Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 75,203
- 157,377
Ifuatayo ni hadithi kuhusu uvumilivu katika ndoa na mahusiano. Hakuna haja ya kugombana kwa kimahusiano. Kuwa tayari kusamehe kwani hiyo ndio siri ya Ndoa kudumu kwa muda mrefu.
Soma na ubarikiwe.
Nilipokuwa mdogo, mama alikuwa akitupikia chakula. Usiku mmoja ambao siwezi kuusahau ni siku fulani hivi ambayo alituandalia chakula cha usiku baada ya kurudi toka kazini akiwa amechoka sana. Baba yangu anapenda sana kula viazi vitamu vya kuchemshwa, hivyo basi siku hiyo alituandalia chakula na akaweka mezani maziwa na viazi vitamu ambavyo kimsingi vilikuwa vimeungua mno baada ya yeye mama kujisahau kuwa aliviweka jikoni.
Mimi nilikuwa nikisubiri nione nani atagundua kuungua kwa viazi na kusema chochote, cha kushangaza baba alikula vile viazi na kuniuliza mimi siku yangu iliendaje na kama nilifanya kazi yangu ya shule (homework). Sikumbuki nilimwambia baba nini siku ile ila nakumbuka nilimsikia mama akiomba msamaha kwa baba kwa kuunguza viazi.
Na sitasahau maneno ambayo baba alimwambia mama. "Mama Tweve napenda sana viazi vilivyoungua ungua, wala usiwe na wasiwasi" Baadae usiku huo huo nilienda kumuaga baba na kumtakia usiku mwema sebuleni na kumuuliza kama ni kweli alipenda viazi ambavyo mama aliviunguza. Baba aliweka mikono begani mwangu na kuniambia; "Mama yako alikuwa na kazi nyingi sana kazini kwake leo na alikuwa amechoka mno.
Hata hivyo viazi vilivyoungua havimuumizi mtu yeyote, ila unajua ni nini kinaumiza? Maneno makali ya kejeli!" Akaendelea kuniambia "unajua mwanangu Hezron maisha yameandamwa na vitu pamoja na watu wasio wakamilifu kwa asilimia mia moja, mimi sio bora kwa kila kitu ninasahau kumnunulia nguo mama yako, muda mwingine nasahau kuwanunulia nguo nyie, nasahau siku za kuzaliwa kwenu na vitu kama hvyo" Akaendelea..
"Kitu nilichojifunza kwa miaka yote ni kwamba kujifunza kukubaliana na makosa ya wenzetu na kuchagua kusheherekea tofauti zetu ni moja ya vitu muhimu vya kutengeneza mahusiano yenye afya, yanayokua na ya kudumu. Maisha ni mafupi mno kuamka na majuto. Wapende watu wanaokujali na kuwa na msamaha kwa wale wanaojaribu kukudidimiza." Maneno ya baba yalinipa matumaini mapya juu ya maisha, na maono chanya juu ya kuishi na watu wa jamii mbalimbali.
Mpaka leo sishangai nikiwa natengeneza marafiki wengi kila kona nayokuwepo na kila sehemu niliyopitia. Sina pesa ila yote haya ni kutokana na kuwa na maono chanya, na kukubaliana na tofauti za wenzangu. Tofauti zangu na zako mimi huzisheherekea badala ya kunitenga na wewe.
Basi vivyo hivyo napenda kuwaambia marafiki zangu, mzingatie hayo katika Ndoa na mahusiano yenu. Inaweza kuwa ni mwarobaini wa matatizo ya kimahusiano. Enjoy your marriage and relationship and don't give room to the devil to infiltrate your home.
Bless you.
Nimeitoa mahali.