Tanzania Sweetheart
Member
- Mar 17, 2020
- 46
- 63
MTUNZI: FAKI A. FAKI
SEHEMU YA KWANZA
Fikiria kwamba uko chumbani na mke wa rafiki yako aliyeko safarini. Mwanamke anakwambia kwamba anakupenda. Anakulaghai kwa maneno mpaka unalainika. Unaamua kulala naye baada hatatoka chumbani mwako usiku ule.
Asubuhi kunapokucha unamuamsha mwenzako aende kuoga awahi kurudi nyumbani kwake ili watu wasije wakaona amelala kwako.
Lakini unagundua kuwa mwenzako huyo si mzima. Alishakufa tangu usiku. Ahadi yake imemfikia akiwa kwako. Ulilala na maiti!.
Utafanyaje? Utakwenda polisi kutoa taarifa ya kifo chake? Utamsubiri mumewe uje umwambie? Au utawafahamisha majirani zako kuwa umefiwa na mke wa rafiki yako chumbani mwako?
Ninaamini kwamba unaweza kuchanganyikiwa na pengine utachukua hatua ya kipumbavu kama niliyochukua mimi na kusababisha nitamani kufa kuliko kuwa hai.
Sasa ungana nani katika simulizi hii mpya kuanzia sehemu hii ya kwanza hadi mwisho wake.
SASA ENDELEA
Jina langu ni Macheo Nurdin Macheo. Umri wangu ni miaka thelathini na tano, mkazi wa Ilala jijini Dar.
Nyumba niliyokuwa ninaishi ni ya urithi wa marehemu baba yangu. Tuliirithi mimi na mdogo wangu wa kiume anayefanya kazi Morogoro.
Baada ya masomo yangu nilipata kazi Idara ya Ardhi lakini sikuendelea nayo kwa miaka mingi nikafukuzwa kazi. Nilifukuzwa mimi na wenzangu wawili kwa makosa ya ulanguzi wa viwanja.
Baada ya hapo niliamua kujiajiri mwenyewe ajira isiyo rasmi. Nikawa dalali wa nyumba, viwanja na pia mashamba. Ilikuwa kazi nzuri na wakati mwingine mbaya. Nzuri kwa sababu kuna kipindi inaweza kukuingizia pesa nyingi unapompatia mtu nyumba, kiwanja au shamba. Lakini inakuwa mbaya pale wateja wanapokosekana.
Pamoja na hali hiyo niliweza kuishi vizuri ingawa sikuweza kumiliki usafiri wangu mwenyewe kama ilivyokuwa hapo mwanzo ambapo nilikuwa nikitumia gari la serikali hata kwa shughuli zangu binafsi.
Kabla ya kufukuzwa kazi, tayari nilikuwa nimeshafunga ndoa na msichana mmoja Mnyamwezi wa Tabora ambaye nilikutana naye hapa hapa Dar, tukapendana na kuamua kuoana. Alikuwa anaitwa Sakina.
Niliishi naye kwa miaka mitatu kabla ya kupata ujauzito. Ule mwaka ambao nafukuzwa kazi ndio alipata mimba. Machungu ya kufukuzwa kazi yakapozwa na furaha ya mke wangu kupata ujauzito kwani tulikuwa tunatamani kupata mtoto.
Nilikuwa na rafiki yangu anaitwa Machibya. Nilijuana naye baada ya kumtafutia nyumba ya kuishi. Nilimpatia nyumba pale pale Ilala. Ilikuwa nyumba ya kupangisha iliyokuwa na karibu vyumba sita. Machibwa alikuwa mnyamwezi wa Nzega. Alikuja Dar kikazi.
Tulizoea kuitana shemeji kwa vile mke wangu alikuwa mnyamwezi kama yeye. Machibya alikuwa na mke wa kizaramu wa hapa hapa Dar. Aliwahi kunitambulisha kwa mke wake na mimi niliwahi kumtambulisha kwa mke wangu. Siku moja moja tulikuwa tunatembeleana majumbani.
Siku moja wakati mke wangu akiwa mjamzito, tulikuwa tumelala usiku. Mke wangu aliamka ghafla akaketi kitandani na kuanza kutetemeka.
Mimi nilikuwa macho, nikawa namtazama. Nilipoona anazidi kutetemeka nikamuuliza.
“Sakina una nini?”
Sakina hakujibu, badala yake alianza kupiga kelele. Hapo nilipata hofu nikainuka na kumshika.
“Sakina una nini? Unajisikia kuumwa?”
Akaanza kutikisa kichwa. Kwanza nilidhani anatikisa kichwa kuashiria kuwa hakuwa anaumwa. Lakini jinsi alivyokuwa anakitikisa kwa nguvu na kwa mfululizo, nilianza kufikiria mengine.
“Una nini?” nikamuuliza sasa kwa sauti kali.
“Hatari! Hatari! Hatari!” akasema akiwa amenitolea macho.
Nikahisi alikuwa amepandisha shetani. Jasho lilikuwa linamkatika.
“Hatari ya nini?” nikamuuliza.
“Hatari inanikabili mimi, ninapigwa vita!” akaniambia kwa mkazo.
“Sasa ni hatari gani na ni nani anayekupiga vita?”
“Yuko mtu hanitaki mimi, anataka niondoke”
“Uondoke wapi?”
“Hapa nyumbani”
“Ni nani?”
“Mwanamke, namjua vizuri”
“Mbona mimi simjui”
Nilipomuuliza hivyo alinyamaza akaendelea kutetemeka.
“Mbona mimi simjui?” nikamuuliza tena.
“Utamjua tu, utamjua tu muda si mrefu. Atajitokeza mwenyewe”
“Huyo mwanamke anataka nini?”
Badala ya kunijibu alipiga kelele huku akisema.
“Nasikia harufu ya damu! Nasikia harufu ya damu ndani ya nyumba yangu”
“Mbona sikuelewi, kwani wewe ni nani?”
“Mimi ni Mwalimu Ruhani, natoka Bara Arab. Nataka kukwambia kitu”
“Kitu gani?’
“Kiti wangu akifikisha miezi minane aende Tabora”
“Kwanini?” nikamuuliza.
ITAENDELEA....
Sent using Jamii Forums mobile app