Hadithi: Kitanda cha Kuwadi

Aug 1, 2016
7
17
KITANDA CHA KUWADI

LUCY aligonga mlango, na kabla hajajibiwa, akaingia moja kwa moja hadi ndani. Alipokwisha kuingia, ndipo macho yake yalipiga kwenye sofa. Akamwona Teddy akiendelea kusoma kitabu kilichokuwa mikononi mwake, akiwa amelijilaza kifuani pa Eddy, aliyekuwa akimchezea nywele zake kwa mkono mmoja, ilhali ule mwingine ukiendelea kubadili idhaa za runinga kwa rimoti.

“Wenyewe humu ndani,” Lucy alisema baada ya kukutanisha macho na Eddy, aliyekuwa ameugeuzia uso wake mlangoni kufuatia kuhisi mchakato wa miguu, “hamjambo?”

Eddy hapendezwi na kasumba ya Lucy kuingia ndani bila kukaribishwa, walakini alizidhibiti hisia zake; ghadhabu zilibaki moyoni, uungwana akauvaa usoni. Akamlaki, “Oh, Lucy!”
“Karibu shoga,” Teddy naye alimkaribisha huku akijiinua toka kwa Eddy.

“Ahsanteni wapendwa,” Lucy alijibu akitabasamu. Akaendelea, “na kumradhi kwa kukuvamieni ghafla!”
“Ah, usijali Lucy, hapa ni kwako!” Eddy alijafaragua kumtoa hofu. Siku zote Insafu na uadilifu, vimekuwa kama kwamba ni mavazi kwa Eddy. Kama kaburi lifichavyo maiti, vivyo hivyo, ukakasi wowote moyoni mwake, aliudhibiti kwa furaha ya usoni.

“Haya, karibu uketi mrembo!” Teddy alimwonesha kwa ishara ya kidole mahala pa kuketi.

“Hata nakaa basi,” Lucy alijibu, “nataka tu nikuudhi kidogo shemeji yangu!” alimalizia sentensi yake huku akimgeukia Eddy.

“Haki ya Mungu, mwaka huu nitakutoza faini, Lucy!” Eddy alitania na kufanya kicheko hafifu. Alikwishaelewa shida ya Lucy; kumchukua Teddy na kwenda naye kwake. “Haya, huyo hapo, kazi kwenu!”

“Ahsante mwaya shemeji yangu,” Lucy alijibu huku akiachia tabasamu. Alimgeukia Teddy akimwashiria watoke.

Teddy alijisogeza karibu ya Eddy. Akambusu juu ya paji la uso, akimwambia, “I love you!” kisha akainuka. Alitoka akifuatana na Lucy. Hakuwa na haja ya kujiandaa kwa libasi wala manukato, kwakuwa hawakuwa wakienda mbali. Dera lake nadhifu la rangi ya manjano, lilitosha kuyasitiri maungo yake.

Macho ya Eddy, yaliendelea kuwaangalia akina Lucy, hadi walipopotelea kwenye korido nyembamba, inayokwenda moja kwa moja hadi kwenye mlango wa nyuma. Huko ndiko inakoanzia sehemu ya pili ya upande anaoishi Lucy. Kisha, macho yalihamia kwenye picha iliyoning’inizwa juu ya mlango huo wa korido, ikimwonesha Eddy akiwa ametinga suti maridadi ya rangi ya kahawia. Teddy akiwa ndani ya shela aghali. Wote wakiwa na nyuso zenye bashasha. Nyuma yao, wakionekana wazazi na ndugu zao. Mwaka mmoja tu umepita, tangu picha ile ilipopigwa. Ilikuwa siku ya harusi yao.

Lucy Kingu, msichana wa Kizigua, mwenye kila sababu ya kuitwa mrembo kwa namna Muumba alivyokisanifisha vyema kiwiliwili chake. Ufupi usiochusha na mirindimo mithili ya Mjaluo, vilimfanya kila aliyekutana naye, ageuke mara mbilimbili kumtazama. Na hata lafudhi yake ni ya pwani, ambayo siku zote huitolea puani, kiasi cha kuweza kumfanya nyoka atoke pangoni. Ima kuhusu ucheshi wake, imedhihiri, ni wa kiwango cha kuweza hata kuingia ndani mwa watu bila kukaribishwa. Maisha yake ya fahari na anasa yalisadifu mwonekano wake. Ingawaje, vyanzo vya kipato chake viliendelea kuwa fumbo lililokosa mfumbuaji.

Lucy ni mpangaji mwenzao na akina Eddy, katika nyumba hiyo, ambapo Eddy na mkewe, walipanga upande wa mbele, ilhali yeye Lucy, akiwa amepanga upande wa sehemu ya nyuma, wa mjengo huo aghali na wa kisasa.

Aghalabu, siku za Jumamosi na Jumapili, Lucy humfuata Teddy na kwenda naye kwake kwa minajili ya kumsaidia mambo kadhaa ikiwemo, usafi wa nyumba pamoja upangaji wa samani za ndani. Siku nyingine, kupanga vyombo kabatini na ghasia za namna hiyo. Kama ilivyo kawaida ya mazoea, yakajenga tabia. Ikafikia kiasi, hata kama hapakuwa na cha kufanya, bado Lucy alimwendea Teddy kwa ajili ya kwenda kupiga naye soga tu.

Tabia hii haikumpendeza sana Eddy. Walakini aliipuuza, hakuyona madhara yake kwa nyakati zile. Ukizingatia, Lucy na Teddy hawakuwa na wasaa wa kutosha kuonana na kuwa pamoja mara kwa mara, zaidi ya mwishoni mwa wiki, tena kwa muda mchache tu. ‘Shemeji, nimekuja kumuiba bibiye kidogo!’ ama,‘Nataka nikuudhi kidogo shemeji yangu.’ Ndiyo yalikuwa maneno matamu toka kwa Lucy, akiyatumia kama utangulizi wa kumlainisha Eddy pindi amtakapo Teddy.
Upole wa Eddy uliosababishwa na uungwana wake, haukuweza kukabiliana na uchakaramu wa Lucy kila alipodiriki kumhitaji Teddy. Ingawaje, Teddy naye hakuonekana kuufurahia sana mchezo huo wa kuchukuliwa mara kwa mara, lakini hakuupinga.
____________

“MBONA kama leo umechangamka sana shosti. Kunani?” Teddy alimsaili Lucy hali usoni amekunja ndita kiudadisi.

“Kha! Ina maana umesahau?” Lucy alijibu akimgeukia Teddy. Taratibu, waliteremka kwenye ngazi za mlangoni. “Si nilikwambia leo ndiyo Frank anakuja!”

“Oh, No Lucy! Kama mambo yenyewe ndo hayo, hata huko kwako siingii tena!” Teddy aligomea nje ya mlango wa Lucy. “Haya mambo yataniletea matatizo-nilishakwambia.”

“Jamani Teddy, tafadhali usifanye hivyo. Jamaa alikuwa anaomba siku hii ifike haraka aje mkutane. Leo ghafla tu ubadilike kama tumbo la kuharisha!”

“Lucy, siku ile haikuwa serious kihivyo – viweje ukalibebea bango?” Teddy alimjia juu Lucy.

Ghadhabu zilimvaa Lucy. Macho yakambadilika. Alitamani hata amrarue Teddy. Lakini alijitahidi kujidhibiti. Akauvaa uso wa nyani anayesubiri kuuawa kutafuta huruma. Akasema, “Vyovyote iwavyo, nisamehe mimi shoga’angu. Tafadhali usiniangushe. Hebu fikiria, mtu na heshima zake ameacha majukumu yake kwa ajili yako, halafu ghafla tu iwe bure bileshi!”

Maneno ya Lucy yalimmaliza nguvu na kumlainisha kabisa Teddy.
Takribani mwezi sasa, tangu Lucy alipoanza kumkuwadia Frank kwa Teddy, bila ya kujali kuwa Teddy ni mke wa mtu. Vishawishi na maneno matamu vilimwisha Lucy bila dalili ya mafanikio. Wa aidha, Frank naye kupitia kwa Lucy, alijitahidi kumwagizia Teddy vijizawadi vya mara kwa mara, hadi kufikia siku hiyo ambapo, kwa mujibu wa Teddy ni kwamba haikuwa serious. Tangu awali, Lucy alishawishi ifanyike miadi baina yao hapo nyumbani kwake. Lengo likiwa kutokum-makinisha Eddy juu ya kinachoendelea. Na, kwakuwa Teddy hakupinga, Lucy alilichukulia kwa umuhimu huo, akiamini ule usemi wa Kiyunani, kwamba,‘kimya humaanisha ndiyo’.

Nikirudi kwangu muda huu, Eddy atahisi kuna jambo. Teddy alijifikiria. Haikuwa kawaida yake kutoka nyumbani kwake na kwenda kwa Lucy, kisha arudi ghafla namna ile. Hivyo, hofu ikawa, huenda angezua maswali toka kwa Eddy.

“Lakini ni maongezi tu Teddy!” Lucy alimtoa Teddy kwenye lindi la mawazo. Teddy alipouinua uso wake kumtazama, akapata mwanya wa kuendelea. “Kama utaogopa kuongelea naye hapo sitting room, mi’ nitakusabilieni chumba changu.”

Zikateketea sekunde kadhaa wakati Teddy akitafakari. Hatimaye, alilegeza msimamo. “Okay fine, kwa heshima yako Lucy. Ila, nitakaa naye dakika tano tu, si’ zaidi ya hapo.”

Shangwe ililipuka moyoni mwa Lucy. Alitamani ambebe Teddy mgongoni kwa furaha. Kufanikisha mpango huo wa ukuwadi, alijiongezea thamani kwa mfadhili wake, Frank.
“Hayo ni maamuzi yenu shosti. Wala sina pingamizi.” Lucy alijibu. Akaongezea, “kwahiyo chumbani au sitting room?”
Baada ya kukosekana jibu la haraka, Lucy alipendekeza. “Ila mimi nashauri tu, bora mkaongelee chumbani, maana sitting room anaweza kutokea mtu akaingia, akakuhamisheni kwenye mazungumzo – yote kwa yote, chaguo ni lako!”
Teddy aliafiki chumbani.

Walipanda ngazi. Wakaingia ndani. Teddy akawa wa kwanza kujitosa chumbani, kwakuwa chumba kilikuwa mwanzo kabisa kabla ya kuifikia sebule. Lucy akiwa amechanulisha tabasamu usoni, haraka alikwenda barazani kumwendea Frank.

Ambacho Teddy na Lucy hawakuking’amua ni kwamba, wakati wakiendelea kujibizana na kushawishiana pale nje, Eddy alikuwa akiwaona kupitia madirisha madogo ya msalani. Ilitokea kwa sadfa tu, Lucy na Teddy walipotoka kule kwake, Eddy aliinuka na kwenda msalani. Baada ya kukidhi haja yake na kusimama, ndipo aliwashuhudia wakilumbana.
____________

CHUMBA cha Lucy ni chenye kupendezesha macho na kuburudisha ubongo. Si tu kwa hewa mwanana iliyopozwa kwa kiyoyozi, bali pia kwa namna upangaji wa samani ulivofanywa kisanii; Kitanda kikubwa cha futi sita kwa sita, kiliegeshwa mashariki mwa chumba; Runinga kubwa na bapa ya Samsung iliyokuwa ikicheza nyimbo za Kihindi kwa sauti hafifu, ilibandikwa kiufundi ukutani huku nyaya zitokazo kwenye ungo ulioegeshwa juu ya paa la vigae, na zile zinazokwenda kwenye deki, zikiwa zimejaladiwa vema na tranki maalumu, ili kufanya mazingira kuwa nadhifu; Kaskazini mwa kitanda, paliwekwa viti viwili maridadi vilivyochongwa kwa mninga, katikati vilitenganishwa na meza ndogo ya kioo; Jokofu dogo lilikuwa dhiraa chache nyuma ya kabati kubwa la nguo lililopambwa kwa maua. Vyote hivyo, vikiwa juu ya zulia zito na laini mithili ya sufi.

Baada ya kuingia chumbani, Teddy alijibwaga kitandani kiasi cha kufanya miguu yake ipepee angani. Lakini ghafla, haikupita muda akiwa hapo kitandani, kama aliyejihadhari jambo, upesi aliinuka kitandani. Akahamia kwenye moja kati ya viti viwili. Bila shaka, hakutaka Frank amkute kitandani, kitu alichohisi kingemtengenezea fikara mbaya kichwani.

Haikuchukua walau dakika moja tangu Teddy alipoketi, mlango ukafunguliwa. Frank akaingia. Moyo wa Teddy ulipiga kwa kasi ya ajabu. Akajikuta akipoteza mhimili wa kujiamini, akawa mithili ya mbwa aliyemwona chatu. Hakuelewa ni kwanini hasa aliingiwa na hali ile ya kutojiamini. Pengine ni kwa sababu haikuwahi kutokea, hata siku moja, akakaa faragha ya mapenzi na mwanaume mwingine zaidi ya mumewe tangu alipoolewa. Ama pengine, ni nyota tu ya Frank iliizidi nguvu ile ya kwake.

Baada ya kufunga mlango, Frank aligeuka na kumwangalia Teddy. Uso wake ulichanulisha tababasamu. Alimsogelea na kumsabahi kwa bashasha. “Oh, mrembo – mambo!”

“Poa, karibu!” Teddy alijibu. Alijilazimisha kuiondosha hofu iliyokwishaanza kumnyima hali ya kujiamini kiasi cha kumkosesha uhuru.

Frank alijongea. Akaketi kwenye kiti kidogo kilichobaki jirani na alichokalia Teddy. Sasa, wakawa wanawajihiana uso kwa macho, wakitenganishwa na kile kijimeza kidogo cha kioo. Harufu ya marashi aliyojinyunyizia Frank, ilibadili kabisa reha ya chumba hicho kiasi cha kumnyanyasa Teddy kisaikolojia, baada kukiri kwamba yeye hakuwa akinukia.

“Teddy,” Frank aliita akimtazama Teddy, uso ungali ukichanua kwa tabasamu. Teddy alipoyagonganisha macho yake yaliyojaa junaa, akakosa pozi. Akamfanya Frank kuendelea. “Bahati iliyoje kukutana nawe leo hii. Nimefurahi sana.”
“Mimi pia.” Teddy alijibu akiyakwepesha macho yake yaliyokolea wanja wa chini.

“Hii ni bahati kubwa sana kwangu. Sina budi kukushukuru!” Frank alisema, sauti yake ikikosa haraka.

“Bahati kukutana tu?” Teddy alisaili. Akafuatisha kicheko hafifu ili kukabiliana na hofu iliyokuwa imemganda moyoni. Hakutaka kuonekana mshamba, asiyejiamini, au anayejirahisi.
Ambacho Teddy alianza kukisahau ni kwamba, zile dakika tano alizosisitiza kuzitumia bila kuzidisha japo sekunde, zilikwishakukatika.

“Naam.” Frank alisadikisha maneno yake. Huku akiendelea kumtazama Teddy, hakuwa haba wa maneno. “Ni bahati iliyoje kukutana kwa mara ya kwanza na mtu niliyempenda hata akafanikiwa kuichachafya akili yangu!”

“Mmh, wanaume kwa uongo! Vile ulivyo serious utadhani ni kweli unenayo!”

“Kha! Hivi huamini kweli, Teddy?” Frank alijiulizisha huku akiitoa ile meza ndogo katikati yao. Akaiweka pembeni. Akakiburuza kiti chake. Akamsogelea Teddy kwa karibu, hadi magoti yalipogoteana.

“Teddy,” Frank alisema, mikono yake akiipeleka na kuikutanisha na ile ya Teddy. Kwa sauti nzito, yenye kuutetemesha moyo wa Teddy, akasema, “Nakupenda sana. Sina hata chembe ya ulaghai. Na sijaanza leo kukupenda!”
Kikapita tena kimya kifupi, Teddy aliyahamisha tena macho yake. Akayazugisha runingani. Frank aliiinua mikono ya Teddy. Akaibusu.

Mapigo ya moyo ya Teddy yalibadilika. Joto la aina yake likampanda. Dakika tano zikawa kumi. Mara, kumi na tano. Akafunua kinywa, “Lakini Frank, ujue mi’ ni mke wa mtu!”
“I know Teddy. Ninakuahidi sitakubughudhi, wala kukuharibia ndoa yako,” Frank alijitetea. “Na nakuhakikishia, wewe ndiye utakuwa mratibu wa mipango yote katika mahusiano yetu!”
Waliangaliana.

Macho ya Frank yenye kiu na tamaa ya huba yalizidi kuimarika ilhali yale ya Teddy, yenye hofu na kutojiamini yakizidi kulainika. Teddy aliposhindwa kumtazama Frank, akakwepesha kwa aibu.

Frank aliinuka kwenye kiti. Akamsogelea Teddy na kumuinamia. Akambusu kwenye paji la uso. Kama haitoshi, akapiga magoti. Akamwambia kwa sauti ya kubembeleza, “Teddy, tafadhali niamini. Nakupenda! Nakupenda ile mbaya!”

Unajisikiaje kubembelezwa kwa kupigiwa magoti na tajiri, kijana mtanashati? Wazo lilimjia Teddy.

Frank, kijana mkwasi, anamiliki vituo kadhaa vya mafuta; petrol na diesel. Kama haitoshi, anamiliki jengo kubwa la biashara jijini Dar es Salaam, liitwalo Home of Shopping. Zaidi, ana utitiri wa nyumba na magari ya kifahari. Sehemu ndogo ya urithi wa marehemu baba yake, pamoja na biashara za haramu, vilimfanya aendelee kudumu kwenye orodha ya vijana wadogo wenye ukwasi wa kusaza.

Frank hachoshi kumtazama. Urefu kimo chake. Ucheshi haiba yake. Jamali sura yake. Utajiri tunu yake. Na, kama walivyo vijana wengi wakwasi, wanawake ugonjwa wake (ingawaje hili hakuna wa kulithibitisha hadharani kwakuwa lilifanyika faraghani).

Nani asiyeiota bahati ya kuliliwa na mtu huyu? Teddy aliendelea kutafakari, hata asitambue, muda huo tayari alikuwa amemkumbatia Frank.

Frank hakuruhusu kuipoteza nafasi hiyo ya kukumbatiwa. Akamsogezea Teddy mdomo wake. Milio mithili ya ile ya kasuku ilisikika baina yao. Taratibu, ulimi wa Frank uliaanza kutalii kinywani mwa Teddy. Joto nalo, halikufanya ajizi kuwachemka maungoni. Wakazoana msobemsobe. Wakajibwaga kitandani huku dera la Teddy likipeperushwa na upepo. Piga picha mwenyewe. Kama upepo tu umelipeperusha, vipi litamshinda Frank?

Bashasha na taadhima usoni, ni udhihirisho wa uungwana moyoni. Kwa hivi, kwa mwonekano wa Frank, Teddy alijihisi yu katika mikono salama. Hivyo, bila hiyana, alimsabilia Frank mwili wake. Akamsusia maungo yake.
____________

HADITHI: Kitanda cha Kuwadi
MTUNZI: Maundu Mwingizi

***ITAENDELEA kesho papa hapa!
 
KITANDA CHA KUWADI (02)

TANGU Eddy alipotoka msalani, ambapo alimwona mkewe akilumbana jambo na Lucy, akili yake haikutulia asilani. Hofu na mashaka vilimwandama kwa mkupuo huku mtungo wa maswali ukizidi kujirefusha kichwani mwake.

Nini kinaendelea baina yao? Mbona kama kuna kitu Lucy alikuwa anamlazimisha Teddy? Alitafakari.

Maswali hayo yalimfanya aanze kujutia kuuacha urafiki wa Teddy na Lucy ukishamiri namna ile. Akadhamiria kuupiga marufuku. Ingawaje alimwamini mno Teddy, walakini upepo wa wivu ulikwishaanza kuvumisha harufu ya usaliti ndani ya kingo za moyo wake.

Haraka, alijiinua kwenye sofa. Akaiendea simu yake. Akaichukua ili ampigie Teddy kumtaka arudi haraka. Pasi na kutarajia, baada ya kuipiga, aliisikia simu ya Teddy ikiita mumo humo ndani. Ilikuwa juu ya kabati la vyombo. Nguvu zilimwisha. Akaishia kusonya.

Kitendo hicho cha simu ya Teddy kuitia humo ndani, kilimfanya Eddy anyong’onyee kabisa. Mrindimo wa maswali kichwani mwake, viliufanya mwili upooze, akili inyong’onyee. Kwa hasira, alipiga ngumi kwenye ukuta. Ndipo akashusha pumzi na kujibwaga kitini.

Au nimfuate hukohuko? Alijiuliza.

Nitaonekana nina gubu! Akajionya.

Hakuiona sababu ya msingi ya kumfuata mkewe ghafla namna ile, zaidi ya hisia za wivu tu. Alirudi kitini kuugulia maumivu ya hisia.
____________

BAADA ya takribani dakika ishirini na tano kukatika wakiwa kitandani kwa kuwadi wao, ndipo Teddy alitanabahi, akiwa tayari amekwishafika kileleni mwa mlima. Mafuriko ya raha yalimfanya ajihisi kama aliyekuwa amepenyezwa hadi mbinguni, na kwamba sasa ameshushwa kwa parachuti hadi duniani. Mshale wa joto la mwili pamoja na ule wa mapigo ya moyo iliyokuwa imepanda juu, ilianza kushuka taratibu.

Hakufanyiwa takalifu yoyote. Bali, udhaifu wake mwenyewe uliopelekea apoteze mhimili wa kujiamini baada ya kumwona Frank tangu alipoingia, ndiyo ulimpelekea Teddy ajikute akifanya kile ambacho hakukitarajia kwa wakati ule. Majuto yakageuka mjukuu. Alitenda kosa kudhani kwamba, iko faragha baina ya mwanaume na mwanamke, bila ya nyaya za hasi na chanya kusababisha mtafaruku. Lakini, hapakuwa na namna tena ya kuubadili ukweli kwamba mambo yote waliyamaliza siku ya kwanza. Tena, kwenye kitanda cha kuwadi. Haraka alijing’atua toka kifuani mwa Frank.

“Frank, acha niwahi. Mume wangu asije akapata wasiwasi!” Alisema huku akisimama na kuaanza kuvaa nguo zake.

“Oh, Teddy, mbona haraka hivyo?” Frank alijiinua toka kitandani akiwa mtupu. “Anyway, Teddy! Ahsante kwa kila kitu, I promise you hautojutia kuwa nami!”

Alipomsogelea, wakakutanisha tena midomo yao kwa sekunde kadhaa. Ndipo Frank akamwachia. Akaiendea suruali yake na kutoa wallet. Akatwaa noti tano. Dola mia tano. Akamkabidhi Teddy.

Teddy aligeuka. Akamkata Frank jicho kali. Akamtupia swali, “Ndivyo Lucy alivyokwambia hivyo?”

“Kwamba?” Frank alihoji akijihisi hofu kwamba labda ametoa pesa ndogo.

“Kwamba ninajiuza!” Teddy alijibu huku ndita zikitengeneza mfano wa mataruma ya reli juu ya paji la usoni wake.

Kama utazibadili kwa shilingi ya Kitanzania, dola miatano ni zaidi ya shilingi milioni moja. Lakini Teddy hakujali hilo.
Ingawaje Teddy alitaka kuitukuza hadhi na utu wake, lakini pia hakuwa mtu mwenye dhiki ya pesa, ndiyo maana alipata kiburi kile. Wakati, Teddy ni Meneja Masoko kwenye kampuni ya Manyema Furniture Center, Eddy ni Afisa Ukaguzi Msaidizi katika Benki Kuu ya Tanzania. Njaa itoke wapi? Fauka ya hayo, Eddy alijikhini na kujikusuru alimradi mkewe apate kila atakacho.

“Oh No, Teddy! Nimejihisi upendo tu kukupa pesa. Thamani yako kwangu ni mara milioni ya hiki kijisenti nilichotaka kukupa.” Frank alijitetea.

Teddy alimkata tena jicho. Akaondoka bila ya kumuaga. Macho ya Frank yalibaki yakitazama sehemu za chini ya kiuno cha Teddy zikitaabika kadri alivyokuwa akipiga hatua, hadi alipoutwaa mlango na kutoka.

Pamoja na urefu wa Teddy kwa takribani futi tano na nusu, bado shepu yake haikuchusha. Ilijikata vema. Ikajitengeneza mithili ya namba nane. Hakuwa mweupe wala mweusi, bali mng’avu wa ngozi. Na zaidi, akikutazama ni kama anakuita.

‘Ah, kwisha habari yake…hana ujanja tena kwangu!’ Frank alijisemea huku akirusha ngumi hewani. Ishara ya ushindi alioupata kwa kile alichofanikisha kukifanza na Teddy. Pamoja na kujifaragua huko kwa Frank, walakini kwa dakika chache walizotumia, alikiri moyoni mwake kwamba, Teddy ni fundi.

Teddy alipotoka, alimkuta Lucy barazani, “Heh shoga, mbona mbiombio kama unayekimbizwa?”

“Mnh, shoga! Acha nimuwahi huyu bwana asije akapata hofu bure.”

“Tangu lini Eddy akapata hofu kwa kukaa kwako huku kwa nusu saa tu?” Lucy alibeza, “usipojiangalia, utajikamatisha mwenyewe!”

Maneno ya Lucy yalimwingia Teddy hata akajiona bahaluli wa kutupwa. Hapakuwa na sababu ya kuhamanika vile. Lakini alishindwa kuuhimili mfadhaiko wa majuto nafsini mwake. Mosi; alikusudia kufanya mazungumzo tu, walakini bila ya kutaraji, maongezi yakazaa tendo. Pili; tangu afunge ndoa na Eddy, hakuwahi kutoka nje ya ndoa yake. Kwa hivyo, ile ilikuwa ni mara yake ya kwanza. Uko wapi moyo usiofadhaika katika mazingira kama hayo?

“Unapagawa utafikiri huyo Eddy hafanyagi huko nje,” Lucy alikejeli. “Poa roho yako mtoto wa kike. Wewe ndiye nahodha wa moyo wako.”

Juu ya kabati la vyombo palikuwa na mfuko wa laini, wenye nembo ya kampuni ya Home of Shopping. Ndanimwe, mlikuwa na zawadi; kitabu, manukato na kalamu yenye nembo ya Home of Shopping. Vyote, vikiwa ni zawadi za Teddy toka kwa Frank. Ingawaje Frank bado alikuwa chumbani, Lucy aliutwaa ule mfuko na kumkabidhi Teddy bila hiyana. Teddy aliupokea bila ya kuhoji wala kudadisi. Akaondoka zake.
____________

KITOKEO cha nyumbani kwa Lucy, aliingia kwake. Alimkuta Eddy amejilaza kwenye sofa. Upole na uaminifu wa Eddy, vilimfanya Teddy ajihisi mwenye dhambi kila alipomtazama. Nafsi ilimsuta. Aliogopa hata kumsogelea. Alipitiliza moja kwa moja hadi juu ya meza ya chakula ambapo aliuweka mfuko aliopewa na Lucy. Akajifanya akilitandika vyema zuria la mezani. Tahayari iliendelea kutanda usoni mwake.

Eddy alimgeukia, akamwangalia kwa mshangao. Haikuwa kawaida kwa Teddy kurejea nyumbani akiwa katika hali ile. Mara zote ambazo Teddy hutoka japo kwa robo saa tu, huagana kwa mabusu. Na, arejeapo hukaribishana kwa mabusu. Sasa leo hata jambo hakuna!

Yameanza lini haya? Eddy alitafakari.

Joto la mapenzi yao halikuwahi kupoa hata siku moja. Tangu walipofunga ndoa, huenda kanisani pamoja. Huoga pamoja. Hula chakula pamoja. Kwa hivi, unapojitokeza walakini, hata kwa kiwango kidogo mithili ya punje ya haradani, ungalidhihirika tu hata ungalikuwa gizani.

Eddy akiwa anakitaabisha kichwa chake kutafakari, mara pua zilihisi harufu ya manukato ambayo si yeye, wala Teddy, ambaye huyatumia. Machale yalianza kumcheza kama mbwa aliyenusa mtara wa windo.

Kwa kawaida, macho ni kioo cha nafsi. Kinaakisi yote yaliyofichika kwa ndani. Na, kama kioo, macho huakisi yaliyomo ndani ya mtu kwa mwonekano wake. Kwa hivyo, kupitia macho ya Teddy, tayari hisia za Eddy ziliufasiri mwonekano mpya wenye mashaka.

Yawezekana akawa ananisaliti!
Wazo la kusalitiwa, Eddy alijaribu kulifutilia mbali. Walakini haikuwezekana. Usaliti ni miongoni mwa mambo ambayo hayazami upesi katika bahari ya sahau ya mwanadamu. Kwa hivi, mara zote, mawimbi ya fedheha ya kusalitiwa huibua mafuriko ya hisia za machungu moyoni. Pamoja na hayo, Eddy hakutaka kuonesha hisia zo zote kwa Teddy, ili endapo kama uko uchafu autendao, basi asije akamzindua kabla ya kumgundua.

Bila kumaizi kinachoendelea kichwani mwa Eddy, Teddy aliingia msalani. Eddy akautumia mwanya huo kuupekua mfuko aliotoka nao kwa Lucy. Nani amemnunulia hivi vitu? Lucy anaweza kuwa ndiye aliyemnunulia zawadi hizi? Ili iweje hasa? Eddy alihisi kupagawa baada ya kuviona vitu vilivyomo. Kining’inizio cha ufunguo (key holder), kalamu, pamoja na mfuko laini. Vyote vikiwa na nembo ya Home of Shopping. Si rahisi Teddy kuagiza kalamu supermarket ilhali ofisini kwake kuna kalamu za kila namna.

Nini kinaendelea hapa?
Eddy alizidi kuwaza. Mshale wa wivu ulimchoma kwa nguvu zaidi moyoni. Maumivu makali ya hisia za kusalitiwa yakaubabua moyo wake.

Mja mwenye busara anapotaka kumdhoofisha mtu, kwanza humfanya mtu huyo ajione imara na mwenye nguvu kubwa kuliko uhalisia, ili amghafilishe na kumfanyea alale fofofo katika usingizi wa dhana hewa ya uimara wake. Baada ya hapo, huwa rahisi mno kumshambulia na kummaliza. Kwa busara hiyo, Eddy alijifanya kutoshitukia chochote. Alitaka kumpa ujasiri Teddy ajione mmakinifu, ili iwe rahisi kumhadaa na kumkamata kirahisi endapo, uko mchezo mbaya auchezao.

Siku ikapita!

Maisha yaliendelea. Eddy akiwa amechukua hadhari mpya juu ya usuhuba baina ya Lucy na Teddy.
Kwa upande wao, Lucy na Teddy, hawakuonana takribani siku tatu tangu kukutana kwa Teddy na Frank. Hadi siku ya siku, Lucy alipomtembelea Teddy ofisini kwake.

“Enhee mwenzangu, kisa cha kuondoka siku ile kama tuna ugomvi?” Lucy alimdodosa Teddy mara baada ya kusalimiana na kuketi.
Siku hiyo wateja hawakuwa wengi ofisini mwa Teddy. Ikawapa wasaa wa kutosha kupiga soga.

“Ah, mwenzangu hofu! Nisijekumpoteza bure Eddy wangu kwa anasa za dunia!”

Lucy aliangua kicheko cha dharau. Ndipo akasema, “Ila kuna kitu sijui niseme umeniudhi au umenifurahisha?” Aliangaza huku na kule kama yupo anayeweza kuwasikia. Akaendelea, “Jamaa aliniambia umemsurprise vilivyo!”

Kauli hiyo ya Lucy ilimletea Teddy hisia mbaya kichwani. Kwamba, Frank ameshindwa kukaa na neno. Yaani, amemsimulia Lucy mambo waliyoyafanya chumbani, ilhali yeye alidhamiria kumficha Lucy juu ya alichokifanya Frank. Kwakuwa Lucy amekwishaonesha kujua kilichotokea, alijihadhari huenda akamuudhi kumficha jambo ambalo amekwishalijua. Akaamua aitumie fursa hiyo, yeye mwenyewe, kujiwahisha kumsimulia. Alimweleza kila kitu kinaganaga; kuanzia muundo hadi mitindo.

Lucy alimaka baada ya Teddy kumaliza masimulizi yake. “Heh shoga! Kumbe mlimaliza kila kitu?”

“Kha! Kwani we ulivyosema amekwambia nimemfanyia surprise, ni surprise gani?”

“Mi’ hakuniambia hayo. Alichoniambia ni kwamba baada ya maongezi na romance, alikupa dola mia tano ukazikataa. Hiyo ndiyo surprise niliyokusudia!”

Lah! Teddy aliuma kidole. Kwa sababu ya kujishitukia kwake, alijikuta amevujisha siri ambayo awali aliazimu kuitunza isimfike Lucy. Lawama alizotaka kumtupia Frank kwa kushindwa kutunza siri, sasa alijitupia mwenyewe.

“Yeap sikuchukua pesa zake, miye sifanyi biashara!” Alijifanya kujibu kama ambaye hajajutia uropokaji wake. Walakini, moyo ulimchoma.

“Japo tukio hilo limekupandisha chati kwake, ila kukataa pesa zote hizo shoga, kwa kitendo cha dakika ishirini na tano, miye nisingethubutu ujinga huo!”

“Shaurilo, utakuwa mtumwa wa ngono kwa kuendekeza pesa!” Teddy alimjibu shoga yake, akikunja nne..

“Kwahiyo umetumika bure bileshi!” Lucy alisema, akiangua kicheko. “Hata kama huna dhiki, lakini hiyo pesa ungewapelekea hata kijijini kwenu. Si’ wangekuoombea hata dua!”

“Shoga we! Kutegemea dua itokanayo na sadaka chafu, ni sawa na kutegemea kupata makaa ya mgomba. Hutopata kitu zaidi ya jivu tupu.” Teddy alijibu huku akitabasamu. “Miye sikutaka mazoea. Akishaanza kuhonga yule, atageuka ruba an’nate kama mwiba. Miye mke wa mtu hivyo!”

Unaweza kujiuliza, endapo Teddy aliyafahamu yote hayo, viweje basi alishawishika kutenda hiyana dhidi ya mumewe pamoja na utu wake? Chambilecho wahenga, kumsoma mwanamke, inahitaji vitabu vingi kama jozi ya karata. Na bado, yawezekana usifanikiwe kumfahamu.

“Kha! Mke wa mtu nd’o nini?” Lucy alimaka.
“Hujui?” Teddy alisaili huku akicheka, “mwanamke hakuumbwa kuja kuwa tembe la kila jogoo!”

“Vivyo hivyo kwa mwanamume. Hakukuletwa duniani kuja kuwa fahali wa kila mtamba. Lakini mbona wao, akiwemo huyo mumeo, wanatuchanganya tu kila siku!” Lucy alidhihaki.

Wakiwa katikati ya maongezi, aliingia kijana mmoja. Mtumishi wa hapo ofisini kwa Teddy. Wakapiga kimya. Alikwenda kuchukua mifuko ya kuwafungashia wateja zawadi za kalamu na shajara kwa wanunuao samani.

“Subiri nikufundishe kitu,” Lucy aliendelea kumghilibu Teddy baada ya yule kijana kutoka. “Kwakuwa mumeo anakuamini; hana shaka juu yako, inabidi huu mchezo uucheze vyema. Usibadili mfumo wa maisha yenu hata chembe, ili kuepuka kuingiza harufu ya usaliti ndani ya nyumba yako!”

Unawezaje kuizuia harafu ya manukato isisambae, ilhali unaendelea kuyapuliza? Nisiingize harufu ya usaliti ndani hali ya kuwa naendelea kusaliti? Teddy alijiuliza kichwani. Akajifanya hajaelewa, “Unamaanisha nini?”

“Nina maana hii; mathalani, endapo huwa mnatabia za kuachiana simu zenu, usibadilike ukaanza kutembea nayo kwapani. Kama unataka kuwasiliana na Frank sajili namba nyingine, ambayo utakuwa unaiacha hukuhuku ofisini. Tena, mtakuwa mkichat mchana tu. Ikitokea kuna dharura ya usiku, utakuwa unatumia hata simu yangu.” Aliweka kituo kupisha mate yalainishe koromeo lake. “Na, mkitaka kukutana, mara moja kwa wiki, siyo mbaya, alimuradi siyo nje ya chumbani kwangu. Maana, naona kama bado una mawenge wewe! Usije ukajikamatisha mwenyewe!”

“Mnh! Lucy kwa ushawishi tu, hujambo mama!” Teddy alijifanya kudhihaki, ila maneno ya Lucy yalimwingia vilivyo, hususani hilo la matumizi ya simu.

“Cha msingi kaa ukijua, hata kama huna njaa ya pesa, usikubali kutoka kapa. Hadi sasa mwenziyo tayari amekwishajilia vyake kwako. So, hata siku ikifikia hatua unataka kumtema, hakikisha nawe umemla mfukoni. Sasa kazi kwako!” Lucy alihitimisha. Akainuka kwa ajili ya kuondoka zake.

Teddy akainuka naye ili kumsindikiza.
Lucy aliibeba dhamana ya kuwa ‘mtu wa kati’ ili kuhakikisha singeli baina ya Frank na Teddy inaendelea kuchezeka bila ya machokoraa kuiharibu.
____________

WANABALAGHA wanasema, siri ni ya watu watatu tu, endapo wawili kati yao wamefariki. Sasa, ingawaje Teddy alijiapiza kuitunza siri hii, lakini ni wazi hakuwaelewa wanabalagha. Siri yao hii, ni ya watu watatu kweli, lakini wote wangali hai; Teddy, Frank na Lucy. Je, itabaki kuwa siri?
Hakujali!

Teddy alikutana tena na Frank kwa mara ya pili, kisha mara ya tatu ya nne, ya tano, na kuendelea. Mlemle, chumbani kwa Lucy. Tena, kitandani kwake. Hakujihadhari kwamba, cheche huzaa moto; na kijito huzaa mto. Penzi lilichipua ghafla mithili ya uyoga. Likasimika na mizizi imara.
Ingawaje Teddy alijitahidi mno kuuzingatia ushauri wa Lucy kwamba, asibadilishe kabisa mfumo wake wa maisha na mumewe ili kutomgutua, lakini kanuni za kimaumbile zilimgomea mara kadhaa. Kila alipokwenda kwa Lucy kukutana na Frank, alirejea kwake akiwa hoi bin taabani kiasi cha kushindwa kuyamudu vema majukumu ya nyumba kama mke.

Hali hiyo, ilimfanya Eddy azidishe udadisi.
Jumamosi moja, kama ilivyo ada, Lucy aliingia nyumbani kwa Eddy, kwa ajili ya kumchukua Teddy. Baada ya salamu, kama kawaida, aliwasilisha ombi lake. “Eddy namuomba kidogo wifi akan…” Kabla hajamalizia alichokusudia kusema, akajikuta amepiga kimya. Kuna kitu amekosea. Alikijutia. Akajaribu kuyapanga upya maneno. Kabla hajayatongoa, Eddy akamuwahi.

“Oh! haina shida. Mi’ mwenyewe nataka nifike Posta Mpya mara moja.”

Eddy alitoa ruhusa. Lucy alishukuru Mungu.
“Okay, Teddy haya miye natangulia!” Lucy aliaga. Akaondoka, akimwacha Teddy anaagana na mumewe.

“Sasa siyo uhamie huko. Mimi nitarudi kwenye saa tisa,” Eddy alimwambia mkewe akitazama saa yake ya mkononi.
Ilitimu saa tano na robo asubuhi.

“Sawa hubby. Kama kawaida yangu, nusu saa tu nitakuwa nimesharudi.”

Wakakumbatiana. Wakaagana kwa mabusu.
Wa kwanza kutoka alikuwa Teddy. Akachukua ufunguo wake kabisa ili akirudi afungue tu. Dakika chache, Eddy naye akatoka. Kwa kawaida, Eddy anapotoka hutumia gari yake. Hutokea mbele kabisa ya nyumba yao iliyoko Ilala Boma, ikitazamana na barabara ya Uhuru. Lakini siku hiyo, alitoka bila ya gari. Wala, hakutokea barabara ya Uhuru. Alitokea mlango mdogo. Mlango huo hutokea Ilala Boma kwa nyuma, ambapo ndipo upande wa pili wa nyumba yao; upande anaokaa Lucy.

Kauli ya Lucy kumwita Teddy wifi ilimzidishia Eddy mashaka na kiu ya kutaka kujua. Siku zote amekuwa akimwita Lucy dada, na akimwita Eddy shemeji, viweje leo ghafla amekuwa wifi! Wifi kwa nani?

Akiwa amekwishatoka ndani, na sasa anatembea, alitupia macho yake usawa wa geti dogo la kuingilia kwa Lucy. Ndipo akaliona gari la thamani, Hummer, likiwa limeegeshwa mlangoni. Mapigo ya moyo yakamwenda mbio.

“Ni nani mwenye gari hiyo?” Eddy alijisemea peke yake. “Ni mgeni wa Lucy au mtu wa Te…’ Akawahi kuzifutilia mbali hisia mbaya dhidi ya mkewe.

Gari liliegeshwa mbele ya mlango mdogo wa kuingilia kwa Lucy. Pamoja na kuziondoa hisia mbaya dhidi ya mkewe, mapigo ya moyo hayakuacha kumwenda mbio.

Ndiyo kawaida ya moyo. Unapohisi jambo baya, au hata zuri, ghafla tu hubadili mapigo yake yaliyozoeleka. Sasa, jambo hili ni baya au zuri hata mapigo ya moyo wa Eddy yakabadilika? Kama ni jambo zuri, ni lipi? Na kwa uzuri gani hasa? Yumkini si jambo zuri. Kama ni jambo baya, ni lipi? Na ni ubaya gani?

Mapigo ya moyo yalimwongezeka maradufu baada ya macho ya Eddy kutua kwenye jalada la gurudumu la akiba lililofungwa nyuma ya gari lile. Lilivishwa nembo ya Home of Shopping. Alimjua fika mmiliki wa biashara ile, Frank Majumbi; kijana mdogo mwenye ukwasi mkubwa unaonasibishwa na biashara za dawa za kulevya azifanyazo kwa siri. Kilichomshitua Eddy si tu biashara za Frank, bali tabia ya umalaya aliyo nayo. Huko mjini, anafahamika kwa tabia hiyo. Akiamua kumfuatilia msichana, hata awe mke wa mtu anayefichwa ndani kama ulimi, ni muhali kwake kumkosa. Kwake yeye, Frank, kupoteza mamilioni ya pesa ni aula kuliko kumkosa mwanamke aliyemkusudia.

Kumbukumbu za Eddy zikarudi nyuma hadi siku ile Teddy alipoingia ndani akiwa na mfuko laini wenye nembo ya Home of Shopping. Pamoja na kalamu yenye nembo ya kampuni hiyohiyo.

Si’ bure. Kuna kitu hapa! Je, mle ndani anamfuata Lucy mwenyewe au kuna mchezo nachezewa? Hisia za wivu zikazalisha uchungu mfano wa sumu ya nyoka, uliotambaa kwa kasi ndani ya moyo wa Eddy.

Hisia za kuzabwa kelbu usoni, huumiza mara dufu kuliko hata maumivu halisi ya kelbu hilo. Maumivu hayo ya hisia ya kusalitiwa, yaliuchakaza moyo wa Eddy. Lakini, bado alijikaza kisabuni. Alijipa moyo kwamba, huenda lile gari si’ la Frank. Hutokea gari ya mtu mwingine ikawekewa jalada kwenye gurudumu la akiba la kampuni nyingine kwa malipo maalumu ikiwa ni sehemu ya matangazo ya biashara.

Wazo lingine likamkatalia. Kwa ughali wa magari ya namna ile, si’ rahisi kwa tajiri mmiliki, kuweka kava la kampuni nyingine kwenye gari yake ili kumtangazia biashara kwa malipo. Hata kwa urafiki, haiwezekani.

Lucy anaweza kuwa anamkuwadia mke wangu kwa Frank? Mungu eupushie mbali, nitamuua hadharani. Eddy aliwaza.

HADITHI: Kitanda cha Kuwadi

MTUNZI: Maundu Mwingizi (MwanaBalagha)

***ITAENDELEA hapa kesho penye uhai.
 
KITANDA CHA KUWADI (03)

Wazo jingine lilimjia. Huenda kuna mtoko wa siri baina ya mmliki wa gari ile, ambaye hisia zake zilimwambia lazima ni Frank, pamoja na Teddy. Hivyo, alijongea hadi mbele kidogo, ambako kuna duka la vyakula. Akachagua kiti kilichokuwa kwenye meza yenye utulivu. Akaketi, apate kuona endapo Teddy atatoka na mwenye gari ile.

“Karibu kaka!” Sauti kavu toka kwa mhudumu wa kike ilimwingia Eddy.

“Ahsante. Niletee maji ya moto makubwa.”
“Kilimanjaro au Uhai?”

“Lete yoyote!”

Mhudumu aliondoka. Alirejea dakika chache baadaye akiwa na trei lenye chupa ya maji na bilauri. Akamhudumia Eddy. Eddy akamlipa.
Alikaa pale bila kuona mtu akitoka mle ndani kwa Lucy kwa muda wote. Baadaye, alitupia macho kwenye saa yake ya mkononi. Ilitimu saa sita na robo. Kwa maana kwamba, ametumia takribani saa nzima akiwa pale. Aliinuka. Akarejea kwake; ambapo kwa makubaliano yake na Teddy, muda ule Teddy angekwisharudi.

Alipofika kwake, hakumkuta Teddy. Hapo ndipo alipozidi kuchanganyikiwa.
Hakutaka kumpigia simu. Akawasha runinga. Akajilaza kwenye sofa ili Teddy akirejea, amkute hapo.
____________

TEDDY hakuwa na haraka ya kurudi. Japo aliahidi kurudi kwake ndani ya nusu saa tu, lakini alijua fika mumewe angerejea mishale ya saa tisa alasiri. Akamweleza hivyo Frank. Wakawa huru. Huko chumbani kwa Lucy, waliimaliza mizungu yote; mipya na ya zamani. Tayari, pombe ya penzi la Frank, ilikwishaichachua togwa ya penzi la Eddy. Ikailevya chakari akili ya Teddy.

“Teddy, najuta kukuchelewa hadi ukaolewa.” Frank alimtamkia Teddy maneno hayo akiwa juu yake. Akampiga busu mdomoni. “Upendo wangu umefikia kiwango cha kumwonea wivu mpaka mumeo. Unaweza ukapiga picha mwenyewe hapo, ni kwa namna gani kwako sijiwezi asilani!”

“Mungu hakupanga, Frank. Hata mimi, sasa nakiri umeuteka nyara moyo wangu!”
Uongo wa mahaba ukavitawala vinywa vyao.
____________

ILIPOTIMU saa nane mchana bila ya Eddy kumwona Teddy, alikata shauri. Akainuka. Akatoka tena mpaka kule grocery alipoketi awali. Akiwa huko, aiiona ile gari ikiwa palepale. Vilevile alivyoacha awali.
Wanafanya nini hawa muda wote huu? Eddy alijiuliza huku akijipigapiga kichwani kwa ghadhabu.

Biashara za Lucy sizijui zote. Je, na huyo Teddy naye ana biashara gani ya kumweka muda wote huo na hwa matajiri wa mjini? Akiwa katikati ya tafakuri nzito, geti la nyumbani kwa Lucy likafunguliwa. Akatekwa umakini ili kumtambua aliyefungua geti hilo. Macho yalimtoka kuangalia kule kwa Lucy, alihisi kitu kama radi kikiucharaza moyo wake.

Hakutaka kukurupuka, alijitahidi kuilazimisha staamala ya moyo. Naam, alimshuhudia Frank Majumbi, akitoka kwa Lucy. Moja kwa moja, akaingia kwenye gari yake. Akatimua vumbi wakati anaondoka.

Frank ndiye alikuwa kwa Lucy tangu saa tano mpaka sasa? Eddy akaiangalia saa yake. Haikuwa na hiyana - ikamweleza bayana. Kwamba, ilikwishakutimu saa nane na nusu.
Muda wote huo alikuwa na Lucy pekee? Alikuwa na Teddy au alikuwa nao wote kwa pamoja? Na kwanini Frank hajatembea na dereva wake? Bila shaka ni ujio wa siri.

Eddy alijihisi kuishiwa nguvu. Akajilaza juu ya meza ya plastiki aliyoichagua kupumzikia. Ilimchukua takribani dakika saba akipumbaa akili. Ndipo akainuka. Akaanza kutembea, kurejea kwake; ambapo alikuta milango i-wazi.

Teddy amekwisharudi! Kwanini arudi mara tu baada ya Frank kutoka? Yamkini, ni yeye ndiye aliyekuwa naye. Eddy alijivurumishia maswali kichwani mwake wakati akiingia ndani. Macho yake yalijitahidi kuangaza huku na kule hadi yalipokita kwenye marumaru. Akaona majimaji yaliyoachia alama za nyayo za mtu zilizotokea bafuni, kuelekea chumbani.
Kwanini amefikia kuoga moja kwa moja? Eddy alijisaili.

Kifua cha Eddy kikageuka mfano wa kengere huku moyo wake ukiwa kama kigongeo cha kengere hiyo. Mapigo ya moyo yalikita utadhani yanakaribia kuachia nyufa kifuani. Eddy aliendelea kuwaza huku akielekea chumbani, ambapo alimkuta mkewe akiwa amejitupa kitandani kama aliyekufa. Frank alimchosha vilivyo.

“Teddy,” Eddy aliita. “Mbona unalala saa hizi?”
“Aah basi tu. Najihisi mchovu tu!” Teddy alijibu papohapo.
Hakuwa usingizini.

Kuna kitetemeshi cha mashaka kwenye sauti yake. Kipi kimemchosha? Au Frank? Laa, haiwezekani. Eddy alitapatapa mithili ya kuku mwenye kiu kali ya maji.

Mgogoro uliozuka baina ya Eddy na hisia zake mwenyewe, ulimzidishia maumivu makali moyoni. Walakini, alijivika amani ya bandia, akiamini kuwa, moyo wenye jeraha hufichwa na uso wenye furaha. Alikwenda hadi kwenye kioo. Akawa kama anayejiangalia bila hofu. Alijihisi kukonda ndani ya muda mfupi.

“Ulirudi saa ngapi?” Eddy alijitahidi kuuliza kwa sauti tulivu, ili kutoamsha hisia hasi kwa Teddy.
“Oh, ilikuwa..” Teddy alishindwa kumalizia jibu lake la kubuni. Hakulitegea swali hilo, “Sidhani hata kama ilizidi nusu saa tangu ulipotoka!”
Uongo wa kwanza!

Kitu kisichoonekana kikamkaba Eddy kooni kwa hasira… Dukuduku!

Alitamani kumnyakia Teddy kama nyani kwa jinsi ghadhabu zilivyomzidia. Alijaribu kumeza funda la mate, kulilegeza dukuduku lake. Kitendo cha Teddy kuanza kumdanganya, kilimfanya azidiwe na mafuriko ya hisia mbaya moyoni mwake.

Uongo ni kama mende, ukimwona mmoja tu, fahamu kuwa kuna wengine. Tayari Eddy ameukamata uongo wa kwanza wa Teddy. Bila shaka, amekwishamdanganya mara nyingi. Na si ajabu, akaendelea.

Eddy alitoka chumbani hadi ukumbini. Akajibwaga sofani. Moyo ulimwuma mithili ya kidonda. Kila dalili na harufu mbaya ya usaliti vilimwingia kichwani mwake. Akiwa hapo amejilaza, macho yake yakiendelea kuhesabu paa, Teddy naye alitoka chumbani. Akajumuika pamoja naye hapo ukumbini.

Teddy ananisaliti kwa Frank. Lucy ndiye kuwadi wao! Na uchafu wao wanaufanyia mumohumo kwa Lucy. Hisia ziliendelea kuchachamaa kichwani mwa Eddy.

Eddy alitamani kumvuta Teddy karibu yake. Asemezane naye kwa maneno, kuutafuta ukweli. Walakini, alijizindua kwa maneno ya wenye busara. Kwamba, haja ikishughulikiwa kwa matendo hupatikana upesi. Lakini, ikishughulikiwa kwa maneno, huchelewa kama sadaka. Kwa hivi, alichagua kutumia vitendo.

Wahenga walinena, mchuzi wa mbwa hunywewa ungali wa moto. Eddy hakutaka kulaza damu. Akapaza sauti akimwelekea Teddy, akijitahidi kukidhibiti kitetemeshi cha ghadhabu katika sauti yake. “Hebu niazime simu yako mara moja!”

Bila kusuasua, Teddy akanyanyuka. Akampelekea simu. Akarejea kwenye sofa alilokuwa ameketi. Hakuwa na wasi kwani mara kadhaa Eddy huichukua simu hiyo na kuperuzi bila kukuta majanga. Ni kweli kwamba, zamani hakuwa na majanga. Sasa amekuwa nayo. Lakini hakuwa na hulka ya kuwasiliana mambo ya mapenzi na Frank, kwa kutumia simu hiyo.

Tofauti na mara zote ashikapo simu hiyo, siku hii Eddy alianza kwa kuperuzi meseji zote anazowasiliana mkewe kuanzia kwenye WhatsApp, facebook na hata zile meseji za kawaida. Kote hakukuta kitu kibaya. Akahamia kwenye namba alizohifadhi. Akaitazama namba moja baada ya nyingine kwa umakini. Nako, hakuuona utata!

Japo Teddy alikuwa na hakika kwa namna ambavyo anaucheza mchezo ule, hakuna kitu ambacho Eddy atakifumania kwenye simu ile, lakini bado hofu ya kihalifu haikumwacha mtulivu. Mara zote, alimtupia mumewe jicho la wizi apate kumsoma usoni. Alihangaika hivyo mpaka alipomwona Eddy akiiweka simu ile juu ya meza. Akashusha pumzi. Alitamani akaichukue. Akajionya asijekumshangaza Eddy.

Wakati utulivu ukiendelea kuishambulia akili ya kila mmoja wao, Eddy alikumbuka kitu. Alishika simu yake. Akatuma ujumbe mfupi kwa rafiki yake, Twalib Ngahoma. Akawa anasubiri majibu. Dakika moja, mbele akajibiwa meseji yake. Alitumiwa namba ya simu na Twalib Ngahoma – namba ya Frank Majumbi.

Twalib na Eddy ni marafiki wa siku nyingi tangu wangali chuoni. Baada ya kuhitimu masomo, Eddy aliajiriwa NBC Bank na baadaye BOT. Twalib aliajiriwa na Home of Shopping. Japo kwa wakati huo, Twalib alikwishaacha kazi hapo Home of Shopping.

Eddy akaichukua tena simu ya Teddy. Akaiandika namba ile aliyotumiwa na Twalib, kwa utulivu bila ya Teddy mwenye kuhisi hatari. Kisha, alifanya kama anapiga simu ili kujua kama namba ile Teddy ameihifadhi simuni mwake? Na kama ndiyo, atakuwa ametumia jina gani?

Naam, mambo yakadhihirika. Ni kweli ameisevu, kwa jina la Princess Kassum.
Utata mwingine. Kwanini amemsevu kwa jina bandia?

Nguvu zilimwisha Eddy. Jasho lilianza kumtiririka makwapani. Mapigo ya moyo yalimbadilika tena. Baada ya kujituliza, likamjia wazo lingine.

Alimwandikia meseji Lucy kwa kutumia simu ya Teddy, ili kumfanya Lucy ajue anawasiliana na rafikiye, Teddy. Shabaha ya Eddy ikiwa ni kuchokoza hisia za Lucy, ili kama kipo akijuacho, lazima atapagawa - na kufunguka. Meseji ilisomeka hivi:

Lucy nimekwisha-nimekwisha! Hakuna siri tena, Eddy amejua kila kitu. Nani amenichoma jamani?

Baada ya dakika chache, Lucy akajibu meseji:
Mungu wangu! We’ Teddy umechanganyikiwa au? Usiniambie…kweli Eddy amejua? Nilikuonya Teddy uwe makini…nikakwambia kwa hayo mawenge yako utajikamatisha- haya sasa kiko wapi! Je, umeshamtahadharisha Frank?

Kusikia jina la Frank, almanusura wazimu umpande Eddy. Kufikia hapo, akapata picha kamili kwamba, Lucy ndiye mratibu wa mpango unaoendelea baina ya Frank na Teddy. Mpango wa Ukuwadi wa mapenzi.

Eddy alijikaza. Akaendelea kubahatisha. Akamjibu Lucy kwa meseji:

Huna hata aibu Lucy, mimi nimekuwa chizi mpaka nijikamatishe? Hivi kwanini lakini umeamua kunitenda hivi? Ndoa yangu ikivunjika wewe utapata nini? Tena ulivyokosa huruma ukaamua na kuongeza na yako, eti nimelala na Frank mara mbili nzima Lol – utafikiri uliniona.

Kama matarajio ya Eddy yalivyokuwa, haikuchukua muda. Majibu ya ghadhabu kutoka kwa Lucy yakatiririka kwenye simu ya Teddy:

Tena koma ushike adabu yako. Sikukufunga kamba. Ulikuwa na hiyari ya kukubali au kukataa. Kama kweli ungelikuwa mtakatifu, ungelikubali kufuniliwa siku ileile ya kwanza tu? Kama mimi ndiye niliyetoa siri hiyo, kwanini niseme eti umelala naye mara mbili wakati ninahakika kuwa umeburuzwa zaidi ya mara kumi mpaka? Au haukuwa wewe uliyenisimulia mpaka ujinga wako wa kutumika bila kinga?

Mikono ya Eddy ilikuwa ikikitetemeka mpaka akashindwa kuishika simu. Jasho lilimfumuka licha ya kiyoyozi kilichokuwa humo ndani. Moyo ulikuwa ukipiga ndani ya kifua chake kama kwamba utaachia nyufa.

Ni kweli Teddy humsimulia Lucy mambo yote afanyayo faragha mpaka yale ya aibu. Ushoga ulifikia kiwango cha juu kabisa.

Lucy naye bila kutafakari, alijikuta akifunguka kwa ghadhabu baada ya kuona anatuhumiwa kitu kizito ambacho hajakifanya.

Eddy akiwa mwishoni kabisa mwa uvumilivu, simu ya Teddy ikaita. Lucy ndiye aliyepiga. Eddy akamwita Teddy apokee. Teddy alipomsogelea Eddy, alihisi mabadiliko. Macho ya Eddy na jasho lake vilimgongea kengele ya hatari kichwani. Akajikuta akiichukua simu kwa mashaka makubwa ili akaongelee pembeni.

“Pokea hapahapa!” Eddy aliamuru.

“Heh! Kuna nini mume wangu?”

“Pokea!” Eddy alifoka.

“Hallow!” Teddy alipokea kwa hofu na sauti ya kitetemeshi.

“We’ Teddy hivi uko sawa kweli?” Lucy alisaili kwa sauti kali na ya mshangao.

“Ndiyo niko sawa!” Teddy alijibu kwa mshangao.

Papohapo Eddy aliinyakua simu na kuikata. Walibaki wakitazamana mithili ya majogoo yanayokaribia kurukiana.

“Eddy, kuna nini mume wangu?”

“Hujui eh?” Eddy alijibu. “Teddy, yaani leo ni-” kabla Eddy hajamalizia maneno yake, iliingia tena meseji kwenye simu ya Teddy kutoka kwa Lucy. Kama kawaida, kibuyu hakifichi mbegu, Lucy alifunguka zaidi;

Kumbe simu unayo mwenyewe, we ni mpumbavu sana Teddy. Mimi niliyekuwa nikikusabilia chumba changu kila siku ufanyie umalaya wako leo nikuvujishie siri ili iweje? Kati yako wewe na Frank ni nani hata siku moja alifua japo mashuka tu mliyokuwa mkiyatumia? Kama ningeamua kukuchafua si ningemweleza huyo mumeo jinsi ulivyokuwa ukimsifia Frank kwamba ni kidume hasa kuliko mumeo! Sasa sitaki matatizo. Kuanzia leo mtafute sehemu ya kukutania. Hapa kwangu siyo guest. Ukome kabisa.

HADITHI: Kitanda cha Kuwadi
MTUNZI: Maundu Mwingizi

*** ITAENDELEA...
 
Iko vizuri hongera Mkuu. Ni ubunifu sahihi ingawaje naona kama imewahi sana kufikia point ya utambuzi labda kama ina flash back & forward.
 
Itaendelea ndio, lini ????

Hii lini inaendelea?
 
Back
Top Bottom