na kumwambia kuhusu msichana huyo ni kwa jinsi gani alitamani sana kuonana naye.

Hakutaka kumficha, alimwambia wazi kwama alihitaji sana kufanya naye mapenzi kwa sababu zile sifa ambazo walimmwagia zilikuwa si mchezo.

Hilo halikuwa tatizo, Mambili alimwambia ajiandae kwani tayari alimpeleka hotelini ambapo huko angekaa kwa siku moja na kwenda kuonana naye ikulu.

“Hapana! Huku asije! Yaani akija huku hatutofanya mapenzi, nipo na familia yangu,” alisema rais.

Hilo halikuwa tatizo, alimwambia usiku wa siku hiyo, majira ya saa nane alitakiwa kujiandaa na kwenda huko kama alivyokuwa akifanya hata kwa wanawake wengine.

Alichokifanya ni kumpigia simu Bhoke na kumwambia kwamba rais angekwenda hapo hotelini kuonana naye. Kipindi hicho ndicho ambacho msichana huyo alikuwa amemaliza kufanya mapenzi na kijana wa massage hivyo kumwambia hakuna tatizo.
 
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2016
Messages
104,185
Likes
294,432
Points
280
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2016
104,185 294,432 280
SEHEMU YA 38

Ilipofika majira ya saa nane, rais akaondoka ikulu na kuelekea hotelini kificho. Gari lake halikusindikizwa kwa ving’ora, ilikuwa ni siri kubwa, alikuwa na dereva wake tu na alivalia kofia kubwa aina ya Marlboro.

Hawakuchukua muda mrefu wakafika hapo hotelini. Kabla ya kutoka, kwanza akaanza kuangalia huku na kule, alitaka kuhakikisha uilinzi unakuwa wa kutosha mahali hapo na kusiwe na mtu yeyote ambaye anatakiwa kugundua kama yupo mahali hapo.

Kulipoonekana kupo salama, akateremka na dereva wake na kuanza kuelekea ndani. Ilikuwa ni vigumu kugundulika na watu wengine, alipitiliza mpaka kwenye lifti, akaingia na kuanza kuelekea juu.

Mapigo yake ya moyo yalikuwa juu, hakuamini kama alikuwa akienda kuonana na msichana huyo ambaye aliambiwa kuhusu sifa zake nyingi kwamba alikuwa mrembo, mwenye figa matata ambayo ingemtoa udenda kila mwanaume ambaye angeyapitisha macho yake kwa huyo msichana.

Alipofika kwenye floo husika, akateremka na kuufuata mlango wa chumba alichokuwepo Bhoke na kuugonga. Msichana huyo akaufungua, akashtuka mno mara baada ya macho yake kugongana na ya Rais Edmund.
“Mungu wangu!” alijikuta akisema huku akiwa na mshtuko mkubwa.
Rais akaingia mpaka ndani, akakifuata kitanda na kukaa.

Bhoke hakujiamini, alimwangalia rais, hakuamini kama alikuwa yeye, wakati mwingine alihisi kama alikuwa kwenye moja ya ndoto ya kusisimua sana. Alimsogelea na kumwangalia vizuri, alitaka kupata uhakika kama alikuwa mwenyewe ama alimfananisha.
“Unanishangaa sana mpenzi,” alisema Rais Edmund.

Macho yake yalikuwa kwa Bhoke tu, alimwangalia msichana huyo, jinsi alivyokuwa, alichanganyikiwa, vile alivyoambiwa kuhusu Bhoke alihisi kudanganywa sana kwani msichana huyo alikuwa mzuri mara ya mia ya vile alivyokuwa ameambiwa.

Alikuwa chotara wa Kizungu, mwenye nywele ndefu, figa matata na uso wake ulikuwa na tabasamu pana huku kwa nyuma akiwa na mzigo matata ambao kwa wanaume wa Pemba ama Mombasa ilikuwa ni lazima kuhonga jumba kubwa au hata shamba la minazi.
 
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2016
Messages
104,185
Likes
294,432
Points
280
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2016
104,185 294,432 280
SEHEMU YA 39

“Wewe ni mzuri sana,” alisema rais huku akimwangalia Bhoke ambaye bado hakuonekana kujiamini hata kidogo.
“Asante sana.”
“Umesema unaitwa nani?” aliuliza.
“Bhoke!”

“Oh! Nani kwenu Mzungu?”
“Baba! Ni Mjerumani!”
“Ooh! Asante kufahamu hilo!” alisema rais.

Bhoke akaomba ruhusa ya kwenda kuoga, halikuwa tatizo, alikwenda na alipofika huko akaanza kujimwagia maji.

Ni kwamba alitoka kufanya mapenzi na kijana wa massage lakini baada ya kuoga na kujisugua huku akijishika chini ya kitovu chake, mwili wake ukaanza kumshika kwa hamu tena.

Akaanza kusisimka, hamu aliyokuwanayo kipindi cha nyuma ikaanza kurudi tena. Alichanganyikiwa, alipagawa kupita kawaida na pale bafuni alipokuwa alihisi kama kulikuwa na vidudu fulani vilikuwa vikimtembelea mwilini mwake.

“Aagghh!” alijikuta akiguna baada ya mkono wake kuupitisha kwenye kifua chake.

Alishindwa kuvumilia, ulikuwa ni upumbavu kutaka kumaliza hamu yake bafuni na wakati pale chumbani kulikuwa na mwanaume.

Haraka sana akatoka na kuanza kumfuata rais pale kitandani. Kwa jinsi umbo lake lilivyojengeka, namba nane ilikuwa ikionekana vizuri kabisa kitu kilichomchanganya rais huyo ambaye tayari alibaki na boksa tu.

Bhoke akamsogelea, kitu cha kwanza alichokifanya ni kuanza kubadilishana naye mate. Rais alichanganyikiwa, hata kwenye tendo kama hilo kulikuwa na wazoefu wake na huyo Bhoke alikuwa mmoja wapo.

Ulimi wake ulipokuwa kinywani mwa rais alijua ni kwa jinsi gani alitakiwa kuutembeza, alijua ni kwa jinsi gani alitakiwa kunyonya ulimi wa mwanaume yeyote yule.

Palepale kitandani rais akachanganyikiwa, hakujua kulitokea nini lakini ghafla alijiangalia, boksa haikuwepo tena mwilini mwake, ilikuwa pembeni kabisa, ilitolewaje? Hakujua hata kidogo.

Siku hiyo alianza kufanya mapenzi na msichana huyo, usiku mnene lakini wala hakuonekana kuchoka.

Bhoke alikuwa mtaalamu, alijua dhahiri kwamba mwanaume aliyekuwa mbele yake alikuwa na madaraka, kama angetumia nguvu kubwa kuhakikisha anampagawisha basi angeweza kupata pesa nyingi na asingekuwa na matatizo yoyote yale maisha yake yote.
 
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2016
Messages
104,185
Likes
294,432
Points
280
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2016
104,185 294,432 280
SEHEMU YA 40

Tendo lilichukua saa moja lakini rais alikuwa hoi, hakuwa anajiweza, aliburuzwa kupuita kawaida na kila alipomwangalia Bhoke hakumpatia picha.

“Haya mambo umejifunza wapi?” aliuliza rais huku kijasho kikimtoka japokuwa kiyoyozi kiliwashwa.

“Nilifundwa na kufundika,” alijibu Bhoke.
“Umenichanganya sana! Nakuahidi situkuacha,” alisema rais, alipomaliza, akasimama, akaenda kuoga, alipomaliza akavaa nguo zake na kuondoka huku akiahidi kumfanyia mambo makubwa msichana huyo.

*** Johnson alifika jijini Washington DC huku lengo lake likiwa ni kwenda katika Gereza la Shelton Hill kwa lengo la kumuona Bruce.

Mwanaume huyo alikuwa mtu muhimu sana, kwake, ili kupata pesa ambazo hakujua mahali zilipokuwa ilikuwa ni lazima aonane na mwanaume huyo.

Gereza hilo halikuwa likiingiwa na watu hovyo, watu ambao walitakiwa kwenda kumtembelea mwanaume huyo walikuwa ndugu zake tu hivyo kulikuwa na ugumu wa yeye kama yeye kwenda kuonana na Bruce.

Alichokifanya ni kuwatafuta ndugu wa mwanaume huyo na kuanza kuongea nao, aliwaambia lengo lake kubwa lilikuwa ni kutaka kuonana na mwanaume huyo kwani kuna jambo moja kubwa alilotaka kuongea naye, hivyo kama wangemsaidia katika hilo angewashukuru sana.

“Ni kuhusu pesa zilipo?” aliuliza mmoja wa ndugu zake, huyo aliitwa Campbell.

Johnson akashtuka, hakutegemea kusikia hilo, akawaambia ndiyo, alihitaji kuzungumza naye kuhusu jambo hilo na hivyo ndugu hao kumwambia kwamba isingewezekana hata kidogo kulizungumzia jambo hilo kwani katika maisha yake yote ya humo gerezani, kulikuwa na watu wengi waliokuwa wakitaka kujua kuhusu hiozo pesa lakini hakuwa radhi kusema mahali zilipokuwa.

“Kwa hiyo hawezi kabisa kusema mahali zilipo?” aliuliza Johnson huku akiwaangalia ndugu hao.
“Hata kidogo!”
 
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2016
Messages
104,185
Likes
294,432
Points
280
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2016
104,185 294,432 280
SEHEMU YA 41

Majibu aliyopewa yalimnyong’onyeza sana, hakujua ni kitu gani alitakiwa kufanya.

Aliondoka hapo New York na kurudi hosteli, ilikuwa ni lazima ajipange, ajue ni kwa jinsi gani alitakiwa kupambana kuhakikisha anazungumza na mwanaume huyo na kumwambia kuhusu mahali pesa zilipo.

Kwa sababu hakuwa mwepesi kusema kuhusu jambo hilo, kitu kilichokuja kichwani mwake ni yeye mwenyewe kwenda huko gerezani, afungwe hata kwa miezi sita, wakati akiwa huko afanye kila liwezekanalo kuhakikisha anaonana na mwanaume huyo na kujenga urafiki.

“Mh! Ila hii nayo hatari sana,” alijisemea.
Dola bilioni tano kilikuwa kiasi kikubwa cha pesa, hazikuwa pesa ndogo za kuzipotezea tu, ilikuwa ni lazima apambane kuhakikisha anazipata kwa kujua mahali zilipokuwa.

Kwenda gerezani hakukuwa na tatizo ila alitakiwa kuwa na uhakika wa kuzipata pesa hizo. Kwenye hilo aliendelea kufikiria kwamba kama angekwenda huko, ni kwa jinsi gani angemlaghai mwanaume huyo kumwambia mahali pesa hizo zilipokuwa?

“Inabidi nimtumie mwanamke,” alijisemea.
Hapo, mwanamke ambaye alikuja kichwani mwake kwa haraka alikuwa Bhoke.

Alihisi kwamba alihitaji msichana ambaye alikuwa mrembo lakini ingekuwa vigumu kufanya kazi na mwanamke wa Kimarekani kwa kuwa angeweza kudhulumiwa endapo tu angegundua kwamba kulikuwa na pesa nyingi nyuma ya kila kitu kilichokuwa kikiendelea.
Kuonana na Bhoke ilikuwa ni lazima arudi nchini Tanzania.

Kama yeye angefungwa jela na kumwambia msichana huyo ajifanye kuwa ndugu yake ambaye mara kwa mara angekuwa akimtembelea hapo, je, angekuwa radhi kufanya mapenzi na Bruce ambaye angemuunganisha kwake na kumfanya kuwa demu wake?

Hapo hakupata jibu, ila cha kwanza ilikuwa ni lazima akae na kuzungumza na msichana huyo.
|
|
|

Je, nini kitaendelea?
 
Smart911

Smart911

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2014
Messages
22,189
Likes
20,630
Points
280
Smart911

Smart911

JF-Expert Member
Joined Jan 3, 2014
22,189 20,630 280
Safi sana...


Cc: mahondaw
 
S

SAW_111

Member
Joined
Aug 18, 2017
Messages
85
Likes
55
Points
25
S

SAW_111

Member
Joined Aug 18, 2017
85 55 25
SEHEMU YA 41

Majibu aliyopewa yalimnyong’onyeza sana, hakujua ni kitu gani alitakiwa kufanya.

Aliondoka hapo New York na kurudi hosteli, ilikuwa ni lazima ajipange, ajue ni kwa jinsi gani alitakiwa kupambana kuhakikisha anazungumza na mwanaume huyo na kumwambia kuhusu mahali pesa zilipo.

Kwa sababu hakuwa mwepesi kusema kuhusu jambo hilo, kitu kilichokuja kichwani mwake ni yeye mwenyewe kwenda huko gerezani, afungwe hata kwa miezi sita, wakati akiwa huko afanye kila liwezekanalo kuhakikisha anaonana na mwanaume huyo na kujenga urafiki.

“Mh! Ila hii nayo hatari sana,” alijisemea.
Dola bilioni tano kilikuwa kiasi kikubwa cha pesa, hazikuwa pesa ndogo za kuzipotezea tu, ilikuwa ni lazima apambane kuhakikisha anazipata kwa kujua mahali zilipokuwa.

Kwenda gerezani hakukuwa na tatizo ila alitakiwa kuwa na uhakika wa kuzipata pesa hizo. Kwenye hilo aliendelea kufikiria kwamba kama angekwenda huko, ni kwa jinsi gani angemlaghai mwanaume huyo kumwambia mahali pesa hizo zilipokuwa?

“Inabidi nimtumie mwanamke,” alijisemea.
Hapo, mwanamke ambaye alikuja kichwani mwake kwa haraka alikuwa Bhoke.

Alihisi kwamba alihitaji msichana ambaye alikuwa mrembo lakini ingekuwa vigumu kufanya kazi na mwanamke wa Kimarekani kwa kuwa angeweza kudhulumiwa endapo tu angegundua kwamba kulikuwa na pesa nyingi nyuma ya kila kitu kilichokuwa kikiendelea.
Kuonana na Bhoke ilikuwa ni lazima arudi nchini Tanzania.

Kama yeye angefungwa jela na kumwambia msichana huyo ajifanye kuwa ndugu yake ambaye mara kwa mara angekuwa akimtembelea hapo, je, angekuwa radhi kufanya mapenzi na Bruce ambaye angemuunganisha kwake na kumfanya kuwa demu wake?

Hapo hakupata jibu, ila cha kwanza ilikuwa ni lazima akae na kuzungumza na msichana huyo.
|
|
|

Je, nini kitaendelea?
Umetisha mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
K

kisukari

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2010
Messages
4,104
Likes
1,533
Points
280
K

kisukari

JF-Expert Member
Joined Jul 16, 2010
4,104 1,533 280
Hii hadithi inanisikitisha kidogo. Maybe bhoke atabadilika. Maana mama alikuwa malaya mwisho mtoto na yeye akamzidi mama
 

Forum statistics

Threads 1,249,898
Members 481,140
Posts 29,714,308