nameless girl
JF-Expert Member
- Apr 22, 2012
- 4,195
- 2,690
Kwa anayehitaji vitabu vya Joram Kiango, Dar es salaam usiku, Kiguu na njia na zawadi ya ushindi, karibuni kwa namba 0763044459 au 0712504985.
SURA YA KWANZA
Mwanzo wa Kisa na Mkasa
Ilikuwa mara yangu ya kwanza kumuona baba akitokwa na machozi. Kwa kweli, ilikuwa mara yangu ya kwanza kumuona mwanamume yeyote mwenye umri wa baba akilia, iwe sirini au hadharani. Kitendo cha mwanamume kutokwa na machozi, iwe kwasababu ya maumivu au majonzi, hakikupata kukubalika katika jamii yetu.
Nakumbuka nilipokuwa mtoto mdogo, wa miaka mitatu au minne hivi, nilipojikwaa na kuumia au kupigana na wenzangu nikalia. Baba alikuwa akinicharaza bakora huku akisema, “Mwanaume gani wewe unalia? Mwanaume halii!”
Babu yangu pia, mzee Karimanzila, aliwahi kunicheka sana kwa suala hilo la kulia. Siku hiyo mtego nilioutega mwituni ulikuwa umemnasa kanga mkubwa sana. Rafiki yangu mmoja tuliyekuwa naye porini aliniita kwa sauti kubwa kuniarifu juu ya kanga huyo. Lakini nilipofika kwenye mtego huo nilimkuta Katato, ambaye alituzidi sana kwa umri na umbile, akimfungua kanga huyo kwa madai kuwa ni mtego wake. Tulibishana naye sana. Kwa kunikomoa Katato alimwachia kanga wangu, ambaye aliruka na kutokomea zake mwituni. Nilijaribu kupigana naye lakini akanizidi nguvu na kunitia ngeu katika paji la uso. Nililia njia nzima hadi kijijini. Babu aliposikia habari hizo aliniita na kunidhihaki kwa kusema, “Ukiona mwanaume analia ujue na roho ya kike. Angestahili kuvaa gauni badala ya kaptula.”
“Lakini yule alikuwa kanga wangu wa kwanza. Nimekwishanasa njiwa, hondohondo na kware. Leo nimebahatika kumnasa kanga. Ningefurahi sana kumchinja na kumla!” Nilimjibu babu.
Babu alitabasamu kidogo kisha akasema, “Kanga elfu moja utawala. Tatizo ni hayo machozi. Machozi ya mwanaume yanatakiwa kuwa adimu sana. Leo jioni uje nikusimulie kisa cha mwanaume aliyepokonywa mke kwa ajili ya machozi.”
Nilizipenda sana hadithi na simulizi za babu. Kwa ujumla, kijiji kizima na hata vile vya jirani vilipendelea sana kuja kwetu kumsikiliza babu akisimulia matukio mbalimbali yaliyomkuta katika maisha yake. Hadithi zake zilijaa miujiza na maajabu kiasi kwamba baadhi ya watu walidiriki kumwita ‘mwongo’ au ‘anatia chumvi’. Lakini yeye aliwacheka watu wa aina hiyo na kuwaambia, “Hamjaiona dunia. Dunia yenu ni kijiji hiki pekee. Mimi nimeizunguka. Nimefika upande wa pili wa dunia!”
Hiyo ilikuwa kauli yake ya mara kwa mara, kauli ambayo iliongeza utamu wa simulizi zake. Hakika babu mwenyewe alikuwa hadithi, tena hadithi ya kusisimua kuliko zile simulizi zake. Inadaiwa kuwa, utotoni, akiwa na umri wangu, alitoweka kijijini hapo kama mzuka. Alitafutwa kwa siku kadhaa bila mafanikio. Watu walidhani kuwa ameliwa na simba au mamba. Lakini alipoibuka miaka kadhaa, baadaye, akiwa na simulizi tele za ‘kuizunguka dunia,’ watu walibadilika na kuamini kuwa alichukuliwa na mashetani ya chini ya bahari.
Pamoja na kuzipenda hadithi zake, pamoja na kiu ya kusikia kisa hicho cha ‘machozi ya mwanamume’ bado hasira dhidi ya kanga wangu aliyepeperushwa kwa makusudi na maumivu toka kwenye ngeu ya paji la uso kwa mara ya kwanza vilinifanya nikatae kwenda kumsikiliza.
Hivyo, kumwona baba akilia lilikuwa jambo jipya kabisa katika maisha yangu. Alikuwa kaketi juu ya gogo, mikono yake yote miwili ikiwa imekishika kichwa chake huku macho yake yakitazama mbele yake, ingawa ilikuwa dhairi kuwa haoni kitu chochote kutokana na wingi wa machozi. Nilijikaza na kumsogelea kwa nia ya kumuuliza kulikoni. Lakini mara nilipomfikia ushujaa ulinitoka. Nikajikuta nikiambulia kukaa ubavuni mwake, juu ya gogo lilelile. Kwa mshangao wangu, baba alifanya kitu ambacho hakupata kukifanya huko nyuma. Alinikumbatia kwa mkono wake mmoja huku mkono wake wa pili ukifuta machozi ambayo yalimiminika kwa wingi zaidi.
“Mwanangu!” nilimsikia akiniita kwa sauti ndogo yenye kigugumizi.
Sikumbuki kama niliitikia au la.
Wala yeye hakuzungumza neno jingine.
Nilipopata nafasi nilijichopoa toka katika mikono yake na kuingia ndani kwa dhamiri kuu mbili. Dhamiri ya kwanza ilikuwa kuficha machozi, ambayo mie pia yalianza kunilengalenga. Dhamiri ya pili ikiwa kumpata mama ili anifafanulie kisa na mkasa wa hali hiyo.
Mama hakuwepo. Wala hakuwepo mtu wa kumuuliza kwani mimi nilikuwa mtoto pekee katika familia hiyo. Na nilipatikana kwa shida baada ya mama na baba kuhangaika kwa waganga kwa zaidi ya miaka kumi. Hatimaye, walimpata mganga mmoja aliyebobea, ambaye alimtibu mama kwa kuchanganya mitishamba aina ya Mhusu na Mnywanya ambayo mama alitakiwa kunywa kwa siku mbili. Siku chache baadaye alitangaza kuwa yu mjamzito. Hapo mganga alimbadilishia dawa na kumnywesha mti uliotajwa kuwa Sagamba mara kwa mara hadi nilipozaliwa.
Miaka mingine kumi tayari ilikuwa imepita bila dalili za kupatikana mdogo wangu. Mganga wake alishakufa na hakupata kumwonyesha mtu yeyote miti ile. Hivyo, mimi nilikuwa kama mboni ya jicho kwa baba na mama, ingawa hawakutaka kamwe nijisikie hivyo.
Wakati nikihangaika bila mafanikio kuwaza na kuwazua namna ya kumnyamazisha baba, mara nilimwona mama akirudi nyumbani, huku kafuatana na babu. Kumbe yeye pia alikuwa amehangaika sana kumtuliza baba na kumuuliza kulikoni bila mafanikio. Ndipo lilipomjia wazo la kutembea mwendo wa zaidi ya dakika ishirini hadi kwa babu ambaye kwa bahati alikuwa nyumbani.
Kama kawaida yake, tofauti na watu wengine wote kijijini hapo, babu alikuwa amevaa kaptula yake nyeupe, shati jeupe, soksi nyeupe na viatu vyeusi. Akiwa miongoni mwa watu wengi waliovaa lubega za kaniki, miguu yao ikikanyaga chini, siku zote babu alionekana mtu wa aina ya pekee.
“Kuna nini?” babu alimuuliza mwanawe akiwa ameketi pale nilipoketi mimi muda mfupi uliopita. “Kuna nini?” alirudia na kuongeza, “Nasikia tangu umetoka kuonana na Mwami umerudi unalia. Kuna nini?”
Baba hakujibu mara moja. Alimtazama baba yake kwa muda kabla hajainuka taratibu na kumshika babu mkono. “Ni mambo mazito yaliyonipata leo. Twende faragha nikusimulie, ingawa nimekula kiapo cha kutotoa siri hii nje.”
Walikwenda pembeni, mahala ambapo masikio yangu na ya mama yasingeweza kusikia wanachozungumza. Hapo waliteta kwa muda mrefu, baba akizungumza babu akisikiliza. Baadaye, nilimwona babu akicheka na kuzungumza kwa muda kabla hawajarudi na kuketi tena kwenye gogo. Mama alipoona wametulia, aliingia ndani na kuwaletea kibuyu cha togwa ya mahindi. Waliinywa taratibu huku wakiwa kimya.
Nadhani togwa hii ilikuwa kali kwani baada ya muda mfupi nilimwona baba akichangamka huku babu akizungumza kwa sauti ya juu kidogo.
Sikubahatika kupata mtiririko wa maongezi yao. Lakini mawili matatu niliyoweza kudonoa katika matamshi yao yalinifanya nipate hisia kuwa nilihusika kwa njia moja au nyingine na majonzi yao. Imani hiyo ilijengeka zaidi pale nilipomsikia babu akisema kwa sauti ya juu kidogo, “Mjukuu wangu mie! Nadhani mwanangu hunifahamu hata kidogo. Haiwezekani!”
...