Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,746
- 25,672
MIMI NI MWENYE DHAMBI, NISAMEHE MUNGU 1
MTUNZI: NYEMO CHILONGANI
SIMU: 0718 069 269
MAHALI: DAR ES SALAAM
INSTAGRAM: nyemochilongani
Mwenyekiti wa Chama cha Vijana cha Casfeta (Christian Ambassador Students Fellowship Tanzania), Samuel Mpelele alikuwa akiendelea kuhubiri katika mkutano wa Injili uliokuwa ukifanyika katika Uwanja wa mpira wa Chekereni.
Huo ulikuwa mkutano wa Injili ulioandaliwa na vijana waliookoka mkoani Kilimanjaro. Watu walikuwa kimya uwanjani hapo huku wakimsikiliza Samuel ambaye alikuwa akitiririka jasho jingi huku akiendelea kuhubiri mahali pale.
Kila mtu alikuwa akiingiwa na maneno yale ambayo alikuwa akiyaongea katika mkutano ule kwa kutumia kipaza sauti kilichoonganishwa na spika kadhaa zilizokuwa katika uwanja huo. Samuel alionekana kujawa na nguvu za Mungu, kadiri alivyokuwa akihubiri na ndivyo ambavyo watu walizidi kupiga makofi huku wengine wakianza kulia.
Huo ulikuwa ni mkutano wa pili kuandaliwa na wanafunzi wa Chama cha Casfeta mkoani Kilimanjaro, mkutano ambao ulikuwa ukiongozwa na mwenyekiti wa chama hicho mkoani hapo, Samuel Mpelele, mwanafunzi aliyekuwa akisoma katika shule ya Uhuru hapo Kilimanjaro. Watu waliokuwa wakimsikiliza ambao hawakuwa wameokoka, siku hiyo wakaokoka kwani maneno ambayo alikuwa akiongea mahali pale yalionekana kumgusa kila mmoja.
Samuel Mpelele alikuwa mtoto wa mchungaji Christopher Mpelele wa Kanisa la Praise and Worship lililokuwa Mwenge jijini Dar es Salaam. Kwa sababu alizaliwa katika familia iliyomjua Mungu, familia iliyomcha Mungu, Samuel akajikuta akimuabudu Mungu maishani mwake huku wazazi wake wakiwa muongozo mkubwa katika maisha yake.
Mara nyingi Samuel alikuwa akielekea kanisani na kumuona baba yake akihubiri, moyoni alifurahi kupita kawaida, nae akaanza kujisikia msukumo wa kufanya kama ambavyo baba yake alivyokuwa akifanya kila alipokuwa madhabahuni. Katika kipindi hicho, kumuona mtu akiwa anahubiri ndicho kilikuwa kitu ambacho kilikuwa kikimfurahisha mno maishani mwake.
Maisha ya Samuel yakawa ni kwenda kanisani na kumuomba Mungu aweze kuonekana katika maisha yake tu. Moyoni mwake alikuwa akijisikia wito kabisa kwamba nae alitakiwa kuwa kama baba yake kuhubiri madhabauni.
Mchungaji Mpelele tayari aliiona karama ya uhubiri aliyokuwa nayo mtoto wake, alichokifanya ni kuanza kumpa ushirikiano katika kila kitu juu ya karama ambayo alikuwa nayo.
Huo ulikuwa ni wakati ambao Samuel alikuwa darasa la saba, alipomaliza shule, matokeo yake hayakuwa mazuri na hivyo kupelekwa katika shule ya Sekondari ya Uhuru iliyokuwa mkoani Kilimanjaro. Huko, Samuel akajiunga katika Kikundi cha Casfeta, kikundi kilichoanza kumuweka karibu na watu wengi ambao walikuwa wakimuabudu Mungu katika maisha yao shuleni pale.
Shule hiyo ilikuwa ni ya mchanganyiko, kulikuwa na wanafunzi ambao hawakwenda kanisa na wala hawakujua makanisa yalikuwa sehemu gani, kuna wanafunzi wengine ambao walikuwa wakielekea kanisani kila siku katika maisha yao lakini hawakuweza kubadilika, bado walikuwa wakiendelea kuvuta sigara na kunywa pombe pamoja na kufanya starehe za aina mbalimbali.
Ukiachana na hao, kulikuwa na Waislamu ambao wengi wao hawakuwa wakienda msikitini, tena mbaya zaidi wengine wakiwa watoto wa maustadhi wakubwa katika mikoa waliyotoka.
Wao pamoja na watoto wa wachungaji na viongozi wa makanisa mengine ndiyo waliokuwa wakiongoza kwa fujo na tabia chafu shuleni hapo.
Ukiachana na hao, kulikuwa na wanafunzi wengine waliokuwa Waislamu safi. Walikuwa wakielekea misikitini kuswali swala tano. Maisha yao yalikuwa tofauti na maisha ya watu wengine, walikuwa wakiishi kipole sana, hawakuwa wagomvi, walimheshimu kila mtu, kila wakati, walikuwa wakiongea maneno ya dini huku wakiwataka hata watu wengine wabadilike na kumuabudu Allah.
Kwa kifupi, shule ile ilikuwa na watu waliochanganyika ila kwa watoto wa wachungaji na maustadhi ndio ambao walikuwa wakiongoza kwa maovu shuleni pale.
Wao hawakupenda dini, walijiona kuzaliwa katika familia ambazo zilikuwa zikiijua dini, hivyo nao wakajiona kuwa hata kama wasingekwenda kanisani au msikitini, maisha yao yalikuwa na ulinzi wa kutosha.
Walimu hawakuyapenda maisha waliyokuwa wakiishi vijana hao, mara kwa mara walijitahidi sana kuwarekebisha lakini maneno yao hayakusaidia chochote kile, bado vijana hao waliendelea kuwa hivyohivyo.
Shule nzima, watoto wa viongozi wa dini ndio waliokuwa wakitenda yale waliyotakiwa kuyatenda kama wazazi wao. Kwa upande wa dini ya kikristo alikuwepo Samuel au Sam kama alivyojulikana, mtoto wa mchungaji wa Kanisa la Praise and Worship lililokuwa Mwenge jijini Dar es Salaam pamoja na Sadiki Hamidu, mtoto wa Ustadhi Hamidu ambaye alikuwa imamu katika msikiti wa kichangani uliokuwa Magomeni jijini Dar es salaam.
Wawili hao ndiyo waliokuwa mifano mizuri ya kuigwa shuleni hapo huku walimu wakiwataka wanafunzi wote kuishi maisha kama jinsi watu hao wawili walivyokuwa wakiishi. Wanafunzi hawakuonekana kuelewa, kila siku walikuwa wakivuta bangi huku matendo ya ngono yakiwa ya hali ya juu kupita kawaida.
“Inasikitisha sana Sadiki kila ninapowaona vijana wenzangu wa Kikristo wakiwa wanafanya matendo machafu kama wafanyayo,” Samuel alimwambia Sadiki huku akionekana kuwa na huzuni.
“Wewe ni kama mimi Samuel. Waislamu tunatakiwa kuswali swala tano kwa siku na kufuata nguzo tano za Kiislamu lakini wenzangu hawataki kufuata kama Allah anavyotaka tufanye. Inaniuma sana Samuel,” Sadiki alimwambia Samuel kwa sauti ya unyonge. Wawili hao walikuwa pamoja japokuwa walikuwa viongozi wa dini tofauti. Wao ndio waliokuwa chachu kubwa ya kuwafanya watu waliokuwa na dini tofauti kuwa pamoja zaidi.
Shuleni hapo hakukuwa na mitafaruku ya kidini, hakukuwa na mtu ambaye alikuwa akiidharau dini ya mwenzake, kila mtu alijiona sawa na mwenzake mbele za Mungu. Bado Samuel alikuwa akiendelea kuhubiri, watu walionekana kumkubali kupita kawaida, kila wakati watu walikuwa wakitikisa vichwa vyao kuonyesha ni jinsi gani walikuwa wakimkubali Samuel aliyekuwa akiendelea kuhubiri. Mara baada ya mkutano kumalizika, akawaita watu ambao walitaka kufanyiwa maombezi, akawafanyia maombezi na mkutano kufungwa.
Hayo ndio yalikuwa maisha yake shuleni hapo. Kila siku alikuwa akimuabudu Mungu na kumuomba usiku na mchana, alimtegemea Mungu zaidi ya alivyowategemea wazazi wake katika maisha yake.
Taaluma yake darasani wala haikuwa mbaya, ilikuwa ikiridhisha sana kiasi kilichomfanya kuwa miongoni mwa wanafunzi kumi ambao walikuwa wakifanya vizuri shuleni hapo.
“Unapaswa kubadilisha maisha yako na kumfuata Yesu Kristo Catherine,” Samuel alimwambia Catherine, msichana aliyekuwa akimuoneshea hisia za kimapenzi toka zamani shuleni hapo.
“Nimeshindwa mchungaji. Nimeshindwa kabisa,” Catherine alimwambia Samuel kwa sauti ya chini iliyosikika kimahaba.
“Kwa nguvu zako kamwe hautoweza. Muache Mungu ayabadilishe maisha yako. Unapoelekea si sehemu ambayo Yeye anataka wewe uende,” Samuel alimwambia Catherine.
“Kwa hiyo nifanye nini mchungaji?”
“Muombe sana Mungu akubadilishe.”
“Na kama nikishindwa kubadilika?”
“Mungu ashindwi kitu au labda uwe haujaamua moyoni mwako. Ukiamua, Mungu ashindwi kitu chochote katika maisha yako,” Samuel alimwambia Catherine.
Hayo ndio yalikuwa maneno ambayo kila siku Samuel alikuwa akimwambia Catherine juu ya maisha yake. Catherine alikuwa akijitahidi sana kuishi katika maisha ya kutotenda dhambi lakini bila kulazimishwa, mara kwa mara alijikuta akitenda dhambi.
Kuna kipindi kikafika, Catherine akajiona kushindwa kabisa kuuzuia moyo wake hasa pale ulipoamua kumuingiza Samuel. Akazidi kumpenda mvulana huyo na kumhitaji kupita kawaida. Japokuwa Catherine alikuwa akijua fika kwamba alikuwa akimpenda Samuel lakini aliogopa kumfuata na kumwambia ukweli juu ya mapenzi aliyokuwa nayo juu yake, hivyo akaamua kubaki na dukuduku moyoni mwake.
Siku zikaendelea kukatika mpaka kufika kipindi ambacho Catherine akajiona kushindwa kujizuia kabisa, akaona hakuwa na jinsi na wala asingeendelea kubaki kimya, hivyo akaamua kumfuata Samuel kwa lengo la kumwambia ukweli bila kujali Samuel angemchukuliaje.
“Unasemaje?” Samuel aliuliza huku akionekana kutokuamini.
“Ninakupenda mchungaji.”
“Ndio maana kila siku nakwambia muombe sana Mungu kama unataka ayabadilisha maisha yako. Bila Yesu ni kazi bure maishani mwako Catherine,” Samuel alimwambia Catherine.
“Nakupenda Samuel.”
“Hilo ni pepo. Njoo kwenye ibada yetu ya maombezi saa kumi jioni uje uombewe. Hilo ni pepo la uzinzi,” alisema Samuel, muda huo walikuwa darasani.
Samuel hakuridhika, alichokifanya ni kumfanyia maombi Catherine. Hiyo wala haikubadilisha kitu chochote kile, bado moyo wa msichana huyo ulikuwa kwenye mapenzi kwa Samuel.
“Ninashindwa Samuel,” alisema Catherine baada ya maombi.
“Unashindwa nini?”
“Kuacha kukupenda.”
“Haiwezekani. Haujataka kumruhusu Yesu kuingia moyoni mwako Catherine.”
“Nimemruhusu ila bado ninakupenda. Kadiri siku zinavyozidi kwenda mbele nazidi kukupenda Samuel,” Catherine alimwambia Samuel kwa sauti ya chini iliyojaa mahaba.
“Ngoja niendelee kukufanyia maombi” Samuel alisema huku akisimama.
“Ila usiniguse tena. Nifanyie maombi hivi hivi bila kunigusa” alisema Catherine, Samuel akashangaa.
“Kwa nini?”
“Unaponigusa......”
“Kuna nini?”
“Nasikia vijidudu vikinitembelea mwilini mwangu. Mwisho wa siku napata tabu hasa niwapo kitandani peke yangu usiku,” alisema Catherine.
Samuel akanyamaza kwa muda na kuanza kumwangalia Catherine usoni, uso wa Samuel ukaonekana kubadilika kama mtu ambaye alikuwa akimuona kiumbe fulani cha ajabu machoni mwake. Alichokifanya ni kuanza kumfanyia maombi Catherine bila kumgusa kama ambavyo alivyotaka iwe.
Hayo ndio yalikuwa maisha ambayo yaliendelea shuleni hapo, bado Catherine alionekana kuwa karibu na Samuel, kila siku alikuwa akitaka kufanyiwa maombi na Samuel lakini kamwe hakuweza kubadilika. Moyo wake ulionekana kuwa mgumu kubadilika, hakumruhusu Mungu kuubadili moyo wake, mapenzi yalikuwa yakimtesa kupita kawaida.
“Vipi mchungaji?” Sadiki alimuuliza Samuel katika kipindi ambacho alikuwa akionekana kuwa na mawazo.
“Mungu anahitajika sana kuyabadilisha maisha ya wanafunzi shuleni hapa. Kuna wengine wanatumiwa na shetani katika kutujaribu watumishi wa Mungu. Ila kamwe tutasimama imara” Samuel alimwambia Sadiki.
“Umekwishajaribiwa?” Sadiki alimuuliza.
“Ndio. Kuna yule msichana Catherine huwa kila siku anakuja, ishu yake ileile, nimfanyie maombi ila moyo wake hajauweka tayari kumpokea Yesu” Samuel alimwambia Sadiki.
“Pole sana ndugu yangu ila maisha yako hayatofautiani na mimi,” Sadiki alimwambia Samuel.
“Kwa nini?”
“Unamjua yule Mariamu msichana tunayesoma nae kidato cha tatu?” Sadiki aliuliza.
“Mariamu yupi? Wapo watatu darasani.”
“Yule mweupe.”
“Ninamfahamu.”
“Huwa kila siku ananitaka, mara kwa mara ananiandikia barua za kimapenzi,” Sadiki alimwambia Samuel.
“Mungu wangu!”
“Ndio hivyo. Jana tu alikwenda kuninunulia kanzu mpya pamoja na kofia kama zawadi” Sadiki alimwambia Samuel.
“Haya ni majaribu na inapaswa tuyashinde. Mungu wetu hashindwi” Samuel alimwambia Sadiki.
“Ndio hivyo. Ninapenda niendelee kumcha Allah katika maisha yangu. Sipendi kumpa ibilisi ruhusa ya kuyachezea maisha yangu. Namcha Allah si kwa sababu wazazi wangu wanamcha Allah, hapana, ninamcha Allah kwa sababu ninatakiwa kumcha Allah kwani Yeye ndiye muongozo wa maisha yangu” Sadiki alimwambia Samuel.
Hayo ndio yalikuwa majaribu yao ya kila siku. Mara kwa mara wasichana hao walionekana kama kutumwa na shetani kwa ajili ya kuwajaribu katika maisha yao. Japokuwa walikuwa wakiwaepuka sana lakini kila siku walimuomba Mungu aweze kuwashindia katika vita hivyo ambavyo kwao vilionekana kuwa vigumu sana, walihitaji msaada wa Mungu kuyashinda majaribu hayo ambayo kwao yalionekana kuwa makubwa zaidi ya uwezo wao.
Je, nini kitaendelea?