Hadithi: Kama Sijakoma, Sitakoma Tena

Hadithi: Kama Sijakoma, Sitakoma Tena

SEHEMU YA PILI
“Ni kwa sababu ya usalama wake. Halafu hii ni mimba yake ya kwanza, muache akajifungulie kwao” mke wangu akaniambia.
“Sawa. Nimeelewa”
“Utamsafirisha?”
“Ndiyo nitamsafirisha”
“Asante sana. Kwaheri”
Hapo hapo mke wangu akarudi katika hali yake ya kawaida. Akanitazama kisha akaniuliza.
“Mbona tumeketi?”
Ina maana hajui alichozungumza? Nikajiuliza.
“Nilikuwa nakusikiliza wewe” nikamjibu.
“Wanisikiliza mimi?” akaniuliza kwa mshangao.
“Una maana hujui ulichokuwa unazungumza?”
“Sijui, niambie nilikuwa nazungumza nini?”
Nikamueleza vile alivyozungumza.
“Labda nilipandisha shetani” akaniambia.
“Kwani wewe una shetani?”
Sakina akabetua mabega yake.
“Sijui” akasema.
“Hujawahi kupandisha shetani kabla ya leo?”
“Nilishawahi lakini zamani”
“Basi shetani wako amenieleza hivyo”
“Sasa umeelewa nini?”
“Nilichoelewa ni kukupeleka wewe Tabora ukifikisha miezi minane. Mengine sikuyaelewa”
“Labda una mwanamke anayenipiga vita, shetani wangu asingekwambia hivyo”
“Amini kwamba mimi sina mwanamke zaidi yako wewe mke wangu”
“Unajua mashetani wanaona. Asingekwambia hivyo isipokuwa kuna kitu amekiona”
“Labda kama wewe mwenyewe una mawazo hayo. Niliwahi kusikia mashetani husema kile kilicho moyoni mwa mtu”
“Mimi sina mawazo hayo. Kwani niliwahi kukwambia jambo kama hilo?”
“Basi tulale”
“Tusilale, nipeleke maliwatoni (chooni)”
Nikampeleka maliwatoni, tuliporudi tukalala.
Yale maneno ya shetani wa mke wangu niliyazingatia. Ujauzito wake ulipofikia miezi minane nikamsafirisha kwao Tabora.
Makubaliano yetu yalikuwa akae huko hadi atakapojifungua na kumaliza arobaini, ndiyo nimtumie nauli arudi Dar.
Mke wangu alipoondoka kwenda Tabora nikawa mpweke sana. Nikiondoka nyumbani asubuhi mara nyingi kurudi ni usiku. Nikimaliza shughuli zangu mchana ninakwenda kupiga stori na marafiki zangu hadi saa sita usiku.
Siku moja katika pitapita yangu nikakutana na mke wa yule rafiki yangu Machibya. Tulikutana karubu na soko la Ilala. Alikuwa anatoka sokoni.
“Vipi shem?” akaniuliza.
“Poa shem, za kupotea?”
“Nzuri, mwenzangu hajambo?”
Nilijua alikusudia mke wangu, nikamwambia.
“Hajambo lakini hayupo kwa sasa”
“Amekwenda wapi?”
“Amekwenda kwao Tabora kusalimia wazee”
“Atarudi lini?”
“Atachelewa kidogo”
“Sawa shem, haya kwaheri. Nawahi nyumbani nikamuandalie mzee”
“Nisalimie sana”
“Nitakusalimia sana”
Baada ya hapo tuliachana, kila mmoja akashika njia yake. Baada ya siku ile nikawa nakutana na yule msichana mara kwa mara. Alikuwa na mazoea ya kupita kwenye masikani yangu, mtaa wa Arusha ambapo palikuwa na ofisi yangu.
Kila alipopita alikuwa akisimama na kunisalimia. Na mimi humfuata na kusalimiana naye. Mazoea yalipozidi kunoga nikawa namsindikiza hadi nusu njia.
Kuna siku aliniomba namba yangu, nikamwambia mume wake anayo namba yangu.
“Nataka unipe wewe mwenyewe, siwezi kumwambia mume wangu anipe namba yako” akaniambia.
“Kwanini? Mwambie tu atakupa”
“Akiniuliza naitaka namba yako kwa ajili gani, nitamjibu nini?”
“Basi ngoja nikupe”
Nikampa namba yangu.
Aliijaza kwenye simu yake na kuniambia.
“Ngoja na mimi nikupe namba yangu”
Akaipiga ile namba yangu, simu yangu ikaita.
“Namba yangu ndiyo hiyo” aliniambia.
“Unaitwa nani?” nikamuuliza.
“Naitwa Nikole, na wewe unaitwa nani?”
Ilikuwa kama tunajuana sasa, nikamuuliza.
“Kumbe hujui jina langu?”
“Mume wangu ndiye anayelijua lakini mimi silijui, nakuita shem tu”
“Mimi naitwa Macheo”
“Nimefurahi kulijua jina lako”
Akaliandika kwenye simu yake pamoja na namba yangu.
Baada ya hapo tukaagana. Usiku wake akanipigia simu. Ilikuwa saa tatu usiku. Akaniambia.
“Hello Macheo!” Hakutumia tena neno shemeji.
“Oh shem, habari ya saa hizi?”
“Nzuri. Hilo jina la shem linachosha bwana, liache niite Nikole”
Nikacheka kidogo lakini tayari alishanipa wasiwasi. Nilikuwa najiuliza kwanini aniambie vile.
“Mzee yuko wapi?” nikamuuliza ili kutaka kujua kama alitamka vile mbele ya mume wake.
“Ametoka” akanijibu haraka.
Sasa nikapata jibu. Nikamuuliza tena.
“Amekwenda wapi saa hizi?’
“Achana naye. Tuzungume yetu. Unajua kuna kitu nataka nikwambie lakini naomba kiwe ni siri ya mimi na wewe”
Moyo ulinilipuka!
ITAENDELEA
 
Kabla hamjaleta upuuzi wenu muwe mnajipanga kwanza.
Story za kuungaunga...mnajaza server bure!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kabla hamjaleta upuuzi wenu muwe mnajipanga kwanza.
Story za kuungaunga...mnajaza server bure!

Sent using Jamii Forums mobile app
Kunamajitu Humu Yanakera Sana! Kwahio Unataka Mleta Stori Ashinde Nakukesha Jf Akikuridhisa Wewe? Unadhan Hana Kaz Zakufanya?
Hata Kama Akileta Epsode 1/wiki
Ninafac Yake! Hana Hasara Hata Akiacha! Sasa Unapo Mlaumu Unashangaza Sana. Kama Vepe Anzisha Nawewe Uwe Unashinda Jf! Tumbaf Sana
 
Nilipoona umeandika 'Vepe' nikaona hakuna haja ya kujibizana na gasho.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
KAMA SIJAKOMA, SITAKOMA TENA
MTUNZI: FAKI A FAKI

SEHEMU YA TATU

“Kitu gani hicho?” nikamuuliza.

“Wewe ni mtu mkubwa na ni muelewa, si lazima nikueleze kila kitu. Unaweza kugundua kitu kwa akili yako” akaniambia. Sauti yake ilikuwa tulivu sana.

“Ukiniambia hivyo unanipa mtihani, ninaweza kufikiria mengi lakini siyo yaliyoko moyoni mwako. Ni vizuri uniambie” nikamwambia ingawa nilishajua alichokikusudia.

“Huwezi hata kukisia?”

“Siwezi”

“Nakupenda” akaniambia ghafla.

Aliponiambia hivyo palipita kimya cha sekunde kadhaa kwa upande wake na wangu kisha ghafla nikaisikia sauti yake.

“Umenisikia?”

“Nimekusikia”

“Nimesikia gari imesimama nje, nafikiri ni mume wangu amerudi. Tutaongea zaidi wakati mwingine. Usiku mwema” akaniambia na kukata simu.

Siku ile nilikuwa nimewahi kurudi nyumbani. Wakati nazungumza na Nikole nilikuwa nimeketi sebuleni kwangu.

Nikaiweka simu yangu chini na kuanza kuwaza. Kilichonitia mashaka ni kuwa Nikole alikuwa na mume wake na mume huyo alikuwa rafiki yangu ingawa urafiki wetu haukuwa mkubwa kivile.

Isitoshe mimi pia nilikuwa na mke wangu ingawa kwa kipindi kile hakuwepo.

Baada ya kuwaza sana niliona isingekuwa vizuri kujiingiza katika uhusiano wa kimapenzi na mke wa mtu.

Japokuwa nilipitisha uamuzi huo niliendelea kumuwaza msichana huyo karibu usiku kucha na pia nilimuota.

Niliota niko naye chumbani kwake kisha ghafla mume wake akatokea na kutufumania. Hapo hapo nikagutuka.

Siku iliyofuata msichana alinipigia tena simu saa sita mchana.

“Mambo?” akaniambia.

“Poa…vipi?”

“Safi tu, za tangu jana?”

“Safi, niambie”

“Jana tulikatiza mazungumzo yetu. Yule bwana alitokeaa ghafla. Lakini nadhani ulinielewa?”

“Nilikuelewa”

“Sasa unaniambiaje?”

“Nasita kukupa jibu kwa sababu wewe ni mke wa mtu halafu mtu mwenyewe niko karibu naye sana”

“Usijali. Nimekwambia itakuwa siri yetu, hawezi kujua”

“Nafikiri hakitakuwa kitu kizuri”

“Kwani mke wako si hayupo kwa sasa na umeniambia atachelewa kurudi”

“Atachelewa kidogo”

“Sasa nani anakuliwaza?”

“Nimejipa likizo ya muda mfupi”

“Usifanye hivyo, mimi nimekupenda”

“Unajua mume wako akijua itakuwa sio vizuri”

“Hawezi kujua, sisi si watoto wadogo tuna akili zetu”

“Basi acha nifikirie kwanza”

“Fikiria halafu utaniambia”

“Sawa”

Msichana akakata simu.

Hata huo muda wa kufikiria sikuupata. Msichana alikuwa akinipigia simu mara kwa mara kunishawishi. Alipokwenda au kurudi sokoni alikuwa akipita pale pale kwenye masikani yangu ili nimuone.

Napenda nikiri kuwa msichana mwenyewe alikuwa mzuri na alikuwa akijua kubembeleza. Siku chache tu baadaye akafanikiwa kuubadili moyo wangu.

Msichana alipoona ninaelekea kukubaliana naye alinipigia simu jioni akaniambia atakuja nyumbani kwangu saa moja usiku.

“Usije nyumbani” nikamwambia.

“Unaogopa nini Macheo, mume wangu hayupo”

“Amekwenda wapi?”

“Amekwenda Tabora. Ameondoka leo jioni”

“Saa moja ni mapema sana, njoo saa mbili. Kutakuwa kutulivu”

“Sawa. Nitakuja saa mbili, unisubiri”

Tulipomaliza kuzungumza nilijiambia kwa vile mke wangu hakuwepo na mume wa Nikole amesafiri isingekuwa vibaya kuwa naye.

Ilipofika saa mbili kasorobo tayari nilikuwa nyumbani nikisubiri nipigiwe simu. Saa mbili kasoro dakika tano Nikole akanipigia simu.

“Ninakuja, niko kwenye teksi. Acha mlango wazi” akaniambia.

“Sawa, njoo tu”

Nikaenda kufungua mlango na kuusindika ili Nikole akifika asiwe na haja ya kubisha, asukume mlango tu na kuingia kama mwenyeji.

Bila shaka alipopiga simu alikuwa yuko karibu kwani muda ule ule teksi ikasimama barazani.

ITAENDELEA
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom