Hadithi : Mcheza Filamu Za Ngono

Hadithi : Mcheza Filamu Za Ngono

MCHEZA FILAMU ZA NGONO 7.

Miaka saba ilikuwa imekwenda sana tangu kipindi kile ambacho mvulana Daniel alipokuwa ameangukia katika mapenzi ya msichana Katie katika kipindi kile ambacho walikuwa wakiishi mitaani. Katika kipindi hiki hakuwa nchini Marekani tena, alikuwa akitembea katika nchi mbalimbali kama baharia ambaye alikuwa akifanya kazi katika meli kubwa ya Metropoza iliyokuwa ikizunguka sehemu mbalimbali duniani.
Picha za Katie alikuwa akiziangalia mara kwa mara, alimkumbuka sana msichana huyo kutokana na uzuri mkubwa ambao alikuwa nao, alimkumbuka kwa kila kitu japokuwa alijua fika kwamba msichana huyo kwa sasa alikuwa akiigiza filamu za ngono ambazo zilikuwa zikimuingizia fedha za kutosha.
Alikuwa amefanya kazi ya ubaharia kwa miaka zaidi ya saba, uzoefu wake mkubwa ambao alikuwa nao Daniel ndio ambao uliwafanya hawa nahodha wa meli hiyo kumpa uongozi huku akimlipa kiasi kikubwa cha fedha.
Daniel alikuwa akiyakumbuka vizuri maisha yake ya nyuma ambayo alikuwa ameishi zamani, yalikuwa maisha ya shida ambazo kila siku zilikuwa zikimpelekea kutafuta fedha maishani mwake pasipo kujali ni aina gani ya shida ambazo angeweza kukutana nazo.
Maishani mwake alipenda sana maendeleo, alitamani pia kuwa na msichana Katie ambaye alikuwa akimfahamu toka walipokuwa wadogo, wakicheza wote na kufanya mambo mengi pamoja. Katika kipindi kile, japokuwa Katie alikuwa akijitahidi kutokumuonyeshea mapenzi ya wazi lakini Daniel alikuwa na uhakika wa asilimia mia moja kwamba msichana yule alikuwa akimpenda sana.
Kwake, kitendo cha Katie kujiunga na uigizaji wa filamu za ngono ukaonekana kumuumiza sana lakini hakujua ni kitu gani ambacho alikuwa akitakiwa kukifanya zaidi. Kama kumshauri, alikuwa amemshauri sana lakini Katie hakuonekana kubadilika.
Daniel alikuwa na uhakika kwamba katika kipindi hicho Katie hakuwa akikumbuka kitu chochote kile ambacho kilikuwa kimepita katika maisha yao. Ingawa alikuwa akiendelea kufanya kazi ya ubaharia lakini akili yake wala haikuacha kumfikiria Katie ambaye kadri siku zilivyozidi kwenda mbele ndivyo alikuwa akiendelea kunawili.
Kwa kipindi hiki, Daniel alikuwa mnyonge sana japokuwa alikuwa na kiasi kikubwa cha fedha, maisha yake katika kipindi hiki hayakuwa nchini Marekani tena, alikuwa akiishi nchini Uingereza katika jiji la Newcastle ambako huko alikuwa amenunua nyumba kubwa na ya kifahari.
Fedha ambazo alikuwa amezipata katika ubaharia wake ndizo ambazo akaamua kufungulia mghahawa ambao ulikuwa ukitumiwa sana na wachezaji wa mpira wa klabu ya Sunderland ambao walikuwa wakifika sana mahali hapo kwa ajili ya kupata kifungua kinywa na hata chakula cha jioni hasa mara baada ya kutoka mazoezini.
Ingawa maisha ya Uingereza hakuyapenda sana kutokana na baridi lakini akaamua kuvumilia tu. Kwake alijiona kuwa mtafutaji ambaye alitakiwa kukaa sehemu yoyote ile katika dunia hii mpaka pale ambapo angebadilisha maisha yake na kuishi kama tajiri mmoja mkubwa nchini hapo na kurudi nchini Marekani na kununua nyumba na maisha ya kifahari kuanza rasmi.
Maisha ya Daniel yalikuwa yamelenga mambo mengi sana, hakutaka kutumia fedha zake vibaya, alikuwa akiishi nchini Uingereza kama mgeni tu na hivyo kuna siku angehitaji kurudi nchini kwake. Kutokana na kuanza kuingiza fedha nyingi, wasichana mbalimbali wa hapo Newcastle walikuwa wakipenda kumfuatilia kwa lengo la kuwa nao lakini Daniel hakukubaliana nao, kazi yake ilikuwa ni kutembea nao kwa zamu na kuwaacha tu.
Maishani mwake hakutaka kuwa na msichana yeyote yule zaidi ya Katie ambaye bado alikuwa akiigiza filamu za ngono kama kawaida yake. Miezi ikakatika na ndipo hapo Daniel aipojiona kuwa na utayari wa kurudi nchini Marekani kwa ajili ya kuendelea na maisha katika nchi hiyo huku tayari akiwa ameingiza zaidi ya kiasi cha paundi milioni tano.
Kitu cha kwanza mara baada ya kufika nchini Marekani ni kuanza kufungua biashara nyingi ambazo zilionekana kumuingizia fedha na kisha kuanza kumtafuta Katie simuni. Msichana huyo hakuwa akipatikana kabisa jambo ambalo lilimfanya kuendelea kumtafuta zaidi na zaidi. Ingawa alikuwa akiiangalia mikanda ya filamu ya Katie ambayo alikuwa akiigiza akifanya mapenzi na wanaume mbalimbali lakini bado alikuwa akihitaji kuwa nae katika maisha yake.
Baada ya kipindi kirefu kupita, Daniel akaja kupata taarifa ambayo ilionekana kumshtua sana, taarifa ambayo ilimfanya kuchanganyikiwa kupita kawaida. Katie alikuwa akitarajia kufunga ndoa, aliuhisi moyo wake ukichomwa na msumali wa moto na kisha tundu hilo kumwagiwa tindikali.
Hakuziamini taarifa zile jambo ambalo likamfanya kutembelea katika website ya Katie na kuangalia. Kile ambacho alikuwa amekioa katika magazeti mbalimbali nchini Marekani kilikuwa sawa sawa na kile ambacho alikuwa amekikuta katika website ile.
Daniel akajiona akikosa nguvu kabisa, akaanza kupiga hatua kuelekea katika kochi na kisha kutulia. Mawazo yakaanza kumuandama kichwani mwake. Katika maisha yake, hakuona kama kulikuwa na mtu ambaye alitakiwa kumuoa Katie na kuishi nae tofauti na yeye, jambo lile likaonekana kumtia hasira sana.
Alichokifanya ni kuanza kupeleleza juu ya mwanaume ambaye alikuwa akitarajiwa kufunga ndoa na Katie. Alijitahidi kumtafuta zaidi na zaidi lakini hata picha yake akashindwa kuipata mpaka siku ya harusi ilipofika na watu hao kufunga ndoa.
Daniel akaonekana kuchanganyikiwa zaidi, alijua fika kwamba ndoto zake za kutaka kuishi na Katie hapo baadae zilitakiwa kufutika kunzia muda huo. Kila siku alikuwa akishinda chumbani akilia huku picha za Katie ambazo alipiga nae kipindi cha nyuma walipokuwa mitaani utotoni zikiwa mikononi mwake.
Mapenzi yake yalikuwa makubwa kwa Katie, alimpenda sana kuliko msichana yeyote katika dunia hii. Alimuona kuwa msichana ambaye alihitaji thamani kubwa sana katika maisha yake. Hakuwa radhi kuwa na msichana mwingi, msichana ambaye alikuwa akimpenda na kumhitaji alikuwa Katie tu.
Alipokuja kuiona picha ya Gibson kwamba ndiye alikuwa mume halali wa Katie, Daniel akapigwa na mshangao. Kwanza akaanza kumwangalia vizuri Gibson huku akijaribu kujilinganisha nae, hakuwa akifanana na Gibson hata kidogo.
Hapo hapo akaanza kumchukia Gibson, hakujali kama Katie ndiye ambaye alikuwa amemtongoza Gibson na hatimae kuoana, yeye alichokuwa akikijali kwa wakati huo ni kuendelea chuki kwa Gibson tu huku ngozi ya Gibson kuwa nyeusi ndicho kilikuwa kitu ambacho kilimkasirisha zaidi na zaidi.
Daniel hakuwa radhi kumuona Gibson akila raha pamoja na mwanamke ambaye alikuwa akimpenda tangu utotoni, hakuwa radhi kuona Gibson akila raha na msichana ambaye alikuwa amefanya nae mapenzi sana mitaani, hakuwa radhi kuona Gibson akila raha na msichana ambaye alikuwa akiishi nae kwa karibu zaidi ya mtu yeyote, kitu alichokuwa akikitaka kwa wakati huo ni kuyarudisha mapenzi ambayo yalikuwa yamepotea na kusahaulika tu.
Hakukuwa na njia nyingine zaidi ya kuyarudisha mapenzi ya Katie kwake zaidi ya kufanya kitu kimoja tu, cha kumuua Gibson. Aliamini kwamba kama asingefanya hivyo, basi kwake lingekuwa jambo gumu sana kuweza kumpata Katie ambaye alionekana kuwa kwenye mapenzi mazito na mwanaume huyo.
Alichokifanya ni kuanza kuandaa mipango kabambe, mipango ambayo ingemmaliza Gibson na kisha kumsahaulisha katika kichwa cha Katie na baada ya hapo angeweza kumfuata Katie na kumwambia juu ya jinsi alivyokuwa akiendelea kujisikia ndani ya moyo wake, amkubalie, amuoe na hatimae kutimiza ndoto yake ambayo alikuwa akiiota kila siku.
Alichokifanya ni kuwakodisha vijana ambao walitakiwa kuucheza mchezo ule kwa makini sana bila kukosea sehemu yoyote ile. Vijana wakakubaliana nae kwa malipo makubwa ambayo wala hayakuonekana kuwa tatizo kwa Daniel ambaye kwa kipindi hicho alikuwa na fedha za kutosha.
Sehemu ambayo ilitakiwa Gibson auawe ilikuwa ni Texas, jiji ambalo kwa kiasi fulani lilionekana kuwa kama jangwa. Kila kitu kikapangwa, vijana wakaomba siku mbili za kujiandaa na hatimae baada ya hapo kukamilisha kila kitu.
“Kwa hiyo baada ya kumteka tumuue au tukusubirie wewe umuue?” Kijana mmoja alimuuliza Daniel.
“Nataka kumuua mimi mwenyewe. Tena kwa mkono wangu” Daniel aliwaambia.
“Sawa sawa. Usijali. Tutakamilisha kila kitu” Kijana yule alimwambia Daniel na kisha kuondoka.
*****
Maisha ya mapenzi bado yalikuwa yakiendelea kama kawaida kwa wapendanao, Gibson na Katie. Walikuwa na ukaribu mkubwa sana huku kila siku wakiwa wanatawala vyombo vya habari nchini Marekani. Bila kupenda, Gibson akaanza kuwa maarufu nchini Marekani jambo ambalo lilimpelekea kuanza kujulikana kila sehemu hasa katika nchi nyingine.
Bado malengo yake yalikuwa ni yale yale, kwa msichana Katie, kitu ambacho alikuwa akikihitaji ni kupata fedha tu. Alikuwa amekwishagundua kwamba Katie alikuwa na fedha nyingi, hivyo alijitahidi kuonyesha kila kitu hasa mapenzi ya dhati ili mwisho wa siku apate kile ambacho alikuwa amekipanga kukipata.
Katie akaonekana kuanza kubadilika, akajifanya kuacha kuigiza filamu za ngono jambo ambalo likaonekana kuwakasirisha watu wengi nchini Marekani ambao walikuwa na kiu ya kutaka kumuona akiigiza filamu zile.
“Sasa tufanye nini?” Bwana Donald, mkurugenzi wake alimuuliza.
“Nitakuwa nikiigiza kama kawaida” Katie alijibu.
“Sasa akiziona itakuwaje?”
“Usihofu. Nitakuwa namwambia kwamba hizo zilikuwa filamu za zamani ambazo zilikuwa zimekwishatengenezwa hata kabla ya kukutana nae” Katie alijibu huku akitabasamu.
“Utaweza kweli kumshawishi hadi akubaliane nawe?”
“Ndio. Mwanamke atabakia kuwa mwanamke, hatosema kitu chochote kwa mwanamke, atakubaliana nami tu” Katie alijibu.
Alichokifanya baada yakufika nyumbani ni kumsubiri Gibson atoke kazini na ndipo hapo alipomwambia kila kitu kilichokuwa kinaendelea. Japokuwa Gibson alijifanya kuumia lakini akakubaliana nae jambo ambalo lilimfanya Katie kumpa mapenzi moto moto.
“Au tufanye kitu kimoja ili kukupa uhuru” Gibson alimwambia Katie.
“Kitu gani?”
“Wewe igiza tu filamu zako. Ila nataka kukuwekea sharti moja tu” Gibson alimwambia Katie.
“Sharti gani?”
“Hakikisha cd hizo hazionekani machoni mwangu. Yaani kama ukitaka kuziangalia ziangalie kwa siri. Umenielewa mke wangu?” Gibson alimuuliza Katie.
“Nimekuelewa mpenzi na ninashukuru kwa ruhusa yako. Nakuhakikishaia kila kitu kitakuwa kama ulivyoniambia” Katie alimwambia Gibson ambaye akili yake ilikuwa ikifikiria fedha tu na huku akiwa ameshaanza kutuma fedha kisiri katika akaunti yake iliyokuwa nchini Tanzania.
******
Vijana watatu wakajipanga vilivyo huku lengo lao katika kipindi hicho likiwa ni kukamilisha kazi ambayo walikuwa wamepewa na Daniel ya kumteka Gibson na kisha kumpeleka sehemu ya siri ambako huko wangempigia simu bosi wao na kisha kumueleza kila kilichoendelea.
Wakaandaa bunduki zao, walikuwa wamejiandaa na utekaji nyara ambao mara kwa mara ulikuwa ukifanyika sana nchini Marekani hasa kwa watoto wa watu wenye fedha na watekaji hao kudai kiasi kikubwa cha fedha.
Walichokuwa wameelekezwa ni mahali ambapo kulikuwa na uwezekano wa Gibson kupatikana na kisha kumpeleka sehemu yoyote ile ambayo kusingekuwa rahisi kwa Katie kuweza kuwasiliana nae mpaka pale atakapouawa na mkono wa Daniel.
Mipango ilikuwa imekamilika kabisa, saa 4:18 asubuhi, gari aina ya Mc Lloyd lilikuwa limesimama mbali kidogo na nyumba kubwa aliyokuwa akiishi Katie na Gibson katika mghahawa mmojawapo wa Mc Donald. Vijana wale waliendelea kusubiri zaidi na zaidi huku kengo lao likiwa ni kutaka kumuona Gibson akitoka ndani ya nyumba ile kwa ajili ya kufanya kile ambacho walikuwa wametumwa.
Saa 6:24, gari ndogo aina ya Ferrari yenye viti viwili ikaanza kutoka ndani ya nyumba ile. Vijana wale wakatoka katika mghahwa ule na moja kwa moja kulifuata gari lao na kuingia ndani. Wakaanza kulifuatilia gari lile kwa mwendo wa taratibu uliojaa angalizo kubwa.
Bunduki zao zilikuwa tayari, walikuwa wamejiandaa kwa kitu chochote kile ambacho kingetokea mahali hapo, kitu ambacho kingewafanya kutofanikisha mpango ambao walikuwa wameupanga kuufanya kwa wakati huo.
Waliendelea kulifuata gari lile la kifahari mpaka lilipoingia katika duka moja kubwa la nguo ambalo lilikuwa likitumika sana na masupastaa au na watu ambao walikuwa na fedha nyingi na za kutosha. Vijana wale hawakutaka kuingia, wakasubiri nje huku wakiwa garini mwao.
Muda ulikuwa ukizidi kwenda zaidi na zaidi lakini hakukuwa Gibson na Katie hawakuweza kutoka ndani ya duka lile, waliendelea kusubiri zaidi na zaidi na baada ya dakika arobaini na tano, wakawa wanatoka huku mikononi mwao wakiwa na mifuko miwili mikubwa ambayo waliipeleka ndani ya gari lao na kisha kuingia na kuanza kuondoka mahali hapo.
Vijana wale hawakutaka kusubiri mahali hapo, walichokifanya ni kuanza kuwafuatilia kwa mara nyingine tena. Waliendelea kuwafuatilia zaidi na zaidi mpaka kufika katika barabara ya mtaa wa Vikingstone ambako hakukuwa na magari mengi kabisa na kisha kulipita gari lile na kulisimamisha gari lao mbele na kuteremka kwa kasi ya kikomandoo.
Katie ambaye alikuwa katika usukani alibaki akiwa amepigwa na mshangao mkubwa ulioambatana na mshtuko, hakuonekana kufahamu ni kitu gani ambacho kilikuwa kinaendelea mahali hapo, hata kabla hajajua afanye kitu gani, vijana wale wakawa wamekwishalifikia gari lile na kuvivunja vioo vya dirishani kwa kutumia vitako vya bunduki zao.
Hawakutaka kuuliza kitu chochote kile, kutokana na kutokuwa na uwepo wa watu katika barabara ya mtaa ule wa kifahari iliwafanya kuwa na uhuru mkubwa wa kuwafanya chochote walichotaka kufanya. Mara ya kwanza Gibson alitaka kuonyesha ubabe lakini alipoziona bunduki mbele ya macho yake, akatulia.
Wakateremshwa garini mule na kisha kupelekwa katika gari lile walilokuja nao vijana wale na kisha safari ya kuelekea katika sehemu ambayo walitakiwa kuwapeleka kuanza kwa wakati huo. Muda wote Gibson na Katie walikuwa wakitetemeka kwa hofu, watu ambao walikuwa nao ndani ya gari lile walionekana kuwa watu wenye roho mbaya ambao muda wote walikuwa wakinuka damu.
Gari likachukua barabara ya Melville 46 na kisha kuanza kuelekea katika mji wa Baldwin huku lengo lao kubwa katika kipindi hicho ni kwenda kwenye jiji la Texas ambalo lilikuwa katika upande wa mashariki wa jiji hilo la New York karibu kabisa na mji wa Greenvale.
Mwendo wa gari lao haukuwa wa kasi sana, walikuwa wakizihofia kamera za barabarani ambazo zingewafanya kuwafuatilia zaidi endapo mwendo wao ungeonekana kuwa wa kasi zaidi tofauti na magari mengine. Waliendelea na safari ile kwa muda wa dakika kumi na ndipo hapo walipochukua barabara ya magari yaendayo kasi ya Hoy Hills huku wakiwa na dakika thelathini kabla ya kufika katika jiji la Texas.
Muda wote huo, hakukuwa na mtu ambaye aliufungua mdomo wake, wote walikuwa kimya kabisa ndani ya gari lile. Katie alitamani kuuliza juu ya kitu ambacho kilikuwa kinaendelea mahali hapo lakini hakupewa jibu lolote lile zaidi ya wote kupewa onyo la kutokuongea kitu chochote kile.
Huku gari likiendelea kwa mwendo wa kasi ya zaidi ya kilometa themanini kwa saa, simu ya kijana mmoja katika ya vijana wale watatu ikaanza kuita
“Mko wapi?” Sauti ya Daniel iliskika.
“Tupo katika barabara ya Hoy Hills” Kijana yule alijibu.
“Mko nae hapo?”
“Ndio. Tupo nao wote”
“Ina maana hadi Katie?” Dany aliuliza huku sauti yake ikisikika kujaa mshangao.
“Ndio bosi’
“Hapana. Huyo msichana simuhitaji kabisa. Mshusheni arudi zake. Ila mshusheni katika sehemu ambayo hamtoonekana kirahisi” Daniel alisema.
Kila kitu ambacho Daniel alikuwa ameamuru kwa wakati huo ndicho ambacho kilitakiwa kufanyika kwa haraka sana, tena bila ya kuulizwa swali lolote lile. Gari lilipofika katika kituo cha mafuta, Katie akateremshwa na kisha kuanza kupelekwa bafuni ambako kijana mmoja alikuwa pembeni yake akiigiza kuwa kama mpenzi wake ili kuwaondoa wasiwasi watu wachache ambao walikuwa wakipishana nao.
Walipofika chooni, Katie akafungwa kamba katika bomba la maji na kisha kijana yule kurudi garini na kuendelea na safari yao huku Gibson akizidi kutetemeka kadri muda ulivyokuwa unazidi kwenda mbele.
Baada ya dakika zaidi ya arobaini wakaingia katika jiji la Texas ambalo lilikuwa likionekana kuwa kama jangwa. Jiji hili ndilo ambalo lilikuwa limepakana kwa ukaribu sana na nchi ya Mexico na watu wengi ambao walikuwa wakiishi katika jiji hilo walikuwa wakitoka katika nchi hiyo huku muda mwingi wakiwa wanavaa makofia makubwa ya Malboro huku wakijulikana sana kwa jina la Cow Boys.
Hali ya hewa haikuwa ya baridi sana kama ilivyokuwa jijini New York, kutokana na sehemu kubwa kuwa jangwa, hali ya joto ndio ambao ilikuwa ikitawala sana hasa katika nyakati hizo za mchana. Moja kwa moja wakaanza kuelekea katika sehemu ambayo ilikuwa na jumba kubwa bovu bovu na kisha kumuingiza humo.
Gibson akatulia ndani ya jumba lile ambalo lilionekana kuwa na hadhi ya kujengwa katika sehemu kama ile ya jangwa huku vijana wale wakiwa nje wakimsubiria Daniel ambaye alikuwa amewataarifu kwamba ni lazima angefika mahali hapo haraka iwezekanavyo.
Ndani ya dakika hamsini, gari la kifahari aina ya Penina 11 likaanza kuingia ndani ya eneo hilo na kisha Daniel kuteremka huku akiwa amevalia suti nyeupe na macho yake yakiwa yamefunikwa na miwani ya mwanga. Akawasalimia vijana wale huku uso wake ukionyesha kuwa na furaha na kisha kukabidhiwa bunduki na kuanza kupiga hatua kuingia ndani ya jumba lile.
Uamuzi ambao alikuwa ameuweka Daniel kwa kipindi hicho ulikuwa ni uamuzi mmoja tu ambao wala haukuhitaji hata ushauri kutoka kwa mtu yeyote yule, hakutaka maelezo yoyote yale, kadri alivyokuwa akipiga hatua kuufuata mlango wa jumba lile na ndivyo ambavyo hasira zake zilivyokuwa zikizidi kumpanda. Kichwa chake kilikuwa kikimfikiria Katie, alimuona Gibson kuwa kiziuzi kikubwa kwa yeye kuwa na msichana yule ambaye alikuwa akimpenda kuliko mwanamke yeyote yule.
“Hakuna maelezo, hakuna maswali na wala hakuna mahojiano, hapa ni kuua tu” Daniel alisema huku akiwa amekwishaingia ndani ya jumba lile huku mkono ulioshika bunduki ile ukimtetemeka kwa hasira kali. Mtu ambaye alikuwa akimwangalia katika kipindi hicho, alikuwa Gibson ambaye alikuwa akitetemeka kupita kawaida.
“Ninakuua” Daniel alijisemea huku akimnyooshea Gibson bunduki ile.
“Paaaaa...paaaaaa...paaaaa...” Risasi zilisikika zikitoka katika bunduki aliyoishika Daniel huku uso wake ukionyesha tabasamu pana.

Je nini kitaendelea?
Je Gibson ameuawa?
Je Daniel atafanikiwa kumpata Katie kama anavyotaka?
Je ni nini kitaendelea katika maisha yao hawa?
Itaendelea.
 
MCHEZA FILAMU ZA NGONO 8.

Katie alikuwa chooni huku akiwa amefungwa kamba mikononi mwake na kisha ile kamba kufungwa katika bomba. Muda mwingi alikuwa akipiga kelele za kuomba msaada lakini wala hakukuwa na mtu yeyote ambaye alifika mahali hapo na kumsaidia.
Katie hakutaka kukata tamaa, aliendelea kupiga kele zaidi na zaidi. Kichwa chake kwa wakati huo kilikuwa kikimfikiria mume wake ambaye alikuwa ametekwa na kupelekwa asipopafahamu. Alitamani kuifungua kamba ile na kisha kuichukua simu ambayo ilikuwa mfukoni mwake lakini kitu kile kilionekana kuwa kigumu kufanyika.
Tayari mambo yakaonekana kuwa magumu kwa upande wake, kamwe asingeweza kuendelea kupiga kelele kama asingeonyesha jitihada za kutaka kujisaidia yeye mwenyewe. Alichokifanya mahali hapo ni kuanza kuzifungua kamba zile kwa kutumia meno yake.
Japokuwa mara ya kwanza kazi ilionekana kuwa rahisi sana lakini baadae ikaonekana kuwa ngumu tofauti na hisia zake. Alijitahidi kufungua zaidi na zaidi, alichukua zaidi ya dakika thelathini na ndipo ambapo kamba zile zikafunguka.
Akaanza kuugonga mlango wa choo kile, aligonga zaidi mpaka pale ambapo muuzaji wa mafuta alipokuja na kisha kuufungua mlango wa choo kile. Nywele za Katie zilikuwa zimevurugika sana, zilikuwa timtim kama chizi. Akaanza kuelezea kile kilichokuwa kimetokea na kisha kupiga simu polisi.
Kila mwananchi ambaye aligundua kwamba mwanamke yule aliyekuwa amesimama mbele yao alikuwa Katie, wengi wakatamani kutaka kupiga nae picha, uadimu wa kukutana na masupastaa waliokuwa wakiishi nchini mwao ndio ilikuwa sababu mojawapo iliyomfanya kila mmoja kutaka kupiga picha na Katie japokuwa alikuwa katika hali mbaya.
Ndani ya dakika tano, polisi wakaingia mahali hapo na kisha kuanza kuchukua maelezo ya awali ya Katie na kisha kumpakiza garini na kuondoka nae. Garini, Katie hakuwa na amani, alikuwa akimfikiria mume wake ambaye alikuwa ametekwa na watu ambao wala hakuwa akiwafahamu.
Maswali mfululizo yalikuwa yakijikusanya kichwani mwake juu ya watekaji wale ambao walikuwa wamemteka mume wake mpendwa. Hakujua kama mpaka katika kipindi hicho Gibson alikuwa mzima au alikuwa ameuawa. Amani haikupatikana moyoni mwake, muda wote alikuwa akitokwa na machozi tu.
Alipofikishwa katika kituo kikuu cha polisi cha New York, akaanza kutoa maelezo kwa kirefu zaidi. Katika kila kitu ambacho alikuwa akikieleza mahali hapo, polisi mmoja alikuwa akiandika katika faili lake ambalo lilikuwa mezani. Kila kitu kilipokamilika, akaruhusiwa kuelekea nyumbani huku mapolisi wakianza kazi yao.
Katie akarudi mpaka nyumbani, moyo wake ulikuwa katika maumivu makali kupita kawaida. Hisia kwamba Gibson alikuwa ameuawa zikaanza kumjia kichwani kitu ambacho kikamfanya kuwa na wasiwasi kupita kawaida. Muda mwingi alikuwa akilia tu, miezi sita ambayo alikuwa amekaa na mume wake ulionekana kuwa muda mfupi sana, alikuwa akihitaji kuwa nae zaidi na zaidi mpaka pale ambapo mkataba wa ndoa yao ungeisha na kufikiria ni kitu gani ambacho kingeendelea maishani mwao.
Katie hakutaka kubaki kimya, akaanza kuwataarifu marafiki zake na ndugu zake na kisha kuwaelezea kile ambacho kilikuwa kimetokea jambo ambalo liliwafanya wafike nyumbani hapo kwa ajili ya kumfariji. Hakujua ni nani ambaye aliwapata taarifa waandishi wa habari, lakini ndani ya nusu saa tayari walikuwa wamekwishafika nyumbani hapo na kisha kuanza mahojiano nae.
Katie hakutaka kuficha, akaanza kuelezea kila kitu ambacho kilikuwa kimetokea bila kuficha kitu hata kimoja. Kila mmoja akaonekana kushangaa, utekaji wa mtu mkubwa haukuwa umefanyika kwa kipindi kirefu sana nchini Marekani, utekaji ambao ulikuwa ukifanywa mara nyingi ulikuwa ni wa watoto tu.
Lengo la watekaji wala halikueleweka kabisa, waandishi wa habari, polisi pamoja na watu wengine ambao walikuwa wamesikia kila kiichotokea wakaonekana kushangaa kupita kawaida. Tayari kukaonekana kuna namna, tena kitu ambacho walikuwa wamekifikiria zaidi ni kwamba watekaji hao walikuwa wamekwenda kumuua Gibson.
‘Hata kama watamuua....nitataka kuuona mwili wake” Katie alisema huku akilia kama mtoto na ndugu, marafiki zake wakimfariji.
******
Milio mitatu ya risasi ilikuwa imesikika mahali hapo, uso wa Daniel ulikuwa ukionyesha tabasamu pana kama njia mojawapo ya kuonyesha kwamba tayari alikuwa amekamilisha kile ambacho alikuwa ametaka kifanyike mahali hapo.
Gibson alibaki kimya huku akitetemeka, hakuamini kama risasi zile tatu ambazo zilikuwa zimepigwa, zilikuwa zimepita pembeni yake. Haja ndogo tayari ilikuwa imekwishamtoka, alikuwa akitetemeka kwa hofu kubwa. Japokuwa alikuwa na miaka zaidi ya ishirini lakini hiyo ndio ilikuwa mara yake ya kwanza kuusikia mlio wa risasi.
Gibson akaanza kujipapasa kuona kama kweli hakukuwa na risasi ambayo ilikuwa imepenya mwilini mwake, mwili wake ulikuwa vile vile, wala haukuwa umejeruhiwa kwa risasi yoyote ile jambo ambalo lilimfanya kumwangalia Daniel ambaye uso wake ulikuwa ukionyesha tabasamu pana.
“Kama nikitaka kukuua, naweza kukuua sasa hivi, tena ndani ya sekunde moja tu. Ila ukiona risasi imepita pembeni yako, basi jua sitaki kukuua” Daniel alimwambia Gibson ambaye alikuwa kimya huku akizidi kutetemeka.
Daniel hakutaka kuendelea kumnyooshea bunduki Gibson kitu ambacho kilimfanya kuiweka kiunoni mwake na kisha kuanza kumsogelea. Tayari Daniel alikwishaona kwamba kama angeendelea kuishika bunduki ile basi kusingekuwa na maelewano yoyote yale ambayo yangeweza kufanyika mahali hapo, aliona kuwa na uhitaji wote wa kuweza kuificha bunduki ile kutoka mbele ya Gibson ili waweze kuongea vizuri na kufikia muafaka.
“Nimekuacha kwa sababu moja kubwa” Daniel alimwambia Gibson ambaye bado alikuwa akionekana kuwa na wasiwasi na kuendelea.
“Kitu kikubwa ambacho ninakitaka kutoka kwako, achana na Katie. Yule ni msichana wangu ninayempenda sana kutoka moyoni. Ninapoongea sasa hivi, nataka uachane nae” Daniel alimwambia Gibson.
“Itakuwa ngumu sana” Gibson alimwambia Daniel.
“Kwa nini?”
“Mkataba wa ndoa yetu haujakwisha kabisa. Ndio kwanza miezi sita imekatika” Gibson alimwamba Daniel.
“Hata kama. Ninachotaka uachane nae tu. Nitakupa ofa kama utaweza kufanya hivyo ndani ya wiki moja” Daniel alimwambia Gibson.
“Ofa gani?”
Hilo ndilo swali ambalo Daniel alikuwa akitaka kulisikia kutoka kwa Gibson. Alijua fika kwamba Gibson alikuwa akimpenda sana Katie ila aliona kuwa kama alitaka watu hao watengane basi ilikuwa ni lazima afanye kitu kimoja kikubwa, atumie fedha tu.
Kumfuata Katie na kumrubuni kwa fedha ili aachane na Gibson lilikuwa jambo gumu sana na hii ilikuwa kwa sababu msichana huyo alikuwa na kiasi kikubwa cha fedha. Gibson, kwake ndiye ambaye alionekana kuwa mtu mzuri ambaye angeweza kuyazima mapenzi aliyokuwa nayo kwa Katie kama tu angeweza kumuahidi kiasi fulani cha fedha.
“Nina dola milioni kumi. Nataka uachane na Katie tu” Daniel alimwambia Gibson.
Gibson akajiona kama kutokusikia vizuri kile ambacho alikuwa ameambiwa, alimwangalia Daniel mara mbili mbili huku akionekana kutokuamini kile ambacho alikuwa ameambiwa mahali pale. Akaileta kalkuleta ya kichwani mwake, akazibadilisha fedha zile katika thamani ya fedha za kitanzania, zilikuwa zaidi ya bilioni ishirini, yaani angepata zaidi ya shilingi bilioni ishirini tu endapo angefanikisha kuachana na Katie.
Ofa ile ikaonekana kuwa nzuri kwake, hakuamini kama mwisho wa siku angeweza kupata kiasi kikubwa namna ile kwa kufanya kitu kidogo tu, cha kuachana na Katie. Tamaa ya fedha ambazyo alikuwa nayo ikazidi kuota mizizi moyoni mwake, alikuwa radhi kumfanyia Katie kitu chochote isipokuwa kumuua endapo tu angeahidiwa kiasi cha fedha kama kile ambacho alikuwa ameahidiwa.
Hakutaka kujiona chizi, hakutaka kujiona kutokuwa na bahati, ofa ile ilikuwa ni vigumu sana kukatalika moyoni mwake, na si kwa yeye tu bali hata kwa Watanzania wote ambao walikuwa wakikaa nchini Tanzania. Kumuacha Katie kwake wala hakukuonekana kuwa na tatizo lolote lile.
“Ofa imekubalika” Gibson alimwambia Daniel maneno ambayo yalimfanya Daniel kutabasamu zaidi.
“Ila inakubidi kuwa makini” Daniel alimwambia Gibson.
“Umakini gani?”
“Nitazituma fedha katika akaunti yako, nataka ndani ya wiki, kila kitu kiwe kimefanikiwa, usipofanikisha ndani ya wiki. Nitakuua. Umesikia?” Daniel alimwambia Gibson.
“Ndio”
“Ok! Kumbuka ni ndani ya wiki tu” Daniel alisisitiza.
“Sawa”
Daniel akaonekana kuwa mwenye furaha zaidi, alionekana kufurahia sana kwa kuwa Gibson wala hakuonekana kuwa mgumu kuikubali ofa ile. Alichokifanya mahali hapo ni kutoa karatasi na kumkabidhi Gibson na kisha kuandika akaunti yake ya benki ambayo angependa fedha hizo ziingizwe.
“Mbona namba hii ngeni machoni mwangu?” Daniel aliuliza mara baada ya kuiona namba ambayo Gibson alikuwa ameiandika.
“Hiyo ni namba ya akaunti yangu ya nchini Tanzania. Nataka nikiachana nae tu nirudi nchini Tanzania. Au wazo baya hilo?” Gibson aliuliza.
“Wazo zuri. Tena zuri sana” Daniel alimwambia Gibson na kisha kumruhusu kuondoka mahali hapo kuelekea garini tayari kwa kurudi jijini New York pamoja nao.
Muda wote Gibson alikuwa akionekana kuwa na furaha kupita kawaida, kila siku maisha yake alikuwa akiyaona kuwa na bahati kubwa. Alikumbuka kwamba alikuwa amesoma katika shule za kawaida sana na wala hakufikiria kama angekua tajiri, lakini kwa sababu ya mapenzi tu, yakamfanya kuwa tajiri nchini Tanzania.
Huku akiendelea kuumiliki utajiri mkubwa, kiasi kikubwa cha fedha ambazo angeweza kukiingiza kwa miaka mitatu, alikuwa akikiingiza ndani ya masaa machache tu, yaani pale ambapo angemwambia Katie kwamba ule ndio ulikuwa mwisho wa mahusiano yao, kwa maana hiyo wangeachana na kurudi nchini Tanzania.
Walipita katika njia nyingine kabisa mpaka kutokea jijini New York ambako wakamuacha. Gibson akaanza kutembea kuelekea katika stesheni ya treni na kisha kupanda treni na kuelekea nyumbani kwake, pembeni mwa jiji hilo la New York. Kichwa chake kwa wakati huo kilikuwa kikifikiria kitu kimoja tu, kufika nyumbani na kumwambia Katie kwamba asingeweza kuendelea nae tena na hivyo mkataba wa ndoa yao uvunjwe haraka iwezekanavyo.
“Mmmh! Nitaanzia wapi sasa hadi kumwambia tuvunje ndoa?” Gibson alijiuliza.
“Ila poa. Nitajua nimwambie nini” Alijijibu mwenyewe.
*****
Gibson akaingia ndani, waandishi wa habari ambao walikuwa ndani ya eneo la nyumba hiyo kwa ajili ya kumhoji Katie wakaanza kumsogelea huku wakiviweka mbele vyombo vyao vya kuekodia sauti. Kila mwandishi akaonekana kumshangaa Gibson, wakati huo habari ilikuwa ikiripotiwa kwamba alikuwa ametekwa, je kwa nini alikuwa mahali hapo muda huo? Je aliwatoroka watekaji au walimuacha? Na kama walimuacha bila kumjeruhi, lengo lao la kumteka lilikuwa nini?
Kila mwandishi ambaye alikuwa akijiuliza maswali hayo hakupata jibu, mtu pekee ambaye angewapa majibu ya kutosha na kuridhisha alikuwa mmoja tu, Gibson. Gibson hakutaka kuongea kitu chochote kile, alichokifanya ni kuendelea kupiga hatua mpaka ndani ya nyumba yake.
Katie, ndugu zake na marafiki zake wa karibu wakashtuka, hawakuamini kama Gibson alikuwa akiingia ndani ya nyumba ile kwa wakati ule na wakati alikuwa ametekwa masaa kadhaa yaliyopita. Katie akashindwa kuvumilia, akainuka, akaanza kupiga hatua kumfuata Gibson, alipomfikia, akamkumbatia kwa furaha.
Katie akashindwa kuyazuia machozi yake ya furaha, yakaanza kumtoka huku akiwa bado amemkumbatia Gibson. Gibson akaanza kumbembeleza Katie kwamba kwa wakati huo hakutakiwa kuhofia kitu chochote kile kwa sababu alikuwa amerudi akiwa mzima wa afya kama alivyokuwa ametekwa.
Katie akamjitoa mwilini mwa Gibson na kisha kuanza kumwangalia kwa mtindo wa kumchunguza. Alikuwa akimwangalia kwa makini kama alikuwa amejeruhiwa au la. Mwili wake ulikuwa vile vile, hakukuwa na jeraha lolote lile.
“What happened to you? (Nini kilikutokea?)” Katie alimuuliza Gibson.
“I ascaped (Nilitoroka)” Gibson alijibu.
“Thank you Jesus! I was just worring about you. Where did they take you to? (Asante Yesu! Nilikuwa nikihofia kuhusu wewe. Walikupeleka wapi?)” Katie alimuuliza Gibson.
“They planned to take me to Texas but when we arrived Shealbon, five kilometre to Texas, I ascaped? (Walipanga kunipeleka Texas lakini tulipofika Shealbon, kilometa tano kabla ya kuingia Texas, niliwatoroka)” Gibson alijibu.
“How did you escape? (Ulitoroka vipi?)”
“I fought them (Nilipigana nao)
“Sure? (Kweli)
“Yeah” Gibson alijibu.
Waliendelea kuongea zaidi na zaidi huku Katie akishindwa kabisa kuificha furaha yake ambayo alikuwa nayo, muda wote alikuwa pembeni ya mume wake akimkumbatia tu, alishindwa kumuachia, aliona kama angekaa mbali nae kidogo basi angeweza kuondoka mikononi mwake kitu ambacho hakuwa akikitaka kitokee.
Kichwa cha Gibson kilikuwa kikiwaza kitu kingine kabisa, hakuyafikiria mapenzi hata kidogo, kitu ambacho alikuwa akikifikiria sana kwa wakati huo ni fedha ambazo alikuwa ameahidiwa na Daniel kama angefanikiwa kuvunja ndoa yake na mkewe, Katie.
Mpaka kufika kipindi hicho wala hakujua angeanzia wapi, alimuona Katie akiwa na mapenzi ya kweli sana kwake jambo ambalo ilikuwa ni vigumu sana kuufanya uamuzi ule ambao alikuwa ameambiwa kuufanya ndani ya wiki moja. Mapenzi ya Katie ndio ambayo yalikuwa yakimuweka katika hali ngumu ya kuufanya uamuzi ule.
Dhahiri alionekana kuwa katika wakati mgumu kuufanya uamuzi ule lakini kiasi cha fedha ambacho alikuwa ameahidiwa kilikuwa ni kiasi kikubwa sana ambacho angeonekana kuwa mjinga sana kama asingekifanya kile ambacho alikuwa ameambiwa kukifanya.
Usiku, mawazo yake yalikuwa yakimfikiria Daniel na kufikiria kile ambacho alikuwa ameambiwa kukifanya. Japokuwa mke wake, Katie kwa wakati huo alikuwa kwenye wakati mgumu wa kumtaka mume wake wafanye mapenzi lakini kwa Gibson wala mawazo yake hayakuwa yametulia kabisa, hakujisikia kabisa kufanya kitu hicho.
Katie hakutaka kutulia, alikuwa akimpapasapapasa mumewe mpaka pale hamu ya kufanya tendo lile ilipomshika na kuanza kufanya. Kwa kipindi kile, tendo lile wala halikuwa na utamu wowote kwa upande wa Gibson, mawazo yake yalikuwa yakimfikiria Daniel tu, hasa kitita ambacho alikuwa ameahidiwa kukipata pale atakapokamilisha kuvunja mkataba wa ndoa na Katie.
Siku ya kwanza ikakatika, bado Gibson alikuwa kwenye wakati mgumu sana kukamilisha mpango ambao alikuwa ameambiwa na Daniel kuukamilisha. Muda mwingi alikuwa akionekana kuwa mpole, furaha ambayo alikuwa nayo katika kipindi cha nyuma ilikuwa imepotea kabisa.
Katie akaonekana kuwa na wasiwasi, kamwe hakutaka kumuona mume wake akiwa katika hali ya unyonge jambo ambalo alikuwa akimuuliza sana lakini Gibson alikuwa akimficha kwa kumwambia sababu nyingine ambazo wala hazikuwa na maana yoyote ile.
Siku ya pili ilikuwa imekwishakatika na ya tatu kuingia. Bado Gibson alikuwa akiendelea kujiuliza ni sababu gani ambazo angezisema ili kuuvunja mkataba wa ndoa ambao walikuwa wamewekeana katika kipindi walichooana. Kwa Gibson, mambo yalionekana kuwa magumu sana, kila alivyokuwa akimwangalia Katie na kuona jinsi alivyokuwa akimpenda, alijiona kufanya kosa kubwa sana kama angeamua kufanya hivyo.
Siku ya nne ikaingia, ya tano na hatimae wiki nzima kukatika. Bado Gibson alikuwa kwenye wakati mgumu, wasiwasi wa kuuawa tayari ukaanza kumuingia kama ahadi iliyotolewa na Daniel endapo asingeweza kukamilisha kile ambacho alikuwa amemwambia. Siku moja baada ya wiki ilipoingia, akashtukia akipigiwa simu na namba ngeni, alipoipokea, alikuwa Daniel.
“Umefikia wapi?” Sauti ya Daniel ilisikika ikiuliza.
“Bado sijaanza kazi. Nahofia utanigeuka” Gibson alimwambia.
“Kukugeuka! Kivipi?”
“Kama nikikamilisha kufanya ulichoniambia, halafu fedha haujaniingizia, hauoni tatizo hilo?” Gibson alimuuliza.
“Ok! Nakuingizia nusu ya fedha. Utakapokamilisha, nakumalizia” Daniel alimwambia Gibson.
“Hapo utakuwa haupo sawa. Ziingize zote kabisa”
“Sasa nitaingizaje fedha zote na wakati kitu ninachokitaka hakijafanyika?”
“Sasa na mimi nitauvunjaje mkataba wa ndoa na wakati fedha zangu hazijamaliziwa?”
“Ok! Kwa hiyo nikiingiza zote utakamilisha kila kitu?”
“Ndio”
“Sawa. Nakwenda kukuingizia leo hii hii. Na ninataka kazi ifanyike ndani ya masaa ishirini na nne. Umenielewa?” Daniel aliuliza huku sauti yake ikiwa imebadilika na kuwa ya hasira zaidi.
“Nimekuelewa”
Ndani ya masaa mawili, meseji ikaingia ndani ya simu ya Gibson kumtaarifu kwamba kiasi cha dola milioni kumi kilikuwa kimeingizwa ndani ya akaunti yake. Gibson hakuamini kama kweli fedha zile zilikuwa zimekwishaingizwa kwenye akaunti yake. Kazi ilikuwa imebakia moja tu kwa wakati huo, kuuvunja mkataba wa ndoa yake na Katie.
Siku hiyo ofisini hakukukalika hata kidogo, muda wote alikuwa akifikiria ni kwa namna gani angeweza kufanya kile ambacho alikuwa amekipanga kukifanya. Akaanza kupekua katika kabati la mafaili yake na kisha kutoa karatasi kadhaa ambazo zilikuwa zikionyesha ni kiasi gani cha fedha alikuwa amekituma nchini Tanzania.
Tayari yeye binafsi alikuwa amekwishatumia zaidi ya dola elfu sabini nchini Tanzania ambazo zilikuwa sawa na shilingi milioni mia na hamsini. Tayari kwa wakati huo alijiona kuwa na fedha za kutosha na hii ilionekana kutosha kabisa kurudi nchini Tanzania.
“Nitaanzisha timbwili nyumbani” Gibson alisema.
“Yaani leo hakulaliki mpaka mkataba uvunjwe” Gibson alijisemea na kuanza safari ya kuelekea nyumbani.
Siku hiyo alionekana kupania kile ambacho alikuwa amekipanga kukifanya, hakutaka kuendelea kuishi na Katie tena kwa kuwa alikuwa amekwishaingiziwa kiasi kikubwa cha fedha katika akaunti yake. Hakujua ni aina gani ya maumivu ambayo angeyapata Katie, kitu ambacho alikuwa akikijali kwa wakati huo kilikuwa fedha tu.
Alipofika nyumbani, akaegesha gari na kuteremka huku akianza kuelekea ndani. Alichokifanya hapo ni kujifanya kuwa na wasiwasi mkubwa mno kitu ambacho kilionekana kuwashangaza hata wafanyakazi wa ndani. Gibson siku hiyo alionekana kutokujiamini kabisa, alikuwa akionekana kuwa na mashaka makubwa sana usoni mwake.
Hata Katie aliporudi nyumbani hapo, bado Gibson alikuwa akiigiza kuwa katika hali ile ile, hali ya kuwa na mashaka makubwa. Katie alipomuuliza sababu, hakujibu kitu zaidi ya kuendelea kuonekana katika hali ile ile ambayo ilikuwa ikimtia wasiwasi Katie.
“Kuna nini mpenzi?” Katie aliuliza kwa sauti ya unyonge.
“Nimepokea simu ya kifo” Gibson alijibu.
“Simu gani tena?”
“Ya kifo. Nimeambiwa nijiandae kufa. Muda wowote ninauawa kuanzia sasa hivi. Aina ya kifo changu kitakuwa ni kama cha John F. Kennedy, kufyatuliwa risasi kadhaa za kichwa” Gibson alisema huku akionekana kuwa na wasiwasi.
“Hapana mpenzi, hautakiwi kuwa na wasiwasi kabisa. Ngoja niwapigie simu polisi” Katie alimwambia Gibson.
“Hapana mke wangu. Ni lazima niondoke hapa”
“Uondoke? Uelekee wapi tena?”
“Nyumbani, Tanzania”
“Kufanya nini?”
“Nafikiri nitakuwa salama kutoka katika mikono ya watu hawa wanaonitafuta” Gibson alijibu.
“Mbona umechukua uamuzi wa haraka sana?”
“Ndio hivyo mke wangu”
“Kwa hiyo utaniacha mimi mwenyewe? Utakubali kukaa mbali nami?” Katie aliuliza huku akionekana kuwa na wasiwasi.
“Inawezekana. Najua haya yote yanatokea kwa ajili yako, kama ningekuwa nimemuoa mwanamke wa kawaida nadhani haya yote wala yasingenitokea kabisa. Nilitekwa, nikatoroka, leo hii napokea simu ya kifo, nadhani maisha yangu yapo ukingoni kama nitaendelea kuishi katika nchi hii ya ugeni” Gibson alisema.
“Kwa maana hiyo unataka tuachane?” Katie alimuuliza Gibson.
Gibson alibaki kimya, swali ambalo alikuwa ameulizwa likaonekana kuwa gumu kujibika, akayapeleka macho yake usoni mwa Katie, Katie alikuwa amebadilika sana, macho tayari yalikuwa mekundu hali iliyoonyesha kwamba muda wowote ule machozi yangetiririka mashavuni mwake.
“Mbona kimya tena? Kwa maana hiyo unataka tuachane?” Katie alimuuliza tena.
“Kama inawezekana” Gibson alijibu.
“Haiwezekani. Haiwezekani hata kidogo. Hapa mpaka mkataba uishe” Katie alimwambia Gibson maneno ambayo yalionekana kumchanganya.
Kwa haraka sana mawazo yake yakahamia kwa Daniel, tayari kukataa kwa Katie kulionekana kumsababishia kifo kutoka kwa Daniel ambaye alikuwa amekwishamuingizia kiasi kikubwa cha fedha katika akaunti yake. Gibson akaonekana kuchoshwa na jibu la Katie ambaye alianza kulia.
“Kuvunja mkataba wa ndoa. Haiwezekani kabisa” Katie alimwambia Gibson katika kipindi ambacho simu ya Gibson ilikuwa ikiita, alipoichukua na kuiangalia, ilikuwa namba ya Daniel, namba ambayo ilikuwa ikimtia wasiwasi.
“Umefikia wapi?” Daniel alimuuliza Gibson.
“Bado kwanza” Gibson alijibu kwa sauti ya chini ambayo alihakikisha Katie asikii.
“Sawa. Una masaa mawili tu. Usipokamilisha. Tunakuja kukua humo humo ndani” Daniel alimwambia Gibson na kisha kukata simu huku akimwacha Gibson akitokwa na kijasho chembamba kilichojaa wasiwasi.

Je nini kitaendelea?
Je Gibson ataweza kuvunja mkataba wa ndoa na Katie?
Itaendelea.
 
MCHEZA FILAMU ZA NGONO 9.

Tayari mambo yalikwishaanza kuwa magumu kwa Gibson, simu ambayo alikuwa ameipokea kutoka kwa Daniel ikaanza kumtia kiwewe kupita kawaida. Hakutulia, muda wote alikuwa amkimsisitizia Katie kwamba ilikuwa ni lazima wauvunje mkataba wa ndoa yao ili aweze kuikoa nafsi yake ambayo ilikuwa ikisakwa sana.
Baada ya kulalamika sana, Katie akakubali kishingo upande. Moyoni mwake ilikuwa imemuuma kupita kawaida, mapenzi yake makubwa bado yalikuwa kwa Gibson ambaye kwa wakati huo alitaka wavuje mkataba wa ndoa wa miaka mitano ambao walikuwa wameandikishiana.
Walichokifanya ni kuelekea mahakamani ambako huko mkataba ukavunjwa. Ingawa Gibson alikuwa akifanya hivyo lakini moyo wake ulikuwa ukimuuma kupita kawaida. Nguvu ya fedha ndio ambayo ilikuwa imempelekea kufanya kitu kama kile ambacho wala hakuwa akitaka kukifanya.
“Nitarudi Tanzania tu. Tena haraka iwezekanavyo” Gibson alijisemea.
Alikaa nchini Marekani kwa siku mbili zaidi huku akionana na Daniel ambaye alikuwa akimpa pongezi kwa kile ambacho alikuwa amekifanya, na baada ya hapo, akakata tiketi na kurudi nchini Tanzania kwa kutumia ndege ya American Airlines.
Ndani ya ndege hakuwa na raha hata kidogo, kwanza akili yake ilikuwa ikimfikiria sana Katie ambaye alikuwa amemuacha katika hali ya unyonge mkubwa huku akiwa amemuumiza kupita kawaida. Ukiachilia na Katie, pia mawazo yake yalikuwa yakimfikiria mke wake aliyemuacha nchini Tanzania, Prisca pamoja na mtoto wake, Genuine.
Gibson hakujua kama Prisca alikuwa amekwishajua kilichoendelea au la. Kitu ambacho alikuwa akitaka kukifanya mahali hapo ni kuusoma mchezo tu. Kwanza angeangalia Prisca angempa mapokezi gani, hapo ndipo ambapo angegundua kwamba siri ilikuwa imevuja au bado iliendelea kuwa siri.
Alitumia zaidi ya masaa ishirini katika ndege ile na ndipo ndege ilipotua katika uwanja wa Mwl Julius Nyerere huku ikiwa ni saa tisa usiku. Kwa sababu ilikuwa ni usiku sana, Gibson hakutaka kurudi nyumbani, alichokifanya ni kwenda kulala kwenye hoteli ya New African.
Usiku wala hakulala, kichwa chake kilikuwa kikiwafikiria watu wawili kwa wakati huo. Kwa Katie, alijiona kufanya uamuzi mkubwa na mgumu kufanyika, kuna wakati mwingine alijiona bora amefanya uamuzi ule kwani ulikuwa na manufaa kuliko kuendelea kuishi na mwanake huyo ambaye alikuwa akicheza filamu za ngono.
Katika kichwa chake, kwa wakati mwingine alikuwa akimfikiria sana mke wake, Prisca. Hakujua mwanake huyo angesema kitu gani hasa mara baada ya kuishi nchini Marekani kwa zaidi ya miezi sita bila kuwasiliana nae. Akili yake ikaanza kufikiria uongo mbalimbali ambao alitakiwa kumwambia Prisca mara baada ya kufika nyumbani kwake.
“Nitamdanganya tu, wanawake ni rahisi sana kuukubali uongo” Gibson alijisemea.
“Mmmh! Lakini miezi sita bila mawasiliano! Hivi kama isingekuwa Daniel si mpaka mwaka ungetimia bila kufanya mawasiliano na Prisca. Kweli nilifanya kitu kibaya sana” Gibson alijisemea na kisha kupatwa na usingizi huku ikiwa imetimia saa kumi na mbili alfajiri.
Alikuja kuamka ikiwa saa saba mchana muda ambao aliagiza chakula na kuletewa chumbani na kisha kuanza kula. Kichwa chake kwa wakati huo kilikuwa kikifikiria namna ya kumwambia Prisca ili aweze kumuelewa. Ni kweli kwamba alitunga uongo mbalimbali lakini kwa wakati ho, kila uongo ambao alikuwa ameutunga ulionekana kutokufaa, yaani aliuona kuwa uongo wa kitoto.
Ilipofika saa tisa, akajitoa mhanga na kuanza kuelekea nyumbani kwake. Kadri gari ilivyokuwa ikizidi kusogea na ndivyo ambavyo wasiwasi ulivyokuwa ukimshika zaidi na kuufanya moyo wake kududa kupita kawaida.
Alichukua dakika thelathini hadi kufika nyumbani ambako akateremka ndani ya taksi na kisha kumlipa dereva na kuanza kulifuata geti la nyumba yake. Mapigo yake ya moyo yakazidi kudunda zaidi na zaidi kana kwamba kulikuwa na hatari kubwa mbele yake. Alipolifikia geti, akabonyeza kengele na mlinzi kuja kufungua.
“Karibu sana kaka” Mlinzi alimkaribisha huku akimpokea begi.
“Subiri kwanza. Shemeji yako yupo?” Gibson aliuliza hata kabla hajaingia ndani.
“Hayupo. Aliondoka kwenda kwa wazazi wake” Mlinzi alimjibu.
“Dah! Toka lini?”
“Mwezi wa tano huu” Mlinzi alimjibu Gibson jibu ambalo likaonekana kumtia wasiwasi.
“Duh! Kwa nini sasa?”
“Nilimsikia Rehema akisema kwamba kisa kilikuwa picha”
“Picha gani?”
“Hakutaka kuniambia”
“Ok! Rehema mwenyewe yupo?”
“Ndio” Mlinzi alijibu.
Gibson akaanza kupiga hatua kuingia ndani na kisha kuufuata mlango wa kuingilia sebuleni. Kwa wakati huo alikuwa akitaka kuongea na Rehema ambaye alikuwa mfanyakazi wa ndani na kisha kumuuliza kuhusu picha ambazo mpaka hapo zikaonekana kumchanganya.
“Picha gani?” Gibson alimuuliza Rehema.
“Kuna picha alipewa zikionyesha kwamba ulipiga na mzungu” Rehema alijibu.
“Sasa kupiga picha na wazungu si kawaida sana hasa unapokuwa Marekani au Ulaya. Kipi hasa kilichomfanya kuondoka hapa nyumbani?” Gibson aliendelea kuuliza.
“Hizo hizo picha”
“Picha?”
“Ndio. Ulipiga ukiwa na mwanamke wa kizungu ambaye alikuwa amevaa shela la harusi huku wewe ukiwa umevaa suti, yaani lilionekana kuwa tukio la kufunga ndoa” Rehema alimwambia Gibson ambaye akabaki kimya.
Tayari kila kitu kiichoendelea nchini Marekani kikaonekana kujulikana kwa Prisca, kwa maana hiyo kama Prisca aliweza kuujua ukweli basi iliwezekana hata wakwe zake na wazazi wake walikuwa wakiufahamu ukweli. Kitu alichokifanya mahali hapo ni kutoka nje, kuchukua gari na kisha kuanza kuelekea nyumbani kwao huku akioneknana kuchanganyikiwa.
Tayari kwa wakati huo alijiona kufanya makosa makubwa, asingeweza kuelekea nyumbani kwa kina Prisca bila wazazi wake, alichokuwa akikifanya kwa wakati huo ni kumfuata baba yake, mzee Lyimo pamoja na mama yake ili waweze kuelekea nyumbani kwa kina Prisca kwa ajili ya kumuombea msamaha kwa kila kilichotokea nchini Marekani.
“Umefanya upumbavu mkubwa sana” Mzee Lyimo alimwambia Gibson kwa sauti ya juu.
“Nafahamu baba, nafahamu kwamba nimefanya kosa kubwa lakini ninahitaji kusamehewa pia kama ambavyo ninaomba msamaha” Gibson alimambia baba yake.
“Yaani umetutia doa hata sisi wenyewe. Tumeonekana tumekulea katika maisha ya ajabu ajabu. Eti unaondoka hapa na kuelekea Marekani kufunga ndoa, tena na mwanamke malaya ambaye anacheza filamu za ngono. Huo ni ujinga sana” Mzee Lyimo alisema maneno ambayo yalimfanya Gibson kushtuka.
Hapo ndipo alipogundua kwamba wazazi wake walikuwa wakifahamu kila kitu kilichoendelea na hadi kazi ambayo Katie alikuwa akiifanya ilikuwa imekwishagundulika. Kwake, tayari mambo yakaanza kuonekana kuwa magumu, alijua fika kwamba kwa hatua ile ambayo alikuwa amefikia, ilikuwa ngumu sana kwa Prisca kuweza kumsamehe.
Gibson akaanza kueleza kila kitu ambacho kilikuwa kimetokea katika maisha yake pamoja na Katie, wazazi wake walikuwa kimya huku wakimsikiliza kwa makini kwani walihitaji kufahamu kila kitu kuona ni kwa namna gani wangeweza kuwaelezea wazazi wenzao ili kukubaliana nao na kumsamehe Gibson.
“Kwa hiyo ukaamua kuvunja mkataba wa ndoa?” Mzee Lyimo alimuuliza.
“Ndio. Niliamua kuuvunja kwa sababu nilijiona kuwa na uhitaji mkubwa wa kuja Tanzania na kumuona mke wangu na mtoto wangu. Kamwe nisingeweza kukaa zaidi bila kuwaona wao” Gibson alidanganya.
Gibson, mzee Lyimo na mama yake, Bi Yustina wakaanza kuelekea nyumbani kwa mzee Steven huku lengo lao likiwa ni kumuombea msamaha kijana wao ambaye alikuwa ameamua kutubu dhambi zake juu ya kile ambacho alikuwa amekifanya nchini Marekani.
Walipofika nyumbani kwa mzee Steven, wote wakateremka na kuanza kuelekea getini kisha mlinzi kuwafungulia na kuanza kuingia ndani ya eneo la nyumba hiyo. Wakaanza kuufuata mlango wa kuingilia sebuleni ambao wakaugonga na kukaribishwa ndani.
Mzee Steven na mkewe, Bi Magreth walikuwa sebuleni hapo, walipowaona wazee wenzao wanaingia, wakawakaribisha kwa furaha lakini mara walipomuona Gibson akiingia pamoja nao, wakabadilika kabisa. Nyuso za furaha ambazo walikuwa nazo zikawa zimekwishabadilika kabisa, walionekana dhahiri kutokumpenda Gibson kwa wakati huo. Hata pale Gibson alipowasalimia, hakukuwa na mtu aliyeitikia.
Wakakaa kochini na kisha kuanza kuongea na baadae kumpa ruhusa Gibson kuongea. Ila kabla hajaanza kuongea, Prisca akaitwa mahali hapo, alipomuona mume wake, akaanza kulia. Prisca alikuwa mgumu kubembelezeka, alizidi kulia zaidi na zaidi huku Gibson akiangalia chini kwa aibu.
Prisca alilia kwa muda mrefu, aliponyamaza, Gibson akaanza kuelezea kila kitu ambacho kilitokea katika maisha yake na Katie tangu kipindi kile walipokutana kazini. Gibson alikuwa mkweli, ila katika sehemu moja tu hakutaka kuwa mkweli, hakutaka kuwaeleza wazazi wake kwamba alikuwa amevunja mkataba wa ndoa kwa sababu alipewa kiasi kikubwa cha fedha, alichokisema yeye ni kwamba alivunja mkataba wa ndoa kwa sababu alijua kile alichokuwa akikifanya kutokuwa kizuri, hivyo alihitaji kurudi nyumbani kuishi na mkewe aliyekuwa akimpenda.
Alipomaliza kuelezea kila kitu akaanza kuomba msamaha. Ilikuwa ni ngumu sana kwa Prisca kumsamehe Gibson kwa sababu kile alichokuwa amemfanyia kilikuwa kitu kibaya sana kilichomuumiza moyo wake. Yalipita masaa mawili huku Gibson akiomba msamaha huku akilia kama mtoto na ndipo Prisca akaamua kumsamehe tena huku msaada wa wazazi wao ukiwa umesaidia kwa asilimia kubwa.
Baada ya hapo, Gibson akaamua kuishi na mke wake, Prisca kwa amani, hakutaka kusikia kitu chochote kutoka kwa mwanamke Katie. Moyoni mwake hakujua kabisa, hakujua kwamba alikuwa amemjeruhi sana Katie, na hivyo muda si mrefu kuanzia hapo angetaka kulipiza kiasi kwa kile kilichotokea. Huko Marekani, Katie alikuwa amebadilika, alikuwa kama mbogo aliyejeruhiwa huku akimtafuta mtu aliyemjeruhi.
Baada ya hapo, maisha yataanza kubadilika, huzuni itaingia, hasira za Katie zikabadilisha kila kitu, furaha ikawa huzuni na majonzi. Kwa Gibson hilo wala hakulitambua, alikuwa akiendelea kuishi na Prisca huku akijua kwamba yeye na Katie yalikuwa yamekwisha, kumbe ilikuwa tofauti kabisa kwani ndio kwanza mambo yalikuwa yakianza tena ngoma ikiwa mbichi kabisa...na kama gazeti, ndio kwanza ulikuwa umeanza ukurasa wa kwanza.

Je nini kitaendelea?
Je Katie atafanya nini kudhirisha hasira zake?
Je maisha yataendelea kuwa ya furaha kwa Gibson na mkewe, Prisca?
 
MCHEZA FILAMU ZA NGONO 10

Vyombo vingi vya habari nchini Marekani vilikuwa vikitangaza kuhusiana na kuvunjika kwa ndoa kati ya mwanamke ambaye alikuwa maarufu duniani katika uigizaji wa filamu za ngono, Katie pamoja na mwanaume kutoka nchini Tanzania, Gibson.
Kila mtu ambaye aikuwa akiziangalia taarifa zile katika vyombo mbalimbali vya habari hakuonekana kushtuka sana kutokana na kufahamu kwamba kuna siku kitu kama kile kingetokea kutokana na Katie kuwa miongoni mwa watu ambao waikuwa wakiigiza filamu za ngono duniani.
Kila kitu kilionekana kubadilika sana katika maisha ya Katie, mwanaume ambaye alikuwa akimheshimu sana, Gibson kwa wakati huo hakuwa pamojanae. Katie akawa mwanamke wa kulia tu, kila siku alikuwa akijifungia chumbani kwake na kulia kupita kawaida.
Moyo wake ulikuwa ukimuuma kupita kawaida. Kuna wakati alikuwa akijuta sababu zilizompelekea kuolewa na mwaname ambaye wala hakuwa amekaa nae sana katika mahusiano huku wakati mwingine akijuta sababu ambazo zilimpelekea kutokumwambia Gibson ukweli juu ya kazi ambayo alikuwa akiifanya ya uigizaji wa filamu za ngono.
Alijua ni lazima kungekuwa na sababu moja kubwa ambayo ilimfanya Gibson kuamua kufanya uamuzi wa namna ile kwani alijua kwamba Gibson hakuwa na lengo la kumuacha kwa wakati ule kutokana na sababu kubwa ya kumruhusu kwa moyo mmoja kuendelea kuigiza filamu za ngono.
Wasiwasi ukaanza kumuingia Katie kwamba kulikuwa na mtu ambaye alikuwa nyuma ya mpango ule wote, alichokifanya kwa wakati huo ni kuanza kupeleleza. Kazi ya upelelezi ilikuwa kubwa sana kitu ambacho kikamfanya kuwaita vijana maalumu kwa ajili ya kuifanya kazi ile.
Vijana waliifanya kazi ile kwa moyo mmoja, waliangaika kila sehemu lakini mwisho wa siku hawakupata kitu. Katie akaonekana kuchanganyikiwa, alichokifanya kwa wakati huo ni kuanza kuyafuatilia maisha ya Gibson tu.
Alijua fika kwamba Gibson alikuwa akielewa kila kitu juu ya sababu ambazo zilimfanya kutaka ndoa ivunjwe kwa haraka sana, umuhimu wa kumuuliza Gibson ulikuwa ukionekana kufaa kwa asilimia zaidi ya mia moja.
Katie akaanza kugundua vitu fulani, kwanza akaanza kujiuliza juu ya siku ile ambayo Gibson alikuwa ametekwa na kisha kumwambia kwamba alikuwa amewatoroka watekaji. Swali ambalo lilikuwa kichwani mwa Katie ni kwa namna gani Gibson alikuwa ameweza kupigana na watekaji hata bila kujeruhiwa katika sehemu yoyote ya mwili wake na wakati watekaji wale walikuwa na bunduki?
Katie akaanza kuingiwa na wasiwasi, akaanza kujua kwamba kulikuwa na kitu ambacho kiliendelea na aliamini kwamba kitu hicho ndicho ambacho kilimfanya Gibson kutaka kuachana nae na kuuvunja mkataba wa ndoa ambao walikuwa wameusaini.
“There’s something (Kuna kitu)” Katie alisema.
Wazo jingine likaingia kichwani mwa Katie, akaanza kugundua kwamba kulikuwa na kitu ambacho kilikuwa kikiendelea nchini Tanzania ambacho hicho nacho kilikuwa kimechangia kwa asilimia kubwa kwa Gibson kuamua kufanya vile.
Katie akaanza kugundua kwamba kulikuwa na uwezekano Gibson alikuwa na mpenzi nchini Tanzania ambaye alikuwa ameishika akili yake kupita kawaida na ndio maana alitaka kuachana nae ili aeze kurudi nchini Tanzania na kuendelea na maisha yake.
Alichokifanya kwa wakati huo ni kuwatuma vijana wake nchini Tanzania kwa ajili ya kuufanya upelelezi ambao kwake aliuona kumletea majibu yote. Alihitaji kila kitu kifanyike huku akiwaelekeza kwamba ilikuwa ni lazima kwao kufikia katika mbuga ya Mikumi ili kupata ukweli juu ya kila kitu kuhusiana na Gibson.
“Nitawagawia kila kitu, ninachokitaka kutoka kwenu watatu ni kunipa kila kitu nitakachotaka kukifahamu” Katie aliwaambia vijana wake watatu ambao walikuwa wakijiandaa kuja nchini Tanzania.
“Sawa! Hautakiwi kuhofia kitu chochote. Kuna kingine?” Reuben aliuliza.
“Ndio! Kama anaishi na mwanamke, inatakiwa mmuue kama kisasi changu” Katie aliwaambia.
“Sawa! Kingine bosi”
“Ni hivyo tu” Katie alisema.
Alichokifanya kwa wakati huo ni kuwagawia vijana wale kiasi cha dola milioni moja kwa ajili ya kuja nchini Tanzania huku fedha nyingine akiwatumia pale ambapo wangekuwa wanazihitaji wakati watakapokuwa nchini Tanzania.
Harakati za kutafuta viza zikaanza mahali hapo, wala hawakupata tabu kutokana na kuelezea katika ubalozi wa Tanzania kwamba walikuwa wakitaka kuja nchini Tanzania kwa ajili ya kufanya utalii tu. Mara baada ya kupata viza, wakakata tiketi za ndege na siku iliyofuata kuanza safari ya kuja nchini Tanzania kufanya kile ambacho kilikuwa kikitakiwa kufanyika tu.
****
Reuben, Filbert na Andrew walikuwa ndani ya ndege ya Gulf Airlines wakielekea nchini Tanzania. Muda wote walikuwa wakiongea mambo mbalimbali ambayo walitakiwa kuyafanya nchini Tanzania, ramani kubwa ya nchi ya Tanzania ilikuwa mikononi mwao kwa kuwa walikuwa wakihitaji msaada mkubwa sana wa kufika kule walipoelekezwa bila kumuuliza mtu yeyote yule.
Ndege ilichukua masaa zaidi ya ishirini na ndipo ikaanza kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl Nyerere. Walipofika hapo, hawakutaka kukaa sana, walichokifanya ni kukata tiketi ya ndege ya kuelekea Morogoro huku lengo lao likiwa ni kufika katika mbuga ya Mikumi na moja kwa moja kuelekea katika hoteli iitwayo Mikumi National Park ambako huko ndipo wangeanza kumuulizia mtu ambaye walikuwa wakimtafuta, Gibson Lyimo.
Safari ya kwenda mkoani Morogoro ikaanza kwa kutumia ndege ya Precious na baada ya saa moja kuingia mkoani Morogoro ambako wakaanza kuyafuata magari ya kuelekea katika mbuga hiyo na kisha kuanza safari. Kila mmoja akilini mwake alikuwa akifikiria lake tu, mtu ambaye walitakiwa kumuua hakuwa huyo Gibson bali mtu ambaye alitakiwa kuuawa alikuwa mwanamke ambaye alikuwa akiishi nae katika kipindi hicho.
Walipofika katika hoteli hiyo iliyokuwa mbugani, wakachukua vyumba na kutulia huku upelelezi ukifanyika chini kwa chini. Walikaa katika hoteli hiyo kwa muda wa siku mbili na ndipo walipoamua kumuulizia Gibson kupitia kwa mkurugenzi wa hoteli hiyo.
“Mnamuuizia Gibson! Huyo mtu aliacha kazi kipindi kirefu cha nyuma. Kwa sasa hivi ni miongoni mwa watu wenye fedha nyingi sana hapa nchini” Mkurugenzi wa hoteli hiyo, Massawe aliwaambia.
“Kwa hiyo hatuwezi kupafahamu anapokaa?” Reuben aliuliza.
“Anakaa Dar es Salaam. Labda kama mnataka kulipia ili mfanyakazi wangu awapelekea huko mpaka nyumbani kwake” Massawe aliwaambia.
Reuben na wenzake hawakuwa na jinsi, kitu ambacho walikuwa wakikitaka kwa wakati huo ni kumfahamu mwanamke ambaye alikuwa akiishi na Gibson na kisha kufanya kile ambacho walikuwa wameagizwa, walichokifanya ni kumlipa mkurugenzi na kisha kupewa kijana mmoja ambaye walianza safari nae ya kuelekea Dar es Salaam.
Njiani hawakukaa kimya, mara kwa mara walikuwa wakimuuliza maswali mbalimbali kijana yule ambaye walikuwa nae kama namna mojawapo ya kuchunguza zaidi na kufahamu mambo mbalimbali kuhusiana na jiji la Dar es Salaam ambalo walikuwa njiani kuelekea uko.
Walipofika Dar es Salaam, moja kwa moja wakakodi teksi mbili ambazo ziliwapeleka mpaka hotelini na kisha Reuben peke yake kutoka na kuelekea uko alipokuwa akiishi Gibson huku akiongozana na yule kijana.
“Do you see that house? (Unaiona nyumba ile?)” Kijana yule alimuuliza Reuben huku akimuonyeshea nyumba aliyokuwa akiishi Gibson.
“Please! Stop the car (Tafadhali! Simamisha gari)” Reuben alimwambia dereva ambaye alisimamisha gari lile.
“Thank you for your help (Asante kwa msaada wako)” Reuben alimwambia kijana yule huku akimtaka dereva kuwarudisha hotelini.
“So, why dont you want to meet him? (Kwa hiyo kwa nini hautaki kuonana nae?)” Kijana yule alimuuliza Reuben.
“I wanted to know the place (Nilitaka kupafahamu)”Reuben alimwambia.
****
Mchakato bado ulikuwa ukiendelea kama kawaida, walihitaji kufanya mambo yao kwa haraka haraka hata kabla wiki haijakatika na kuwakutia ndani ya jiji la Dar es Salaam. Kitu ambacho walikuwa wakikitaka katika kipindi hicho kilikuwa ni bunduki tu.
Hawakutaka kumuua mke wa Gibson kwa kutumia silaha yoyote zaidi ya bunduki, wakaanza kuangalia uwezekano wa kupata bunduki lakini kila walivyoangalia, hawakuona dalili ya kuweza kuipata aina ya silaha hiyo.
Hawakutaka kujiuliza maswali mengi sana, wakaona kwamba hata mikono yao ilikuwa na nguvu sana kukabiliana na huyo mtu tena alikuwa mwanamke, kwao alionekana kutokuwa na usumbufu wowote ule. Wakajipanga upya, ilikuwa ni lazima utekaji ufanyike, tena kwa haraka sana.
Hawakujiuliza sana kuhusiana na usafiri ambao wangeutumia siku hiyo, teksi ya kukodi ndio ambayo ingetumika katika kufanya safari zao za huku na kule. Walichokifanya mara baada ya kuweka majadiliano ya muda mrefu, wakachukua ramani ambayo ilikuwa katika begi na kisha kuanza kuiangalia kwa makini.
Wakaanza kupanga kila kitu kwamba mara baada ya kumaliza kufanya kazi ambayo ilikuwa imewaleta nchini Tanzania basi ilikuwa ni lazima kuondoka kuelekea nchini Kenya tena kwa gari kwa kupitia njia ya Tanga, njia ambayo ingewafanya kutokea Mombasa na kisha huko kupanda ndege na kurudi nchini Marekani.
Kwao, kazi hiyo wala haikuonekana kuwa ngumu hata kidogo, waliona kwamba ingeweza kufanyika ndani ya masaa machache hata kabla ya kumtaarifu Katie na kumwambia kwamba kazi aliyokuwa amewatuma ilikuwa imefanyika, tena kwa mafanikio makubwa bila kuwa na tatizo hata moja.
Walipanga mambo mengi sana, walichokuwa wameanza kukifanya ni kuanza kwenda katika mtaa aliokuwa akiishi Gibson na kisha kuangalia mandhari yote. Hawakuona kama kungekuwa na ugumu sana, mitaani huko wala hakukuwa na kamera kama ilivyokuwa katika mitaa mingi jijini New York ambayo ilikuwa ikikaliwa na matajiri, mpaka hapo, tayari wakaiona kazi hiyo ya kumteka Prisca kuwa nyepesi sana.
Muda mwingi walikuwa wakishinda ndani ya chumba cha hoteli huku mishemishe yao ikiendelea kama kawaida, kila kitu ambacho walikuwa wakikipanga kilionekana kutokufaa, hivyo walikifuta na kuanza kupanga tena.
“I will be a doctor (Nitakuwa daktari)” Reuben aliwaambia wenzake.
“Ok! We will be your assistants (Sawa! Tutakuwa wasaidizi wako)” Filbert alimwambia Reuben.
Mpango ambao walikuwa wameufikia kwa wakati huo ilikuwa ni lazima wajifanye madaktari ambao walikuwa wametoka nchini Marekani kuja nchini Tanzania kwa ajili ya kuwatibia watoto na kuwapa chanjo ambayo ingekuwa na uwezo wa kuzuia magonjwa mbalimbali hasa katika kipindi cha ukuaji.
Wote walikuwa wamekwishajua kwamba Gibson alikuwa akiishi na mwanamke ambaye alikuwa na mtoto mdogo hivyo kama wangetumia njia hiyo ingekuwa ni rahisi kwao kumpata mwanamke huyo na kisha kutoroka nae kuelekea porini na kumuulia huko huko mbele ya safari kabla ya kuanza safari ya kuelea nchini Marekani.
Mpango ulikuwa umekwishapita, walichokifanya siku hiyo ni kwenda kwenye kituo kikubwa cha upokeaji na usambazaji madawa, MSD (Medical Store Departiment) na kisha kuanza kujitambulisha kama madaktari wakubwa ambao walikuwa wametoka nchini Marekani kwa nia ya kuja hapa kwa ajili ya kuwafanyia tiba watoto.
Wasimamizi hawakuonekana kufahamu kitu chochote kile, mbaya zaidi wala hawakuomba hata vitambulisho kutokana na kiasi kikubwa cha fedha kutolewa kwa kila aliyekuwa na nia ya kuomba vitambulisho vyao hasa katika ngazi za chini.
Kila mtu ambaye alikuwa akipewa fedha, alikuwa akiwaruhusu kufanya mambo mengine ambayo wala hayakutakiwa kufanywa kwa mtu yeyote ambaye hakuonyesha kitambulisho cha kumjulisha kama alikuwa daktari.
“Madawa hayatoki mpaka nivione vitambulisho vyao” Mkuu wa usambazaji madawa katika kitengo hicho, mzee Samweli alimwambia msaidizi wake.
“Ila mkuu inab.....”
“Nimesema hakuna. Kama wao ni madaktari iliwabidi waje na madawa yao kama watu wengine wanavyofanya. Wanakuja huku halafu dawa wanategemea kwetu, hauoni kama huu ni ujinga?” Mzee Samweli aliuliza.
“Kama ukiangalia, unaweza kusema ni ujinga, ila naomba ujifikirie mkuu, ni mara ngapi tumekuwa na vitu hapa nchini halafu tukashindwa kuvitumia? Wape nafasi waokoe roho za watoto wetu” Mrisho alimwambia mzee Samweli.
“Sasa wao wameigia ndani ya nchi yao kama nani? Mbona hatujasikia taarifa za ujio wao?” Mzee Samweli aliuliza.
“Wamesema kwamba walipokuja hapa hawakuja kama madaktari bali walikuja kama watalii mkuu” Msaidizi, Mrisho alimwambia Samweli.
“Kumbe ni watalii! Sasa utalii na udaktari unaingiliana vipi hapo?” Mzee Samweli aliuliza.
“Wao ni madaktari ambao wamekuja huku kwa ajili ya kufanya utalii kama sehemu ya mapumziko yao ya likizo. Walipofika hapa, wamesikitishwa na hali waliyoikuta hasa kwa watoto. Kwa hiyo sasa, wameamua kuuvua utalii na kuuweka pembeni na kisha kuuvaa udaktari wao na kuingia kazini huku wakiwa na lengo moja tu, kuwanusuru watoto wetu ambao wapo katika matatizo makubwa hasa katika kipindi cha ukuaji” Mrisho alielezea kwa kirefu.
“Hebu waite kwanza niwaone” Mzee Samweli alimwambia Mrisho ambaye aliwaita Reuben na wenzake ndani ya chumba kile.
Mazungumzo yakaanza upya ndani ya chumba kile. Reuben na wenzake walikuwa wamevaa nyuso za bandia, nyuso ambazo zilikuwa zikionyesha kwamba walikuwa na uhitaji wa kuwasaidia watoto wa Kitanzania ambao walikuwa wakikua huku wakishambuliwa na magonjwa mbalimbali.
Japokuwa walikuwa wakiongea mengi na kukubalika lakini wakaona kwamba kulikuwa na kitu cha ziada ambacho kilitakiwa kufanyika zaidi, umwagaji wa fedha ndani ya ofisi hiyo. Hawakutaka kuchelewa, walianza kujiumauma mwisho wa siku noti za dola mia moja zikawekwa mezani. Kwa haraka haraka mzee Samweli akazichukua na kuanza kuziangalia, zilikuwa noti za dola mia moja zilizokuwa kumi.
Kiasi cha dola elfu moja kilionekana kuwa kiasi kikubwa hasa kwa mtanzania kama mzee Samweli ambaye maisha yake yalikuwa yakitegemea sana mshahara wa kawaida. Wala hakutaka kujiuliza kama alitakiwa kuzichukua au kuziacha, alichokifanya ni kuziingiza mfukoni.
“Mrisho, hebu wapeleke stoo na kisha wape watakachokihitaji” Mzee Samweli alimwambia Mrisho ambaye alifanya kama alivyoambiwa.
Kwa Mtanzania, fedha ndio ilikuwa kila kitu, uwepo wa fedha ulikuwa na nafasi kubwa ya kubadilisha mambo mengi ambayo wala yasingeweza kubadilishwa. Fedha ikaonekana kuwa kila kitu, fedha hizo hizo ndizo ambazo zilikuwa zikiwafanya Reuben na wenzake kupelekwa katika stoo ya madawa ambako huko wakachagua madawa wanayoyataka na kisha kuondoka.
Kazi ilikuwa imebaki moja tu, kwanza ilibidi kwenda katika serikali ya mtaa wa Masaki na kuelezea kile ambacho kilikuwa kimewaleta mahali pale, walipofika huko, walimwaga kiasi kidogo cha fedha na wakaruhusiwa kufanya kazi zao katika mtaa huo.
Hawakuishia hapo, napo wakaenda mpaka katika hospitali ya Halmashauri iliyokuwepo Masaki na kisha kuongea na uongozi wa hospitali ambao ulionekana kuwa na furaha kupita kawaida, Reuben, Filbert na Endrew wakakaribishwa kuanza kufanya kazi katika hospitali hiyo.
Matangazo yakaanza kufanyika mitaani kwamba kulikuwa na chanjo ambayo ilikuwa ikitolewa kwa watoto waliokuwa chini ya miaka mitano na hivyo wazazi wao walitakiwa kuwapeleka watoto wao wao wenyewe kutokana na kutakiwa kuulizwa maswali mengi kuhusiana na watoto, chanjo hiyo ilitakiwa kufanyika siku inayofuatia.
“Nitampeleka Genuine huko huko kesho asubuhi” Prisca alimwambia mumewe, Gibson.
“Ni vizuri sana. Usimwache mfanyakazi ampeleke, si umesikia kwamba ni mzazi mwenyewe ndiye anayetakiwa kumpeleka?”
“Nimesikia mume wangu. Nitampeleka tu. Si wamesema mwisho jioni? Nitahakikisha nampeleka hata saa kumi” Prisca alimwambia Gibson.
“Hapana mpenzi. Nenda uko hata asubuhi. Usikawie, hauwezi kujua wingi wa watu. Wahi zako asubuhi tu” Gibson alimwambia Prisca.
“Sawa. Usijali mume wangu” Prisca aliitikia na kulala huku akiwa na hamu ya kumpeleka mtoto wake akapatiwe chanjo ya kumkinga na magonjwa mbalimbali katika kipindi chake cha ukuaji.

Je nini kitaendelea?
Je Katie atakamilisha mpango wake?
Kuanzia kesho hadithi hii itakuwa ikitoka mara mbili. Mchana na usiku.
 
MCHEZA FILAMU ZA NGONO 11

Gibson alikuwa amekaa ofisini mwake huku akiendelea kufanya kazi zake kama kawaida. Kwa wakati huo, akili yake alikuwa ameituliza kwa mke wake tu, hakutaka kumfikiria Katie wala kitu chochote ambacho kilikuwa kimetokea katika maisha yake pamoja na Katie.
Alikuwa amekwishaomba msamaha kwa mke wake kwa hiyo wala hakutaka kumkasirisha tena na wala hakutaka kutembea nje ya ndoa. Moyo wake ulikuwa ukimpenda mke wake zaidi ya kitu chochote kile katika maisha yake.
Mtoto wao, Genuine alikuwa chachu kubwa ya mapenzi yao, alimpenda sana mtoto wake na kumthamini sana. Mara kwa mara alikuwa akitamani kuwa karibu nae, kila alipokuwa akimwangalia Genuine, alikuwa akiona umuhimu wa kumpenda zaidi mke wake, Prisca.
Gibson aliendelea kufanya kazi zake kama kawaida. Ilipofika saa nne asubuhi, akaanza kujisikia hali ya tofauti moyoni mwake. Moyo ukaanza kujaa majonzi huku ukiwa mzito. Hali hiyo haikuonekana kuwa ya kawaida moyoni mwake, akaacha kufanya kila kitu na kutulia.
Hali haikuonekana kubadilika, bado alikuwa akiendelea kuihisi hali ile ile. Amani moyoni mwake ikatoweka, alichokifanya kwa wakati huo ni kuichukua simu yake na kuanza kuangalia baadhi ya namba, alipoona ameridhika, akampigia simu mke wake.
“Umefikia wapi?” Gibson alimuuliza Prisca.
“Kuhusu nini mpenzi?”
“Kumpeleka mtoto hospitalini”
“Ndio najiandaa mpenzi. Nilikuwa nikimnywesha uji kwanza”
“Sawa. Nisubiri nakuja”
“Vipi kuhusu kazi?”
“Hakuna tatizo mpenzi. Moyo wangu umekuwa mzito sana kubaki ofisini, amani imenitoweka kabisa moyoni” Gibson alimwambia Prisca.
“Mmmh! Sasa tatizo nini?”
“Bado sijajua. Nisubiri nije huko huko. Nitataka kuwa karibu na familia yangu” Gibson alimwambia Prisca.
“Sawa. Nakusubiri mpenzi” Prisca alijibu na kisha kukata simu.
Gibson hakutaka kuendelea kubaki ndani ya ifisi ile, alichokifanya ni kutoka na kisha kuanza kuelekea sehemu ya magari na kuchukua gari lake na kuanza kuelekea nyumbani kwake. Hali ya moyo wake wala haikubadilika kabisa, ilikuwa vile vile. Mawazo yalikuwa yakimsonga kichwani mwake, hakujua ni kitu gani ambacho kilikuwa kikitaka kutokea ambacho mpaka katika wakati huo kilikuwa kimemkosesha amani kabisa.
“Kuna nini tena? Mbona najisikia hivi moyoni?” Gibson alikuwa akijiuliza mara kwa mara lakini hakupata jibu lolote lile.
Kadri muda ulivyozidi kwenda mbele na ndivyo ambavyo hali ile ilivyozidi zaidi na zaidi, alikuwa akiendesha gari lake lakini akili yake ilikuwa ikifikiria mambo mengi kwa wakati huo. Alikuwa akizifikiria biashara zake kwa kuona kwamba labda kungekuwa na kitu kingetokea au aliona dalili fulani lakini kila alipokuwa akijzifikiria, hakuona jambo lolote lile baya.
Alifika nyumbani baada ya dakika kumi, kitu cha kwanza ni kuelekea chumbani kwake, alipokuta mke wake, akamkumbatia kwa furaha. Akaendelea kumuelezea mke wake juu ya hali ambayo alikuwa nayo moyoni, Prisca ndiye mtu pekee ambaye alikuwa akimtoa wasiwasi moyoni mwake.
“Usijali mume wangu. Kila kitu kitakuwa salama tu na wala halitotokea jambo lolote lile baya” Prisca alimwambia Gibson.
“Una uhakika?”
“Yeah! Hatutakiwi kuogopa kitu chochote kile mpenzi” Prisca alimuondoa wasiwasi Gibson.
“Ok! Twende huko hospitalini. Leo sitaki kukaa mbali nanyi kabisa. Ninyi ndio kila kitu kwangu” Gibson alimwambia Prisca.
Alipomaliza kujiandaa, Prisca na Gibson wakaanza kuelekea garini na kisha kuanza safari ya kuelekea katika hospitali hapo Masaki. Walitumia dakika chache sana wakawa wamekwishafika katika hospitali ile ambapo Prisca akaelekea kujiandikisha na kurudi benchini kwa mumewe.
“Vipi?”
“Nimejiandikisha tu”
“Kwa hiyo inabidi usubiri hapa kama wenzako?”
“Ndio”
“Sawa”
Waliendelea kukaa katika lile benchi huku wanawake wengine wakiendelea kufika mahali pale pamoja na watoto wao. Baada ya dakika thelathini, zamu ya Prisca ikafika na kuingia ndani ya chumba kile kwa ajili ya kuhudumiwa huku Gibson akimsubiria benchini.
Dakika ziliendelea kusonga mbele lakini Prisca hakutoka nje ya chumba kile jambo ambalo lilionekana kumtia wasiwasi Gibson na kuwakasirisha wanawake wengie ambao walionekana kuwa na haraka. Gibson akaendelea kuwa mvumilivu, nusu saa ya kwanza ikapita, saa moja likatimia lakini Prisca hakuweza kutoka ndani ya chumba kile.
Gibson akaonekana kushikwa na wasiwasi, hakujua ni kitu gani ambacho kilikuwa kikiendelea ndani ya chumba kile mpaka mke wake kucheleweshwa kutoka namna ile na wakati wanawake wengine walikuwa wakitumia dakika tano hadi kumi.
Gideon akasimama na kuanza kuusogelea mlango ule na kisha kutaka kuufungua, mlango ulikuwa umefungwa kwa ndani. Tayari Gibson akazidi kushikwa na wasiwasi zaidi, alicokifanya ni kuwasiliana na ofisi ya dokta mkuu ambaye akafika mahali hapo haraka sana.
Wote wakajaribu kufungua mlango lakini wala haukufunguka. Kila mmoja alibaki kuwa na maswali juu ya kitu ambacho kilikuwa kikiendelea ndani ya chumba kile.
“Ngoja nipitie mlango wa nyuma” Dokta kuu, Kimaro alimwambia Gibson.
“Kuna mlango wa nyuma?” Gibson aliuliza.
“Ndio”
Gibson hakutaka kumuacha daktari aende peke yake, alichokifanya ni kwenda pamoja nae. Walipofika nyuma, mlango ulikuwa umefungwa lakini walipojaribu kuufungua, ulifunguka. Kila mtu akapigwa na mshangao, ndani ya chumba kile hakukuwa na mtu yeyote yule jambo ambalo lilionekana kumshtua kila mtu.
“Hawapo. Mungu wangu! Mke wangu na mtoto wangu!” Gibson alisema kwa mshtuko.
*****
Huduma za kuwahudumia watoto zilikuwa zikiendelea kama kawaida hu wakiwa wamekabidhiwa chumba ambacho kilikuwa na mlango wa nyuma ambao ulionekana kuwa kama mlango wa tahadhari. Japokuwa mlango huo ulikuwa haujafunguliwa kwa muda wa miaka mitatu lakini Reuben akahitaji mlango huo ufunguliwe.
Hakukuwa na daktari ambaye alileta ubishi wowote ule, mlango ukafunguliwa. Saa nne asubuhi, huduma ya chanjo kwa watoto ikaanza, wanawake wengi walikuwa wamewaleta watoto wao kwa ajili ya kufanyiwa chanjo. Walichokifanya Reuben, Filbert na Andrew ni kuwaandikisha wanawake ambao walikuwa wakiwaleta watoto wao pamoja na majina ya wanaume ambao walikuwa wamezaa nao.
Hiyo ndio ilionekana kuwa nafasi pekee ambayo ingewafanya wao kumjua mwanamke ambaye angekuja mahali hapo na kuona kwamba huyu alikuwa mke wa mtu ambaye walikuwa wakimtafuta, Gibson. Wanawake walizidi kumiminika hospitalini hapo pamoja na watoto wao ambako moja kwa moja wakajiandikisha majina yao.
“Is she here? (Yupo hapa?)” Reuben alimuuliza Filbert ambaye alikuwa akiendelea kuandikisha majina.
“Nope. She ain’t here (Hapana. Hayupo hapa)” Filbert alijibu.
Bado wanawake walikuwa wakiendelea zaidi na zaidi kujiandikisha katika kupata huduma za watoto wao kupatiwa chanjo katika hospitali ile kutoka kwa wazungu ambao walionekana kuja kutoa msaaada bila kufahamu lengo ambalo lilikuwa limewaleta mahali pale na kujifanya kutoa huduma hiyo.
Dakika ziliendelea kwenda mbele mpaka pale ambapo Prisca alipokuja kujiandikisha. Filbert akaonekana kushtuka, hakuamini kwamba hatimae walikuwa wamempata mtu ambaye walikuwa wakimsubiria kwa kipindi kirefu. Alichokifanya ni kusimama na kuelekea ndani ya chumba kile cha tiba huku lengo lake likiwa ni kuongea na wenzake.
“She is here (Yupo hapa)” Filbert aliwaambia.
“Are you sure? (Una uhakika?)
“100% (Asilimia mia moja)”
Reuben hakuonekana kuamini, alichokifanya ni kuufungua mlango huku akijifanya kuwaangalia wanawake ambao walikuwa wamekusanyika katika mabenchi. Wanawake zaidi ya ishirini walikuwa wamekaa kwenye mabenchi yale huku mwanaume akiwa mmoja tu, Gibson.
“There she is (Yule pale)” Fibert alimwambia Reuben.
Tabasamu pana likaonekana usoni mwa Gibson, tayari alikuwa ameyaona mafanikia makubwa mbele yao, kitendo cha Prisca kufika mahali pale kilionekana kumfurahisha kupita kawaida. Alikuwa na uhakika wa asilimia mia moja kwamba yule ndiye alikuwa mke wa mtu ambaye walikuwa wakimsubiria mahali hapo kutokana na Gibson mwenyewe kuonekana pembeni yake.
Walichokifanya ni kuendelea kutoa huduma kama kawaida yao. Waliandaa kila kitu, gari ambalo walikuja nalo tayari walikuwa wamekwishalipeleka nyuma ya chumba kile ili lisiwape usumbufu wowote wakati wa kutoka katika hospitali hiyo.
Wanawake waliendelea kuingia na kutoka mpaka pale zamu ya Prisca ilipowadia. Akasimama huku akiwa amembeba mtoto wake, genuine na kuingia ndani ya chumba kile huku mume wake, Gibson akiwa amemuacha benchini.
Kitu alichokifanya Reuben wakati Prisca ameingia ndani ni kumchukua mtoto wake, Daniel na kisha kumvutisha Prisca kitambaa kilichokuwa na dawa ya usingizi, wala hazikupita hata sekunde kumi, Prisca akapitiwa na usingizi mzito.
Hakukuwa na muda wa kuchelewa mahali hapo, walichokifanya ni kumbeba Prisca pamoja na mtoto wake na kisha kuanza kuelekea nae nje ambako wakawaingiza ndani ya gari. Kila kitendo ambacho kilikuwa kikiendelea mahali hapo, hakukuwa na mtu ambaye alikuwa akikiona kutokana na lile gari kupakiwa nyumba kabisa ya chumba kile, mahali ambapo si watu wengi walikuwa wakifika mara kwa mara.
“What next? (Nini kinafuata?)” Andrew aliuliza.
“Lets get out of here (Tuondokeni mahali hapa)” Reuben aliwaambia na kisha Andrew kuwasha gari lile.
Andrew hakutaka kuendesha gari kwa mwendo wa kasi kwa kuogopa kushtukiwa, alichokifanya ni kuendesha gari kwa mwendo wa taratibu na kutoka nje ya hospitali ile huku kukiwa hakuna hata mtu mmoja ambaye alikuwa akifahamu kitu ambacho kilikuwa kikiendelea mahali pale.
Safari ambayo walikuwa wameipanga kwa wakati huo ilikuwa ni kuondoka na kuelekea Tanga ambako huko wangeumuua Prisca porini na kuunganisha safari yao kuelekea Mombasa na kisha kuelekea Nairobi ambako wangepanda ndege na kuelekea nchini Marekani huku wakiwa wamekwishakamilisha kila kitu walichokuwa wameambiwa wakamilishe nchini Tanzania.

Je nini kitaendelea?
Je Reuben na wenzake wataweza kumuua Prisca kama walivyopanga?
Je watekaji wataweza kukamatwa?
Itaendelea saa moja kamili usiku.
Usikose.
 
MCHEZA FILAMU ZA NGONO 12

Kila mmoja alionekana kuchanganyikiwa, kutokumkuta mtu yeyote ndani ya chumba kile kuliwachanganya zaidi. Gibson hakuonekana kuamini kile ambacho alikuwa akikiona, hakuamini kama mke wake, Prisca pamoja na mtoto wake, Genuine hakuwa ndani ya chumba kile. Kila mmoja alikuwa akijiuliza mahali ambapo walikuwepo watu hao lakini hakukuwa na mtu ambaye alikuwa na jibu.
Kitu walichokifanya ambacho kilikuwa ni cha haraka sana ni kuwasiliana na polisi na kisha kuwaelezea kila kitu ambacho kilikuwa kimetokea. Ni ndani ya dakika kumi, mapolisi wa kituo cha Masaki wakafika mahali hapo huku wakiongozana na polisi wa kituo cha Oysterbay.
Dokta akaanza kuelezea kila kitu ambacho kilikuwa kimetokea hospitalini hapo kuhusiana na wazungu hao ambao walikuwa wamefika mahali hapo kama madaktari ambao walifika mahali hapo kwa ajili ya kutoa chanjo kwa watoto wadogo walio chini ya miaka mitano.
“Unasema walitoka wapi?” Gibson aliuliza.
“Nchini Marekani” Dokta alijibu.
Tayari Gibson akaonekana kuwa na wasiwasi mwingi mahali hapo, kichwa chake kikawa kama kimekwishahisi kitu fulani ambacho kilikuwa kimeendelea mahali hapo. Gibson akaondoka na kwenda kukaa pembeni kabisa ya polisi wale huku akionekana kuwa mwingi wa mawazo.
“Vipi?” Dokta alimuuliza mara baada ya kumuona akiwa ameelekea kule pembeni.
“Mke wangu na mtoto wangu”
“Usijali. Tumekwishatoa taarifa polisi, wanalifanyia kazi” Dokta alimwambia Gibson.
Polisi hawakutaka kulala, mtu ambaye alikuwa akilalamika kwamba mke wake na mtoto wake walikuwa wametekwa na watu kutoka nchini Marekani na ambao walijifanya kama madaktari walikuwa wakimfahamu sana. Gibson alikuwa ni tajiri mkubwa nchini Tanzania ambaye alikuwa akisaidia watu mbalimbali nchini hasa wale ambao walikuwa na matatizo mbalimbali.
Ni ndani ya dakika arobaini, waandishi wa habari wakafika mahali hapo na kuanza kupewa maelezo juu ya kile ambacho kilikuwa kimetokea. Muda wote Gibson hakuwa muongeaji, alikuwa kimya huku akionekana kuwa mwingi wa mawazo.
“Ni Katie. Huyu atakuwa Katie tu” Gibson alijisemea.
Mawasiliano yakaanza kufanyika, tayari polisi walikwishajua kwamba watekaji hao bado wangekuwa ndani ya jiji la Dar es Salaam tu. Simu zikaanza kupigwa sehemu mbalimbali kwa ajili ya kuimarisha ulinzi huku aina ya gari lile ambalo walikuwa wameondoka nalo likiwa linatolewa taarifa kwa kila aliyeambiwa japokuwa namba zake hawakuwa wakizifahamu.
Walichokiona kwa wakati huo, walijua fika kwamba watu hao walikuwa na uwezekano wa kuondoka kuelekea Bagamoyo, Barabara ya Morogoro au ile ya kwenda Mtwara. Kitu walichoona kuwa cha maana ni kuwasiliana na polisi wote ambao walikuwa katika sehemu hizo na kuwaambia kwamba ulinzi na upekuzi wa magari ulikuwa ukihitajika kufanyika tena kwa haraka sana.
Vyombo vya habari hasa televisheni na redio vikaanza kutangaza kile ambacho kilikuwa kimetokea, kila mtu akaonekana kushangaa, taarifa ile ilionekana kuwashtua kupita kawaida. Kila mtu akalaani kitendo kile ambacho kilikuwa kimetokea, utekaji ulionekana kuwa kitu kigeni sana kutokea nchini Tanzania.
“Watekaji ni lazima wakamatwe na mateka ni lazima wapatikane wakiwa hai” Kamanda mkuu wa jeshi la polisi, Oswald aliwaambia waandishi wa habari huku mapolisi wakiwa wamekwishaanza kazi yao.
****

Taarifa ile ilikuwa ikiendelea kusambazwa kama kawaida na ilivuma kwa kasi hata zaidi ya upepo. Kila mtu ambaye alikuwa akisikia alionekana kutokuelewa ni kitu gani ambacho kilikuwa kimetokea mpaka Prisca na mtoto wake kutekwa manyara.
Polisi wakaanza kuzunguka ndani ya jiji la Dar es Salaam huku lengo lao likiwa ni kulitafuta gari lile ambalo lilikuwa linaendeshwa na watekaji wale. Kila kona, polisi walikuwa wakizunguka zunguka, watu ambao walikuwa wakisafiri kwa kutumia ndege, safari zilikuwa zimesimamishwa kwa muda, msako ulikuwa ukiendelea kila kona.
Kwa wakati huo, Gibson pamoja na dokta mkuu wa hospitali ya Masaki, dokta Philip walikuwa wamekwishafikishwa katika kituo cha polisi kwa ajili ya maelezo zaidi. Kila mmoja alikuwa akitoa maelezo yake juu ya kila kitu ambacho kilikuwa kimetokea.
“Ina maana hamna uhakika kwamba watu hao walikuwa madaktari?” Manase ambaye alikuwa polisi aliyehusika zaidi kwenye kuhoji watu alimuuliza dokta Philip.
“Sikuwa na uhakika lakini kila nilipoona vibari vyote walivyokuwa navyo, niliridhika nao na wala sikutaka kuhoji maswali zaidi” Dokta Philip alijibu.
“Kwa hiyo walikuwa na vibali vyote?”
“Ndio”
Manase hakutaka kuendelea kubaki ndani ya chumba kile, akawaacha na kisha kuelekea nje ambako huko akaanza kuongea na polisi wengine, simu zikaanza kupigwa sehemu mbalimbali na kisha kurudi tena ndani ya chumba kile.
Hadi kufikia wakati huo, hali ilionekana kuwachanganya kupita kawaida. Ni kweli walikuwa na uhakika kwamba watu wale hawakuwa madaktari lakini walivipata wapi vibali ambavyo viliwaonyesha kwamba wao walikuwa madaktari?
Kila swali ambalo walikuwa wakijiuliza lilionekana kuwachanganya kupita kawaida, kwao, watu hao wakaonekana kujiandaa kupita kawaida katika kufanya kila kitu ambacho walikuwa wamepanga kukifanya kwa wakati huo.
“Unahisi kitu chochote kile?” Manase alimuuliza Gibson.
“Ndio”
“Kitu gani?”
“Kuna mtu amehusika katika tukio hili”
“Mtu gani?”
“Kuna mwanamke mmoja amehusika”
“Mwanamke yupi?”
“Katie”
“Ndiye nani huyo?”
“Mcheza filamu za ngono aishiye nchini Marekani”
Manase na dokta Phillip wakaonekana kushtuka, jibu ambalo alilitoa Gibson likaonekana kuwashangaza sana. Hawakujua ni kwa nini Gibson aliwaamba maneno yale, hawakujua kama Gibson alikuwa na uhakika juu ya kile ambacho alikuwa amekisema au la.
“Unatuchanganya. Ndiye nani huyo?” Manase aliendelea kuuliza.
“Mcheza filamu za ngono” Gibson alijibu.
Hapo ndipo Gibson alipoanza kuelezea kila kitu kilichotokea katika maisha yake huku akizungumzia kwa undani kila kitu ambacho alikuwa amekifanya pamoja na Katie. Kila mmoja alikuwa makini akimsikiliza, mpaka anamaliza, kila mmoja alikuwa na uhakika kwamba Katie alikuwa amehusika katika mchezo mzima.
“Amehusika katika hili” Manase alimwambia Gibson.
Manase akatoka ndaniya chumba kile na kisha kuanza kuongea na wenzake kuhusiana na kila kitu ambacho alikuwa ameambiwa na Gibson. Taarifa zikaanza kutolewa sehemu mbalimbali ila kitu kikubwa ambacho kilikuwa kikihitajika kwa wakati huo ilikuwa ni kuhakikisha kwamba watekaji wale wanakamatwa na hatimae kumtaja mhusika aliyewatuma kufanya utekaji ule.
“Kuna tetesi zozote?”
“Ndio. Watu wa Chalinze walisema kwamba waliliona gari hilo likipita kwa kasi”
“Kuelekea wapi?”
“Kama si Kilimanjaro, basi itakuwa Tanga”
“Sawa sawa. Wapigieni simu polisi wa Segera na kuwaambia kwamba inawapasa kuangalia kwa makini magari yote yatakayopita huku sisi tukianza safari kwenda huko” Manase aliwaambia na kisha kutoka nje ya ofisi ile pamoja na Gibson na dokta Manase na kisha kuanza kuelekea Segera ambako walijua fika kwamba watekaji wale wasingeweza kuvuka salama bila kukamatwa.
“Chochote kitakachotokea kwa familia yangu. Nitawaua wote waliohusika” Gibson alisema huku akionekana kuwa na hasira.
****
Mara baada ya kutoka katika hospitali ya Masaki moja kwa moja safari ya kuelekea Tanga ikaanza huku wakiwa wamekwishajikamilisha kwa kila kitu. Andrew ambaye alikuwa katika usukani akiliendesha gari lile wala hakutaka wachukue muda mwingi kuchelewa njiani, kila alipoona kwamba hakukuwa na magari mengi barabarani, alikuwa akiendesha kwa mwendo wa kasi.
Prisca bado alikuwa amelala usingizi mzito huku mtoto wake, Genuine akiwa analia kupita kawaida kiasi ambacho akaanza kuonekana kuwa kero kwa watekaji wote ambao walikuwa ndani ya gari lile. Kadri Genuine alivyokuwa akizidi kulia na ndivyo ambavyo kelele zile zilionekana kuwa kero zaidi.
Hawakujua ni kitu gani ambacho walikuwa wakitakiwa kukifanya kwa wakati huo, vichwani mwao kulikuwa kukifikiriwa vitu viwili tu, ilikuwa ni lazima wamtupe mtoto huyo barabarani au kama walikuwa wakitaka kwenda nae basi ilikuwa ni lazima kufanya kitu ambacho kingemfanya mtoto yule kutokulia kwa sauti kubwa kama ilivyokuwa.
“What should we do? (Tunatakiwa tufanye nini sasa?)” Filbert aliuliza.
“Open the window (Fungua dirisha)” Reuben alimwambia Filbert.
“What for? (Ili iweje?)” Filbert aliuliza huku akionekana kushtuka.
“I want to do something (Nataka kufanya kitu)” Reuben alimwambia Filbert.
“This is crazy Reuben, dont dare to do what you want to do (Huu ni upuuzi Reuben, usithubutu kufanya hicho unachotaka kukifanya)” Filbert alimwambia Reuben.
“I have to do this Fil. If I ain’t do this, then, we are going to die (Inanibidi nifanye hiki Fil. Kama sitofanya hivi, tunakwenda kufa)” Reuben alimwambia Filbert.
Mtafaruku bado ulikuwa ukiendelea ndani ya gari huku Andrew akiwa bize kuendesha gari kwa kasi. Kitu ambacho alikuwa akikitaka Reuben kilikuwa ni kumtupa mtoto Genuine dirishani huku gari likiwa kwenye mwendo ule wa kasi lakini Filbert hakutaka kuona kitu hicho kikitokea.
Walikuwa wamekwishafika Kimara, sehemu ambayo magari mengi yalikuwa barabarani huku hata idadi kubwa ya watu ikiwa pembezoni mwa barabara. Kitu alichokuwa akikitaka Filbert ni kumtupa Genuine katika eneo ambalo halikuwa na wakazi wengi kwani kama wangefanya vile mahali pale basi ilikuwa ni lazima kugundulika tu.
Safari ilikuwa ikiendelea kama kawaida, hakukuwa na mtu yeyote ambaye alikuwa akilitilia mashaka gari lile ambali bado lilikuwa likiendelea na safari ya kuelekea Tanga. Kutokana na mwendo wao kuwa mkali, walichukua dakika arobaini wakawa wamekwishafika Chalinze.
“Twende kulia” Reuben alimwambia Andrew ambaye akakata kulia. Ramani ambayo walikuwa nayo mikononi mwao ndio ambayo ilikuwa ikiwaongoza katika kila njia ambayo walikuwa wakienda kwa wakati huo. Lengo lao kubwa kwa wakati huo lilikuwa ni kufika Tanga ambapo huko wangeonganisha mpaka Mombasa na kuelekea Nairobi na kisha kuchukua ndege na kurudi nchini Marekani hasa mara baada ya kukamilisha kumuua Prisca.
Walitembea na gari lao kwa muda wa dakika thelathini, wakaanza kufika katika maeneo mengi ambayo hayakuwa na makazi, maeneo ambayo yalikuwa na miti mingi sehemu zilizoonekana kuwa kama pori. Hapo ndipo makubaliano yale yakafikiwa muafaka, walitakiwa kumtupa Genuine kupitia dirishani huku gari likiwa katika mwendo ule ule wa kasi.
Huku wakiwa wamekwishakubaliana kitu cha kufanya, ghafla Prisca akaamka kutoka katika usingizi na kuanza kushangaa mahali ambapo alipokuwa. Fahamu zilivyomjia vizuri, akaonekana kukumbuka kila kitu.
Kitu cha kwanza akaanza kumtafuta mtoto wake, tayari alikuwa katika mikono ya Reuben ambaye alikuwa akijiandaa kumtupa nje Genuine kupitia katika dirisha lile huku Filbert akiwa amekwishafungua dirisha.
Hata kabla Prisca hakuongea kitu chochote kile, Reuben alikifanya kitu kimoja tu, akamtupa Genuine nje kupitia dirisha huku gari likiwa katika mwendo mkali wa kilometa 120 kwa saa. Kilichosikika ni sauti ya Genuine tu ambaye akajigonga katika miti kadhaa, damu zikatapakaa katika kila mti aliojiginga na kuwa mwisho wake.
Lilikuwa ni tukio kubwa na baya katika macho ya Prisca, hakuamini kile ambacho alikuwa amekiona kwa wakati ule. Akapiga uy owe mmoja tu, akajikuta akipoteza fahamu, tukio ambalo alikuwa amelishuhudia kutupwa kwa mtoto wake lilionekana kumshtua, kumuumiza kupita kawaida.
Hakukuwa na mtu yeyote ambaye alikuonekana kujali, kitu ambacho walikuwa wakikitaka mahali hapo ni kufika Tanga ambapo wangeonganisha mpaka Mombasa, ila kabla ya kufika Mombasa, ilibidi wamuue Prisca na kisha kuendelea na safari ya kuingia Mombasa.
“Kuna tatizo mbele yetu” Andrew aliwaambia huku wakiwa wamekaribia kufika Segera, njia panda ya kuendea Kilimanjaro na Tanga.
“Kuna nini?”
“Kuna magari mengi yanaonekana kusimamishwa, nafikiri kuna kitu kinaendelea” Filbert alijibu.
“Tumia mpango B” Reuben alimwambia Andrew huku akiangalia ramani aliyokuwa ameishika.
“Usijali. Nimekusikia kiongozi” Andrew aliitikia.
****
Mpango B ukafanyika mahali hapo, Andrew akakata kona kulia na kuingia kichakani. Mwendo ulikuwa ni wa kasi sana, katika kipindi hicho tayari walikuwa wamekwishashikwa na wasiwasi kwamba polisi walikuwa wamekwishagundua na hivyo walikuwa katika kila njia kuhakikisha wanakamatwa.
Bado Andrew alikuwa akiendesha gari kwa kasi, katika kipindi hicho walidhamiria kuingia mkoani Tanga ambako wangeanza kuelekea Zigaya ambako wala hakukuwa mbali sana kuingia Mombasa nchini Kenya.
Kila mtu aklini mwake alikuwa akifikiria lake kwa wakati huo, ni kweli kwamba walikuwa wakitamani sana kufika nchini Kenya ambako huko wangechukua ndege na kuelekea nchini Marekani lakini uwepo wa Prisca ndani ya gari uliwafanya kuchanganyikiwa.
Lengo kubwa hasa ambalo lilikuwa limewaleta nchini Tanzania lilikuwa ni kumuua Prisca lakini cha kushangaza, mpaka muda huo hawakuwa wamekamilisha kile kilichokuwa kimewaleta nchini Tanzania japokuwa Prisca walikuwa nae.
Safari ilikuwa ikiendelea zaidi huku ramani ambayo walikuwa nayo ndio ambayo ilikuwa ikiwasaidia katika kuwaongoza kule ambako walikuwa wakiendelea kwenda mbele. Kwanza kitu ambacho walikuwa wakikitaka kwa wakati huo kilikuwa ni kuingia Tanga mjini ambako wangeongeza mafuta kwenye gari lao na kisha kuendelea na safari yao kama kawaida.
Masaa mawili yakakatika huku wakiwa bado wakitembea porini na ndipo wakaamua kuingia barabarani. Hapo, Andrew akaongeza mwendo zaidi, walijiona kuwa nyuma ya muda, walikuwa wakitaka kufika haraka iwezekanavyo ili kazi yao izidi kuwa nyepesi zaidi.
Wakaingia Tanga mjini saa sita kasoro mchana na moja kwa moja kuanza kuelekea katika kituo cha mafuta kwa ajili ya kuongeza mafuta kabla ya kuendelea na safari yao zaidi. Hakukuwa na mtu ambaye alikuwa na wasiwasi wowote ule, wakazi wengi wa Tanga hawakuonekana kulitilia umakini tangazo ambalo lilikuwa limetolewa katika vyombo mbalimbali vya habari juu ya utekaji ambao ulifanyika jijini Dar es Salaam.
“Lets make hurry (Tufanyeni haraka)” Filbert aliwaambia.
“Dont worry. We are safe in here (Usihofu. Hapa tupo salama)” Reuben alimwambia Filbert huku akionekana kutokuwa na wasiwasi wowote ule.
“There is no more peace. I have seen the news on the television about us (Hakuna amani hapa. Nimeona habari kwenye runinga kuhusu sisi)” Filbert aliwaambia.
“Thats not true. When did you learn to undrestand Swahili language? (Hiyo si kweli. Umejifunza lini lugha ya Kiswahili?)” Reuben aliuliza huku uso wake ukiwa na tabasamu.
“I saw Gibson on the television, then tell me what do you think is goin on (Nimemuona Gibson runingani, aya niambie unafikiri nini kinaendelea?)” Filbert alikuwa akijitahidi kuelezea kila kitu ambacho alikuwa amekiona kwenye televisheni lakini hakukuwa na mtu yeyote ambaye alionekana kumuamini, wote walimuona Filbert kuwa mtu muoga sana.
Kitu ambacho walikuwa wakikitaka kwa wakati huo ni kula chakula hata kabla safari yao haijaendelea zaidi na zaidi. Wakaenda hotelini na kuingia ndani, wakala chakula na kisha kuendelea na safari yao.
Muda wote huo, Prisca alikuwa amepoteza fahamu, mshtuko mkubwa ambao alikuwa amekutana nao ulikuwa ulimfanya kuwa katika usingizi mzito mpaka katika kipindi hicho. Hakukuwa na mtu ambaye alionekana kujali, kupoteza fahamu kwa Prisca kulionekana kuwa nafuu kwao kwa kuamini kwamba hakukuwa na usumbufu wowote kwa wakati huo ndani ya gari.
Wakaanza kushika barabara ya kuelekea Mombasa, daladala nyingi zilikuwepo njiani, idadi ya watu ilikuwa kubwa barabarani huku kila sehemu kukionekana kuwa na uchangamfu mkubwa. Kitu ambacho walikuwa wamekifanya kwa wakati huo, waliandaa fedha za kutosha kwa kuamini kwamba kama wangefika mpakani, wasingeruhusiwa kuvuka ila kwa kutumia dola ambazo walikuwa nazo, wala kusingekuwa na tatizo lolote lile.
Safari iliendelea mbele zaidi na zaidi, tayari walikuwa wamekamilisha asilimia themanini ya kazi ambayo walikuwa nayo na zilibakia asilimia ishirini tu, za kuingia Mombasa, kusafiri mpaka Nairobi na kisha kuchukua ndege na kurudi nchini Marekani huku wakiwa na ushindi mkubwa mioyoni mwao kitu ambacho kingekuwa furaha kubwa kwa Katie ambaye alikuwa amewatuma nchini Tanzania.
“Tufanyeni kitu kimoja” Filbert aliwaambia.
“Kitu gani?” Reuben aliuliza.
“Tumuueni huyu mwanamke kabla hatujaingia nchini Kenya. Yaani namaanisha kabla hatujafika mpakani”
“Wazo lako zuri. Nafikiri umeona kwamba anaweza kutuletea matatizo hapo mpakani”
“Hilo ndilo nililolifikiria” Filbert aliwaambia.
Wazo ambalo lilitolewa na Filbert likaonekana kufaa sana, walichokifanya kwa wakati huo ni kukata kona na kisha kuanza kuingia porini, sehemu ambayo wangeweza kumuua Prisca huko na kisha kuendelea na safari yao ya kuelekea mpakani.
Ghafla, Prisca akarudiwa na fahamu, akabaki akimwangalia kila mtu ndani ya gari lile. Kwa mara ya kwanza hakuonekana kukumbuka kitu chochote kile ila baada ya sekunde kadhaa, akakumbuka mambo mengi, likiwepo lile la kutupwa kwa mtoto wake, Genuine.
Prisca akaanza kulia, akamvamia Reuben kwa lengo la kupambana nae kwa kile kitendo cha kumtupa mtoto wake nje ya gari na wakati gari hilo lilikuwa kwenye mwendo wa kasi. Reuben akafanikiwa kumdhibiti Prisca ambaye akalazwa kitini huku akiwa amekandamizwa na kiganya cha Reuben.
Walipofika porini zaidi, gari likasimamishwa na kisha Reuben kumtoa Prisca nje ya gari huku akiwa amemshika shingoni. Prisca alikuwa akilia kama mtoto, akili yake kwa wakati huo ilikuwa kama imechanganyikiwa, hakumpenda Reuben hata kidogo, alikuwa akimchukia kupita kawaida.
“Niachieeeeee....niachieeee” Prisca alikuwa akipiga kelele lakini Reuben hakuweza kumuachia.
Kila kitu kwa wakati huo kikaonekana kuwa na amani, mazingira yalionekana kumridhisha kila mtu. Kitendo kilichokuwa kikitakiwa kufanyika mahali hapo kilikuwa ni kumuua Prisca na kisha kuondoka kuelekea mpakani.
Alichokifanya Reuben kwa wakati huo ni kuanza kumkaba roba kali Prisca. Prisca akabaki akitoa milio ya tofauti tofauti huku akijitahidi kutaka kuitoa mikono ya Reuben shingoni mwake lakini wala hakuweza kufanikiwa hata kidogo. Kadri muda ulivyozidi kwenda mbele na ndivyo ambavyo Reuben alivyomkaba zaidi na zaidi.
Ghafla, Prisca akaanza kuona kizunguzungu huku giza la mbali likianza kuonekana mbele yake. Tayari kwa wakati huo alikuwa amebakisha muda mchache sana wa kuwa hai, muda ambao wala haukuzidi hata dakika mbili. Giza lile alilolkuwa akiliona kwa mbali likaanza kumsogelea zaidi na zaidi, baada ya hapo, akayafumba macho yake huku akihisi mtoa roho akiwa amekwishamfikia kwa ajili ya kuichukua roho yake.

Je nini kitaendelea mahali hapo?
Je Prisca amekufa?
Je watekaji watakamatwa?
 
MCHEZA FILAMU ZA NGONO 13

Mhudumu wa mghahawa wa Casannova ambao ulikuwa katika hoteli ile ile ya Cassanova bado alikuwa akiwahudumia wateja wake, Reuben, Filbert na Andrew kama kawaida yake. Kila wakati alikuwa akiitwa na kurudi huku akiwa na vinywaji mbalimbali mikononi mwake.
Hamadi hakuonekana kuwa na wasiwasi na wateja wale, alikuwa akiendelea kuwahudumia kama kawaida yake. Hakutaka kuongea nao hata kidogo japokuwa moyo wake ulikuwa na shauku kubwa ya kutamani kuongea na wazungu.
Wazungu wale kwake walionekana kuwa tofauti kidogo, walionekana kuwa haraka huku muda mwingi macho yao wakiwa hawayatulizi sehemu moja. Hamadi hakuonekana kujali sana hali ambayo walikuwa nao, kitu ambacho alikuwa akiendelea kukifanya ni kuendelea kuwahudumia kama kawaida tu.
Wateja wote zaidi ya ishirini ambao walikuwa kwenye mghahawa ule walikuwa wamekwishahudumiwa na wakati huo walikuwa wakiendelea kula kitendo ambacho kilimfanya Hamadi na wahudumu wengine wa mghahawa ule kutulia pembeni huku nao wakiangalia televisheni.
Habari ya utekaji ikaanza kutolewa, kila mhudumu alionekana kuwa na utulivu mkubwa kuangalia televisheni ambayo ilikuwa imewekwa kituo cha televisheni ya Taifa. Taarifa ile ikaonekana kumshtua kila mmoja, mtangazaji alikuwa akitangaza kwamba kulikuwa na wazungu watatu ambao walikuwa wamehusika na utekaji wa mwanamke mmoja na mtoto mmoja ambaye alikuwa na umri wa takribani mwaka mmoja.
“Watekaji hao wanakisiwa kukimbilia mkoani Kilimanjaro, Tanga, Arusha au Manyara” Mtangazaji alisema huku akionekana kutokuwa na uhakika.
Hapo ndipo ambapo Hamadi alipoanza kuwaangalia wazungu wale ambao walikuwa mezani. Kwanza akaanza kuwahesabu kwamba walikuwa watatu kama ambavyo mtangazaji alikuwa ametangaza kwenye televisheni, akawaangalia tena, wawili nywele zao zilikuwa nyeupe na mmoja nywele zake zikuwa nyeusi, nao wale wazungu walikuwa vile vile.
Kila kitu ambacho kilikuwa kikitangazwa kuhusiana na watekaji nyara wale, kilikuwa kikifanana sana na wazungu wale ambao walikuwa wamekaa katika mghahawa ule. Hamadi akashindwa kuvumilia, tayari alikuwa na uhakika kwamba wale watekaji ambao walikuwa wakizungumziwa kwenye televisheni walikuwa wale wazungu ambao walikuwa katika mghahawa ule.
Alichokifanya Hamadi ni kutoka na kuanza kuelekea jikoni. Alipofika huko, akachomoa simu yake na kuanza kupiga namba za polisi ambazo zilikuwa zikijulikana sana 911. Simu ikaanza kuita, wala haikuita muda mrefu, ikapokelewa na sauti nzito ya mwanaume kusikika.
“Karibu katika kitengo cha usalama wa Taifa” Sauti ile ilisikika.
“Hallow. Naitwa Hamadi hapa, nipo Tanga Mjini barabara ya kumi na tatu” Hamadi alisema huku akionekana kuwa na haraka.
“Kuna tukio lolote lile limetokea huko?”
“Ndio. Hapa kwenye mghahawa nawaona watu watatu ambao taarifa zinasema kwamba wanatafutwa na jeshi la polisi kwa tukio walilolifanya la utekaji” Hamadi alisema.
“Sawasawa. Wapo vipi hao watu?”
“Ni wazungu watatu. Wana kila sifa ambazo mtangazaji wa televisheni alivyotangaza” Hamadi alisema.
“Upo Tanga sehemu gani?”
“Barabara ya kumi na tatu katika hoteli ya Cassanova hapa. Fanyeni haraka, naona kama wanataka kuondoka” Hamadi alisema na kisha kukata simu.
Hamadi akarudi tena ndani ya mghahawa. Reuben na wenzake bado walikuwa wakiendelea kunywa kama kawaida yao, walichukua dakika mbili tu baada ya Hamadi kutoka jikoni wakasimama, wakalipia na kuondoka mahali hapo.
Hamadi aliwaona polisi wakichelewa kufika mahali hapo, alionekana kuwa na shauku ya kuwaona polisi wakifika hapo, wakiwakamata na kisha kupewa zawadi nono ambayo ilikuwa imeandaliwa kwa mtu yeyote ambaye angefanikisha kukamatwa kwa watu wale.
Wala hazikupita dakika nyingi, defender ya polisi ikasimama nje ya mghahawa ule na kisha polisi kuruka chini kikomandoo na kuelekea ndani ya mghahawa ule ambapo moja kwa moja wakamhitaji Hamadi.
“Wapo wapi?” Polisi mmoja alimuuliza huku akiwa ameshika bunduki.
“Wameondoka muda mchache uliopita”
“Unajua wameelekea wapi?”
“Wameelekea kule upande wa kaskazini”
“Wamekwenda na gari gani?”
“Starlet nyeusi”
“Sawa. Twende garini tuwafuate” Polisi yule alisema.
Hamadi hakuwa na wasiwasi, alichokifanya ni kupanda ndani ya defender ile ambayo ilikuwa na polisi zaidi ya kumi ambao walikuwa na bunduki na kisha kuanza kuelekea kule gari lile la watekaji lilipoelekea.
Mpaka kufikia kipindi hicho polisi wakawa na uhakika kwamba watekaji wale walikuwa njiani kuelekea mpakani mwa nchi ya Tanzania na Kenya, kuingilia ndani yamji wa Mombasa. Dereva wa defender lile alikuwa akiendesha kwa mwendo wa kasi sana, mpaka kufika ndani ya dakika ishirini, walikuwa wakiliona gari lile kwa mbele umbali wa nusu kilometa.
“Watakuwa ndio wenyewe wale. Ongeza kasi dereva” Polisi ambaye alionekana kuwa kiongozi alimwambia dereva.
Gari likaongezwa kasi, kila polisi ambaye alikuwa na bunduki akaanza kuikoki bunduki yake. Tayari muda wa vita ukaonekana kufikia, walitakiwa kupambana kiume mpaka kuona kwamba wanawaokoa mateka ambao walikuwa wameshikiliwa.
Gari lile la watekaji likaenda kwa umbali fulani, wakaliona likikata kona upande wa kushoto na kuingia porini, nao walipofikia eneo lile, wakakata kona na kuingia porini. Tayari mpaka kufikia kipindi hicho walikuwa na uhakika kwamba watu wale walikuwa watekaji na kulikuwa na uhakika wa asilimia mia moja kwamba mateka wale bado walikuwa nao.
Wakaendelea kuelekea kule porini mpaka kufika sehemu ambayo kulikuwa na gari lile tu. Walipoanza kulisogelea na kulifikia, hakukuwa na mtu yeyote yule zaidi ya khanga moja tu ambayo alikuwa ameivaa Prisca.
Wakaanza kusogea mbele zaidi mpaka kufika sehemu ambayo wakaanza kusikika minong’ono ya watu. Wakajificha na kuanza kuchungulia kule minong’ono ilipokuwa ikitokea, macho yao yakatua kwa watekaji wale huku Reuben akiwa amemkaba Prisca ambaye alikuwa akijitahidi kujitoa katika roba ile.
Kila mmoja alijua kwamba ule ndio ulikuwa mwisho wa Prisca, polisi mmoja ambaye alikuwa akisifika kwa shabaha akaandaa bunduki yake tayari kwa kuwalenga. Mapolisi walionekana kutokuwa na wasiwasi hata kidogo, tayari walikwishagundua kwamba watekaji wale wala hawakuwa na bunduki yoyote ile.
“Mlenge yule aliyemkaba mwanamke yule” Polisi kiongozi alimwambia.
“Kichwani au wapi?”
“Usimuue. Mlenge kwenye ule mkono uliomkaba mwanamke”
“Nimekuelewa”
Mlio wa risasi ukasikika mahali hapo, Reuben akaanza kupiga uyowe mkubwa sana, damu zilikuwa zikimtoka mkononi ambao ulikuwa umepigwa na risasi. Filbert na Andrew wakaona kwamba tayari kila kitu kilikuwa kimeharibika, walichokifanya ni kuanza kukimbia.
Polisi yule wa shabaha wala hakuwa na haraka, alichokifanya ni kuilenga miguu yao, wote wakajikuta wakianguka chini kama mizigo huku wakilia kama watoto. Hawakutaka kumuacha Reuben vile vile, nae akapigwa risasi nyingine ya mguu, hawakutaka mtu yeyote yule atoroke kutoka katika mikono yao.
“Kweli una shabaha”
“Hii ndio kazi yangu bwana. Hata ungeniambia nilenge jicho, ningelilenga tu”
Polisi wale wakawasogelea na kisha kuwachukua. Wote walikuwa wakilia kwa maumivu makali, risasi zile zilikuwa zimepenya miguuni mwao. Baadhi ya polisi wakaanza kumsogelea Prisca, walipogusa mapigo yake ya moyo, alikuwa akihema kwa mbali sana.
“Tuondokeni” Kiongozi alisema na kisha wote kuingia ndani ya gari huku mapolisi watatu wakiingia ndani ya ile Starlet pamoja na Prisca ambaye alikuwa kimya na safari kuelekea Tanga mjini kuanza.
****
Manase alikuwa akiendesha gari kwa mwendo wa kasi huku Gibson akiwa pembeni yake. Mawazo ya Gibson kwa wakati huo hayakuweza kutulia hata kidogo, muda wote alikuwa akiiwaza familia yake, mke wake, Prisca pamoja na mtoto wake, Genuine.
Akili yake wala haikutulia hata kidogo, kama kuhuzunika tayari alikuwa amehuzunika sana kiasi ambacho wakati mwingine alikuwa akishikwa na hasira hata zaidi ya simba aliyejeruhiwa. Maswali kibao yalikuwa yakijazana kichwani kwake kuhusiana na watekaji ambao alikuwa na uhakika kwamba walikuwa wametumwa na msichana Katie, msichana ambaye alikuwa amemuoa na kuachana nae kwa sababu kulikuwa na mtu mwingine ambaye alikuwa akimhitaji zaidi.
Hakukuwa na mtu ambaye alikuwa akiongea kitu chochote ndani ya gari, kila mtu alikuwa kimya huku wakionekana kuifuatilia kwa ukaribu safari hiyo ambayo kwao waliiona kwamba ingezaa matunda kwa kile kitu ambacho walikuwa wakikifuata.
“Wanasemaje? Wamewakamata?” Gibson alimuuliza Manase ambaye alikuwa amemaliza kuongea na simu.
“Bado wanaendelea na upekuzi wa kila gari. Nadhani tunaweza kukutana nao njiani pia” Manase alimjibu Gibson.
Safari bado ilikuwa ikiendelea kama kawaida tena gari likiendeshwa kwa mwendo wa kasi sana. Baada ya umbali fulani, wakafika katika eneo ambalo lilikuwa na watu kadhaa wasiozidi ishirini ambao walikuwa wamezunguka kitu karibu na kichaka huku mikono yao ikiwa kichwani.
Hawakutaka kusimama wala kushuhudia ni kitu gani ambacho kilikuwa kikiendelea mahali pale, walichokifanya ni kuendelea na safari yao huku wakionekana kuwa na haraka kupita kawaida bila kujua kwamba watu walewalikuwa wameizunguka maiti ya genuine ambaye alikuwa ametupwa wakati gari likiwa katika mwendo wa kasi. Safari iliendelea zaidi na zaidi mpaka kufika Segera, hakukuwa na mtekaji yeyote ambaye alikuwa amekamatwa na polisi wale.
Kila mmoja alionekana kuchanganyikiwa, hawakuonekana kuelewa mahali ambapo watekaji wale walikuwa wamepitia. Kila mmoja alionekana kutokuelewa, mpaka kufikia muda huo hawakuwa na uhakika kama watekaji wale walikuwa wamekwishavuka mahali hapo au bado.
Kadri muda ulivyozidi kwenda mbele na ndivyo ambavyo walionekana kuchanganyikiwa zaidi, kwanza hawakutaka kuendelea na safari yao, walichokifanya ni kupaki gari pembeni hapo Segera na kuanza kuongea kuona nini kilitakiwa kufuata.
“Kwa hiyo tufanye nini?” Dokta Phillip aliuliza.
“Bado sijajua. Yaani hapa nimekwishachanganyikiwa kabisa. Sijui hawa watekaji watakuwa wamepita njia gani na wakati watu kule Chalinze waliwaona wakichukua njia hii” Manase alisema huku akiitoa simu yake.
Muda wote huo Gibson alikuwa amebaki kimya, kichwa chake kilikuwa kikiifikiria familia yake tu. Hakujua mahali ambapo watekaji wale walipokuwa wameichukua familia yake. Muda wote moyo wake ulikuwa ukifahamu kwamba ni msichana Katie ndiye ambaye alikuwa ameucheza mchezo mzima mpaka kufikia muda huo.
“Huku hawajafika” Manase aliongea simuni.
“Hawajafika? Hawajafika vipi na wakati watu wamekamatwa Tanga?” Sauti ya pili ilisikika.
“Wamekamatwa Tanga?” Manase aliuliza huku akionekana kushtuka.
Swali lile likamfanya Gibson pamoja na dokta Phillip kumsogelea Manase ambaye bado alikuwa akiongea na simu kutoka makao makuu ya kituo cha polisi kilichokuwa jijini Dar es Salaam. Aliongea kwa sekunde kadhaa na kisha kukata simu.
“Wamekamatwa mkoani Tanga” Manase aliwaambia huku akionekana kutabasamu.
“Asante Yesu! Na vipi kuhusu familia yangu?” Gibson aliuliza.
“Hilo sijauliza. Cha msingi twendeni Tanga” Manase aliwaambia.
Hakukuwa na kitu kingine cha zaidi cha kufanya zaidi ya kuingia ndani ya gari na safari ya kuelekea Tanga kuanza mara moja. Muda mwingi Gibson alikuwa akiuliza swali lakini maswali yake hayakuwa na majibu zaidi ya kutakiwa kusubiria mpaka pale ambapo wangeingia Tanga na kuangalia kama familia yake ilikuwa salama.
Safari iliendelea kwa muda wa dakika arobaini na tano, wakawa wamekwishafika Tanga ambako wakaelekea mpaka katika kituo kikubwa cha polisi cha mkoa huo. Kutokana na kujulikana na mapolisi wenzake, Manase akaingia mpaka ndani.
“Wapo wapi?” Manase alimuuliza polisi mmoja.
“Wapo ndani”
“Mateka nao wamepatikana?”
“Kwani walikuwa wangapi?”
“Wawili” Manase alijibu.
“Ndio. Ila sisi tumefanikiwa kumpata mmoja tu”
“Yupi?”
“Mwanamke”
“Mliangalia vizuri garini na kuona kwamba hakukuwa na mtoto?”
“Ndio. Tena gari lao lenyewe tumekuja nalo. Nadhani tukiwabana watatueleza mtoto yupo wapi” Polisi huyo alimwambia Manase.
“Kwa hiyo huyo mwanamke yupo wapi?”
“Hospitalini. Kijana mmoja alikuwa akitaka kumuua kwa kumnyonga shingo. Bahati nzuri shabaha za Shabani zilitusaidia” Polisi yule alijibu.
“Mmempeleka hospitali gani?”
“Hospitali ya mkoa”
“Hali yake ilikuwaje?”
“Mbaya. Yaani mbaya sana”
Manase hakutaka kuendelea kukaa ndani ya chumba kile, alichokifanya kwa wakati huo ni kutoka nje na kisha kumfuata Gibson ambaye akaanza kumuelezea kile ambacho alikuwa ameelezewa na polisi aliyekuwa ndani ya chumba kile.
Gibson alionekana kuchanganyikiwa zaidi, hasira kali dhidi ya watekaji wae ikaonekana kumkaba, walichokifanya kwa wakati huo ni kuingia ndani ya gari na kisha kuanza kuelekea hospitalini ambako wala hapakuwa mbali kutoka mahali hapo.
Ndani ya gari bado Gibson alionekana kuwa na hasira kupita kawaida, chuki juu ya Katie ikaanza kumuingia moyoni mwake na kuzidi kuongezeka kadri muda ulivyozidi kwenda mbele. Alimchukia sana Katie, kwake, tayari aliona kwamba kila kitu kilikuwa kimekwisha, hakuona sababu iiyompelekea Katie kuamua kuwatuma watu kuja nchini Tanzania kwa ajili ya kuiteka familia yake.
“Nitamuua huyu mwanamke” Gibson aliwaambia huku akionekana kuwa na hasira za waziwazi.
“Achana nae. Kwanza tuangalie hali ya mke wako” Manase alimwambia Gibson.
“Sawa! Ila haijalishi kama atapona au atakufa. Nitamuua tu” Gibson alimwambia.
“Nakushauri uiachie sheria ili ichukue mkondo wake. Unaweza kujuta hapo baadae kwa kujichukulia sheria mkononi” Manase alimwambia Gibson ambaye alionekana kutokuelewa kabisa.
Baada ya dakika chache wakawa wamekwishafika katika hospitali ya mkoa wa Tanga na kisha kuteremka. Moja kwa moja wakaanza kupiga hatua kuelekea sehemu ya mapokezi ambako wakajitambulisha na kisha kuelekezwa sehemu ambayo walitakiwa kuelekea.
“Twendeni kwa dokta mkuu kwanza” Manase aliwaambia.
“Kwa nini tusielekee kwenye chumba alicholazwa mke wangu na mtoto wangu?” Gibson aliuliza bila kujua kwamba mtoto wake hakuwepo mahali hapo
“Muda wa kuona wagonjwa umekwishapita na ndio maana nawaambia twendeni huko ili tuongee nae na kuturuhusu” Manase aliwaambia.
Hakukuwa na mtu yeyote ambaye alionekana kupinga, walichokifanya ni kuanza kuelekea katika ofisi ya dokta mkuu na kukaribishwa. Uso wa Gibson haukuonekana kuwa na furaha kabisa, muda wote alikuwa akionekana kuwa na majonzi makubwa.
Wakaanza kujitambulisha kwa dokta Mnyuzu na kisha kutaka kupatiwa maelezo yanayotosheleza kuhusiana na mgonjwa wao ambaye alikuwa ameletwa ndani ya hospitali ile ya mkoa. Hata kabla ya kuongea kitu chochote kile, dokta Mnyuzu akakaa kimya kwa muda huku akiwaangali kwa zamu, aliporidhika, akayagandisha macho yake usoni mwa Gibson.
“Mwanamke yule ni mke wako?” Dokta Mnyuzu alimuuliza Gibson.
“Ndio” Gibson alijibu.
“Pole sana. Ni habari mbaya lakini haina budi kukupa. Wewe ni mwanaume, nakuomba ujikaze kiume” Dokta Mnyuzu alimwambia Gibson ambaye hapo hapo akaonekana kuishiwa nguvu, akakiegemeza kichwa chake huku akimwangalia Dokta Mnyuzu.
“Mkeo amefariki” Ilikuwa ni sauti ambayo ilikuwa ikisikika mara kwa mara kichwani mwa Gibson.

Je nini kitaendelea?
Je Prisca amekufa?
Je Gibson atafanya nini akisikia hali ya mkewe?
 
MCHEZA FILAMU ZA NGONO 14

Msichana Katie alikuwa akiendelea kufanyakazi zake kama kawaida huku akionekana kutokuwa na wasiwasi hata kidogo. Muda wote alikuwa bize akifanya kazi zake lakini huku mawazo yake yakiwa yanamfikiria Gibson. Mapenzi ambayo alikuwa nayo kwa Gibson yalikuwa makubwa, pengo kubwa ambalo alikuwa nalo moyoni mwake wala halikuweza kuzibika hata mara moja.
Gibson alikuwa ameuumiza moyo wake kupita kawaida, muda mwingi alikuwa akionekana mpweke, muda wote alikuwa akiomba Mungu vijana ambao alikuwa amewatuma nchini Tanzania wafanye kazi kama ambavyo aliitaka ifanyike. Muda mwingi alikuwa akiwasiliana nao kwa kutumia mtandao wa simu wa Kimataifa wa Tricom ambao ulikuwa ukitumiwa sana na wazungu kutoka Marekani na barani Ulaya.
Kila alipokuwa akiwasiliana nao, aliambiwa kuwa mvumilivu kwa sababu kila kitu kilikuwa kikiendelea kama kilivyotakiwa kiwe. Katie hakuwa na jinsi, kitu ambacho alikuwa akikifanya kwa wakati huo ni kuendelea kuwa mvumilivu kama kawaida.
Katie aliendelea kuwa kwenye lindi la mawazo mpaka kipindi kile ambacho akaanza kupokea maua mbalimbali ya kimapenzi pamoja na zawadi nyingi zilizokuwa zikihusu mapenzi. Katie alionekana kushangaa, hakujua ni mtu gani ambaye alikuwa akimtumia zawadi hizo ambazo zilikuwa zikija mfululizo, yaani asubuhi, mchana na jioni.
Kutokana na hali ambayo alikuwa nayo katika kipindi hicho wala hakutaka kujali sana kuhusiana na maua hayo na wala hakutaka kumjua mtu ambaye alikuwa akimtumia vitu hivyo vyote. Mawazo yake kwa wakati huo yalikuwa yametulia kwa mtu mmoja tu, mtu ambaye alikuwa amemuachia tundu kubwa moyoni mwake, tundu ambalo lilikuwa likiendelea kuuma kadri siku zilivyozidi kwenda mbele.
Zawadi ziliendelea kumiminika nyumbani kwake zaidi na zaidi mpaka kufikia kipindi ambacho akatamani kumuona mtu huyo ambaye alikuwa akitumia muda mwingi kumtumia zawadi mbalimbali. Alichokifanya ni kumpigia simu kupitia namba zake ambazo alikuwa akiziambatisha katika zawadi mbalimbali alizokuwa akimletea.
Siku iliyofuata, mwanaume huyo, Daniel akafika nyumbani kwa Katie na moja kwa moja kukaribishwa ndani. Katie hakuonekana kuamini, mwanaume ambaye alikuwa ameingia ndani ya nyumba yake alikuwa akimfahamu vilivyo, alikuwa Daniel, mtu ambaye alikuwa mpenzi wake na ndiye alikuwa mtu ambaye aliutoa usichana wake katika miaka ya nyuma, kipindi ambacho walikuwa wakiishi mitaani.
Kwa mbali, uso wake ukaanza kuonyesha tabasamu, akaanza kumsogelea Daniel na kisha kumkumbatia. Hiyo ikaonekana kuwa faraja kwake, kumbatio ambalo alikuwa amelipata kutoka kwa Daniel likaonekana kumfariji na kumsahaulisha na Gibson kwa sekunde chache.
Baada ya hapo wakaanza kuongea mambo mengi ya nyuma ambayo yalikuwa yametokea katika maisha yao katika kipindi ambacho walikuwa wakiishi mitaani hata kabla ya Katie kujiingiza katika uchezaji wa filamu za ngono, hatua ambayo ilionekana kumuumiza sana Daniel ambaye alikuwa kwenye mapenzi mazito na Katie.
Daniel hakutaka kuwa nyuma, nae akaanza kumuelezea Katie kuhusu maisha yake toka siku ambayo walikuwa wametengana. Alimuelezea mambo mengi mpaka alivyokwenda nchini Uingereza na kutafuta fedha kwa nguvu mpaka kufikia hatua ya kuwa tajiri mkubwa. Historia zao zilionekana kufanana, walianzia maisha ya mitaani, maisha ambayo hayakuwa na ubora kabisa ila katika muda huo, wote walikuwa matajiri wakubwa.
Daniel hakutaka kukaa kimya, kwa wakati huo bado alikuwa akiona kwamba kulikuwa na uhitaji mkubwa wa kuzielezea hisia zake kwa msichana huyo, Katie na kwa jinsi moyo wake ulivyokuwa umeumia hasa mara baada ya kuona kwamba alikuwa ameolewa na mtu mwingine. Uso wa Daniel ulionyesha dhahiri kwamba alikuwa ameumizwa sana na tukio lile la ndoa na hivyo alikuwa akiomba Mungu kila siku kwamba awe tena na Katie kama ilivyokuwa zamani.
“Unafikiri Mungu amejibu maombi yako?” Katie aliuliza huku akimwangalia Daniel usoni.
“Yeah! Asilimia mia moja” Daniel alijibu huku akionekana kujiamini.
“Bado Daniel Itakubidi uombe sana. Unakumbuka kwamba nilikuacha ingawa ulikuwa kwenye mapenzi nami?” Katie alimuuliza Daniel.
“Ndio! Nakumbuka”
“Nilikuacha kwa sababu nilitaka kuwa huru zaidi ya jinsi nilivyokuwa. Sikuwa na fedha, nilikuwa nikishinda hata masaa kumi bila chakua. Nilitaka kuwa tajiri kama nilivyo kwa sasa. Nitazame sasa, ninaweza kula chochote ninachotaka, ninaweza kwenda popote ninapotaka kwenda. Nina kila kitu kwa sasa Daniel” Katie alimwambia Daniel.
“Ninafahamu. Lakini una maana gani kuniambia hayo yote?” Daniel aliuliza.
“macho yangu” Katie alimwambia Daniel.
“Ninakupenda Katie” Daniel alimwambia Katie.
“Macho yangu yanakwambia kila kitu” Katie alimwambia Daniel.
Daniel akasimama pale alipokuwa amekaa na kisha kuanza kumfuata Katie katika kochi alilokuwa amekaa na kisha kupiga magoti mbele yake. Tayari macho ya Daniel yalikuwa yamekwishabadilika, yakaanza kuwa mekundu kwa wakati huo.
Tayari macho ya Katie yalikuwa yamekwishamueleza kila kitu kwamba kwa wakati huo hakutaka kuwa nae. Kwa kiasi fulani Daniel akaonekana kuchanganyikiwa, alikuwa ametumia kiasi kikubwa cha fedha kwa kumtenganisha Katie na Gibson, sasa ingeleta maana gani kama nae pia asingekuwa na msichana huyo na wakati alikuwa ametoa zaidi ya dola milioni kumi.
Daniel aliona kwamba kulikuwa na kila sababu ya kulipigania penzi lake, aliona kwamba kulikuwa na kila sababu ya kumrudisha Katie katika mikono yake. Hakujali ni kiasi gani cha fedha ambacho angetumia kwa wakati huo, kitu ambacho alikuwa akikitaka ni kumuona Katie akirudi tena katika mikono yake kama ilivyokuwa zamani, nyakati zile walizokuwa wakiishi mitaani kama watoto wa mitaani.
Daniel akamshika Katie mkono huku akimwangalia usoni mwake. Macho ya Daniel yalikuwa yakionyesha kila dalili kwamba kwa wakati huo alikuwa akimhitaji sana Katie zaidi ya kitu chochote kile. Alipoona kwamba mguso wake mkono mwa Katie haukubalisha kitu chochote kile, akaupandisha na kuishika shingo ya Katie kwa mikono yake miwili.
“Ninakupenda”Daniel alimwambia Katie kwa mara nyingine tena.
Mawazo ya Katie yakaanza kurudi nyuma, tayari hali ya huruma ikaonekana kumuingia. Katika maisha yake, hakuwahi kumuona mwanaume akitoa machozi kwa ajili yake kama ilivyokuwa kwa Daniel katika kipindi hicho. Mawazo yake ya nyuma ndio ambayo yalikuwa yakiongeza chachu ya kuona kwamba kulikuwa na kila sababu ya kuwa na mwanaume huyo ambaye kwake alionekana kuwa mvumilivu kupita kawaida.
“Halikuwa chaguo langu sahihi” Katie alimwambia Daniel.
“Ninafahamu. Muache aende zake. Sahau kila kitu kuhusu yeye” Daniel alimwambia Katie.
“Vipi kuhusu kisasi?” Katie aliuliza huku akianza kulia.
“Hakuna uhitaji wa kufanya hivyo” Daniel alimwambia Katie.
Wote wakajikuta wakisimama na kisha kukumbatiana. Japokuwa kwa wakati huo lilikuwa jambo gumu sana kwa Katie kumsahau Gibson lakini akaona kulikuwa na kila sababu za kumsahau mwanaume huyo na kumuacha Daniel achukue nafasi ndani ya moyo wake. Mpaka kufikia hatua hiyo, tayari Daniel alikuwa akijiona kuwa mshindi, kiasi kikubwa cha fedha ambacho alikuwa amekitumia kilionekana kufanya kazi ile ambayo aliikusudia kufanyika.
Huo ndio ukawa mwanzo wa mahusiano yao ya kimapenzi kwa mara ya pili tena. Kila mmoja akaanza kumuahidi mwenzake kwamba angempenda mpaka pale ambapo kifo kingewatenganisha. Hakukuwa na mtu ambaye alikuwa akifikiria maisha ya baade yangekuwaje baada ya hapo, kitu walichokuwa wakikifikiria ni kufunga ndoa na kuishi pamoja hapo baadae.
****
“Unamaanisha mke wangu na mtoto wangu wamekufa” Gibson aliuliza huku akionekana kutokuamini.
Kila mmoja ndani ya ofisi ile akaonekana kumshangaa Gibson. Dokta hakuwa ameongea kitu chochote kuhusiana na mgonjwa wake lakini tayari Gibson akaonekana kufikiria jambo jingine zaidi. Hata kabla ya kuongea kitu chochote kile, dokta akaanza kuyafikiria maneno ya Gibson. Alijua na uhakika kwamba mgonjwa ambaye alikuwa ameletwa hospitalini pale ambaye alitekwa alikuwa mmoja, sasa huyo mtoto alitokea wapi?
Ingawa swali hilo lilianza kumtatiza kichwani mwake lakini dokta Mnyuzu hakutaka kuuliza kitu chochote kile zaidi ya kulifungua faili ambalo lilikuwa mezani mwake na kisha kuanza kuandika vitu fulani ambavyo hakukuwa na mtu yeyote ambaye alivifahamu.
“Mke wako ni mzima japokuwa hali yake ni mbaya sana” Dokta Myuzu alimwambia Gibson.
“Imekuwaje tena?”
“Hali inaonyesha kwamba alikuwa amekabwa kwa kipindi kirefu hali ambayo ilimfanya kutovuta pumzi kwa kiasi kikubwa, mbaya zaidi, kila alipokuwa akijaribu kuvuta pumzi, hiyo hivyo pumzi ndogo ambayo ilikuwa ikiingia, ilikuwa ikiingia na vumbi jingi” Dokta Mnyuzu alimwambia Gibson maneno ambayo yalionekana kumchanganya.
“Kwa hiyo hatopona?”
“Simaanishi hivyo. Kupona anaweza kupona japokuwa inaweza kuchukua muda mrefu kwani tumemuwekea mashine ya hewa ya oksijeni ili tuweze kuona maendeleo yake yatakuwaje?” Dokta Mnyuzu alimwambia Gibson.
“Nakuomba mponyeni mke wangu. Ninampenda sana, sitaki kumpoteza” Gibson alimwambia dokta Mnyuzu.
“Hata sisi hatutaki kumpoteza na ndio maana tunajitahidi kufanya kila tuwezacho kufanya kwa ajili ya kuirudisha afya yake kama ilivyokuwa kabla” Dokta Mnyuzu alimwambia Gibson.
“Na vipi kuhusu mtoto wangu?” Gibson aliuliza.
“Mtoto yupi?” Dokta Mnyuzu aliuliza huku akionekana kushangaa.
“Mtoto wangu, Genuine”
“Sijui kama kuna mtoto aliletwa hapa. Alikuwa na mkeo?”
“Ndio”
“Hapana. Mwanamke aliletwa peke yake” Dokta Mnyuzu alimwambia Gibson.
“Sasa mtoto wangu yupo wapi?” Gibson aliuliza.
“Mmmh! Sijui” Dokta alijibu.
“Kuna kitu nadhani kitakuwa kimeendelea. Maelezo yote juu ya mtoto tutayapata kutoka kwa wale watekaji” Manase aliwaambia.
Hawakutaka kuendelea kusubiri ndani ya ofisi ile, walichokifanya ni kuondoka na kuelekea katika chumba alicholazwa Prisca na kisha kumuangalia. Prisca alikuwa kimya kitandani, kwa kifupi alikuwa akionekana kama mtu ambaye tayari alikuwa amekwishakata roho. Gibson akasimama pembeni yake, tayari macho yake yalikuwa yamekwishaanza kutoa machozi, picha iliyoonekana kwa mkewe ikaonekana kumuumiza sana.
“Prisca mke wangu! Genuine yupo wapi?” Gibson alimuuliza Prisca huku machozi yakimtoka japokuwa alikuwa akifahamu kwamba Prisca asingeweza kujibu kitu chochote kile.
*****
Reuben, Filbert na Edward walikuwa chini ya ulinzi katika chumba kimoja kidogo huku tayari mawasiliano yakiwa yamekwishafanyika na makao makuu ya polisi ya jijini Dar es Salaam na hivyo watu hao walitakiwa kusafirshwa mpaka ndani ya jiji la Dar es Salaam.
Taratibu zote zilikuwa zimekamilika lakini mpaka muda huo ni kamanda Manase ndiye alikuwa akisubiriwa kutokana na kuwa na maswali machache na watu hao. Ilipofika saa kumi na mbili jioni, Manase akaingia katika kituo hicho na moja kwa moja kuelekea katika chumba kile na kuonana na watekaji wote watatu ambao walikuwa chini ya ulinzi wa polisi.
Kamanda Manase akaanza kuwaangalia kwa zamu, alipoona ameridhika, akakiweka chini kiti ambacho alikuwa ameingia nacho ndani ya chumba kile na kisha kutulia. Kwa wakati huo alikuwa akihitaji kufahamu kitu kimoja tu, sehemu alipokuwa mtoto Genuine ambaye hadi katika kipidi hicho hawakuwa wamemuona.
Reuben hakutaka kuficha, akaanza kuelezea kila kitu kilichokuwa kikihusiana na mtoto Genuine. Ilikuwa ni taarifa ambayo ilimhuzunisha sana Manase, hakujua namna ambavyo alitakiwa kuifikisha taarifa ile kwa Gibson ambaye alikuwa akitamani sana kusikia taarifa kuhusu mtoto wake wa pekee.
Manase hakutaka kukaa sana ndani ya chumba kile, alichokifanya ni kuanza kuelekea hospitalini ambako akamkuta Gibson akiwa ndani ya chumba kile huku akiendelea kuongea maneno mengi mbele ya uso wa mke wake japokuwa Prisca hakuwa amefumbua macho.
“Kuna taarifa nimepewa kuhusu mtoto wako” Manase alimwambia Gibson ambaye akamsogelea karibu huku akiwa na shauku ya kutaka kujua zaidi.
“Inasemaje?”
“Njoo nje kwanza” Manase alimwambia Gibson na kisha wote kuelekea nje.
Manase hakutaka kuficha kitu chochote kwa wakati huo, akamwambia Gibson kila kitu ambacho aliambiwa na Reuben ndani ya chumba kile. Gibson akauhisi mwili wake ukifa ganzi, akaanza kutetemeka huku hasira zikianza kumpanda.
“Unasemaje?”
“Hivyo ndivyo ilivyotokea. Kwa kweli imenihuzunisha sana. Huu ni unyama mkubwa sana kuwahi kutokea” Manase alimwambia Gibson.
Hiyo ilikuwa ni taarifa mbaya ambayo iliuumiza moyo wa Gibson kupita kawaida. Machozi yakaanza kutiririka mashavuni mwa Gibson, kile ambacho alikuwa amekisikia kiliuchoma sana moyo wake. Akalifuata benchi na kisha kulikalia huku akikiinamisha kichwa chake chini.
Taswira ya mtoto wake ikaanza kumjia kichwani, alikumbuka mambo mengi kuhusiana na mtoto wake, akalikumbuka tabasamu lake, akaanza kukikumbuka kicheko chake hasa pale ambapo alikuwa akimfanyia vitu ambavyo vilikuwa vikimfanya kucheka.
Katika kila kitu ambacho alikuwa akikifikiria kwa wakati huo kilikuwa kikizidi kumuumiza moyo wake kupita kawaida. Mtoto wake ambaye alikuwa akimpenda sana, kwa wakati huo hakuwa pamoja nae tena, alikuwa ameuawa katika kifo kibaya ambacho kila mtu ambaye angesikia, angeumia moyoni.
Wakati mwingine, alihisi kuisikia sauti moyoni mwake, sauti ambayo ilikuwa ikisisitiza kwamba kila kitu ambacho kilikuwa kimetokea yalikuwa ni matunda ya vitu ambavyo alikuwa amevipanda kabla. Kwa wakati huo ulikuwa muda wa mavuno wa yale ambayo alikuwa amepanda siku za nyuma.
Usaliti ambao alikuwa ameufanya kwa mke wake, Prisca ndio ambao ulikuwa umeleta matatizo yale yote. Alijua fika kwamba kama asingekuwa amemsaliti mke wake, Prisca basi kwa wakati huo asingekuwa katika wakati mgumu kama ambavyo alivyokuwa kwa wakati huo.
“Ila mimi ndiye niliyesababisha haya yote” Gibson alimwambia Manase.
“Najua. Ila kwa sasa hautakiwi kujilaumu. Kila kilichotokea, kimetokea” Manase alimwambia Gibson.
“Nafahamu. Ila naamini kama nisingekuwa nimemsaliti Prisca kipindi cha nyuma, nina uhakika hata jambo hili lisingetokea kwa sasa. Usaliti wangu umenigharimu sana katika maisha yangu. Usaliti ambao niliufanya kipindi kile, hizi ndizo athari zake. Ninajuta kumsaliti mke wangu” Gibson alimwambia Manase ambaye alikuwa kimya kumsikiliza.
“Fedha zilinifanya nimsaliti mke wangu. Hizi hizi fedha haziwezi kunirudishia mtoto wangu. Huu umekuwa ni kama msumali wa moto ndani ya moyo wangu, tukio hili limeniachia kidonda kikubwa moyoni, kidonda ambacho sidhani kama kuna siku kitakuja kupona” Gibson alimwambia Manase.
“Usijali Gibson. Kila kitu ni mipango ya Mungu”
“Hapana. Vitu vingine si mipango ya Mungu. Mungu hakupanga nimsaliti mke wangu, Mungu hakupanga nisafiri kwenda nchini Marekani na kufunga ndoa na msichana Katie. Hii ilikuwa mipango yangu, tamaa zangu za kutaka fedha ndizo ambazo zimenifanya niwe katika hali hii kwa sasa” Gibson alimwambia Manase huku akitokwa na machozi.
“Usilie Gibson. Jikaze. Wewe ni mwanaume” Manase aliendelea kumbembeleza Gibson.
“Kujikaza ni vigumu sana. Inaniuma sana kumpoteza mtoto wangu ambaye nilikuwa nikifanya mambo mengi kwa ajili yake. Inawezekana mtoto wangu angekuwa rais, inawezekana mtoto wangu angekuwa waziri mkuu. Ndoto zake za kufikia mafanikio zimefutika kwa sababu ya tamaa zangu za kutamani sana fedha. Nilichokuwa nikikifikiria ni fedha tu, sikutaka kufikiria ni kitu gani kingetokea baada ya hapo. Moyo wangu unajuta, sijui ni kwa namna gani nitakuwa nikiishi na mke wangu bila ya kuwa na mtoto wetu. Nadhani yatakuwa maisha yatakayoniumiza sana, nadhani yatakuwa ni aina ya maisha ambayo yatanifanya kukosa amani na furaha ndani ya moyo wangu” Gibson alimwambia Manase ambaye alibaki kimya huku nae akianza kuyafikiria maneno ya Gibson.
Gibson aliongea maneno mengi tena kwa sauti ya unyonge. Ingawa maneno yalikuwa mengi lakini hayakuweza kubadilisha kitu chochote kile, ukweli ulibaki vile vile kwamba Genuine alikuwa ameuawa kinyama.
Kila kitu kikapangwa na kisha baada ya siku moja safari ya kurudi jijini Dar es Salaam kuanza. Gibson hakutaka kumuacha mke wake ahudumiwe mkoani Tanga jambo lililompelekea kumsafirisha kuelekea jijini Dar es Salaam kwa kutumia usafiri wa ndege.


Je nini kitaendelea?
 
MCHEZA FILAMU ZA NGONO 15

Watanzania bado walikuwa wakiendelea kulaani kitendo kile cha utekaji ambacho kilikuwa kimefanyika. Muda mwingi watu walikuwa wakitembea na mabango kuelekea katika ubalozi wa Marekani. Maandamano yalikuwa yamefanyika kwa takribani siku tatu mfululizo jambo lililompelekea balozi wa Marekani nchini Tanzania kuwasiliana na serikali ya Marekani ili kuanza kufuatilia kuhusu vijana wao, ikiwezekana harakati zote zifanyike mpaka hukumu ya watekaji wale kufanyika.
Waandishi wengi wa habari walikuwa wakifika katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kuanza kuongea na Gibson ambaye muda mwingi alikuwa akionekana kuwa mnyonge kupita kawaida. Mtu ambaye alikuwa akisubiriwa apate fahamu ni Prisca tu ambaye angeeleza kila kitu na hata mahali ambapo mtoto Genuine alikuwa ametupwa.
Siku zikaendelea kukatika, wazazi wote wa pande mbili pamoja na ndugu na marafiki wa karibu walikuwa wakifika hospitalini pale kwa ajili ya kumjulia hali Prisca ambaye mpaka wiki imekatika lakini bado hakuwa amerudiwa na fahamu.
“Kipindi kirefu kimepita. Hii inaonekana kuwa si kawaida kabisa” Gibson alimwambia dokta Marwa ambaye alikuwa akimshughulikia Prisca kila siku.
“Mshipa wake wa fahamu umeshtuka sana. Mara nyingi watu ambao wanapatwa na tatizo hili huwa wanatumia muda mrefu kitandani. Mshipa wa fahamu unaposhtuka kwa nguvu, huwa wakati mwingine unaweza kuufanya hata uti wa mgongo kupata matatizo. Na ikitokea uti wa mgongo kupata tatizo, mgonjwa anaweza akapooza sehemu moja ya mwili” Dokta Marwa alimwambia Gibson maneno ambayo yalionekana kumshtua.
“Kwa hiyo mke wangu atapooza?”
“Sikuwa na maana hiyo. Hapo nimejaribu kukwambia kitu ambacho mara nyingi hutokea. Mkeo anaweza kurudiwa na fahamu na wala asipate tatizo lolote lile” Dokta Marwa alimwambia Gibson.
Yalikuwa ni maneno makali ambayo yaliuumiza sana moyo wa Gibson, muda mwingi alikuwa akionekana kuwa na wasiwasi kupita kawaida, meneno yale ambayo aliambiwa kwamba mke wake angeweza kupooza yalikuwa yamemtiwa wasiwasi kupita kawaida. Upweke ukaongezeka maishani mwake, kwa wakati huo wala hakutaka kusimamia biashara zake ambazo zilikuwa zikiendelea kumuingizia mamilioni, muda mwingi alikuwa akiutumia kuwa karibu na kitanda alicholazwa mke wake.
“Utarudi katika fahamu zako mpenzi na kuniambia mtoto wangu walimtupa sehemu gani. Hata kama atakuwa amekufa, nitahitaji kuliona hata kaburi lake tu” Gibson alikuwa akimwambia mkewe ambaye bado alikuwa kwenye usingizi wa kifo.
Maisha ya kutokwa na machozi yakawa sehemu ya maisha yake, kila siku alikuwa mtu wa kulia sana jambo ambalo lilikuwa likimpelekea kudhoofika mwili wake kupita kawaida. Watu mbalimbali walikuwa wakimtembelea na kumfariji lakini wala hawakuweza kubadilisha kitu chochote kile, kila siku Gibson alikuwa mtu wa kulia tu.
Wiki ya pili ikakatika, wiki ya tatu ikaingia lakini hakukuwa na mabadiliko yoyote yale. Bado Prisca alikuwa kwenye usingizi wa kifo jambo ambalo lilionekana kuwachanganya hata madaktari wenyewe. Mirija ambayo ilikuwa ikipitishwa katika sehemu yake ya tumbo ndio ambayo ilikuwa ikitumika kumlisha chakula pamoja na kumywesha maji.
“Au amekwishakufa?” Gibson alimuuliza dokta Marwa.
“Hapana. Bado ni mzima. Hata moyo wake unadunda. Tuvumilie hadi mshipa wa fahamu utakapokuwa sawa” Dokta Marwa alimwambia Gibson.
Hakukuwa na cha kufanya kwa wakati huo, waliendelea kusubiri zaidi na zaidi. Mwezi ukakatika, hakukuwa na mabadiliko yoyote ya maendeleo, bado Prisca alikuwa amelala kitandani huku moyo wake ukidunda kwa mbali sana.
****
Katie alikuwa akijiandaa kutoka mtoko wa usiku pamoja na Daniel ambaye alipanga waonane katika mghahawa wa Mc Donald kwa ajili ya kupata chakula cha usiku pamoja na kununua Ice Cream ambazo zilikuwa zikipendwa sana. Huo ulikuwa ni mtoko ambao ulikuwa ukiwahusisha watu wawili ambao walikuwa wameishi sana katika maisha ya mitaani kipindi cha nyuma na wakati huo walikuwa matajiri wakubwa.
Kila vazi ambalo alikuwa akilivaa Katie lilionekana kutokumpendeza jambo ambalo lilimfanya kubadilisha kila aina ya vazi ambalo alikuwa ameliweka katika kabati lake kubwa la nguo. Alianza na gauni jekundu ambalo lilikuwa na maua mawili kiunoni, hilo hakuliona kumfaa kwa siku hiyo, akaamua kuliweka pembeni.
Hapo ndipo alipoamua kuchukua gauni jingine ambalo lilikuwa na rangi mbalimbali zilizopangwa kimpangilio huku likiwa na vitu vilivyokuwa vikinga’aa sana, hilo nalo akaliona kutokufaa kwa usiku huo. Mtoko huo kwake ulionekana kuwa mtoko mmoja mkubwa sana ambao ungewafanya kuongea mambo mengi, kupeana mapenzi na Daniel na hata kufanya mapenzi kama siku ile ya kwanza ambayo walifanya.
Alibadilishabadilisha mavazi zaidi ya kumi na mbili usiku huo na ndipo alipolipata vazi moja ambalo kwake lilionekana kuwa zuri katika usiku huo wa siku hiyo. Baada ya kumaliza kujiandaa, akajipulizia manukato mazuri ambayo yalikuwa na gharama na kisha kulifuata gari lake na kuanza kuelekea katika mghahawa huo.
Ndani ya gari, mawazo yake kwa kipindi hicho yalikuwa yaimfikiria Daniel tu, Gibson kwa wakati huo wala hakutaka kumpa sana nafasi kichwani mwake. Aliona kwamba kila kitu ambacho kilikuwa kimetokea kati yake na Gibson kilitakiwa kusahaulika katika maisha yake na kujipanga upya na Daniel.
Kwa wakati mwingine alikuwa akiwafikiria vijana wake ambao alikuwa amewatuma kwa kufanya kazi moja ya kumuua mwanamke ambaye alikuwa akiishi na Gibson kwa wakati huo. Mpaka kufikia kipindi hicho wala hakuwa amepata taarifa zozote kutoka kwa vijana wake tangu siku mbili zilizopita ambazo zilikuwa siku za mwisho kuongea nao.
Wala Katie hakuchukua muda mrefu akawa amekwishafika katika mghahawa huo ambao mara nyingi sana ulikuwa ukitembelewa na masupastaa nyakati za usiku na kisha kuanza kupiga hatua kuelekea katika meza ambayo Daniel alikuwepo. Mara tu Daniel alipomuona Katie, akainuka na kuanza kumsogelea, alipomfikia, akamkumbatia na kumshushia mabusu kadhaa ya mdomoni.
Wakaifuata meza na kukaa huku mhudumu akija na wote kuagiza chakula ambacho walikiona kufaa sana kula siku hiyo. Wakabaki wakiongea mengi, katika kipindi hicho ndio ulikuwa muda muafaka wa kukumbushiana mambo mengi ya nyuma yaliyopita, hasa katika kipindi kile ambacho walikuwa watoto wa mitaani.
Kipindi kile kilionekana kuwa kipindi kizuri kwao wote, walikula na kinywa huku wote wakionekana kuwa na furaha. Furaha ambazo walikuwa nazo katika kipindi hicho ndizo ambazo ziliwafanya kupeana ahadi ya kuishi pamoja kama mume na mke mara kila kitu kitakapokaa sawa.
Baada ya hapo, moja kwa moja wakaanza safari ya kuelekea katika hoteli ya Pasiphian ambayo ilikuwa kando ya jiji hilo la New York na kisha kulala huko. Usiku wa siku hiyo kwao ukaonekana kuwa usiku wa kukumbuka, walipeana mapenzi ya dhati mpaka kufikia kipindi ambacho kila mtu alikuwa hoi kitandani.
Asubuhi ya siku iliyofuata, wakaongozana wote na kuelekea nyumbani kwa Katie. Hali ambayo waliikuta nyumbani hapo ilionekana kumshtua kila mmoja. Nje, kulikuwa na magari mawili ya polisi huku mapolisi wawili wakiwa nje ya eneo la nyumba ile na huku wengine wakiwa wamekwishaingia ndani ya eneo la nyumba ile.
Katie akaonekana kushtuka, akateremka kutoka garini na moja kwa moja kuwafuata mapolisi ambao walikuwa nje ya nyumba yake. Kitu cha kwanza walichokifanya mapolisi wale mara baada ya kumuona ni kuanza kumsogelea.
“What the hell is going on here? (Kitu gani kinaendelea mahali hapa?)” Katie aliuliza huku akionekana kushangaa.
“We are looking for you mom (Tunakutafuta wewe)” Polisi mmoja alimwambia.
Hapo hapo mapolisi wale wakamwambia dhumuni la wao kufika mahali pale na kisha kumwambia kupanda ndani ya gari huku wale mapolisi ambao walikuwa ndani ya eneo la nyumba yake wakiwa wamekwishafika mahali pale.
Daniel ambaye alikuwa amekwishateremka garini akaanza kuwafuata na kisha kuanza kuwauliza maswali kadhaa ambayo hakukuwa na polisi yeyote ambaye aliyajibu maswali yale. Moja kwa moja safari ya kuelekea katika kituo kikuu cha polisi katika jiji hilo la New York kuanza huku tayari Katie akionekana kuanza kuhisi kitu.
Walipofika kituoni, akateremshwa na kisha kuanza kupelekwa ndani ya jengo hilo ambako akaingizwa ndani ya chumba kimoja kwa ajili ya kuulizwa maswali kadhaa. Polisi mmoja ambaye alivalia suti akaingia ndani ya chumba kile na kisha kuanza kumuuliza maswali kadhaa huku akimtolea picha ambazo walipigwa Reuben, Filbert na Edward nchini Tanzania jambo ambalo lilimfanya kuona kwamba hisia zake zilikuwa zimehusika moja kwa moja na kile ambacho alikuwa akikihisi.
“I want to talk to my lawyer (Nataka kuongea na Mwanasheria wangu)” Katie alimwambia polisi yule kila alipoona maswali yakizidi kuulizwa.
Huo ndio ulikuwa mwanzo wa kesi hiyo ulipoanza huku Reuben na wenzake wakiwa wamepelekwa nchini Marekani. Kwa kuwa Prisca bado alikuwa amepoteza fahamu, Gibson na dokta Philip ndio ambao walikuwa mashahidi wa kwanza katika kesi hiyo ambayo ilikuwa ikivuma sana katika vyombo mbalimbali vya habari duniani.
Kesi ilivuma zaidi ya miezi mitatu, Katie akakutwa na hatia ambayo ikampelekea kufungwa miaka ishirini jela huku vijana wake ambao alikuwa amewatuma kufanya mauaji wakifungwa miaka ishirini na tano jela.
Hiyo ilionekana kuwa hukumu kubwa kwa Katie, muda wote mahakamani alikuwa akilia huku akijaribu kumuomba msamaha Gibson ambaye alishindwa kuvumilia na machozi kumtoka. Hilo halikuweza kubadilisha kitu chochote kile, siku hiyo ndio ambayo Katie alikwenda kuanza kukitumikia kifungo chake katika gereza la South Greeen, gereza lililokuwa kusini mwa jiji la New York nchini Marekani.
Japokuwa Katie alikuwa amefungwa lakini Daniel hakutaka kuachana nae, bado mapenzi ambayo alikuwa nayo kwa Katie yalikuwa makubwa. Mara kwa mara alikuwa akimtembelea gerezani na baada ya mwaka mmoja kufunga ndoa pamoja katika kanisa la gereza lililokuwa hapo hapo gerezani.
Japokuwa maisha yalionekana kuwa magumu, lakini katika kipindi ambacho alikuwa akionana na mke wake Katie yalikuwa yakionekana kuwa rahisi sana. Furaha ikaonekana kutawala katika mahusiano yao japokuwa walikuwa wakiishi tofauti sana. Kwa kuwa walikuwa mume na mke, kila walipokuwa wakikutana walikuwa wakipewa uhuru wa kufanya kila kitu mpaka pale Katie alipojifungua mtoto wa kiume na kumuita jina la Hope kwa kutumaini kwamba kuna siku angetoka gerezani na kuishi pamoja na familia hiyo.
“I love you Katie.....I love you Katie (nakupenda Katie....Nakupenda Katie)” Daniel alimwambia Katie muda mchache mara baada ya kujifungua huku wakiwa wamekumbatiana na mtoto Hope akiwa mikononi mwa Katie.
“I love you too (Nakupenda pia)” Katie alimwambia Daniel.
****
Miezi sita ilikuwa imekatika lakini Prisca hakuweza kurudiwa na fahamu zake. Kila siku Gibson alikuwa akiomba Mungu lakini sala zake zilionekana kutokujibiwa kabisa. Hali ya mke wake, Katie ilikuwa ikimuumiza kila siku, kila alipokuwa akimuona pale kitandani alikuwa akiumia kupita kawaida.
Moyo wake bado ulikuwa na mapenzi ya dhati kwa mke wake huyo ambaye kwake alionekana kuwa kama mfu kitandani pale. Kila siku marafiki zake pamoja na ndugu zake walikuwa wakifika hospitalini pale kwa ajili ya kumuona Prisca ambaye alikuwa hajafumbua macho yake.
Siku ziliendelea kukatika mpaka pale Gibson alipokwenda nchini Marekani kusimamia kesi ya mauaji ambayo ilikuwa ikiwakabiri watu wanne. Kwa jinsi alivyokwenda na kurudi baada ya miezi mitatu wala hakukuwa na mabadiliko yoyote yale, Prisca hakuwa amefumbua macho yake, alikuwa kama jinsi alivyomuacha kabla ya kuondoka.
Siku ziliendelea kukatika. Ilipofika tare 5 mwezi wa 7, siku hiyo ilionekana kuwa kama muujiza kwa Prisca, kwa mara ya kwanza baada ya miezi mingi, akaweza kufumbua macho yake tena. Tukio lile likaonekana kumshtua kila mtu, manesi wote waliona jambo lile kuwa kama muujiza ambao wala hawakuwa wakiutegemea. Kitu walichokifanya ni kumpigia simu dokta Marwa ambaye akafika mahali hapo na kushuhudi kwa macho yake. PRISCA ALIKUWA AMERUDIWA NA FAHAMU.
****
Dokta Marwa hakuweza kuvumilia, kitu alichokifanya kwa wakati huo ni kuchukua simu yake na kisha kumpigia Gibson ambaye baada ya dakika thelathini akawa amekwishafika ndani ya eneo la hospitali hiyo na moja kwa moja kuelekea katika chumba kile. Gibson hakuweza kuyaamini macho yake, machozi ya furaha yakaanza kumtoka, akaanza kumfuata Prisca pale kitandani na kisha kumkumbatia. Muda wote Prisca alikuwa akimshangaa Gibson, kwake alikuwa akionekana kuwa kama mtu mpya.
“Umeamka. Umeamka hatimae” Gibson alimwambia Prisca ambaye bado alikuwa akimshangaa.
Kwa haraka sana Gibson akaichukua simu yake na kisha kuwapigia wazazi wake na kisha kuanza kuwaambia kuhusu muujiza ambao ulikuwa umetokea hospitalini. Wazazi wa pande zote mbili wakafika mahali hapo. Mara Prisca alipowaona wazazi wake, tabasamu pana likatawala uso wake.
Huo ndio ulionekana kuwa muujiza mkubwa. Prisca hakuwa na nguvu za kuongea japokuwa alikuwa amefumbua macho. Baada ya mwezi mmoja kupita, Prisca akaruhusiwa kurudi nyumbani huku kila kitu ambacho alikuwa akikiona kilionekana kuwa kipya machoni mwake.
“Nimewakumbuka sana. Mdogo wangu Dorice yupo wapi?” Prisca aliuliza huku akionekana kuwa mwenye furaha.
“Amekwenda chuoni” Mama yake, Bi Magreth alijibu.
“Mnanitania. Lini ameanza chuo? Si yupo kidato cha pili?” Prisca aliuliza swali ambalo lilimshangaza kila mtu.
“Unasemaje?”
“Toka lini mwanafunzi wa kidato cha pili akaanza chuo?” Prisca aliuliza.
Kila mmoja alionekana kushtuka, si wazazi tu ambao walionekana kushtuka bali hata Gibson mwenyewe alikuwa ameshtuka kupita kawaida. Hakujua ni kitu gani ambacho kilikuwa kimetokea, kila wakati alikuwa akijiuliza kama tukio la kupoteza kumbukumbu lilianza kumfanya kuwa chizi au la.
“Prisca! Unamjua huyu?” Baba yake, mzee Steven alimuuliza huku akimnyooshea Gibson kidole.
“Hapana” Prisca alijibu.
“Haumjui?”
“Ndio. Ni mgeni amekuja leo au?” Prisca aliuliza swali ambalo lilionekana kumshtua kila mtu.
“Ila sisi unatujua?”
“Ndio. Ninyi ni wazazi wangu”
“Ila huyu haumjui?”
“Simjui kabisa. Sidhani kama nilikwishawahi kumuona mtu huyu. Mara ya kwanza kumuona ilikuwa pale hospitalini, nilishangaa kumuona akinikumbatia. Siku nyingine alikuwa akiniletea zawadi pale hospitalini. Kitu cha ajabu, ninyi hamkuonekana kujali, yaani mimi kutembelewa na kuletewa zawadi na mtu nisiyemfahamu mlikuwa mkiona kuwa ni jambo la kawaida sana na wakati nilikuwa nikifikiria sana” Prisca aliwaambia wazazi wake.
“Ok! Kuna mtu yeyote unamkumbuka?” Mzee Steven alimuuliza.
“Namkumbuka rafiki yangu, Pamela, Happy, Everlyn. Hivi Vonso amekwisharudi kutoka Uganda?” Prisca aliuliza maswali ambayo yaliendelea kumshangaza kila mtu.
Hiyo ndio hali ambayo ilikuwa imemtokea Prisca. Mshipa wake wa kumbukumbu ulikuwa umeharibika sana, katika kipindi hicho alikuwa akiwakumbuka watu ambao alikuwa akiishi nao katika kipindi ambacho alikuwa kidato cha tatu. Hakumkumbuka tena mume wake Gibson, kila alipokuwa akimwangalia, kwake alionekana kuwa mtu mgeni.
Prisca hakukumbuka kitu chochote kile, alikuwa akiwakumbuka wazazi wake pamoja na marafiki zake kwa sababu tu alikuwa ameishi nao katika kipindi kirefu. Hakukumbuka kama alikuwa ameolewa, hakukumbuka kama alikuwa amezaa mtoto ambaye alikuwa ameuawa zaidi ya kujishangaa kila alipokuwa akiyaminya matiti yake na kuona yakitoa maziwa.
“Nini kimenitokea mama?” Prisca alimuuliza mama yake.
“Kuna nini?”
“Matiti yangu. Nashangaa yanatoa maziwa kama mwanamke aliyejifungua” Prisca alimwambia mama yake.
“Mmmh! Hebu kesho twende hospitalini, linaweza kuwa tatizo la kiafya” Mama yake alimjibu.
Hayo ndio maisha yake yalivyokuwa. Prisca huyu alikuwa tofauti na Prisca yule ambaye alikuwa akikumbuka kila kitu. Hapo ndipo ambapo Gibson alipoanza kazi ya kuuteka moyo wa Prisca kwa mara nyingine tena. Mara kwa mara alikuwa akienda nyumbani kwao ambako huko alikuwa akikaa nae sana na kuongea pamoja.
Kila walipokuwa wakiongea, Gibson alikuwa akijisikia uchungu moyoni, hakuamini kama mke wake alikuwa amemsahau. Kazi ya kuuteka moyo wa Prisca kwa mara nyingine haikuwa rahisi ingawa alikuwa akijitahidi kadri ya uwezo wake. Mara kwa mara alikuwa akitoka nae na kuelekea ufukweni, katika mighahawa mbalimbali ili mladi kumfanya Prisca kuangukia katika mapenzi yake kwa mara nyingine.
“Unaonekana kama unaniogopa Prisca” Gibson alimwambia Prisca.
“Hapana Gibson. Unajua nahitaji muda zaidi wa kukuzoea. Unaponiona hivi, usijali. Tutaendelea kuzoeana tu” Prisca alimwambia Gibson.
Gibson hakutaka kukata tamaa, kila siku alikuwa akiangaika kumfanya Prisca amzoee na hatimae atamke neno ‘Nakupenda’ mbele ya macho yake. Hali hiyo iliendelea zaidi na zaidi, ukaribu wao ukaendelea kadri siku zilivyozidi kwenda mbele. Mwezi wa kwanza ukapita, mwezi wa pili ukaingia huku bado Gibson akiendelea kumfanya Prisca kujisikia kuwa huru nae.
“Lini utamwambia kwamba unampenda?” Mzee Steven alimuuliza Gibson.
“Muda bado. Ukifika, nitamwambia. Akikubali, nitamuoa kwa mara ya pili tena na kuzaa nae mtoto mwingine” Gibson alimjibu mzee Steven
Hiyo ndio hali ilivyokuwa, kila siku Gibson alikuwa akijitahidi kumfanya Prisca amzoee zaidi na zaidi. Kwa sababu yeye ndiye alikuwa amesababisha hayo yote basi hakuwa na budi kuangaika kumfanya Prisca ampende kwa mara ya pili hasa mara baada ya kupoteza kumbukumbu yake ya miaka saba iliyopita.
“Nitaendelea hivi hivi mpaka nitakapokuja kumuoa kwa mara nyingine tena” Gibson alikuwa akijisemea katika kipindi ambacho alikuwa akielekea Zanzibar pamoja na Prisca kwa ajili ya kuangalia mambo mbalimbali yaliyoachwa na wakoloni.
MWISHO
 
Back
Top Bottom